Yoshua 11:1-23, Yoshua 12:1-24 NEN

Yoshua 11:1-23

Wafalme Wa Kaskazini Washindwa

11:1 Amu 4:2, 7, 23; Za 83:9; Yos 12:19; 15:23-25; 19:36; 1Sam 12:9; 1Fal 9:15; 2Fal 15:29; Neh 11:33; Yer 49:28, 33; Yos 12:20; 19:25Ikawa Yabini mfalme wa Hazori aliposikia habari za mambo haya, akatuma ujumbe kwa Yobabu mfalme wa Madoni, na kwa mfalme wa Shimroni, na kwa mfalme wa Akishafu, 11:2 Yos 12:1; 18:18; Hes 34:11; Kum 3:17; Yos 19:35; 1Fal 15:20; Yos 12:23; 17:11; Amu 1:27; 1Fal 4:11; 1Nya 7:29na pia kwa wafalme wa upande wa kaskazini wale waliokuwa milimani, katika Araba upande wa kusini mwa Kinerethi, kwenye shefela, upande wa magharibi na katika miinuko ya Nafoth-Dori upande wa magharibi; 11:3 Yos 3:10; Hes 13:17; Kut 3:8; Kum 7:1; Amu 3:3-5; 1Fal 9:20; Kum 3:8; Mwa 31:49; Yos 15:38; 18:26; Amu 11:11; 20:1; 21:1; 1Sam 7:5-6; 1Fal 15:22; 2Fal 25:23kwa Wakanaani upande wa mashariki na magharibi; kwa Waamori, Wahiti, Waperizi na Wayebusi katika nchi ya vilima; na kwa Wahivi chini ya Hermoni katika eneo ya Mispa. 11:4 Mwa 12:2; Amu 7:12; 1Sam 13:5; Mwa 22:17; 32:12Wakaja na vikosi vyao vyote na hesabu kubwa ya farasi na magari ya kuvutwa na farasi, jeshi kubwa, kama wingi wa mchanga ulio pwani ya bahari. 11:5 Amu 5:19Wafalme hawa wote wakaunganisha majeshi yao na kupiga kambi pamoja kwenye Maji ya Meromu, ili kupigana dhidi ya Israeli.

11:6 Yos 2:24; Mwa 49:6Bwana akamwambia Yoshua, “Usiwaogope, kwa sababu kesho saa kama hii nitawatia wote mikononi mwa Israeli, wakiwa wameuawa. Utakata mishipa ya nyuma ya miguu ya farasi wao na kuyachoma moto magari yao ya vita.”

Hivyo Yoshua pamoja na jeshi lake lote wakaja dhidi yao ghafula kwenye Maji ya Meromu kuwashambulia, 11:8 Mwa 10:15; Amu 18:7; Yos 13:6naye Bwana akawatia mikononi mwa Israeli. Wakawashinda na kuwafukuza hadi Sidoni Kuu na kuwafikisha Misrefoth-Maimu, hadi Bonde la Mispa upande wa mashariki, hadi pakawa hakuna yeyote aliyebaki. Yoshua akawatendea kama Bwana alivyoamuru. Akakata mishipa ya nyuma ya miguu ya farasi wao na kuchoma moto magari yao ya vita.

11:10 Isa 3:25; Yer 41:2; 44:18Wakati huo Yoshua akarudi na kuuteka mji wa Hazori na kumuua mfalme wake kwa upanga. (Hazori ulikuwa mji mkuu wa falme hizo zote.) 11:11 Kum 7:2; 20:16-17; Hes 31:10Kila aliyekuwa ndani yake wakamuua kwa upanga. Wakawaangamiza kabisa, wala hawakusaza chochote chenye pumzi na akauchoma Hazori kwenyewe kwa moto.

11:12 Hes 33:50-52; Kum 7:2Yoshua akaiteka hii miji yote ya kifalme pamoja na wafalme wake na kuwapiga kwa upanga. Akawaangamiza kabisa wote, jinsi Mose mtumishi wa Bwana alivyowaagiza. Lakini Israeli hawakuichoma moto hata mojawapo ya miji iliyojengwa katika vilima vyao vidogo isipokuwa mji wa Hazori ambao Yoshua aliuchoma moto. 11:14 Kum 20:16; Mwa 22:17; 32:12Waisraeli wakajichukulia nyara zote na mifugo yote ya miji hii, bali waliwaua watu wote kwa upanga hadi walipowaangamiza kabisa, pasipo kumbakiza yeyote mwenye pumzi. 11:15 Kut 34:11; Kum 7:2; Yos 1:7Kama vile Bwana alivyomwagiza Mose mtumishi wake, vivyo hivyo Mose alimwagiza Yoshua, naye Yoshua akafanya kama vivyo, hakukosa kufanya lolote katika yale yote Bwana aliyomwagiza Mose.

11:16 Hes 13:17; Kum 1:7; Yos 10:41Yoshua akaiteka nchi hii yote: nchi ya vilima, Negebu yote, eneo yote ya Gosheni, shefela ya upande wa magharibi, Araba na milima ya Israeli pamoja na shefela zao, 11:17 Mwa 14:6; Hes 24:18; Kum 33:2; Yos 13:5; Kum 3:25; Yos 12:7-8; Kum 3:9; 7:24kuanzia Mlima Halaki ambao umeinuka kuelekea Seiri hadi Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni chini ya Mlima Hermoni. Akawateka wafalme wake wote, akawapiga na kuwaua. Yoshua akapigana vita dhidi ya wafalme hawa wote kwa muda mrefu. 11:19 Yos 9:1-3; 9:15Hakuna mji wowote katika eneo hili uliofanya mkataba wa amani na Israeli, isipokuwa hao Wahivi wa Gibeoni. Wengine wote walishindwa katika vita. 11:20 Kut 4:21; Rum 9:18; Kut 14:17; Kum 7:16; Amu 14:4; Kum 2:30; 1Sam 2:25; 1Fal 12:15; 22:20-23; Yak 1:13-17; Kum 20:16Kwa maana Bwana mwenyewe ndiye aliifanya mioyo yao iwe migumu, ili kupigana vita dhidi ya Israeli ili apate kuwafutilia mbali pasipo huruma, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

11:21 Hes 13:22, 33; Yos 10:3; 15:50; Kum 9:2; Amu 1:10; Yer 3:23Wakati huo Yoshua akaenda kuwaangamiza Waanaki kutoka nchi ya vilima: kuanzia Hebroni, Debiri na Anabu, na kutoka nchi yote ya vilima ya Yuda na kutoka nchi yote ya vilima ya Israeli. Yoshua akawaangamiza kabisa pamoja na miji yao. 11:22 Mwa 10:19; Yos 12:17; 19:13; 1Sam 5:8; 17:4; 1Fal 2:39; 2Fal 14:25; 1Nya 8:13; Amo 6:2; Yos 15:47; 1Sam 5:1; Isa 20:1Hawakubaki Waanaki wowote katika nchi ya Israeli, ila tu katika nchi ya Gaza, Gathi na Ashdodi. 11:23 Yos 21:43-45; Neh 9:24; Kum 1:38; 12:9-10; 25:19; Yos 13:7; Hes 26:53; Za 105:44; Kut 33:14; Yos 14:15Hivyo Yoshua akaiteka nchi hiyo yote kama vile Bwana alivyokuwa amemwagiza Mose, naye Yoshua akawapa Israeli kuwa urithi wao, kulingana na walivyogawanyika katika kabila zao.

Ndipo nchi ikawa na amani bila vita.

Read More of Yoshua 11

Yoshua 12:1-24

Orodha Ya Wafalme Walioshindwa

12:1 Za 136:21; Hes 32:19; 21:13; Kum 3:8; Yos 11:2Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:

12:2 Yos 12:5; Hes 21:21-25; Yos 13:10; Amu 11:19; Hes 32:34; Yos 13:16; Mwa 19:38; 31:21; 32:22; Hes 32:26; Kum 2:36; 3:15; Yos 13:11, 25; 17:1; 20:8; 21:38; Amu 5:17; 7:3; 10:8Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.

Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi. 12:3 Yos 11:2; Mwa 14:3; Hes 33:49; Yos 13:20; Hes 21:20Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi12:3 Yaani Bahari ya Galilaya. hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi12:3 Yaani Bahari Mfu.), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.

12:4 Hes 21:21; 33; Yos 13:30; Mwa 14:5; Kum 1:4Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.

12:5 Kum 3:10; Hes 32:33; Yos 17:1; 20:8; 21:27; 22:7; 13:2, 13; 1Sam 27:8; Kum 3:14Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.

12:6 Kum 3:8; Hes 32:29-33; Yos 13:8Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.

12:7 Yos 11:17Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao: 12:8 Ezr 9:1; Kum 1:7; Yos 3:10; 11:17nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):

12:9 Hes 33:48; Mwa 12:8; Yos 8:1; 7:2; 8:9; 18:13; Amu 1:23; 4:4; 20:18; 21:2; Neh 11:31mfalme wa Yeriko mmojamfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja12:10 Yos 10:1mfalme wa Yerusalemu mmojamfalme wa Hebroni mmoja12:11 Yos 10:3mfalme wa Yarmuthi mmojamfalme wa Lakishi mmoja12:12 Yos 10:3, 33mfalme wa Egloni mmojamfalme wa Gezeri mmojamfalme wa Debiri mmojamfalme wa Gederi mmoja12:14 Hes 14:45; 21:1mfalme wa Horma mmojamfalme wa Aradi mmoja12:15 Hes 33:20; Mwa 38:1; Yos 15:35; Mik 1:15mfalme wa Libna mmojamfalme wa Adulamu mmoja12:16 Yos 10:10; 7:2mfalme wa Makeda mmojamfalme wa Betheli mmoja12:17 Yos 15:34; 16:8; 17:8; 11:22; 1Fal 4:10mfalme wa Tapua mmojamfalme wa Heferi mmoja12:18 Yos 13:4; 19:30; Amu 1:31; 1Sam 4:1; 29:1mfalme wa Afeki mmojamfalme wa Lasharoni mmoja12:19 Yos 11:1mfalme wa Madoni mmojamfalme wa Hazori mmoja12:20 Yos 11:1mfalme wa Shimron-Meroni mmojamfalme wa Akishafu mmoja12:21 Yos 17:11; 21:25; Amu 1:27; 5:19; 1Fal 4:12mfalme wa Taanaki mmojamfalme wa Megido mmoja12:22 Yos 15:23; 19:37; 20:7; 21:32; Amu 4:6-9; Yos 19:11; 21:34; 15:55; 19:26; 1Sam 15:12; 2Sam 23:35mfalme wa Kedeshi mmojamfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja12:23 Yos 11:2mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) 12:23 Au: katika miinuko ya Nafoth-Dori.mmojamfalme wa Goimu katika Gilgali mmoja12:24 1Fal 14:17; 15:33; 16:8, 23; Wim 6:4; Za 135:11; 136:18mfalme wa Tirsa mmoja

wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.

Read More of Yoshua 12