Yoshua 1:1-18, Yoshua 2:1-24 NEN

Yoshua 1:1-18

Bwana Anamwagiza Yoshua

1:1 Kut 14:31; Kum 34:5; Ufu 15:3; Kut 17:9; 24:13; Hes 32:20; Yos 22:2-4Baada ya kifo cha Mose mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Mose: 1:2 Hes 13:29; 35:10; Mwa 15:14; 12:7; Kum 1:24-25“Mtumishi wangu Mose amekufa. Sasa basi, wewe pamoja na watu wote hawa, jiandaeni kuvuka huu Mto Yordani kuingia nchi ambayo karibu nitawapa wana wa Israeli. 1:3 Kum 11:24; Mwa 50:24; Hes 13:2; Kum 1:8Kila mahali nyayo za miguu yenu zitakapokanyaga nimewapa, kama vile nilivyomwahidi Mose. 1:4 Kum 3:25; Mwa 2:14; 10:15; 23:10; Kut 3:8; Hes 34:2-12; Ezr 4:20Nchi yenu itaenea kuanzia jangwa hili hadi Lebanoni, tena kuanzia mto mkubwa wa Frati, yaani nchi yote ya Wahiti, hadi Bahari ile Kubwa1:4 Yaani Bahari ya Mediterania. iliyoko upande wa magharibi. 1:5 Kum 7:24; Mwa 26:3; 39:2; Amu 6:12; 1Sam 10:7; Yer 1:8; 30:11; Mwa 28:1; Kum 4:31Hakuna mtu yeyote atakayeweza kushindana na wewe siku zote za maisha yako. Kama vile nilivyokuwa pamoja na Mose, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe, sitakuacha wala sitakupungukia.

1:6 2Sam 2:7; 1Fal 2:2; Isa 41:6; Yoe 3:9-10; Kum 1:21; 31:6; Amu 5:21; Yer 3:18; 7:7“Uwe hodari na shujaa, kwa sababu wewe ndiwe utakayewaongoza watu hawa kuirithi nchi niliyowaapia baba zao kuwapa. 1:7 Kum 29:9; 1Fal 2:3; 3:3; Ezr 7:26; Za 78:10; 119:136; Isa 42:24; Yer 26:4-6; 32:23; 44:10; Hes 12:7; Ay 42:7; Kum 5:32; Yos 23:6; Kum 4:2; 5:33; 11:8; Yos 11:15Uwe hodari na uwe na ushujaa mwingi. Uwe na bidii kutii sheria yote aliyokupa Mose mtumishi wangu, usiiache kwa kugeuka kuelekea kuume au kushoto, ili upate kufanikiwa popote uendako. 1:8 Kum 28:61; Za 147:19; Kut 4:15; Isa 59:21; Mwa 24:63; Kum 29:9; 1Sam 18:14; Isa 52:13; 53:10; Yer 23:5Usiache Kitabu hiki cha Sheria kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi. 1:9 Kum 31:6; Yos 10:8; 2Fal 19:6; Isa 34:5; 37:6; Kum 1:21; Ay 4:5; Kum 31:8; Yer 1:8Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakuwa pamoja nawe kokote uendako.”

1:10 Kum 1:15Ndipo Yoshua akawaagiza maafisa wa watu akisema, 1:11 Yos 3:2; 1Sam 17:22; Isa 10:28; Mwa 40:13; Hes 35:10; 33:53“Pitieni katika kambi yote mkawaambie watu, ‘Wekeni tayari mahitaji yenu. Siku tatu kuanzia sasa mtavuka hii Yordani ili kuingia na kuimiliki nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa iwe yenu wenyewe.’ ”

1:12 Hes 32:33Lakini kwa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, Yoshua akasema, 1:13 Kut 33:14; Za 55:6; Isa 11:10; 28:12; 30:15; 32:18; 40:31; Yer 6:16; 45:3“Kumbukeni agizo lile Mose mtumishi wa Bwana alilowapa: ‘Bwana Mungu wenu anawapa ninyi raha, naye amewapa nchi hii.’ 1:14 Kum 3:19; Hes 32:26; Kut 13:18; Yos 4:12Wake zenu, watoto wenu na mifugo yenu watakaa katika nchi ile Mose aliyowapa mashariki ya Yordani, lakini mashujaa wenu wote, wakiwa wamevikwa silaha kikamilifu lazima wavuke mbele ya ndugu zenu. Imewapasa kuwasaidia ndugu zenu hadi 1:15 Hes 32:20-22; Yos 22:1-4Bwana awape nao raha, kama alivyokwisha kufanya kwa ajili yenu hadi wao pia watakapokuwa wamemiliki nchi ile Bwana Mungu wenu anayowapa. Baada ya hilo, mwaweza kurudi na kukalia nchi yenu wenyewe, ambayo Mose mtumishi wa Bwana aliwapa mashariki mwa Yordani kuelekea linakochomoza jua.”

1:16 Hes 27:20; 32:25Ndipo wakamjibu Yoshua, “Chochote ambacho umetuagiza tutafanya na popote utakapotutuma tutakwenda. 1:17 Hes 32:25; Kum 1:21; 31:6; Mwa 21:22; 26:24, 28; 1Sam 16:18; 20:13; 1Fal 1:37; Za 20:1-4, 9; Rum 8:31Kama vile tulivyomtii Mose kikamilifu, ndivyo tutakavyokutii wewe. Bwana Mungu wako na awe pamoja nawe tu kama vile alivyokuwa pamoja na Mose. Yeyote atakayeasi neno lako na kuacha kuyatii maneno yako, au chochote utakachowaamuru, atauawa. Uwe imara na hodari tu!”

Read More of Yoshua 1

Yoshua 2:1-24

Rahabu Na Wapelelezi

2:1 Mwa 42:9; Hes 25:1; Yos 3:1; Yoe 3:18; Hes 21:32; Amu 18:2; Hes 33:48; Yos 6:17, 25; Ebr 11:31Kisha Yoshua mwana wa Nuni kwa siri akawatuma wapelelezi wawili kutoka Shitimu, akawaambia, “Nendeni mkaikague hiyo nchi, hasa Yeriko.” Kwa hiyo wakaenda na kuingia kwenye nyumba ya kahaba mmoja jina lake Rahabu na kukaa humo.

2:2 Za 127:1; Mit 21:30Mfalme wa Yeriko akaambiwa, “Tazama! Baadhi ya Waisraeli wamekuja huku usiku huu kuipeleleza nchi.” 2:3 Yos 6:23Hivyo mfalme wa Yeriko akatuma huu ujumbe kwa Rahabu: “Watoe wale watu waliokujia na kuingia nyumbani mwako, kwa sababu wamekuja kuipeleleza nchi yote.”

2:4 Yos 6:22; 6:17; 2Sam 17:19-20; 2Fal 6:19Lakini huyo mwanamke alikuwa amewachukua hao watu wawili na kuwaficha. Akasema, “Naam, watu hao walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka. 2:5 Amu 5:8; 9:35; 16:2; Ebr 11:31Kulipoingia giza, wakati wa kufunga lango la mji, watu hao waliondoka. Sijui njia waliyoiendea. Wafuatilieni haraka. Huenda mkawapata.” 2:6 Amu 15:14; Mit 31:13; Isa 19:9; Kut 1:19; Yos 6:25; 2Sam 17:19; Yak 2:25; Kut 1:17(Lakini alikuwa amewapandisha darini akawafunika kwa mabua ya kitani aliyokuwa ameyatandika darini.) 2:7 Hes 22:1; Amu 3:28; 7:24; 12:5-6; Isa 16:2Basi hao watu wakaondoka kuwafuatilia hao wapelelezi katika njia ile inayoelekea vivuko vya Yordani, mara tu wafuatiliaji walipotoka nje, lango likafungwa.

2:8 Kum 22:8; Amu 16:27; 2Sam 16:22; Neh 8:16; Isa 15:3; 22:1; Yer 32:29Kabla wale wapelelezi hawajalala, Rahabu akawaendea huko juu darini, 2:9 Mwa 35:5; Kut 15:14-15; Mwa 35:5; Kum 2:25; 11:25akawaambia, “Ninajua kuwa Bwana amewapa nchi hii na hofu kuu imetuangukia kwa sababu yenu, kiasi kwamba wote waishio katika nchi hii wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yenu. 2:10 Mwa 8:1; Kut 14:21; Yos 3:17; Za 74:15; Hes 23:22; 21:21; Mwa 10:16; 14:7; Yos 9:10Tumesikia jinsi Bwana alivyokausha maji ya Bahari ya Shamu kwa ajili yenu mlipotoka Misri, pia lile mlilowatendea Sihoni na Ogu, wafalme wawili wa Waamori mashariki mwa Yordani, ambao mliwaangamiza kabisa. 2:11 Mwa 42:28; Kum 2:25; Za 107:26; Yon 1:5; Kut 15:14; Yos 5:1; 7:5; 2Sam 4:1; Za 22; 14; Isa 13:7; 19:1; Yer 51:30; Nah 2:10; 2Fal 5:15; 19:15; Dan 6:26; Mwa 14:19; Hes 20:14; Kum 4:39Tuliposikia juu ya hili, mioyo yetu iliyeyuka na kila mmoja alikosa ujasiri kwa sababu yenu, kwa maana Bwana Mungu wenu ni Mungu juu mbinguni na duniani chini. 2:12 Mwa 24:8; 47:31; 24; 12; Rut 3:10; Mwa 24:14; Kut 3:12; Yos 4:6; 1Sam 2:34; 2Fal 19:29Sasa basi, tafadhali niapieni kwa Bwana, kwamba mtaitendea hisani jamaa ya baba yangu, kwa kuwa mimi nimewatendea hisani. Nipeni ishara ya uaminifu 2:13 Yos 6:23kwamba mtayahifadhi maisha ya baba yangu na mama yangu, ndugu zangu wa kiume na wa kike, pamoja na wale wote walio wa kwao na kwamba mtatuokoa na kifo.”

2:14 1Fal 20:39-42; 2Fal 10:24; Mwa 47:29; Mt 5:7; Amu 1:24; Mt 5:7Wale watu wakamhakikishia Rahabu, “Uhai wetu kwa uhai wenu! Ikiwa hutatoa habari ya nini tunachofanya, wakati Bwana atakapotupa nchi hii, tutawatendea kwa hisani na kwa uaminifu.”

2:15 Yer 38:6, 11; Mwa 26:8; Amu 5:28; 1Sam 19:12; Mdo 9:25; Ebr 11:31Kisha akawateremsha dirishani kwa kamba, kwa kuwa nyumba yake aliyokuwa anaishi ilikuwa sehemu ya ukuta wa mji. 2:16 Yak 2:25; Mwa 14:10; Ebr 11:31Alikuwa amewaambia, “Nendeni vilimani ili wale wafuatiliaji wasiwapate. Jificheni huko kwa siku tatu mpaka watakaporudi, hatimaye mwende zenu.”

2:17 Mwa 24:8; Kut 20:7Wale watu wakamwambia, “Hiki kiapo ulichotuapisha hakitatufunga, 2:18 Yos 6:23; Mwa 7:1; 19:12, 17; Es 8:6; Mdo 11:14; 2Tim 1:16isipokuwa, hapo tutakapoingia katika nchi hii, utakuwa umefunga hii kamba nyekundu dirishani pale ulipotuteremshia na kama utakuwa umewaleta baba yako na mama yako, ndugu zako na jamaa yako yote ndani ya nyumba yako. 2:19 Law 20:9; Eze 33:4; Hes 34:26, 27Ikiwa mtu yeyote atatoka nje ya nyumba yako akaenda mtaani, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe, hatutawajibika. Lakini yule ambaye atakuwa ndani pamoja nawe, kama mkono wa mtu yeyote ukiwa juu yake damu yake itakuwa juu ya vichwa vyetu. 2:20 Mwa 24:8; 47:31Lakini ikiwa utatoa habari ya shughuli yetu tunayofanya, tutakuwa tumefunguliwa kutoka kwenye kiapo hiki ulichotufanya tuape.”

Naye akajibu, “Nimekubali. Na iwe kama mnavyosema.” Kwa hiyo akaagana nao, nao wakaondoka. Yeye akaifunga ile kamba nyekundu dirishani.

Walipoondoka, wakaelekea vilimani na kukaa huko siku tatu, hadi wale waliokuwa wakiwafuatilia wakawa wamewatafuta njia nzima na kurudi pasipo kuwapata. Ndipo wale watu wawili wakaanza kurudi. Wakashuka kutoka kule vilimani, wakavuka mto na kuja kwa Yoshua mwana wa Nuni, na kumweleza kila kitu kilichowapata. 2:24 Yos 10:8; 11:6; Amu 3:28; 7:9; 20:28; 1Sam 14:10; Kut 15:15Wakamwambia Yoshua, “Hakika Bwana ametupa nchi yote mikononi mwetu; watu wote wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yetu.”

Read More of Yoshua 2