Yona 1:1-17, Yona 2:1-10, Yona 3:1-10, Yona 4:1-11 NEN

Yona 1:1-17

Yona Anamkimbia Bwana

1:1 Mt 16:4; 12:39-41; 2Fal 14:25; Lk 11:29-32Neno la Bwana lilimjia Yona mwana wa Amitai: 1:2 Mwa 10:11; 18:20; Yon 3:3; Nah 2:8; Mt 12:41; Ezr 9:6; Yak 5:4“Nenda katika mji mkubwa wa Ninawi ukahubiri juu yake, kwa sababu uovu wake umekuja juu mbele zangu.”

1:3 Za 139:7; Yos 19:46; Mdo 9:36-43; Mwa 4:16; 10:4; Kut 4:13; Isa 23:1; Yer 20:9Lakini Yona alimkimbia Bwana na kuelekea Tarshishi. Alishuka mpaka Yafa, ambapo alikuta meli iliyokuwa imepangwa kuelekea bandari ile. Baada ya kulipa nauli, akapanda melini na kuelekea Tarshishi ili kumkimbia Bwana. 1:4 Za 107:23-26Ndipo Bwana akatuma upepo mkali baharini, nayo dhoruba kali sana ikavuma hata meli ikawa hatarini kuvunjika. 1:5 Mdo 27:18-19Mabaharia wote waliogopa na kila mmoja akamlilia mungu wake mwenyewe. Nao wakatupa mizigo baharini ili meli ipungue uzito.

Lakini Yona alikuwa ameteremkia chumba cha ndani ya meli, mahali ambapo alilala na kupatwa na usingizi mzito. 1:6 Yon 3:8; Mt 8:25; Za 78:34; 107:28Nahodha akamwendea na kusema, “Wewe unawezaje kulala? Amka ukamwite mungu wako! Huenda akatuangalia, tusiangamie.”

1:7 Yos 7:10-18; Hes 32:23; Mit 16:33; Mdo 1:26; 1Sam 10:20; 14:43Kisha mabaharia wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tupige kura tumtafute anayehusika na maafa haya.” Wakapiga kura, kura ikamwangukia Yona.

1:8 Yos 7:19Kwa hiyo walimuuliza, “Tuambie, ni nani anayehusika kwa kutuletea tatizo hili lote? Unafanya kazi gani? Umetoka wapi? Nchi yako ni ipi? Wewe ni kutoka taifa lipi?”

1:9 Dan 2:18; Mdo 17:24; Za 146:6; 96:9; Neh 9:6Akajibu, “Mimi ni Mwebrania, nami namwabudu Bwana, Mungu wa Mbinguni, aliyeumba bahari na nchi kavu.”

Hili liliwaogopesha nao wakamuuliza,

“Umefanya nini?” (Walijua alikuwa anamkimbia Bwana, kwa sababu alishawaambia hivyo.)

Bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Kwa hiyo walimuuliza, “Tukutendee nini ili kufanya bahari itulie kwa ajili yetu?”

1:12 Mhu 9:18; 2Sam 24:17; 1Nya 21:17Akawajibu, “Niinueni mnitupe baharini, nayo itakuwa shwari. Ninajua mawimbi haya makubwa yamewatokea kwa ajili ya kosa langu.”

1:13 Mit 21:30Badala yake, wale watu walijitahidi kupiga makasia wawezavyo ili wapate kurudi pwani. Lakini hawakuweza, kwa kuwa bahari ilizidi kuchafuka kuliko mwanzo. 1:14 Kum 21:8; Za 115:3; Dan 4:35Ndipo wakamlilia Bwana, “Ee Bwana, tafadhali usituue kwa kuondoa uhai wa mtu huyu. Usituhesabie hatia kwa kuutoa uhai wa mtu asiyekuwa na hatia, kwa kuwa wewe, Ee Bwana, umefanya kama ilivyokupendeza.” 1:15 Za 107:29; Lk 8:24Kisha walimchukua Yona, wakamtupa baharini nayo bahari iliyokuwa imechafuka ikatulia. 1:16 Mk 4:41; Hes 30:2; Za 66:13-14Katika jambo hili watu wakamwogopa Bwana sana, wakamtolea Bwana dhabihu na kumwekea nadhiri.

1:17 Mt 12:40; 16:4; Lk 11:30; Yn 4:6-7Lakini Bwana akamwandaa nyangumi1:17 Yaani samaki mkubwa sana. kummeza Yona, naye Yona alikuwa ndani ya tumbo la nyangumi kwa siku tatu, usiku na mchana.

Read More of Yona 1

Yona 2:1-10

Maombi Ya Yona Katika Tumbo La Nyangumi

Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwomba Bwana Mungu wake. 2:2 Za 18:6; 120:1; 86:13; Mao 3:55Akasema:

“Katika shida yangu nalimwita Bwana,

naye akanijibu.

Kutoka kina cha kaburi2:2 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. niliomba msaada,

nawe ukasikiliza kilio changu.

2:3 Za 88:6; 42:7; 2Sam 22:5Ulinitupa kwenye kilindi,

ndani kabisa ya moyo wa bahari,

mikondo ya maji ilinizunguka,

mawimbi yako yote na viwimbi

vilipita juu yangu.

2:4 Za 31:22; Yer 7:15; Isa 49:14; 1Fal 8:38, 48Nikasema, ‘Nimefukuziwa

mbali na uso wako,

hata hivyo nitatazama tena

kuelekea Hekalu lako takatifu.’

2:5 Za 69:1-2Maji yaliyonimeza yalinitisha,

kilindi kilinizunguka;

mwani2:5 Mwani hapa maana yake ni magugu yaotayo kwenye sakafu ya kilindi cha bahari. ulijisokota kichwani pangu.

2:6 Ay 28:9; 17:16; 33:18; Za 30:3Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima,

makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele.

Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni,

Ee Bwana Mungu wangu.

2:7 Za 11:4; 18:6; 77:11-12; 34:6; 130:2; Yer 2:13; 2Nya 30:27“Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka,

nilikukumbuka wewe, Bwana,

nayo maombi yangu yalikufikia wewe,

katika Hekalu lako takatifu.

2:8 1Sam 12:21; Yer 10:8; 2Fal 17:15; Za 31:6; Kum 32:21“Wale watu wanaongʼangʼana na sanamu zisizofaa

hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao.

2:9 Hos 14:2; Ebr 13:15; Hes 30:2; Kut 15:2; Za 50:14; 116:14; 66:13-15; 3:8; 42:4Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,

nitakutolea dhabihu.

Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza.

Wokovu watoka kwa Bwana.”

2:10 Yn 1:17; Mt 8:9Basi Bwana akamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.

Read More of Yona 2

Yona 3:1-10

Yona Aenda Ninawi

3:1 Yon 1:1Ndipo neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili: “Ondoka uende katika mji mkubwa wa Ninawi, ukautangazie ujumbe ninaokupa.”

Yona akalitii neno la Bwana naye akaenda Ninawi. Basi Ninawi ulikuwa mji maarufu sana, ilichukua siku tatu kuuzunguka. 3:4 Yer 18:7-103:4 Kum 18:22Siku ya kwanza, Yona aliingia mjini. Akatangaza: “Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.” 3:5 Mt 12:41; 11:21; Dan 9:3; Lk 11:32Watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, watu wote kuanzia mkubwa sana hadi yule mdogo kabisa, wakavaa nguo za gunia.

3:6 Es 4:1-3; Yer 6:26; Mik 1:10; Ay 2:8-13; Eze 27:30-31; Mao 3:29Habari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, aliondoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua majoho yake ya kifalme, akajifunika nguo ya gunia kisha akaketi chini mavumbini. 3:7 2Nya 20:3; Ezr 10:6; Yoe 2:15Ndipo akatoa tangazo katika Ninawi yote:

“Kwa amri ya mfalme na wakuu wake:

“Msiruhusu mtu yeyote au mnyama, makundi ya ngʼombe au wanyama wengine wafugwao, kuonja kitu chochote, msiwaruhusu kula wala kunywa. 3:8 Za 130:1; Yon 1:6; Isa 1:16; Eze 33:11; Dan 4:27; Yer 25:5; 7:3; Ay 16:17Bali wanadamu na wanyama wafunikwe kwa nguo za gunia. Kila mmoja afanye hima kumwomba Mungu. Waziache njia zao mbaya na udhalimu ulio mikononi mwao. 3:9 2Sam 12:22; Yer 18:8; Yoe 2:14; Za 85:3Ni nani ajuaye? Huenda Mungu akaghairi kwa huruma yake akaacha hasira yake kali ili tusiangamie.”

3:10 Amo 7:6; Yer 18:8; Kut 32:14Mungu alipoona walivyofanya na jinsi walivyogeuka kutoka njia zao mbaya, akawa na huruma wala hakuleta maangamizi juu yao kama alivyokuwa ameonya.

Read More of Yona 3

Yona 4:1-11

Hasira Ya Yona Kwa Ajili Ya Huruma Ya Bwana.

4:1 Mt 20:11; 20:15; Lk 15:28Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika. 4:2 Yer 20:7-8; Kum 4:31; Za 103:8; Kut 34:6; 22:27; Hes 14:18; Yoe 2:13Akamwomba Bwana, “Ee Bwana, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharikisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa. 4:3 Hes 11:15; Ay 7:15; Yer 8:3; 1Fal 19:4Sasa, Ee Bwana, niondolee uhai wangu, kwa kuwa ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”

4:4 Mwa 4:6; Mt 20:11-15Lakini Bwana akamjibu, “Je unayo haki yoyote kukasirika?”

Yona akatoka nje akaketi mahali upande wa mashariki wa mji. Hapo akajitengenezea kibanda, akaketi kwenye kivuli chake na kungojea ni nini kitakachotokea katika mji. 4:6 Yon 1:17Ndipo Bwana, Mungu akaweka tayari mzabibu na kuufanya uote, kumpa Yona kivuli kilichomfunika kichwa ili kuondoa taabu yake, naye Yona akafurahi sana kwa ajili ya ule mzabibu. 4:7 Yoe 1:12Lakini kesho yake asubuhi na mapema Mungu akaamuru buu, autafune mzabibu huo nao ukanyauka. 4:8 Za 121:6; 1Fal 19:4Wakati jua lilipochomoza, Mungu akautuma upepo wa hari wa mashariki, nalo jua likawaka juu ya kichwa cha Yona mpaka akazimia. Akatamani kufa, naye akasema, “Ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”

Lakini Mungu alimwambia Yona, “Je, unayo haki kukasirika kuhusu mzabibu huo?”

Akasema, “Ndiyo, ninayo haki. Nimekasirika kiasi cha kufa.”

Lakini Bwana akamwambia, “Wewe unakasirika kwa ajili ya mzabibu huu, nawe hukuusababisha kuota wala kuutunza. Uliota usiku mmoja, nao ukafa usiku mmoja. 4:11 Eze 33:11; Kum 1:39; Za 36:6; Yon 1:2; 3:2; 3:1Lakini Ninawi ina zaidi ya watu 120,000 ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto, pamoja na ngʼombe wengi. Je, hainipasi kufikiri juu ya mji ule mkubwa?”

Read More of Yona 4