Yohana 9:35-41, Yohana 10:1-21 NEN

Yohana 9:35-41

Upofu Wa Kiroho

9:35 Mt 14:33; 16:16; Mk 1:1; 1Yn 5:13Yesu aliposikia kuwa wamemfukuzia nje yule mtu aliyemfumbua macho, alimkuta akamuuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?”

9:36 Rum 10:14Yule mtu akamjibu, “Yeye ni nani, Bwana? Niambie ili nipate kumwamini.”

9:37 Yn 4:26Yesu akamjibu, “Umekwisha kumwona, naye anayezungumza nawe, ndiye.”

9:38 Mt 28:9Yule mtu akasema, “Bwana, naamini.” Naye akamwabudu.

9:39 Yn 5:22; 3:19; 12:47; Lk 4:18; Mt 13:13Yesu akasema, “Nimekuja ulimwenguni humu kwa ajili ya kuhukumu, ili wale walio vipofu wapate kuona, nao wale wanaoona, wawe vipofu.”

9:40 Rum 2:19Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa karibu naye wakamsikia na kumwambia, “Je, kweli sisi ni vipofu?”

9:41 Yn 15:22-24Yesu akawajibu, “Kama mngekuwa vipofu kweli, msingekuwa na hatia ya dhambi, lakini kwa kuwa mnasema, ‘Tunaona,’ basi mna hatia.

Read More of Yohana 9

Yohana 10:1-21

Mchungaji Mwema

10:1 Yn 10:8, 10“Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, ni mwizi na mnyangʼanyi. 10:2 Mk 6:34; Yn 10:11, 14Yeye anayeingia kwa kupitia kwenye lango ndiye mchungaji wa kondoo. 10:3 Yn 10:4, 5, 14Mlinzi humfungulia lango na kondoo huisikia sauti yake. Huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa nje ya zizi. 10:4 Yn 10:3Akiisha kuwatoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaijua sauti yake. 10:5 Yn 10:27Lakini kondoo hawatamfuata mgeni bali watamkimbia, kwa sababu hawaijui sauti ya mgeni.” 10:6 Yn 16:25; 16:25Yesu alitumia mfano huu, lakini wao hawakuelewa hayo aliyokuwa akiwaambia.

10:7 Za 118:20; Yn 14:6; Mt 7:13; 14Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Amin, amin nawaambia, mimi ndimi lango la kondoo. 10:8 Yer 23:1-2; Eze 34:2Wote walionitangulia ni wevi na wanyangʼanyi, lakini kondoo hawakuwasikia. 10:9 Za 118:20; Yn 14:6; 1Kor 3:15Mimi ndimi lango, yeyote anayeingia zizini kwa kupitia kwangu ataokoka, ataingia na kutoka, naye atapata malisho. 10:10 Yn 1:4; 3:15, 16; 5:40; 20:31; Za 65:11; Rum 5:17Mwizi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. Mimi nimekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele.

10:11 Za 23:1; Mt 2:6; Yn 15:13; 1Yn 3:16“Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. 10:12 Zek 11:16-17Mtu wa kuajiriwa sio mchungaji mwenye kondoo. Amwonapo mbwa mwitu akija, yeye hukimbia na kuwaacha kondoo. Naye mbwa mwitu hulishambulia kundi na kulitawanya. Yeye hukimbia kwa sababu ameajiriwa wala hawajali kondoo.

10:14 Kut 33:12; 2Tim 2:19“Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu nao kondoo wangu wananijua. 10:15 Mt 11:27; Yn 15:16Kama vile Baba anavyonijua mimi, nami ninavyomjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 10:16 Isa 56:8; Mdo 10:34-35; Yn 17:20-21; Efe 2:11-19; Eze 34:23; 1Pet 2:25Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili, inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu, hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja. 10:17 Isa 53:7, 8, 12; Ebr 2:9Baba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena. 10:18 Mt 26:53; Flp 2:8; Ebr 5:8Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.”

10:19 Yn 6:52Kwa maneno haya Wayahudi waligawanyika. 10:20 Mk 3:22; Yn 7:20; 2Fal 9:11Wengi wao wakasema, “Huyu amepagawa na pepo mchafu, naye amechanganyikiwa.”

10:21 Mt 4:24; Kut 4:11; Yn 9:32-33Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mtu aliyepagawa na pepo mchafu. Je, pepo mchafu aweza kufungua macho ya kipofu?”

Read More of Yohana 10