Yohana 8:31-59 NEN

Yohana 8:31-59

Wanafunzi Wa Kweli

8:31 Yn 15:7; 2Yn 9Kisha Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli. 8:32 Gal 5:1, 13; Yak 2:12Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.”

8:33 Mk 3:9; Lk 3:8Wao wakamjibu, “Sisi tu wazao wa Abrahamu, nasi hatujawa watumwa wa mtu yeyote. Wawezaje kusema kwamba tutawekwa huru?”

8:34 Rum 6:16; 2Pet 2:19Yesu akajibu, “Amin, amin nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 8:35 Gal 4:30Mtumwa hakai nyumbani anakotumika siku zote, lakini mwana hukaa nyumbani daima. 8:36 Rum 8:2; Gal 5:1Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli. 8:37 Yn 7:19; 8:40Ninajua ya kuwa ninyi ni wazao wa Abrahamu, lakini mnatafuta wasaa wa kuniua kwa sababu ndani yenu hamna nafasi ya neno langu. 8:38 Yn 5:19, 30; 14:10, 24Ninasema yale niliyoyaona mbele za Baba yangu, nanyi inawapa kufanya yale mliyosikia kutoka kwa baba yenu.”

Yesu Na Abrahamu

8:39 Lk 3:8; Gal 3:7Wakajibu, “Baba yetu ni Abrahamu.”

Yesu akawaambia, “Kama mngekuwa wazao wa Abrahamu mngefanya mambo yale aliyofanya Abrahamu. 8:40 Yn 8:37; 8:26Lakini sasa ninyi mnatafuta kuniua, mtu ambaye nimewaambia kweli ile niliyosikia kutoka kwa Mungu, Abrahamu hakufanya jambo la namna hii. 8:41 Isa 63:16; 64:8; Mal 1:6Ninyi mnafanya mambo afanyayo baba yenu.”

Wakamjibu, “Sisi hatukuzaliwa kwa uzinzi. Tunaye Baba mmoja, Mungu pekee.”

8:42 1Yn 5:1; Yn 16:27; 7:28; 3:17Yesu akawaambia, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa maana nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, ila yeye alinituma. 8:43 Yn 7:17Kwa nini hamwelewi ninayowaambia? Ni kwa sababu hamwezi kusikia nisemacho. 8:44 1Yn 3:8; 2Nya 18:21; Za 12:2Ninyi ni watoto wa baba yenu ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo. 8:45 Yn 18:37Lakini kwa sababu nimewaambia kweli hamkuniamini! 8:46 2Kor 5:21; 1Pet 2:22Je, kuna yeyote miongoni mwenu awezaye kunithibitisha kuwa mwenye dhambi? Kama nawaambia yaliyo kweli, mbona hamniamini? 8:47 Yn 18:37; 1Yn 4:6Yeye atokaye kwa Mungu husikia kile Mungu asemacho. Sababu ya ninyi kutosikia ni kwa kuwa hamtokani na Mungu.”

Maelezo Ya Yesu Kuhusu Yeye Mwenyewe

8:48 Mt 10:5; Mk 3:22; Yn 7:20Wayahudi wakamjibu Yesu, “Je, hatuko sahihi tunaposema ya kwamba wewe ni Msamaria na ya kwamba una pepo mchafu?”

Yesu akawajibu, “Mimi sina pepo mchafu, bali ninamheshimu Baba yangu, nanyi mnanidharau. 8:50 Yn 7:20; 8:54; 10:20Lakini mimi sitafuti utukufu wangu mwenyewe, bali yuko anayetaka kunitukuza, naye ndiye mwamuzi. 8:51 Yn 11:26Amin, amin nawaambia, mtu yeyote akilitii neno langu hataona mauti milele.”

8:52 Zek 1:5; Ebr 11:13Ndipo Wayahudi wakamwambia, “Sasa tumejua kwamba una pepo mchafu. Ikiwa Abrahamu alikufa na vivyo hivyo manabii, nawe unasema ‘Mtu akitii neno langu hatakufa milele.’ 8:53 Yn 4:12Je, wewe ni mkuu kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa na manabii ambao nao pia walikufa? Hivi wewe unajifanya kuwa nani?”

8:54 Yn 16:14; 17:1-5Yesu akawajibu, “Kama nikijitukuza utukufu wangu hauna maana. Baba yangu, huyo ambaye ninyi mnadai kuwa ni Mungu wenu, ndiye anitukuzaye mimi. 8:55 Yn 7:28-29; 15:10Ingawa hamkumjua, mimi ninamjua. Kama ningesema simjui, ningekuwa mwongo kama ninyi, lakini mimi ninamjua na ninalitii neno lake. 8:56 Mwa 18:18; Mt 13:17; Ebr 11:13Baba yenu Abrahamu alishangilia kwamba angaliiona siku yangu, naye akaiona na akafurahi.”

Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza hata miaka hamsini, wewe wasema umemwona Abrahamu?”

8:58 Yn 1:2; 17:5, 24; Kut 3:14; 6:3Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, kabla Abrahamu hajakuwako, ‘Mimi niko.’ ” 8:59 1Sam 30:6; Yn 11:8; 12:36Ndipo wakaokota mawe ili kumpiga, lakini Yesu akajificha, naye akatoka Hekaluni.

Read More of Yohana 8