Yohana 7:14-44 NEN

Yohana 7:14-44

Yesu Afundisha Kwenye Sikukuu

7:14 Mt 26:55Ilipokaribia katikati ya Sikukuu, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha. 7:15 Mdo 26:24; Mt 13:54Wayahudi wakastaajabia mafundisho yake wakasema, “Mtu huyu amepataje kujua mambo haya bila kufundishwa?”

7:16 Yn 3:11; 14:24Ndipo Yesu akawajibu, “Mafundisho yangu si yangu mwenyewe, bali yanatoka kwake yeye aliyenituma. 7:17 Za 25:14; Yn 8:23Mtu yeyote akipenda kufanya mapenzi ya Mungu, atajua kama mafundisho yangu yanatoka kwa Mungu au ninasema kwa ajili yangu mwenyewe. 7:18 Yn 5:41; 8:50-54Wale wanenao kwa ajili yao wenyewe hufanya hivyo kwa kutaka utukufu wao wenyewe. Lakini yeye atafutaye utukufu wa yule aliyemtuma ni wa kweli, wala hakuna uongo ndani yake. 7:19 Kum 32:46; Mt 12:14Je, Mose hakuwapa ninyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja wenu anayeishika hiyo sheria. Kwa nini mnataka kuniua?”

7:20 Mk 3:22; Yn 10:20Ule umati wa watu ukamjibu, “Wewe una pepo mchafu! Ni nani anayetaka kukuua?”

7:21 Yn 5:16Yesu akawajibu, “Nimefanya muujiza mmoja na nyote mkastaajabu. 7:22 Law 12:3; Mwa 17:10-14Lakini kwa kuwa Mose aliwaamuru tohara (ingawa kwa kweli haikutoka kwa Mose bali kwa baba zenu wakuu), mnamtahiri mtoto hata siku ya Sabato. 7:23 Yn 5:8Ikiwa mtoto aweza kutahiriwa siku ya Sabato kusudi sheria ya Mose isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia kwa kumponya mtu mwili wake wote siku ya Sabato? 7:24 1Sam 16:7; 2Nya 10:7; Yn 8:15Acheni kuhukumu mambo kwa jinsi mnavyoona tu, bali hukumuni kwa haki.”

Je, Yesu Ndiye Kristo?

7:25 Yn 7:19Ndipo baadhi ya watu wa Yerusalemu wakawa wanasema, “Tazameni, huyu si yule mtu wanayetaka kumuua? 7:26 Yn 7:48; 4:29Mbona yuko hapa anazungumza hadharani na wala hawamwambii neno lolote? Je, inawezekana viongozi wanafahamu kuwa huyu ndiye Kristo?7:26 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. 7:27 Mt 13:55; Lk 4:22Tunafahamu huyu mtu anakotoka, lakini Kristo atakapokuja, hakuna yeyote atakayejua atokako.”

7:28 Yn 8:14, 26, 42Ndipo Yesu, akaendelea kufundisha Hekaluni, akisema, “Ninyi mnanifahamu na kujua nitokako. Mimi sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, bali yeye aliyenituma ni wa kweli na ninyi hammjui. 7:29 Mt 11:27Mimi namjua kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye alinituma.”

7:30 Yn 10:39Ndipo wakatafuta kumkamata, lakini hakuna mtu yeyote aliyethubutu kumshika kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijawadia. 7:31 Yn 11:45; 12:11, 42; 2:11Nao watu wengi wakamwamini, wakasema, “Je, Kristo atakapokuja, atafanya miujiza mikuu zaidi kuliko aliyoifanya mtu huyu?”

Walinzi Wanatumwa Kumkamata Yesu

Mafarisayo wakasikia watu wakinongʼona mambo kama hayo kuhusu Yesu, ndipo wao pamoja na viongozi wa makuhani wakatuma walinzi wa Hekalu waende kumkamata.

7:33 Yn 16:5, 10, 17, 28Yesu akasema, “Mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo, kisha nitarudi kwake yeye aliyenituma. 7:34 Yn 8:21; 13:33Mtanitafuta lakini hamtaniona, nami niliko ninyi hamwezi kuja.”

7:35 Yak 1:1; Mdo 17:4; 1Pet 1:1Wayahudi wakaulizana wao kwa wao, “Huyu mtu anataka kwenda wapi ambako hatuwezi kumfuata? Je, anataka kwenda kwa Wayunani ambako baadhi ya watu wetu wametawanyikia, akawafundishe Wayunani? 7:36 Yn 7:34Yeye ana maana gani anaposema, ‘Mtanitafuta lakini hamtaniona,’ na, ‘nami niliko ninyi hamwezi kuja’?”

Mito Ya Maji Ya Uzima

7:37 Law 23:36; Isa 55:1; Ufu 22:17Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Yesu akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu yeyote anaona kiu na aje kwangu anywe. 7:38 Isa 58:1; Yn 4:10Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yasemavyo, vijito vya maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.” 7:39 Yoe 2:28; Mdo 2:17, 33; Yn 20:22; 12:23; 13:31-32Yesu aliposema haya alimaanisha Roho Mtakatifu ambaye wote waliomwamini wangempokea, kwani mpaka wakati huo, Roho alikuwa hajatolewa, kwa kuwa Yesu alikuwa bado hajatukuzwa.

Mgawanyiko Miongoni Mwa Watu

7:40 Mt 2:11; Yn 1:21Waliposikia maneno hayo, baadhi ya watu miongoni mwa ule umati wakasema, “Hakika huyu ndiye yule Nabii.”

7:41 Yn 7:52; 1:21Wengine wakasema, “Huyu ndiye Kristo!”

Lakini wengine wakauliza, “Je, Kristo kwao ni Galilaya? 7:42 Mt 1:1; Mik 5:2; Mt 2:5-6Je, Maandiko hayasemi kwamba Kristo atakuja kutoka jamaa ya Daudi na kutoka Bethlehemu, mji alioishi Daudi?” 7:43 Yn 9:16; 10:9Kwa hiyo watu wakagawanyika kwa ajili ya Yesu. 7:44 Yn 7:30Baadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa.

Read More of Yohana 7