Yohana 6:60-71, Yohana 7:1-13 NEN

Yohana 6:60-71

Wafuasi Wengi Wamwacha Yesu

6:60 Yn 6:66; 6:52Wengi wa wafuasi wake waliposikia jambo hili wakasema, “Mafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?”

6:61 Mt 13:57Yesu alipojua kwamba wafuasi wake wananungʼunika kuhusu mafundisho yake, akawaambia, “Je, jambo hili limewaudhi? 6:62 Mk 16:19; Yn 17:5Ingekuwaje basi kama mngemwona Mwana wa Adamu akipaa kwenda zake huko alipokuwa kwanza? 6:63 2Kor 3:6Roho ndiye atiaye uzima, mwili haufai kitu. Maneno haya niliyowaambia ni Roho tena ni uzima. 6:64 Yn 2:24-25Lakini baadhi yenu hamwamini.” Kwa maana Yesu alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini miongoni mwao na yule ambaye angemsaliti. 6:65 Mt 13:11Akaendelea kusema, “Hii ndiyo sababu niliwaambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.”

6:66 Yn 6:60Tangu wakati huo wafuasi wake wengi wakarejea nyuma wakaacha kumfuata.

6:67 Mt 10:2Hivyo Yesu akawauliza wale wanafunzi wake kumi na wawili, “Je, ninyi pia mnataka kuondoka?”

6:68 Mt 16:16Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. 6:69 Mk 1:24; Lk 9:20Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu.”

6:70 Yn 15:16-19; 13:27; 17:12Ndipo Yesu akajibu, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Lakini mmoja wenu ni ibilisi.” 6:71 Mt 26:14; 10:4(Hapa alikuwa anasema juu ya Yuda, mwana wa Simoni Iskariote. Ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili, ndiye ambaye baadaye angemsaliti Yesu.)

Read More of Yohana 6

Yohana 7:1-13

Kutokuamini Kwa Ndugu Zake Yesu

7:1 Yn 1:19; 5:18; Mt 12:18Baada ya mambo haya, Yesu alikwenda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Uyahudi kwa sababu Wayahudi huko walitaka kumuua. 7:2 Law 23:34; Kum 16:16Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. 7:3 Mt 12:46Hivyo ndugu zake Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende Uyahudi ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya. Mtu anayetaka kujulikana hafanyi mambo yake kwa siri. Kama unafanya mambo haya, jionyeshe kwa ulimwengu.” 7:5 Za 69:8; Mk 3:21Hata ndugu zake mwenyewe hawakumwamini.

7:6 Mt 26:18Yesu akawaambia, “Wakati wangu bado haujawadia, lakini wakati wenu upo siku zote. 7:7 Yn 3:19-20; 15:18-19Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini unanichukia mimi kwa sababu ninawashuhudia kwamba matendo yao ni maovu. 7:8 Yn 7:6; Mt 26:18; Yn 8:30Ninyi nendeni kwenye Sikukuu, lakini mimi sitahudhuria Sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.” Akiisha kusema hayo, akabaki Galilaya.

Yesu Kwenye Sikukuu Ya Vibanda

Lakini ndugu zake walipokwisha kuondoka kwenda kwenye Sikukuu, yeye pia alikwenda lakini kwa siri. 7:11 Yn 11:56Wayahudi walikuwa wakimtafuta huko kwenye Sikukuu na kuulizana, “Yuko wapi huyu mtu?”

7:12 Yn 9:16; 10:19; Mt 21:46; Lk 7:16; Yn 6:14Kulikuwa na minongʼono iliyoenea kumhusu Yesu katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.”

Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.” 7:13 Yn 19:38; 20:19Lakini hakuna mtu yeyote aliyemsema waziwazi kumhusu kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi.

Read More of Yohana 7