Yohana 6:25-59 NEN

Yohana 6:25-59

Yesu Ni Mkate Wa Uzima

6:25 Mt 23:7Walipomkuta Yesu ngʼambo ya bahari wakamuuliza, “Rabi, umefika lini huku?”

6:26 Yn 2:11Yesu akawajibu, “Amin, amin nawaambia, ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba. 6:27 Mt 25:46; Yn 4:14; Mt 8:20; 2Tim 2:19; Ufu 7:3Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba amemtia muhuri.”

Ndipo wakamuuliza, “Tufanye nini ili tupate kuitenda kazi ya Mungu?”

6:29 1Yn 3:23; 3:17Yesu akawajibu, “Kazi ya Mungu ndiyo hii: Mwaminini yeye aliyetumwa naye.”

6:30 Yn 2:11; Mt 12:38Hivyo wakamuuliza, “Utafanya ishara gani ya muujiza, ili tuione tukuamini? Utafanya jambo gani? 6:31 Hes 11:7-9; Neh 9:15; Za 105:40Baba zetu walikula mana jangwani, kama ilivyoandikwa, ‘Aliwapa mikate kutoka mbinguni ili wale.’ ”

6:32 Yn 6:49Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, si Mose aliyewapa mikate kutoka mbinguni, bali Baba yangu ndiye anawapa mkate wa kweli kutoka mbinguni. 6:33 Yn 3:13, 31Kwa maana mkate wa Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.”

6:34 Yn 4:15Wakamwambia, “Bwana, kuanzia sasa tupatie huo mkate siku zote.”

6:35 Yn 4:14; 6:48; 7:37Yesu akawaambia, “Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu, hataona njaa kamwe na yeye aniaminiye, hataona kiu kamwe. 6:36 Yn 6:26, 29Lakini kama nilivyowaambia, mmeniona lakini bado hamwamini. 6:37 Yn 17:2-6, 9, 24Wale wote anipao Baba watakuja kwangu na yeyote ajaye kwangu, sitamfukuzia nje kamwe. 6:38 Yn 3:17; 4:34Kwa kuwa nimeshuka kutoka mbinguni si ili kufanya mapenzi yangu, bali mapenzi yake yeye aliyenituma. 6:39 Isa 27:3; Yn 18:9Haya ndiyo mapenzi yake yeye aliyenituma, kwamba, nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali niwafufue siku ya mwisho. 6:40 Mt 25:26Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni kwamba kila mmoja amtazamaye, Mwana na kumwamini awe na uzima wa milele, nami nitawafufua siku ya mwisho.”

Wayahudi wakaanza kunungʼunika kwa kuwa alisema, “Mimi ndimi mkate ulioshuka kutoka mbinguni.” 6:42 Lk 4:22; Yn 7:27, 28Wakasema, “Huyu si Yesu, mwana wa Yosefu, ambaye baba yake na mama yake tunawajua? Anawezaje basi sasa kusema, ‘Nimeshuka kutoka mbinguni’?”

Hivyo Yesu akawaambia, “Acheni kunungʼunikiana ninyi kwa ninyi. Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama asipovutwa na Baba aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho. 6:45 Isa 54:13; 1Kor 2:13Imeandikwa katika Manabii, ‘Wote watafundishwa na Mungu.’ Yeyote amsikilizaye Baba na kujifunza kutoka kwake, huyo huja kwangu. 6:46 Yn 1:18; 7:29Hakuna mtu yeyote aliyemwona Baba isipokuwa yeye atokaye kwa Mungu, yeye ndiye peke yake aliyemwona Baba. 6:47 Mt 25:46Amin, amin nawaambia, yeye anayeamini anao uzima wa milele. 6:48 Yn 6:35, 51Mimi ni mkate wa uzima. 6:49 Yn 6:3, 58Baba zenu walikula mana jangwani, lakini wakafa. 6:50 Yn 6:33Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni, ambao mtu yeyote akiula, hatakufa. 6:51 Ebr 10:10Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu yeyote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”

6:52 Yn 9:16; 10:19Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?”

6:53 Mt 26:26; 8:20; 26:28Hivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 6:54 Yn 6:39Mtu yeyote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 6:56 1Yn 2:24; 3:24Yeyote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. 6:57 Yn 3:17Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu. 6:58 Yn 3:36; 5:24Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.” Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sinagogi huko Kapernaumu.

Read More of Yohana 6