Yohana 5:31-47 NEN

Yohana 5:31-47

5:31 Yn 8:14“Kama ningejishuhudia mimi mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli. 5:32 Yn 5:37; 8:18Lakini yuko mwingine anishuhudiaye na ninajua kwamba ushuhuda wake ni wa kweli.

5:33 Yn 1:7“Mlituma wajumbe kwa Yohana, naye akashuhudia juu ya kweli. 5:34 1Yn 5:9Si kwamba naukubali ushuhuda wa mwanadamu, la, bali ninalitaja hili kusudi ninyi mpate kuokolewa. 5:35 Dan 12:3Yohana alikuwa taa iliyowaka na kutoa nuru, nanyi kwa muda mlichagua kuifurahia nuru yake.

5:36 1Yn 5:9; Yn 14:11; 15:24; 3:17; 10:25“Lakini ninao ushuhuda mkuu zaidi kuliko wa Yohana. Kazi zile nizifanyazo, zinashuhudia juu yangu, zile ambazo Baba amenituma nizikamilishe, naam, ishara hizi ninazofanya, zinashuhudia kuwa Baba ndiye alinituma. 5:37 Yn 8:18; Kum 4:12; 1Tim 1:17Naye Baba mwenyewe ameshuhudia juu yangu. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuona umbo lake, 5:38 1Yn 1:10; 2:4; Isa 26:10; Yn 3:17wala hamna neno lake ndani yenu, kwa sababu hamkumwamini yeye aliyetumwa naye. 5:39 Rum 2:17-18; Lk 24:27, 44; Mdo 13:27Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi. 5:40 Yn 6:44Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima.

5:41 Yn 5:44; 5:34; 1The 2:6“Mimi sitafuti kutukuzwa na wanadamu. Lakini ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu. Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei, lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea. 5:44 Rum 2:29Ninyi mwawezaje kuamini ikiwa mnapeana utukufu ninyi kwa ninyi, lakini hamna bidii kupata utukufu utokao kwa Mungu?

5:45 Yn 9:28; Rum 2:17“Lakini msidhani kuwa mimi nitawashtaki mbele za Baba, mshtaki wenu ni Mose, ambaye mmemwekea tumaini lenu. 5:46 Mwa 3:15; Lk 24:27, 44Kama mngelimwamini Mose, mngeliniamini na mimi kwa maana aliandika habari zangu. 5:47 Lk 16:29-31Lakini ikiwa hamwamini aliyoandika Mose, mtaaminije ninayoyasema?”

Read More of Yohana 5