Yohana 4:27-42 NEN

Yohana 4:27-42

4:27 Yn 4:8Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?”

Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaambia watu, 4:29 Mt 12:23; Yn 7:26, 31“Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Kristo?”4:29 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu.

4:31 Mt 23:7Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Rabi, kula angalau chochote.”

4:32 Ay 23:12; Mt 4:4Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.”

Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?” 4:34 Mt 26:39; Yn 17:4; 19:30Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake. 4:35 Mt 9:37; Lk 10:2Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune?’ Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa! 4:36 Rum 1:13; Mt 25:46Mvunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele. Ili yeye apandaye na yeye avunaye wafurahi pamoja. 4:37 Ay 31:8; Mik 6:15Hivyo kule kusema, ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa. Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.”

Wasamaria Wengi Waamini

4:39 Yn 4:29Wasamaria wengi katika mji ule wakamwamini Yesu kwa sababu ya ushuhuda wa yule mwanamke alipowaambia kwamba, “Ameniambia kila kitu nilichotenda.” Hivyo wale Wasamaria walipomjia, wakamsihi akae kwao. Naye akakaa huko siku mbili. Kwa sababu ya neno lake, watu wengi wakaamini.

4:42 Lk 2:11; 1Yn 4:14Wakamwambia yule mwanamke, “Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu, bali kwa kuwa tumemsikia sisi wenyewe. Tumejua hakika kweli ya kwamba huyu ndiye Kristo, Mwokozi wa ulimwengu.”

Read More of Yohana 4