Yohana 3:22-36 NEN

Yohana 3:22-36

Ushuhuda Wa Yohana Mbatizaji Kuhusu Yesu

3:22 Yn 4:2Baada ya haya, Yesu na wanafunzi wake walikwenda katika nchi ya Uyahudi, nao wakakaa huko kwa muda na kubatiza. 3:23 1Sam 9:4; Mt 3:6Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni karibu na Salimu kwa sababu huko kulikuwa na maji tele. Watu wazima wakamjia huko ili kubatizwa. 3:24 Mt 4:12; 14:3(Hii ilikuwa kabla Yohana hajatiwa gerezani). 3:25 Yn 2:6Mashindano yakazuka kati ya baadhi ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja kuhusu suala la desturi ya kunawa kwa utakaso. 3:26 Mt 23:7; Yn 1:7Wakamwendea Yohana wakamwambia, “Rabi, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ngʼambo ya Mto Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!”

3:27 Ebr 5:4; 1Kor 4:7; Yak 1:17Yohana akawajibu, “Hakuna mtu yeyote awezaye kupata kitu chochote isipokuwa kile tu alichopewa kutoka mbinguni. 3:28 Yn 1:20-23; 3:9; Mt 9:15; Flp 2:2; 2Yn 12Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema, ‘Mimi si Kristo,3:28 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. ila nimetumwa nimtangulie.’ 3:29 Mt 22:2; 2Kor 11:2; Efe 5:25, 27; Ufu 21:9; Wim 5:1Bibi arusi ni wa bwana arusi. Lakini rafiki yake bwana arusi anayesimama karibu naye na kusikiliza kutoka kwake, hufurahi sana aisikiapo sauti ya bwana arusi. Kwa sababu hii furaha yangu imekamilika. 3:30 2Sam 3:1Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi nizidi kuwa mdogo.”

Yeye Aliyetoka Mbinguni

3:31 Yn 8:23; 1Yn 4:5“Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya yote. 3:32 Yn 8:26; 15:15Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna yeyote anayekubali ushuhuda wake. 3:33 Rum 3:4; 1Yn 5:10Lakini yeyote anayekubali huo ushuhuda anathibitisha kwamba, Mungu ni kweli. 3:34 Isa 42:1; Mt 12:18Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humtoa Roho pasipo kipimo. 3:35 Mt 28:18; Yn 17:2Baba anampenda Mwana, naye ametia vitu vyote mikononi mwake. 3:36 Yn 5:24; 6:47Yeyote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.”

Read More of Yohana 3