Yohana 20:10-31 NEN

Yohana 20:10-31

Kisha hao wanafunzi wakaondoka wakarudi nyumbani kwao.

Yesu Anamtokea Maria Magdalene

(Mathayo 28:9-10; Marko 16:9-11)

20:11 Yn 20:5Lakini Maria Magdalene akasimama nje ya kaburi akilia. Alipokuwa akilia, akainama, kuchungulia mle kaburini, 20:12 Mk 16:5; Mdo 10:30naye akaona malaika wawili wamevaa mavazi meupe, wameketi pale mwili wa Yesu ulipokuwa umelazwa, mmoja upande wa kichwani na mwingine upande wa miguuni.

20:13 Yn 20:2, 15Wakamuuliza Maria, “Mwanamke, mbona unalia?”

Akawaambia, “Nalia kwa kuwa wamemchukua Bwana wangu na sijui walikomweka.” 20:14 Mt 28:9; Mk 16:9; Lk 24:16; Yn 21:14Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Yesu amesimama, lakini hakumtambua.

20:15 Yn 20:13Yesu akamwambia, “Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?”

Maria akidhani ya kuwa aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akamwambia, “Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nionyeshe ulikomweka, nami nitamchukua.”

20:16 Yn 5:2; Mt 23:7Yesu akamwita, “Maria!”

Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, “Rabboni!” (maana yake Mwalimu).

20:17 Mt 28:10; Yn 7:33; Mt 28:10Yesu akamwambia, “Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ ”

20:18 Yn 20:1; Lk 24:10, 22, 23Kwa hiyo Maria Magdalene akaenda kuwatangazia wanafunzi wa Yesu, akisema, “Nimemwona Bwana!” Naye akawaambia kwamba Yesu alikuwa amemweleza mambo hayo yote.

Yesu Awatokea Wanafunzi Wake

(Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Luka 24:36-49)

Ikawa jioni ya ile siku ya kwanza ya juma, wanafunzi wake walikuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi. Naye Yesu aliwatokea, akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!” 20:20 Lk 24:36-39, 40; Yn 19:34; 16:20, 22; Lk 24:39, 40; Yn 19:34; 16:20Baada ya kusema haya, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi wake wakafurahi sana walipomwona Bwana.

20:21 Yn 20:19; 3:17; Mt 28:19; Yn 17:18Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi! Kama vile Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawatuma ninyi.” 20:22 Mdo 19:2; Gal 3:2; Yn 7:39; Mdo 2:38; 8:15; 17; 19:2; Gal 3:2Naye alipokwisha kusema haya, akawavuvia, akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. 20:23 Mt 16:19; 18:18Mkimwondolea mtu yeyote dhambi zake, zitaondolewa, na yeyote msiyemwondolea dhambi zake, hazitaondolewa.”

Yesu Anamtokea Tomaso

20:24 Yn 11:16Lakini Tomaso, aliyeitwa Didimasi, yaani Pacha, mmoja wa wale kumi na wawili, hakuwa pamoja nao Yesu alipokuja. 20:25 Mk 16:11Hivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana.”

Lakini yeye akawaambia, “Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake, na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini.”

20:26 Yn 14:27; 20:21Baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwa tena pamoja ndani ya nyumba, naye Tomaso alikuwa pamoja nao. Ndipo Yesu akaja milango ikiwa imefungwa na kusimama katikati yao akasema, “Amani iwe nanyi.” 20:27 Yn 20:25; Lk 24:40Kisha akamwambia Tomaso, “Weka kidole chako hapa na uone mikono yangu, nyoosha mkono wako uguse ubavuni mwangu. Usiwe na shaka, bali uamini tu.”

20:28 Yn 1:1; 20:29; 3:15; 1Pet 1:8Tomaso akamwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu!”

20:29 Yn 3:15; 1Pet 1:8Yesu akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.”

Kusudi La Kitabu Hiki

20:30 Yn 21:25; 2:11; 21:25; Mt 4; 3; 25:46Yesu alifanya miujiza mingine mingi mbele za wanafunzi wake, ambayo haikuandikwa katika kitabu hiki. 20:31 Yn 3:15; 19:35; Mt 4:3; 25:46Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo,20:31 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.

Read More of Yohana 20