Yohana 16:5-33, Yohana 17:1-5 NEN

Yohana 16:5-33

Kazi Ya Roho Mtakatifu

16:5 Yn 16:10, 17, 28; 7:33; 13:36; 14:5“Sasa mimi ninakwenda kwake yeye aliyenituma, lakini hakuna hata aniulizaye, ‘Unakwenda wapi?’ 16:6 Yn 6:22; 14:1Kwa sababu nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni. 16:7 Yn 14:16, 26; 15:26Lakini nawaambia kweli, yafaa mimi niondoke, kwa kuwa nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu, lakini nikienda nitamtuma kwenu. 16:8 1Kor 14:24; Ebr 4:12Naye atakapokuja, atauthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. 16:9 Yn 15:22Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi, 16:10 Rum 1:17; 1Pet 3:18kwa habari ya haki, kwa sababu ninakwenda kwa Baba, nanyi hamtaniona tena, 16:11 Yn 12:31kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.

16:12 1Kor 3:2“Bado ninayo mambo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili sasa. 16:13 Yn 14:17; Za 25:5Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonyesha mambo yajayo. Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi. 16:15 Yn 17:10Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu. Ndiyo maana nimesema Roho atachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi.

16:16 Yn 7:33; 16:22; 14:18-24“Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.”

Huzuni Itageuka Kuwa Furaha

16:17 Yn 16:16; 16:5Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona’? Naye ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninakwenda kwa Baba’?” Wakaendelea kuulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Kitambo kidogo’? Hatuelewi hilo analosema.”

Yesu akatambua kuwa walitaka kumuuliza juu ya hilo, hivyo akawaambia, “Je, mnaulizana nina maana gani niliposema, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona’? 16:20 Mk 16:10; Yn 20:20Amin, amin nawaambia, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi. Ninyi mtahuzunika, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 16:21 Mik 4:9; 1The 5:3Mwanamke anapokuwa na utungu wa kuzaa huwa na maumivu kwa sababu saa yake imewadia. Lakini mtoto akiisha kuzaliwa, yule mwanamke husahau maumivu hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto ulimwenguni. 16:22 Isa 60:14; Lk 24:41, 52; Yn 14:1, 27; Mdo 2:46; 13:52; 1Pet 1:8Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi na furaha yenu hakuna awaondoleaye. 16:23 Mt 7:7; Yn 15:16Katika siku hiyo hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin nawaambia, kama mkimwomba Baba jambo lolote kwa jina langu, yeye atawapa. 16:24 Yn 3:29; 15:11Mpaka sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili.

Amani Kwa Wanafunzi

16:25 Yn 10:6“Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Saa yaja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali nitawaeleza waziwazi kuhusu Baba. 16:26 Yn 16:23, 24Siku hiyo mtaomba kwa Jina langu. Wala sitawaambia kwamba nitamwomba Baba kwa ajili yenu, 16:27 Yn 14:21, 23kwa maana Baba mwenyewe anawapenda, kwa sababu mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Mungu. 16:28 Yn 5:10, 17; 13:3Nilitoka kwa Baba na kuja ulimwenguni, sasa naondoka ulimwenguni na kurudi kwa Baba.”

16:29 Yn 16:25Ndipo wanafunzi wake wakasema, “Sasa unazungumza waziwazi, wala si kwa mafumbo. 16:30 1Fal 17:24; Yn 16:27; 13:3; 2:25Sasa tumejua kwamba wewe unajua mambo yote, wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa jambo hili tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.”

Yesu akawajibu, “Je, sasa mnaamini? 16:32 Yn 16:2, 25; Mt 26:31; 26:56; Yn 8:16, 29Saa inakuja, naam, imekwisha kuwadia, mtakapotawanyika kila mmoja kwenda nyumbani kwake na kuniacha peke yangu. Lakini mimi siko peke yangu kwa sababu Baba yu pamoja nami. 16:33 Yn 14:27; 15:18-21; 1Yn 5:4; Ufu 21:7Nimewaambia mambo haya, ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”

Read More of Yohana 16

Yohana 17:1-5

Yesu Ajiombea Mwenyewe

17:1 Yn 11:41; 12:23; 13:31, 32Baada ya Yesu kusema haya, alitazama kuelekea mbinguni akawaombea na kusema:

“Baba, saa imewadia. Umtukuze Mwanao, ili Mwanao apate kukutukuza wewe. 17:2 Dan 7:14; Yn 6:37, 39Kwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa. 17:3 Flp 3:8; Yn 17:8, 18, 21, 23, 25; 3:17Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. 17:4 Yn 13:31; 19:30Nimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye. 17:5 Flp 2:6; Yn 1:2Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ulimwengu haujakuwepo.

Read More of Yohana 17