Yohana 12:37-50, Yohana 13:1-17 NEN

Yohana 12:37-50

Wayahudi Waendelea Kutokuamini

12:37 Yn 2:11Hata baada ya Yesu kufanya miujiza hii yote mbele yao, bado hawakumwamini. 12:38 Isa 53:1; Rum 10:16Hili lilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema:

“Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu,

na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani?”

12:39 Isa 6:9, 10; Mt 13:14, 15Kwa hivyo hawakuamini, kwa sababu Isaya anasema mahali pengine:

12:40 Isa 6:10; Mt 13:13, 15“Amewafanya vipofu,

na kuifanya mioyo yao kuwa migumu,

ili wasiweze kuona kwa macho yao,

wala kuelewa kwa mioyo yao,

wasije wakageuka nami nikawaponya.”

12:41 Isa 6:1-4; Lk 24:27Isaya alisema haya alipoona utukufu wa Yesu na kunena habari zake.

12:42 Yn 7:48; 9:22Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi. 12:43 Yn 5:44; Rum 2:29Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.

Amwaminiye Yesu Hatabaki Gizani

12:44 Mt 10:40; Yn 5:24Yesu akapaza sauti akasema, “Yeyote aniaminiye, haniamini mimi peke yangu, bali yeye aliyenituma. 12:45 Yn 14:9Yeyote anionaye mimi, amemwona yeye aliyenituma. 12:46 Yn 3:19; 8:12Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kwamba kila mtu aniaminiye asibaki gizani.

12:47 Yn 3:17“Mimi simhukumu mtu yeyote anayesikia maneno yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa. 12:48 Yn 5:45Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho. 12:49 Yn 14:31Kwa maana sisemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema. 12:50 Yn 8:26, 28Nami ninajua amri zake huongoza hadi kwenye uzima wa milele. Hivyo lolote nisemalo, ndilo lile Baba aliloniambia niseme.”

Read More of Yohana 12

Yohana 13:1-17

Yesu Awanawisha Wanafunzi Wake Miguu

13:1 Yn 11:55; 12:33; 16:28Ilikuwa mara tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua ya kuwa wakati wake wa kuondoka ulimwenguni ili kurudi kwa Baba umewadia. Alikuwa amewapenda watu wake waliokuwa ulimwenguni, naam, aliwapenda hadi kipimo cha mwisho.

13:2 Lk 22:3Wakati alipokuwa akila chakula cha jioni na wanafunzi wake, ibilisi alikuwa amekwisha kutia ndani ya moyo wa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni, wazo la kumsaliti Yesu. 13:3 Mt 28:18; Yn 8:42; 17:8Yesu akijua ya kwamba Baba ameweka vitu vyote chini ya mamlaka yake na kwamba yeye alitoka kwa Mungu na alikuwa anarudi kwa Mungu, 13:4 Mt 11:29; 20:29; Lk 12:37hivyo aliondoka chakulani, akavua vazi lake la nje, akajifunga kitambaa kiunoni. 13:5 Lk 7:44Kisha akamimina maji kwenye sinia na kuanza kuwanawisha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa kile kitambaa alichokuwa amejifunga kiunoni.

13:6 1Pet 5:5Alipomfikia Simoni Petro, Petro akamwambia, “Bwana, je, wewe utaninawisha mimi miguu?”

13:7 Yn 13:12Yesu akamjibu, “Hivi sasa hutambui lile ninalofanya, lakini baadaye utaelewa.”

13:8 Yn 3:5; 1Kor 6:11; Efe 5:26; Tit 3:5; Ebr 10:22Petro akamwambia, “La, wewe hutaninawisha miguu kamwe.”

Yesu akamjibu, “Kama nisipokunawisha, wewe huna sehemu nami.”

Ndipo Simoni Petro akajibu, “Usininawishe miguu peke yake, Bwana, bali pamoja na mikono na kichwa pia!”

13:10 Yn 15:3Yesu akamjibu, “Mtu aliyekwisha kuoga anahitaji kunawa miguu tu, kwani mwili wake wote ni safi. Ninyi ni safi, ingawa si kila mmoja wenu.” 13:11 Mt 10:4Kwa kuwa yeye alijua ni nani ambaye angemsaliti, ndiyo sababu akasema si kila mmoja aliyekuwa safi.

Alipomaliza kuwanawisha miguu yao, alivaa tena mavazi yake, akarudi alikokuwa ameketi, akawauliza, “Je, mmeelewa nililowafanyia? 13:13 Mt 26:18; Yn 11:28; Mdo 10:36Ninyi mnaniita mimi ‘Mwalimu’ na ‘Bwana,’ hii ni sawa, maana ndivyo nilivyo. 13:14 1Pet 5:5Kwa hiyo, ikiwa mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewanawisha ninyi miguu, pia hamna budi kunawishana miguu ninyi kwa ninyi. 13:15 Mt 11:29; 1Tim 4:12Mimi nimewawekea kielelezo kwamba imewapasa kutenda kama vile nilivyowatendea ninyi. 13:16 Mt 10:24; Lk 6:40Amin, amin nawaambia, mtumishi si mkuu kuliko bwana wake, wala aliyetumwa si mkuu kuliko yule aliyemtuma. 13:17 Lk 11:28; 1:25Sasa kwa kuwa mmejua mambo haya, heri yenu ninyi kama mkiyatenda.

Read More of Yohana 13