Yohana 12:12-26 NEN

Yohana 12:12-26

Kuingia Kwa Yesu Yerusalemu Kwa Ushindi

(Mathayo 21:1-11; Marko 1:1-11; Luka 19:28-40)

12:12 Mt 21:8; Mk 11:8; Lk 19:35, 36Siku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Yesu angekuja Yerusalemu. 12:13 Za 118:25-26; Yn 1:49Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema,

“Hosana!”12:13 Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe.

“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”

“Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!”

12:14 Mt 21:7Yesu akamkuta mwana-punda akampanda, kama ilivyoandikwa,

12:15 Zek 9:9“Usiogope, Ewe binti Sayuni;

tazama, Mfalme wako anakuja,

amepanda mwana-punda!”

12:16 Lk 18:34; Yn 7:39Wanafunzi wake Yesu mwanzoni hawakuelewa mambo haya, lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yameandikwa kwa ajili yake na alitendewa yeye.

12:17 Yn 11:42Wale waliokuwepo wakati Yesu alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu, waliendelea kushuhudia. 12:18 Yn 12:11; 19:37Ni kwa sababu pia walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu ndiyo maana umati wa watu ukaenda kumlaki. 12:19 Yn 11:47, 48Hivyo Mafarisayo walipoona hayo wakaambiana, “Mnaona, hamwezi kufanya lolote. Angalieni, ulimwengu wote unamfuata yeye!”

Yesu Anatabiri Kifo Chake

12:20 Yn 7:35; Mdo 11:20Basi palikuwa Wayunani fulani miongoni mwa wale waliokuwa wamekwenda kuabudu wakati wa Sikukuu. 12:21 Mt 11:21; Yn 1:44Hawa wakamjia Filipo, ambaye alikuwa mwenyeji wa Bethsaida huko Galilaya, wakiwa na ombi. Wakamwambia, “Tungependa kumwona Yesu.” Filipo akaenda akamweleza Andrea, nao wote wawili wakamwambia Yesu.

12:23 Yn 13:32; 17:1Yesu akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa. 12:24 1Kor 15:36Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi. 12:25 Mk 8:35; Lk 14:26Mtu yeyote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata kwa uzima wa milele. 12:26 Flp 1:23Mtu yeyote akinitumikia lazima anifuate, nami mahali nilipo ndipo mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu akinitumikia, Baba yangu atamheshimu.

Read More of Yohana 12