Yohana 11:45-57, Yohana 12:1-11 NEN

Yohana 11:45-57

Shauri La Kumuua Yesu

(Mathayo 26:1-5; Marko 14:1-2; Luka 22:1-2)

11:45 Yn 11:19; 2:23; 14Hivyo Wayahudi wengi waliokuwa wamekuja kumfariji Maria, walipoona yale Yesu aliyoyatenda wakamwamini. Lakini baadhi yao wakaenda kwa Mafarisayo na kuwaambia mambo Yesu aliyoyafanya. 11:47 Yn 2:11Kwa hiyo viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakaita mkutano wa baraza.

Wakaulizana, “Tufanyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi. Kama tukimwacha aendelee hivi, kila mtu atamwamini, nao Warumi watakuja na kupaharibu mahali petu patakatifu na taifa letu.”

11:49 Lk 3:2; Yn 18:14; Mdo 4:6Mmoja wao aliyeitwa Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mkuu mwaka huo, akasema, “Ninyi hamjui kitu chochote! 11:50 Yn 18:14Hamjui kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa lote liangamie?”

11:51 Mwa 50:20; Kut 28:30; Hes 27:21Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama kuhani mkuu mwaka huo, alitabiri kuwa Yesu angelikufa kwa ajili ya taifa la Wayahudi, 11:52 Isa 49:6; Yn 10:16wala si kwa ajili ya taifa hilo pekee, bali pia kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika, ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja. 11:53 Mt 12:14Hivyo tangu siku hiyo wakawa wanafanya mipango ili wamuue Yesu.

11:54 Yn 7:1Kwa hiyo Yesu akawa hatembei hadharani miongoni mwa Wayahudi, bali alijitenga akaenda sehemu iliyo karibu na jangwa kwenye kijiji kiitwacho Efraimu. Akakaa huko na wanafunzi wake.

11:55 Kut 12:13, 23, 27; Mk 14:1; 2Nya 30:17-18Basi Pasaka ya Wayahudi ilipokuwa imekaribia, watu wengi walitoka vijijini wakaenda Yerusalemu kabla ya Pasaka ili wakajitakase. 11:56 Yn 7:11; 17:7Watu wakawa wanamtafuta Yesu, nao waliposimama kwenye eneo la Hekalu waliulizana, Je, mtu huyu hatakuja kamwe kwenye Sikukuu? Viongozi wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kuwa yeyote atakayejua mahali Yesu aliko, lazima atoe taarifa ili wapate kumkamata.

Read More of Yohana 11

Yohana 12:1-11

Maria Ampaka Yesu Mafuta Huko Bethania

(Mathayo 26:6-13; Marko 14:3-9)

12:1 Yn 11:55; Mt 21:17Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alikwenda Bethania mahali ambako Lazaro aliyekuwa amefufuliwa na Yesu alikuwa anaishi. 12:2 Lk 10:38-42Wakaandaa karamu kwa heshima ya Yesu. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Yesu. 12:3 Yn 11:12Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja12:3 Painti moja ni kama nusu lita. yenye manukato ya nardo12:3 Nardo ni aina ya mafuta yaliyokuwa yanatengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri. safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Yesu na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.

12:4 Mt 10:4Ndipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye angemsaliti Yesu, akasema, “Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 30012:5 Dinari 300 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 300. na fedha hizo wakapewa maskini?” 12:6 Yn 13:29Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi, kwani ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.

12:7 Yn 19:40Yesu akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu. 12:8 Kum 15:11Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.”

Shauri La Kumuua Lazaro

12:9 Yn 11:43, 44Umati mkubwa wa Wayahudi walipojua kwamba Yesu alikuwa huko Bethania, walikuja si tu kwa ajili ya Yesu, lakini pia kumwona Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua. 12:10 Lk 16:31Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia, 12:11 Yn 11:45; 12:18kwa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake Wayahudi wengi walikuwa wanamwendea Yesu na kumwamini.

Read More of Yohana 12