Yohana 11:1-44 NEN

Yohana 11:1-44

Kifo Cha Lazaro

11:1 Mt 21:17; Lk 10:38Basi mtu mmoja jina lake Lazaro alikuwa mgonjwa. Yeye alikuwa akiishi Bethania kijiji cha Maria na Martha dada zake. 11:2 Mk 14:3; Lk 7:38Huyu Maria, ambaye Lazaro kaka yake alikuwa mgonjwa, ndiye yule ambaye alimpaka Bwana mafuta na kuifuta miguu yake kwa nywele zake. 11:3 Yn 11:5, 36Hivyo hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Yesu kumwambia, “Bwana, yule umpendaye ni mgonjwa.”

11:4 Yn 11:40Lakini Yesu aliposikia hayo, akasema, “Ugonjwa huu hautaleta mauti bali umetokea ili kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu.” Pamoja na hivyo, ingawa Yesu aliwapenda Martha, Maria na Lazaro ndugu yao, 11:6 Yn 10:40baada ya kusikia kwamba Lazaro ni mgonjwa, aliendelea kukawia huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi.

11:7 Yn 10:40Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Haya, turudi Uyahudi.”

11:8 Mt 23:7; Yn 8:59; 10:31Wanafunzi wake wakamwambia, “Rabi, Wayahudi walikuwa wanataka kukupiga mawe, nawe unataka kurudi huko?”

11:9 Yn 9:4; 12:35Yesu akawajibu, “Si kuna saa kumi na mbili za mchana katika siku moja? Wala watembeao mchana hawawezi kujikwaa kwa maana wanaona nuru ya ulimwengu huu. 11:10 Yn 12:35Lakini wale watembeao usiku hujikwaa kwa sababu hakuna nuru ndani yao.”

11:11 Mt 9:24; Lk 8:52Baada ya kusema haya, Yesu akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini naenda kumwamsha.”

Wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala usingizi ataamka.” 11:13 Mt 9:24Hata hivyo, Yesu alikuwa anazungumzia kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa, walidhani kwamba anasema Lazaro amelala usingizi tu.

Kwa hiyo Yesu akawaambia waziwazi, “Lazaro amekufa. Hata hivyo nafurahi kwa kuwa sikuwepo huko kabla ya Lazaro kufa, ili mpate kuamini. Lakini sasa twendeni kwake.”

11:16 Mt 10:3; Mdo 1:13Tomaso aliyeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenzake, “Sisi nasi twendeni tukafe pamoja naye.”

Yesu Ndiye Ufufuo Na Uzima

11:17 Yn 11:6, 39Yesu alipowasili huko alikuta Lazaro amekuwa kaburini siku nne. 11:18 Yn 11:1; Mt 21:17Basi Bethania ulikuwa karibu na Yerusalemu umbali wa karibu maili mbili,11:18 Maili mbili ni kama kilomita tatu. 11:19 Yn 11:31; Ay 2:11na Wayahudi wengi walikuwa wamekuja kuwafariji Martha na Maria kwa ajili ya kufiwa na ndugu yao. 11:20 Lk 10:38-42Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alitoka kwenda kumlaki, ila Maria alibaki nyumbani.

11:21 Yn 11:32, 37Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa. 11:22 Yn 11:41, 42Lakini sasa ninajua kuwa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa.”

Yesu akamwambia, “Ndugu yako atafufuka.”

11:24 Dan 12:2; Mdo 24:15Martha akamjibu, “Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho.”

11:25 Yn 1:4Yesu akamwambia, “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi 11:26 Yn 3:15; Mt 25:46na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?”

11:27 Lk 2:11; Mt 4:3; 16:16; Yn 6:14Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana, ninaamini ya kuwa wewe ndiwe Kristo,11:27 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu, yeye ajaye ulimwenguni.”

Yesu Alia

11:28 Mt 26:18; Yn 13:13Baada ya kusema haya Martha alikwenda, akamwita Maria dada yake faraghani na kumwambia, “Mwalimu yuko hapa anakuita.” Maria aliposikia hivyo, akaondoka upesi akaenda mpaka alipokuwa Yesu. 11:30 Yn 11:20; 13:13Yesu alikuwa hajaingia kijijini, bali alikuwa bado yuko mahali pale alipokutana na Martha. 11:31 Yn 11:19; 8:59Wale Wayahudi waliokuwa pamoja na Maria nyumbani wakimfariji walipoona ameondoka haraka na kutoka nje, walimfuata wakidhani ya kwamba alikuwa anakwenda kule kaburini kulilia huko.

11:32 Yn 11:21; 5:18Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa, alipiga magoti miguuni Pake na kusema, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa.”

11:33 Yn 11:38; 12:27; 13:21Yesu alipomwona Maria akilia na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye pia wakilia, Yesu alisikia uchungu moyoni, akafadhaika sana. Akauliza, “Mmemweka wapi?”

Wakamwambia, “Bwana, njoo upaone.”

11:35 Lk 19:41Yesu akalia machozi.

11:36 Yn 11:3Ndipo Wayahudi wakasema, “Tazama jinsi alivyompenda Lazaro!”

11:37 Yn 9:6, 7; 11:21, 32Lakini wengine wakasema, “Je, yule aliyefungua macho ya kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?”

Yesu Amfufua Lazaro

11:38 Yn 11:33; Mt 27:60; Lk 24:2; Yn 20:1Yesu kwa mara nyingine akiwa amefadhaika sana, akafika penye kaburi. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe lilikuwa limewekwa kwenye ingilio lake. 11:39 Yn 11:17Yesu akasema, “Liondoeni hilo jiwe.”

Martha ndugu yake yule aliyekuwa amekufa akasema, “Lakini Bwana, wakati huu atakuwa ananuka kwani amekwisha kuwa kaburini siku nne.”

11:40 Yn 11:23-25Yesu akamwambia, “Sikukuambia kwamba kama ukiamini utauona utukufu wa Mungu?”

11:41 Yn 17:1; Mt 11:25Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe kutoka kaburini. Yesu akainua macho yake juu akasema, “Baba, ninakushukuru kwa kuwa wanisikia. 11:42 Yn 12:30; 3:17Ninajua ya kuwa wewe hunisikia siku zote, lakini nimesema haya kwa ajili ya umati huu uliosimama hapa, ili wapate kuamini ya kuwa wewe umenituma.”

11:43 Lk 7:14Baada ya kusema haya, Yesu akapaza sauti yake akaita, “Lazaro, njoo huku!” 11:44 Yn 19:40; 20:7Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake.

Yesu akawaambia, “Mfungueni, mwacheni aende zake.”

Read More of Yohana 11