Yohana 1:1-28 NEN

Yohana 1:1-28

Neno Alifanyika Mwili

1:1 1Yn 1:2; Yn 17:5; Flp 2:6; Isa 55:11Hapo mwanzo alikuwako Neno, huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 1:2 Ufu 1:8; Mwa 1:1Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu.

1:3 Kol 1:16; Ebr 1:2Vitu vyote viliumbwa kwa yeye, wala pasipo yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. 1:4 1Yn 5:20; Ufu 1:8; Yn 12:46Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu. 1:5 Yn 3:19Nuru hungʼaa gizani nalo giza halikuishinda.

1:6 Mt 3:1Alikuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. 1:7 Yn 3:26; 5:33; 3:15Alikuja kama shahidi apate kuishuhudia hiyo nuru, ili kwa kupitia kwake watu wote waweze kuamini. 1:8 Yn 1:20Yeye mwenyewe hakuwa ile nuru, bali alikuja kuishuhudia hiyo nuru. 1:9 1Yn 2:8; Isa 49:6Kwamba nuru halisi, imwangaziayo kila mtu ilikuwa inakuja ulimwenguni.

1:10 Yn 1:3; Ebr 1:2; 11; 3Huyo Neno alikuwako ulimwenguni na ingawa ulimwengu uliumbwa kupitia kwake, haukumtambua. 1:11 Lk 19:14; Mdo 3:26; 13:46Alikuja kwa walio wake, lakini wao hawakumpokea. 1:12 Isa 56:5; Rum 8:15; Gal 3:26; 2Pet 1:4; 1Yn 3:1Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. 1:13 Tit 3:5; Yak 1:18Hawa ndio wasiozaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.

1:14 1Yn 1:1-2; 4:2; Yn 14:6Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.

1:15 Yn 1:32; 3:32; 5:33; Mt 3:11; Mk 1:7; Lk 3:16; Yn 1:27, 30; 3:31; 8:58; Kol 1:17Yohana alishuhudia habari zake, akapaza sauti, akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ ” 1:16 Kol 1:19; 2:9Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema. 1:17 Kum 32:46Kwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Mose, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo. Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye amemdhihirisha.

Ushuhuda Wa Yohana Mbatizaji

(Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Luka 3:1-18)

1:19 Yn 7:1; 10:24Huu ndio ushuhuda wa Yohana wakati Wayahudi walipowatuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumuuliza, “Wewe ni nani?” 1:20 Yn 3:28; Lk 3:15-16Yohana alikiri waziwazi pasipo kuficha akasema, “Mimi si Kristo.”1:20 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.

1:21 Kum 18:15; Mt 11:4Wakamuuliza, “Wewe ni nani basi? Je, wewe ni Eliya?”

Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.”

“Je, wewe ni yule Nabii?”

Akajibu, “Hapana.”

Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?”

1:23 Mt 3:1; Isa 40:3Akawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Bwana.’ ”

Basi walikuwa wametumwa watu kutoka kwa Mafarisayo 1:25 Mt 21:25wakamuuliza, “Kama wewe si Kristo, wala si Eliya na wala si yule Nabii, kwa nini basi unabatiza?”

1:26 Mt 3:11; Mk 1:7, 8Yohana akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji,1:26 Hapa tafsiri zingine zinasema ndani ya maji. lakini katikati yenu yupo mtu msiyemjua. 1:27 Yn 3:26; Mdo 13:25Yeye ajaye baada yangu, sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake.”

1:28 Yn 3:26; 10:40Mambo haya yote yalitukia huko Bethania, ngʼambo ya Mto Yordani, mahali Yohana alipokuwa akibatiza.

Read More of Yohana 1