Yoeli 1:1-20, Yoeli 2:1-17 NEN

Yoeli 1:1-20

1:1 2Pet 1:21; Ebr 1:1; Yer 1:2; Mdo 2:16Neno la Bwana ambalo lilimjia Yoeli mwana wa Pethueli.

Uvamizi Wa Nzige

1:2 Yoe 2:2, 16; Hos 4:1; 5:1; Isa 7:17; Kum 4:32; Dan 12:1; Mt 24:21Sikilizeni hili, enyi wazee;

sikilizeni, ninyi nyote mnaoishi katika nchi.

Je, jambo kama hili lilishawahi kutokea

katika siku zenu au katika siku za babu zenu?

1:3 Kut 10:2; Za 78:4Waelezeni watoto wenu,

na watoto wenu wawaambie watoto wao,

na watoto wao kwa kizazi kitakachofuata.

1:4 Kut 10:4, 14-15; Amo 7:1; Neh 3:15; Kum 28:39Kilichosazwa na kundi la tunutu

nzige wakubwa wamekula,

kilichosazwa na nzige wakubwa

parare wamekula,

kilichosazwa na parare

madumadu wamekula.

1:5 Isa 24:7; 32:10; Yoe 3:3Amkeni, enyi walevi, mlie!

Pigeni yowe enyi wanywaji wote wa mvinyo,

pigeni yowe kwa sababu ya mvinyo mpya,

kwa kuwa mmenyangʼanywa

kutoka midomoni mwenu.

1:6 Yoe 2:2, 11, 25; Ufu 9:8; Mit 30:25; Za 105:35Taifa limevamia nchi yangu,

lenye nguvu tena lisilo na idadi;

lina meno ya simba,

magego ya simba jike.

1:7 Isa 5:8; Amo 4:9Limeharibu mizabibu yangu

na kuangamiza mitini yangu.

Limebambua magome yake

na kuyatupilia mbali,

likayaacha matawi yake yakiwa meupe.

1:8 Isa 22:2; Amo 8:10; Mit 2:17Omboleza kama bikira aliyevaa nguo ya gunia

anayehuzunika kwa ajili ya mume wa ujana wake.

1:9 Yoe 2:14; Hos 9:4; Isa 22:12Sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji

zimekatiliwa mbali kutoka nyumba ya Bwana.

Makuhani wanaomboleza,

wale wanaohudumu mbele za Bwana.

1:10 Isa 5:6; 24:4; Yer 3:3; Hos 9:2; Hes 18:12; Yer 12:11Mashamba yameharibiwa,

ardhi imekauka;

nafaka imeharibiwa,

mvinyo mpya umekauka,

mafuta yamekoma.

1:11 Yer 14:3; Ay 6:20; Amo 5:16; Kut 9:31; Isa 17:11Kateni tamaa, enyi wakulima,

lieni, enyi mlimao mizabibu;

huzunikeni kwa ajili ya ngano na shayiri,

kwa sababu mavuno ya shambani yameharibiwa.

1:12 Isa 15:6; Kut 28:33; Isa 16:8; Hos 9:1-2; Hag 2:19; Yer 48:33Mzabibu umekauka

na mtini umenyauka;

mkomamanga, mtende na mtofaa,

miti yote shambani, imekauka.

Hakika furaha yote ya mwanadamu

imeondoka.

Wito Wa Toba

1:13 Mwa 37:34; Yer 4:8; 2:17; Hos 9:4; Yoe 2:14Vaeni nguo ya gunia, enyi makuhani, muomboleze;

pigeni yowe, enyi mnaohudumu madhabahuni.

Njooni, vaeni nguo ya gunia usiku kucha,

enyi mnaohudumu mbele za Mungu wangu;

kwa kuwa sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji

zimezuiliwa kufika katika nyumba ya Mungu wenu.

1:14 2Nya 20:3-4; Yon 3:8; Hos 4:1Tangazeni saumu takatifu;

liiteni kusanyiko takatifu.

Iteni wazee

na wote waishio katika nchi

waende katika nyumba ya Bwana Mungu wenu,

wakamlilie Bwana.

1:15 Yer 30:7; 46:10; Isa 2:12; Eze 30:3; Amo 5:8Ole kwa siku hiyo!

Kwa kuwa siku ya Bwana iko karibu;

itakuja kama uharibifu

kutoka kwa Mwenyezi.1:15 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.

Je, chakula hakikukatiliwa mbali

mbele ya macho yetu:

furaha na shangwe

kutoka nyumba ya Mungu wetu?

Mbegu zinakauka

chini ya mabonge ya udongo.

Ghala zimeachwa katika uharibifu,

ghala za nafaka zimebomolewa,

kwa maana hakuna nafaka.

Jinsi gani ngʼombe wanavyolia!

Makundi ya mifugo yanahangaika

kwa sababu hawana malisho;

hata makundi ya kondoo yanateseka.

Kwako, Ee Bwana, naita,

kwa kuwa moto umeteketeza

malisho ya mbugani

na miali ya moto imeunguza

miti yote shambani.

Hata wanyama wa porini wanakuonea shauku;

vijito vya maji vimekauka,

na moto umeteketeza

malisho yote ya mbugani.

Read More of Yoeli 1

Yoeli 2:1-17

Jeshi La Nzige

2:1 Hos 10:2, 7; Kut 15:17; Oba 1:15; Sef 1:14-16; Eze 12:23Pigeni tarumbeta katika Sayuni;

pigeni mbiu katika mlima wangu mtakatifu.

Wote waishio katika nchi na watetemeke,

kwa kuwa siku ya Bwana inakuja. Iko karibu,

2:2 Ay 9:7; Isa 8:22; 13:10; Amo 5:18; Kut 10:14; Dan 9:12; Mt 24:21; Eze 34:12siku ya giza na huzuni,

siku ya mawingu na utusitusi.

Kama mapambazuko yasambaavyo

toka upande huu wa milima

hata upande mwingine

jeshi kubwa na lenye nguvu linakuja.

Jambo kama hili halijakuwepo tangu zamani

wala halitakuwepo tena kamwe

kwa vizazi vijavyo.

2:3 Za 97:3; 105:34-35; Kut 10:12-15; Isa 14:17; Zek 7:14; Isa 1:31Mbele yao moto unateketeza,

nyuma yao miali ya moto

inawaka kwa nguvu.

Mbele yao nchi iko kama bustani ya Edeni,

nyuma yao ni jangwa lisilofaa:

hakuna kitu kinachowaepuka.

Wanaonekana kama farasi;

wanakwenda mbio

kama askari wapanda farasi.

2:5 Ufu 9:9; Isa 5:24; 30:30Wanatoa sauti kama magari ya vita,

wanaporukaruka juu ya vilele vya milima,

kama mlio wa miali ya moto ilayo mabua,

kama jeshi kubwa lililojipanga kwa ajili ya vita.

2:6 Yer 8:21; Isa 13Wanapoonekana, mataifa yanakuwa katika maumivu makuu;

kila uso unabadilika rangi.

2:7 Isa 5:27; Mit 30:27; Ay 16:14Wanashambulia kama wapiganaji wa vita;

wanapanda kuta kama askari.

Wote wanatembea katika safu,

hawapotoshi safu zao.

Hakuna anayemsukuma mwenzake;

kila mmoja anakwenda mbele moja kwa moja.

Wanapita katika vizuizi

bila kuharibu safu zao.

2:9 Yer 9:21; Kut 10:6Wanaenda kasi kuingia mjini;

wanakimbia ukutani.

Wanaingia ndani ya nyumba;

kwa kuingilia madirishani kama wevi.

2:10 Isa 5:30; 13:10; Za 18:7; 102:26; Ufu 9:2; Ay 9:7; Eze 38:19Mbele yao dunia inatikisika,

anga linatetemeka,

jua na mwezi vinatiwa giza,

na nyota hazitoi mwanga wake tena.

2:11 Isa 2:12; Hes 24:23; Ufu 6:17; 18:8; Sef 2:11; Eze 30:3; Yoe 1:15; Yer 50:34; Mal 3:2; Za 29:3Bwana anatoa mshindo wa ngurumo

mbele ya jeshi lake;

majeshi yake hayana idadi,

ni wenye nguvu nyingi

wale ambao hutii agizo lake.

Siku ya Bwana ni kuu,

ni ya kutisha.

Ni nani anayeweza kuistahimili?

Rarueni Mioyo Yenu

2:12 Kum 4:30; Hos 12:6; Eze 33:11; 1Sam 7:3“Hata sasa,” asema Bwana,

“nirudieni kwa mioyo yenu yote,

kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza.”

2:13 Za 34:18; 51:17; 86:5; Mwa 37:29; Hes 14:6; Kut 34:6; Yon 4:2; Isa 57:15; 2Fal 22:19; Mt 5:3-4; Ay 1:20Rarueni mioyo yenu

na siyo mavazi yenu.

Mrudieni Bwana, Mungu wenu,

kwa maana yeye ndiye mwenye neema

na mwingi wa huruma,

si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo,

huona huruma, hujizuia kuleta maafa.

2:14 Yer 26:3; 31:14; Yn 3:9; Sef 2:3; Isa 65:8; Zek 8:13; Yos 14:12; Amo 5:15; Hag 2:19; Mal 3:10Ni nani ajuaye? Yeye aweza kugeuka na kuwa na huruma

na kuacha baraka nyuma yake:

sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji

kwa ajili ya Bwana Mungu wenu.

2:15 2Nya 20:3; Hes 10:2-3; Yer 36:9Pigeni tarumbeta katika Sayuni,

tangazeni saumu takatifu,

liiteni kusanyiko takatifu.

2:16 Kut 19:10; 2Nya 20:13; 1Kor 7:5; Za 19Wakusanyeni watu,

wekeni wakfu kusanyiko;

waleteni pamoja wazee,

wakusanyeni watoto,

wale wanyonyao maziwa.

Bwana arusi na atoke chumbani mwake

na bibi arusi naye atoke katika chumba chake.

2:17 Eze 8:16; Mt 23:35; Kum 9:26-29; Ay 17:6; Za 42:3; Kut 32:11; Isa 37:20; Yoe 1:13; Isa 22:12Makuhani, ambao wanahudumu mbele za Bwana,

na walie katikati ya ukumbi

wa Hekalu na madhabahu.

Waseme, “Wahurumie watu wako, Ee Bwana.

Usifanye urithi wako kitu cha kudharauliwa,

neno la dhihaka kati ya mataifa.

Kwa nini wasemezane miongoni mwao,

‘Yuko wapi Mungu wao?’ ”

Read More of Yoeli 2