Ayubu 8:1-22, Ayubu 9:1-35, Ayubu 10:1-22 NEN

Ayubu 8:1-22

Bildadi Anasema: Yampasa Ayubu Atubu

8:1 Mwa 25:2; Ay 18:1; 25:1Kisha Bildadi Mshuhi akajibu:

8:2 Ay 6:26; 11:2; 2Nya 36:16“Hata lini wewe utasema mambo kama haya?

Maneno yako ni kama upepo mkuu.

8:3 Mwa 18:25; 2Nya 19:7; Kum 32:4; Ay 34:12; Dan 9:14Je, Mungu hupotosha hukumu?

Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki?

8:4 Ay 1:5, 18Watoto wako walipomtenda dhambi,

aliwapa adhabu ya dhambi yao.

8:5 Ay 5:8; 11:13; 22:23Lakini ukimtafuta Mungu,

nawe ukamsihi Mwenyezi,

8:6 Za 7:6; Isa 58:9; Ay 5:24; 5:15; 22:27; Isa 65:24ikiwa wewe ni safi na mnyofu,

hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako,

na kukurudisha katika mahali pako pa haki.

8:7 Ay 21:13; 22:21; 36:11; Za 25:13; Yer 29:11; 31:17Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo,

lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio.

8:8 Kum 4:32; 32:7; Za 71:18; Ay 15:18“Ukaulize vizazi vilivyotangulia

na uone baba zao walijifunza nini,

8:9 Mwa 47:9; 2Nya 10:6; Za 39:5-6; 1Nya 29:15; Ay 7:6kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote,

nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu.

8:10 Mt 1:8; 2:1-2; 4:1Je, hawatakufundisha na kukueleza?

Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao?

8:11 Ay 40:21; Kut 2:3; Isa 19:6; 35:7Je, mafunjo yaweza kumea mahali pasipo na matope?

Matete yaweza kustawi bila maji?

8:12 Isa 34:4; Yer 17:6; Za 129:6; Yak 1:10, 11; 1Pet 1:24Wakati bado yanaendelea kukua kabla ya kukatwa,

hunyauka haraka kuliko majani mengine.

8:13 Za 50:13; 112:10; Mit 10:28; Yer 15:9; Ay 11:20; 18:14; Isa 33:14; Mt 24:51; Lk 12:1Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu;

vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.

8:14 Ay 8:15; 27:18; Isa 59:5Lile analolitumainia huvunjika upesi;

lile analolitegemea ni utando wa buibui.

8:15 Ay 27:18; 8:12; Za 49:11; Mt 7:26-27Huutegemea utando wake, lakini hausimami;

huungʼangʼania, lakini haudumu.

8:16 Za 80:11; 37:35; Isa 16:5; Yer 11:16Yeye ni kama mti ulionyeshewa vizuri wakati wa jua,

ukieneza machipukizi yake bustanini;

huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe,

na kutafuta nafasi katikati ya mawe.

8:18 Ay 14:20; 7:10; Za 37:36; 103:16Unapongʼolewa kutoka mahali pake,

ndipo mahali pale huukana na kusema,

‘Mimi kamwe sikukuona.’

8:19 Za 113:7Hakika uhai wake hunyauka,

na kutoka udongoni mimea mingine huota.

8:20 Mwa 18:25; Ay 21:30; 1The 5:23-24; Za 37:24“Hakika Mungu hamkatai mtu asiye na hatia,

wala kuitia nguvu mikono ya mtenda mabaya.

8:21 Ay 5:22; Ezr 3:13; Isa 35:6; Za 47:5; 107:22Bado atakijaza kinywa chako na kicheko,

na midomo yako na kelele za shangwe.

8:22 Za 6:10; Eze 7:27; 1Sam 8:3; Mit 14:11; Ay 18:6Adui zako watavikwa aibu,

nazo hema za waovu hazitakuwepo tena.”

Read More of Ayubu 8

Ayubu 9:1-35

Hotuba Ya Tatu Ya Ayubu

Hakuna Mpatanishi

Kisha Ayubu akajibu:

9:2 Za 143:2; Rum 3:20; Ay 4:17“Naam, najua hili ni kweli.

Lakini mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?

9:3 Ay 9:32; 40:5; Za 44:21Ingawa mtu angetaka kushindana naye,

asingaliweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja.

9:4 Mit 2:6; 8:6; Mhu 2:26; 2Nya 13:12; Isa 40:26; Ay 5:9; 12:13; Za 93:4; Dan 2:20Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno.

Ni nani aliyempinga naye akawa salama?

9:5 Isa 13:13; Mik 1:4; Mt 17:20; Za 18:7Aiondoa milima bila yenyewe kujua

na kuipindua kwa hasira yake.

9:6 Hag 2:6; 2:21; Ebr 12:26; Isa 2:19-21; 2Sam 22:8Aitikisa dunia kutoka mahali pake

na kuzifanya nguzo zake zitetemeke.

9:7 Yer 4:23; Eze 32:8; Isa 34:4; Sef 1:15; Yoe 2:2Husema na jua, nalo likaacha kuangaza;

naye huizima mianga ya nyota.

9:8 Mwa 1:1, 8; Isa 48:13; Ay 38:16; Za 77:19; Mit 8:28; Hab 3:15Yeye peke yake huzitandaza mbingu

na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.

9:9 Mwa 1:16; Ay 38:31; 32:22; Amo 5:8Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu,9:9 Nyota za Dubu hapa ina maana ya kundi la nyota za kaskazini, ambazo zinaitwa kwa jina la Dubu Mkuu. na Orioni,9:9 Orioni ni kundi la nyota kubwa.

Kilimia,9:9 Kilimia ni jina lililopewa nyota saba (Taurus). na makundi ya nyota za kusini.

9:10 Kum 6:22; Za 72:18; 136:4; Yer 32:20Hutenda maajabu yasiyopimika,

miujiza isiyoweza kuhesabiwa.

9:11 Ay 23:8-9; 35:14Anapopita karibu nami, siwezi kumwona;

apitapo mbele yangu, simtambui.

9:12 Hes 23:20; Isa 43:13; 14:27; Dan 2:21; Rum 9:20; Ay 11:10Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia?

Ni nani awezaye kumwambia, ‘Unafanya nini?’

9:13 Hes 14:18; Ay 10:15; Za 78:38; Isa 3:11; 6:5Mungu hataizuia hasira yake;

hata jeshi kubwa la Rahabu9:13 Rahabu hapa ina maana ya Misri kwa fumbo. lenye nguvu

linajikunyata miguuni pake.

9:14 Ay 9:3“Ni vipi basi mimi nitaweza kubishana naye?

Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye?

9:15 Ay 10:15; 13:19; 34:5-6; 40:5; 42:7; Mwa 18:25; 1Sam 24:12; Za 50:6; 96:13Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu;

ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie.

9:16 Ay 13:22; Rum 9:20-21Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali,

siamini kama angenisikiliza.

9:17 Isa 38:13; 38:13; Yn 1:4; Za 10:10; 83:15; Ay 16:12; 30:16; 16:14; 2:3Yeye angeniangamiza kwa dhoruba

na kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu.

9:18 Ay 7:19; 10:1Asingeniacha nipumue

bali angenifunika kabisa na huzuni kuu.

9:19 Ay 9:4; Neh 9:32; Yer 49:19Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu!

Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani?

9:20 Ay 9:15Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu;

kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia.

9:21 Mwa 6:9; Hes 11:15; Ay 7:15-16; 6:29; 10:1“Ingawa mimi sina kosa,

haileti tofauti katika nafsi yangu;

nauchukia uhai wangu.

9:22 Mhu 9:2-3; Eze 21:3; Ay 3:19Hayo yote ni sawa; ndiyo sababu nasema,

‘Yeye huwaangamiza wasio na makosa pamoja na waovu.’

9:23 Hab 1:3; 1Pet 1:7; Ebr 11:36; Za 64:4Wakati pigo liletapo kifo cha ghafula,

yeye hudhihaki kule kukata tamaa kwa yule asiye na kosa.

9:24 Za 73:3; 73:12; Mhu 8:11; Mao 3:9; Ay 1:15, 17; 10:3; 40:8; Yer 12:1; Isa 41:20Wakati nchi inapoangukia mikononi mwa waovu,

yeye huwafunga macho mahakimu wake.

Kama si yeye, basi ni nani?

9:25 Ay 7:6, 7; 10:20“Siku zangu zapita mbio kuliko mkimbiaji;

zinapita upesi bila kuona furaha hata kidogo.

9:26 Isa 18:2; Ay 39:29; Za 46:3; Hab 1:8Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo,

mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula.

9:27 Ay 7:11Kama nikisema, ‘Nitayasahau malalamiko yangu,

nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,’

9:28 Kut 20:7; 34:7; Ay 3:25; 7:21bado ninahofia mateso yangu yote,

kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia.

9:29 Ay 9:3, 15; Za 37:33Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia,

kwa nini basi nitaabishwe bure?

9:30 Hos 13:12; Isa 1:15-18; Mal 3:2; Ay 31:7; 14:4, 17; 17:9; Yer 2:22Hata kama ningejiosha kwa sabuni

na kutakasa mikono yangu kwa magadi,

9:31 Za 35:7; 40:2; 51:9; Yer 2:22; Nah 3:6; Mal 2:3; Ay 7:20wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezi

kiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana.

9:32 Rum 9:20; Mhu 6:10; Za 143:2; Hes 23:19“Yeye si mwanadamu kama mimi ili niweze kumjibu,

ili kwamba tuweze kushindana naye mahakamani.

9:33 1Sam 2:25; Ay 9:19Laiti angelikuwepo mtu wa kutupatanisha kati yetu,

aweke mkono wake juu yetu sote wawili,

9:34 Ay 6:4; 21:9; Za 39:10; 73:5; 32:4mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu,

ili utisho wake usiendelee kunitia hofu.

9:35 Ay 7:15; 13:21; 7:11Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa,

lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza.

Read More of Ayubu 9

Ayubu 10:1-22

Ayubu: Nayachukia Maisha Yangu

10:1 Hes 11:15; 1Sam 1:10; Ay 7:11; 9:18, 21; 1Fal 19:4“Nayachukia sana haya maisha yangu;

kwa hiyo nitatoa malalamiko yangu kwa wazi bila kujizuia,

nami nitanena kutokana na uchungu wa moyo wangu.

10:2 Ay 13:3; 40:1; Isa 3:13; Hos 4:1; 5:1; Mik 6:2; Rum 8:33Nitamwambia Mungu: Usinihukumu,

bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu.

10:3 Ay 9:24; 22:18; 31:23; Mwa 1:26; Za 138:8; Isa 60:21; 64:8; Za 8:6; 95:6; 100:3Je, inakupendeza wewe kunionea,

kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako,

huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu?

10:4 Mit 5:21; Yer 16:17; 1Sam 16:7; Ay 11:11; 14:16; Za 11:4; 33:15; Mit 15:3; Yer 11:20-23Je, wewe una macho ya kimwili?

Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo?

10:5 Za 102:24; 2Pet 3:8; Ay 36:26; Za 39:5; 90:2, 4Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu,

au miaka yako ni kama ile ya mtu,

10:6 Ay 14:16ili kwamba utafute makosa yangu

na kuichunguza dhambi yangu;

10:7 Ay 10:15; 6:29; 11:4; 16:17; Kum 32:39ingawa wajua kuwa mimi sina hatia,

na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako?

10:8 Za 119:73; Isa 43:7; Mwa 2:7; 2Sam 14:14; Ay 30:15“Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya.

Je, sasa utageuka na kuniangamiza?

10:9 Isa 29:16; 64:8; Mwa 2:7; Ay 7:21; 4:19Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi.

Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena?

Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa,

na kunigandisha kama jibini,

10:11 Za 139:13, 15ukanivika ngozi na nyama,

na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa?

10:12 Mwa 2:7; 24:12; 45:5; 1Pet 2:25Umenipa uhai na kunitendea wema,

katika uangalizi wako umeilinda roho yangu.

10:13 Ay 23:13; Za 115:3“Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako,

nami ninajua kuwa hili lilikuwa katika nia yako:

10:14 Kut 34:7; Ay 7:21; 13:27Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona,

wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa.

10:15 Ay 9:13; 10:7; Isa 3:11; Za 25:18; 25:16Kama nina hatia, ole wangu!

Hata kama ningekuwa sina hatia,

siwezi kukiinua kichwa changu,

kwa kuwa nimejawa na aibu,

na kuzama katika mateso yangu.

10:16 Yer 5:6; Hos 5:14; 1Sam 28:21; Isa 38:16; Za 7:2; 1Sam 17:38; Mao 3:10Kama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba,

na kuonyesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu.

10:17 1Fal 21:10; Ay 16:8; Rut 1:21Wewe waleta mashahidi wapya dhidi yangu

na kuzidisha hasira yako juu yangu;

nazo nguvu zako zinanijia wimbi moja baada ya jingine.

10:18 Ay 3:8; 3:26; Za 22:9; Mhu 4:2; 7:1“Kwa nini basi ulinitoa tumboni?

Ninatamani ningekufa kabla jicho lolote halijaniona.

10:19 Ay 3:3; Yer 15:10Laiti nisingekuwako kamwe,

au ningekuwa nimechukuliwa moja kwa moja

kutoka tumboni kwenda kaburini!

10:20 Mhu 6:12; Ay 7:16-19; 5:7; Za 39:13; Ay 9:25Je, siku zangu chache si zimekaribia kuisha?

Niachie ili niweze kupata muda mfupi wa kufurahi

10:21 2Sam 12:23; Za 88:12; 23:4; Ay 3:13; Mhu 2:9kabla sijaenda mahali ambapo hakuna kurudi tena,

katika nchi ya giza na uvuli wa mauti,

10:22 Ay 3:5; 1Sam 2:9nchi ya giza kuu sana,

yenye uvuli wa giza na machafuko,

mahali ambapo hata nuru ni giza.”

Read More of Ayubu 10