Ayubu 40:3-24, Ayubu 41:1-34, Ayubu 42:1-17 NEN

Ayubu 40:3-24

Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:

40:4 Ay 42:6; Amu 18:19; Ay 29:9; Ezr 9:6; Zek 2:13“Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe?

Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu.

40:5 Ay 9:3; 9:15Nimesema mara moja, lakini sina jibu;

naam, nimesema mara mbili,

lakini sitasema tena.”

40:6 Kut 14:21; Ay 38:1Ndipo Bwana akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli:

40:7 Ay 38:3“Jikaze kama mwanaume;

nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu.

40:8 Ay 15:25; Rum 3:3; Za 51:4“Je, utabatilisha hukumu yangu?

Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe?

40:9 2Nya 32:8; Za 98:1; Kut 20:19; Za 29:3-4Je, una mkono kama wa Mungu,

nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake?

40:10 Za 29:1-2; 45:3; 93:1; 96:6; 104:1; 145:5Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari,

nawe uvae heshima na enzi.

40:11 Nah 1:6; Sef 1:18; Za 18:27; Isa 32:19Fungulia ukali wa ghadhabu yako,

mtafute kila mwenye kiburi umshushe,

40:12 Za 52:5; 1Pet 5:5; Dan 5:20; Mal 4:3; Lk 18:14mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze,

waponde waovu mahali wasimamapo.

40:13 Hes 16:31-34; Ay 4:9Wazike wote mavumbini pamoja;

wafunge nyuso zao kaburini.

40:14 Kut 15:6; Isa 63:5Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia

kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.

40:15 Ay 9:9; Isa 11:7; 65:25“Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi,40:15 Huyu alikuwa mnyama wa nyakati za zamani ambaye hajulikani hasa ni gani.

niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe,

anayekula majani kama ngʼombe.

40:16 Ay 39:11; 41:9Tazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake,

uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake!

40:17 Ay 41:15Mkia wake hutikisika kama mwerezi;

mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja.

40:18 Ay 41:12; Isa 11:4; 49:2Mifupa yake ni bomba za shaba,

maungo yake ni kama fito za chuma.

40:19 Za 40:5; Isa 27:1Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu,

lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake.

40:20 Za 104:14, 26Vilima humletea yeye mazao yake,

nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye.

40:21 Mwa 41:2; Za 68:30; Isa 35:7; Ay 8:11Hulala chini ya mimea ya yungiyungi,

katika maficho ya matete kwenye matope.

40:22 Za 1:3; Isa 44:4Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake;

miti mirefu karibu na kijito humzunguka.

Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu;

yeye yu salama, hata kama Yordani ingefurika hadi kwenye kinywa chake.

40:24 2Fal 19:28; Isa 37:29Je, mtu yeyote anaweza kumkamata yeye akiwa macho,

au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake?

Read More of Ayubu 40

Ayubu 41:1-34

41:1 Za 104:26; Isa 27:1“Je, waweza kumvua Lewiathani41:1 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. kwa ndoano ya samaki,

au kufunga ulimi wake kwa kamba?

41:2 Isa 37:29; Eze 19:4; Isa 30:28Waweza kupitisha kamba puani mwake,

au kutoboa taya lake kwa kulabu?

41:3 1Fal 20:31Je, ataendelea kukuomba umhurumie?

Atasema nawe maneno ya upole?

41:4 Kut 21:6Je, atafanya agano nawe ili umtwae

awe mtumishi wako maisha yake yote?

Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege,

au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako?

Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake?

Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara?

41:7 Ay 40:24Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali,

au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki?

41:8 Ay 3:8Kama ukiweka mkono wako juu yake,

utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena!

41:9 Ay 40:16Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya;

kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini.

41:10 Ay 3:8; 2Nya 20:6; Ufu 6:17; 1Kor 10:22Hakuna yeyote aliye mkali athubutuye kumchokoza.

Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu?

41:11 Ay 34:33; Yos 3:11; Rum 11:35; Mdo 4:24; Mwa 14:19; Kum 10:14Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa?

Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu.

41:12 Ay 40:18; 39:11“Sitashindwa kunena juu ya maungo yake,

nguvu zake na umbo lake zuri.

41:13 Ay 30:11; 39:10Ni nani awezaye kumvua gamba lake la nje?

Ni nani awezaye kumsogelea na lijamu?

41:14 Za 22:13Nani athubutuye kuufungua mlango wa kinywa chake,

kilichozungukwa na meno yake ya kutisha pande zote?

41:15 Ay 40:17Mgongo wake una safu za ngao

zilizoshikamanishwa imara pamoja;

kila moja iko karibu sana na mwenzake,

wala hakuna hewa iwezayo kupita kati yake.

Zimeunganishwa imara kila moja na nyingine;

zimengʼangʼaniana pamoja wala haziwezi kutenganishwa.

41:18 Ay 40:17Akipiga chafya mwanga humetameta;

macho yake ni kama mionzi ya mapambazuko.

41:19 Dan 10:6Mienge iwakayo humiminika kutoka kinywani mwake;

cheche za moto huruka nje.

41:20 Za 18:8Moshi hufuka kutoka puani mwake,

kama kutoka kwenye chungu kinachotokota kwa moto wa matete.

41:21 Ay 4:9; Isa 11:4; 10:17; Yer 4:4Pumzi yake huwasha makaa ya mawe,

nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake.

41:22 Ay 39:11Nguvu hukaa katika shingo yake;

utisho hutangulia mbele yake.

Mikunjo ya nyama yake imeshikamana imara pamoja;

iko imara na haiwezi kuondolewa.

41:24 Mt 18:6Kifua chake ni kigumu kama mwamba,

kigumu kama jiwe la chini la kusagia.

41:25 Ay 39:20; 3:8Ainukapo, mashujaa wanaogopa;

hurudi nyuma mbele yake anapokwenda kwa kishindo.

41:26 Ay 8:18; 40:24Upanga unaomfikia haumdhuru,

wala mkuki au mshale wala fumo.

41:27 Ay 41:29Chuma hukiona kama unyasi,

na shaba kama mti uliooza.

41:28 Za 91:5Mishale haimfanyi yeye akimbie;

mawe ya kombeo kwake ni kama makapi.

41:29 Ay 41:27; 5:22Rungu kwake huwa kama kipande cha jani kavu;

hucheka sauti za kugongana kwa mkuki.

41:30 Isa 28:27; Amo 1:3; Isa 41:15Sehemu zake za chini kwenye tumbo

zina menomeno na mapengo kama vigae vya chungu,

zikiacha mburuzo kwenye matope

kama chombo chenye meno cha kupuria.

41:31 1Sam 2:14; Eze 32:2Huvisukasuka vilindi kama sufuria kubwa ichemkayo,

na kukoroga bahari kama chungu cha marhamu.

Anapopita nyuma yake huacha mkondo unaometameta;

mtu angedhani vilindi vilikuwa na mvi.

41:33 Ay 40:19Hakuna chochote duniani kinacholingana naye:

yeye ni kiumbe kisicho na woga.

41:34 Ay 28:8Yeye huwatazama chini wale wote wenye kujivuna;

yeye ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.”

Read More of Ayubu 41

Ayubu 42:1-17

Sehemu Ya Tano

(Ayubu 42)

Ayubu Anamjibu Bwana

Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:

42:2 Mwa 18:14; Yer 32:17; Mt 19:26; 2Nya 20:6; Efe 1:11“Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote,

wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.

42:3 Ay 34:35; 38:2; Za 40:5Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’

Hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi,

mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua.

42:4 Ay 38:3; 40:7“Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena;

nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’

42:5 Ay 26:14; Rum 10:17; Amu 13:22; Mt 5:8Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako,

lakini sasa macho yangu yamekuona.

42:6 Eze 6:9; Rum 12:3; Kut 10:3; Ezr 9:6Kwa hiyo najidharau mwenyewe,

na kutubu katika mavumbi na majivu.”

Mwisho: Marafiki Wa Ayubu Wanafedheheshwa

42:7 Yos 1:7; Ay 32:3, 8; 9:15Baada ya Bwana kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu. 42:8 Hes 23:29; Eze 45:23; Mwa 20:17; Yak 5:15-17; Ay 22:30Basi sasa chukueni mafahali saba na kondoo dume saba mkamwendee mtumishi wangu Ayubu nanyi mkatoe sadaka za kuteketezwa kwa ajili yenu wenyewe. Mtumishi wangu Ayubu ataomba kwa ajili yenu, nami nitayakubali maombi yake ili nisiwatendee sawasawa na upumbavu wenu. Ninyi hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.” 42:9 Ay 2:11; Mwa 19:21; 20:17; Eze 14:14Kwa hiyo Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi wakafanya kama Bwana alivyowaambia; naye Bwana akayakubali maombi ya Ayubu.

42:10 Kum 30:3; Za 14:7; 126:5-6; Yak 5:11Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, Bwana akamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo mwanzoni. 42:11 Ay 19:13Ndipo ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu mwanzoni, wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yote Bwana aliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu.

42:12 Yak 5:11Bwana akaibariki sehemu ya mwisho ya maisha ya Ayubu kuliko ile ya kwanza. Alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, ngamia elfu sita, jozi za mafahali elfu moja, na punda wa kike elfu moja. Tena alikuwa na wana saba na binti watatu. Binti wa kwanza aliitwa Yemima, wa pili Kesia na wa tatu Keren-Hapuki. Hapakuwepo mahali popote katika nchi ile yote palipopatikana wanawake wazuri kama binti za Ayubu; naye baba yao akawapa urithi pamoja na ndugu zao.

Baada ya hili Ayubu akaishi miaka 140; akawaona wanawe na wana wa wanawe hata kizazi cha nne. 42:17 Mwa 15:15; 25:8Hivyo Ayubu akafa, akiwa mzee aliyekuwa ameshiba siku.

Read More of Ayubu 42