Ayubu 33:1-33
Elihu Anamkemea Ayubu
33:1 Ay 32:10; 6:28; 13:6“Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu;
zingatia kila kitu nitakachosema.
Karibu nitafungua kinywa changu;
maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu.
33:3 Ay 27:4; 36:4Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu;
midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo.
33:4 Mwa 2:7; Ay 10:3; 27:3Roho wa Mungu ameniumba;
pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai.
33:5 Ay 13:18Unijibu basi, kama unaweza;
jiandae kunikabili mimi.
33:6 Ay 9:32; 4:19Mimi ni kama wewe mbele za Mungu;
mimi pia nimetolewa kwenye udongo.
33:7 Ay 13:21; 2Kor 2:4Huna sababu ya kuniogopa,
wala mkono wangu haupaswi kukulemea.
“Lakini umesema nikiwa ninakusikia,
nami nilisikia maneno yenyewe:
33:9 Ay 10:7; 9:30; 16:17‘Mimi ni safi na sina dhambi;
mimi ni safi na sina hatia.
33:10 Ay 13:24Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu,
naye ananiona kama adui yake.
33:11 Ay 13:27; Mit 3:6; Isa 30:21Ananifunga miguu kwa pingu,
tena anaziangalia njia zangu zote kwa karibu.’
33:12 Mhu 7:20; Za 8:4; Isa 55:8-9“Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa,
kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.
33:13 Ay 40:2; Isa 45:9Kwa nini unamlalamikia
kwamba yeye hamjibu mwanadamu?
33:14 Za 62:11; Mwa 30:2; Mt 27:19Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja,
au wakati mwingine kwa njia nyingine,
ingawa mwanadamu anaweza asielewe.
33:15 Mwa 30:2; Mt 27:19Mungu husema na mwanadamu katika ndoto,
katika maono ya usiku,
wakati usingizi mzito uwaangukiapo
wanadamu wasinziapo vitandani mwao,
33:16 Ay 36:10anaweza akasemea masikioni mwao,
na kuwatia hofu kwa maonyo,
33:17 Ay 36:10, 15; 6:4; Za 88:15-16ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya
na kumwepusha na kiburi,
33:18 Yn 2:6; Zek 9:11; Ay 15:22; Mt 26:52kuiokoa nafsi yake na shimo,
uhai wake usiangamizwe kwa upanga.
33:19 Kum 8:5; Za 6:2; Isa 38:13Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake,
kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake,
33:20 Za 102; 4; 107:18; Ay 3:24kiasi kwamba maisha yake yenyewe yanakataa chakula
nayo nafsi yake ikakichukia kabisa hata chakula kizuri.
33:21 Ay 2:5; 16:8Nyama ya mwili wake huisha kwa kukonda,
nayo mifupa yake ambayo mwanzoni ilikuwa imefichika,
sasa inatokeza nje.
33:22 Ay 38:17; Za 9:13; 88:3; 107:18; 116:3Nafsi yake inakaribia kaburi,
nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo.
33:23 Ay 36:9-10; Mik 6:8; Gal 3:19; Ebr 8:6; 9:15; Ay 36:9-10; Mik 6:8“Kama bado kuna malaika upande wake
kama mtetezi, mmoja miongoni mwa elfu,
wa kumwambia mwanadamu lililo jema kwake,
33:24 Isa 38:17kumwonea huruma na kusema,
‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni;
nimepata ukombozi kwa ajili yake’:
33:25 2Fal 5:14ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto;
hurudishwa upya kama siku za ujana wake.
33:26 Mit 8:35; 2Fal 20:2-5; Lk 2:52; Ezr 3:13; Za 13:5Humwomba Mungu, akapata kibali kwake,
huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha;
Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu.
33:27 Hes 22:34; 2Sam 12:13; Ezr 9:13; Yak 2:13; Lk 15:21Ndipo huja mbele za watu na kusema,
‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki,
lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili.
33:28 Kut 15:13; Za 34:22; 107:20; Ay 17:16; 22:20Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni,
nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’
33:29 Yer 10:23; Flp 2:13“Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu;
mara mbili hata mara tatu,
33:30 Za 49:19; Isa 53:11; Zek 9:11ili aigeuze nafsi yake toka shimoni,
ili nuru ya uzima imwangazie.
33:31 Yer 23:18; Ay 32:10“Ayubu, zingatia, nisikilize mimi;
nyamaza, nami nitanena.
33:32 Ay 6:29; 35:2Kama unalo lolote la kusema, unijibu;
sema, kwa maana ninataka uonekane huna hatia.
33:33 Mit 10:8, 10, 19; Za 34:11Lakini kama huna la kusema, basi nisikilize mimi;
nyamaza, nami nitakufundisha hekima.”
Ayubu 34:1-37
Elihu Anatangaza Haki Ya Mungu
Kisha Elihu akasema:
34:2 Ay 32:10“Sikieni maneno yangu, enyi watu wenye hekima;
nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye maarifa.
34:3 Ay 12:11Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno
kama vile ulimi uonjavyo chakula.
34:4 1The 5:21Tujichagulie wenyewe yaliyo sawa,
nasi tujifunze pamoja yaliyo mema.
34:5 Ay 33:9; 6:29; 27:2; 9; 17“Ayubu anasema, ‘Mimi sina hatia,
lakini Mungu ameninyima haki yangu.
34:6 Yer 10:19; Ay 10:3Ingawa niko sawa,
ninaonekana mwongo;
nami ingawa sina kosa,
kidonda changu hakiponi.’
34:7 Ay 9:21; 15:16Ni mtu gani aliye kama Ayubu,
anywaye dharau kama maji?
34:8 Ay 22:15; Za 50:18Ashirikianaye na watenda mabaya
na kuchangamana na watu waovu.
34:9 Ay 9:29-31Kwa kuwa anasema, ‘Haimfaidi mwanadamu kitu chochote
anapojitahidi kumpendeza Mungu.’
34:10 Mwa 18:25; Za 92:15; Rum 3:5“Hivyo nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye ufahamu.
Kamwe Mungu hatendi uovu,
Mwenyezi hafanyi kosa.
34:11 Ay 21:31; 2Kor 5:10; Yer 17:10; Eze 33; 20; Mit 24:12Humlipa mwanadamu kwa ajili ya lile alilotenda;
huleta juu yake kile ambacho matendo yake yanastahili.
34:12 Za 9:16; Kol 3:25Ni jambo lisiloweza kufikiriwa kwamba Mungu angefanya makosa,
kwamba Mwenyezi angepotosha hukumu.
34:13 Ay 36:23; Isa 40:14Je, ni nani aliyemtawaza juu ya dunia?
Ni nani aliyemweka kuwa mwangalizi wa ulimwengu wote?
34:14 Hes 16:22; Za 104:29; Mhu 12:7Kama lilikuwa kusudi la Mungu,
naye akaiondoa Roho yake na pumzi yake,
34:15 Za 90:10; Mwa 2:7wanadamu wote wangeliangamia kwa pamoja,
na mtu angerudi mavumbini.
34:16 Ay 32:10; 34:30“Kama ninyi mnaufahamu, sikieni hili;
sikilizeni hili nisemalo.
34:17 Mwa 18:23; 2Sam 23:3-4; Mit 20:8; Rum 3:5-7; Ay 10:7Je, yeye aichukiaye haki aweza kutawala?
Je, utamhukumu mwenye haki, Aliye na Nguvu Zote?
34:18 Kut 22:28; Isa 40:24Je, si ni yeye awaambiaye wafalme, ‘Ninyi hamfai kitu,’
nao watu mashuhuri, ‘Ninyi ni waovu,’
34:19 Kum 10:17; Mdo 10:34; Law 19:15; Yak 2:5yeye asiyependelea wakuu,
wala haonyeshi upendeleo kwa matajiri kuliko maskini,
kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake?
34:20 Kut 11:4; 12:29; Ay 12:19Wanakufa ghafula, usiku wa manane;
watu wanatikiswa nao hupita;
wenye nguvu huondolewa
bila mkono wa mwanadamu.
34:21 Mit 15:3; Ebr 4:13“Macho yake yanazitazama njia za wanadamu;
anaona kila hatua yao.
34:22 Za 74:20; Ay 3:5; Amo 9:2-3Hakuna mahali penye giza nene, wala uvuli mkubwa,
ambapo watenda mabaya wanaweza kujificha.
34:23 Ay 11:11; Ezr 9:13Mungu hana haja ya kumchunguza mtu sana,
ili apate kuja mbele zake kwa hukumu.
34:24 Ay 12:19; Dan 2:21Bila kuuliza huwapondaponda wenye nguvu nyingi
na kuwaweka wengine mahali pao.
34:25 Ay 11:11; Mit 5:21-23Kwa sababu huyaangalia matendo yao yote,
huwaondoa usiku, nao wakaangamia.
34:26 Mwa 6:5; Ay 8:22; 28:24; Za 9:5; Yer 44:5Anawaadhibu kwa ajili ya uovu wao
mahali ambapo kila mmoja ataweza kuwaona,
34:27 Za 14:3; Isa 5:12; 1Sam 15:11kwa sababu wameacha kumfuata Mungu,
nao hawakuiheshimu njia yake hata moja.
34:28 Kut 22:23; Yak 5:4; Mhu 5:8Wamesababisha kilio cha maskini kifike mbele zake,
hivyo akasikia kilio cha wahitaji.
34:29 Za 28:1; 83:1; 109:1; Rum 8:34; Za 13:1; 97:9; 83:18Lakini kama akinyamaza kimya,
ni nani awezaye kumhukumu?
Kama akiuficha uso wake,
ni nani awezaye kumwona?
Ikiwa ni taifa au mtu mmoja, kwake ni sawa,
34:30 Za 25:15; Mit 29:2-12; 1Fal 12:28-30ili kumzuia mtu mwovu kutawala,
au wale ambao huwategea watu mitego.
“Kama mwanadamu akimwambia Mungu,
‘Nimekosa lakini sitatenda dhambi tena.
34:32 Kut 33:13; Za 27:11; Lk 19:8; Ay 33:27Nifundishe nisichoweza kuona;
kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’
34:33 Mit 17:23; Yn 3:8Je basi, Mungu atakulipa kwa masharti yako,
wakati wewe umekataa kutubu?
Yakupasa wewe uamue, wala si mimi;
sasa niambie lile ulijualo.
“Wanadamu wenye ufahamu husema,
wenye hekima wanaonisikia huniambia,
34:35 Ay 35:16; 38:2; 42:3; 26:3‘Ayubu huongea bila maarifa;
maneno yake hayana busara.’
34:36 Ay 6:29; 22:15Laiti Ayubu angejaribiwa hadi kikomo cha mwisho,
kwa sababu anajibu kama mtu mwovu!
Kwenye dhambi yake huongeza uasi;
kwa dharau hupiga makofi miongoni mwetu,
na kuzidisha maneno yake dhidi ya Mungu.”