Ayubu 30:1-31, Ayubu 31:1-40, Ayubu 32:1-22 NEN

Ayubu 30:1-31

30:1 Ay 12:4; Za 119:21“Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki,

watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau

kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo.

Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu,

kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia?

30:3 Isa 8:21; Ay 24:5; Yer 17:6Wakiwa wamekonda kutokana na kupungukiwa na kwa njaa,

walizurura usiku katika nchi kame iliyo ukiwa.

30:4 Ay 39:6; 1Fal 19:4Katika vichaka walikusanya mimea ya chumvi,

nacho chakula chao kilikuwa mizizi ya mti wa mfagio.

Walifukuzwa mbali na watu wao,

wakipigiwa kelele kama wevi.

30:6 Isa 2:19; Hos 10:8Walilazimika kuishi katika mikondo ya vijito vilivyokauka,

kwenye majabali na mahandaki.

30:7 Ay 6:5; 39:5-6Kwenye vichaka walilia kama punda,

na walijisongasonga pamoja kwenye vichaka.

30:8 Amu 9:4; Ay 18:18Wao ni watoto wa wapumbavu wenye asili ya ubaya,

waliofukuzwa watoke katika nchi.

30:9 Ay 16:10; 12:4; Za 69:11; Mao 3:14; Ay 16:10; Za 69:11; Ay 12:4; Mao 3:14, 63; Ay 17:6“Nao sasa wana wao wananidhihaki katika nyimbo;

nimekuwa kitu cha dhihaka kwao.

30:10 Hes 12:14; Mt 26:67Wananichukia sana na kujitenga nami,

wala hawasiti kunitemea mate usoni.

30:11 Mwa 12:17; Rut 1:21; Ay 41:13; Za 32:9Sasa kwa kuwa Mungu ameilegeza kamba ya upinde wangu na kunitesa,

wamekuwa huru kunitendea waonavyo.

30:12 Za 109:6; Zek 3:1; Za 140:4-5; Ay 16:10Kuume kwangu kundi linashambulia;

wao huitegea miguu yangu tanzi,

na kunizingira.

30:13 Isa 3:12; Za 69:26Huizuia njia yangu,

nao hufanikiwa katika kuniletea maafa,

nami sina yeyote wa kunisaidia.

Wananijia kama watu wapitao katika ufa mpana;

katikati ya magofu huja na kunishambulia.

30:15 Kut 3:6; Za 55:4-5; Hos 13:3; Ay 3:25Vitisho vimenifunika;

heshima yangu imetoweshwa kama kwa upepo,

salama yangu imetoweka kama wingu.

30:16 Za 22:14; Isa 53:12“Sasa maisha yangu yamefikia mwisho;

siku za mateso zimenikamata.

Usiku mifupa yangu inachoma;

maumivu yanayonitafuna hayatulii kamwe.

Kwa uwezo wake mkuu Mungu huwa kwangu kama nguo;

hushikamana nami kama ukosi wa vazi langu.

30:19 Za 40:2; Yer 38:6, 22Yeye amenitupa kwenye matope,

nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.

30:20 Ay 19:7; Mao 3:8; Mt 15:23“Ee Bwana, ninakulilia wewe lakini hunijibu;

ninasimama, nawe unanitazama tu.

30:21 Ay 19:6; Yer 6:23; Isa 9:12; Eze 6:14; Ay 10:3Wewe unanigeukia bila huruma;

unanishambulia kwa nguvu za mkono wako.

30:22 Ay 27:21; 9:17; Yud 12Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo;

umenirusha huku na huko kwenye dhoruba kali.

30:23 2Sam 14:14; Ay 3:19; 10:8Ninajua utanileta mpaka kifoni,

mahali ambapo wenye uhai wote wamewekewa.

“Hakika hakuna yeyote amshambuliaye mhitaji,

anapoomba msaada katika shida yake.

30:25 Za 35:13-14; Rum 12:15; Yn 11:35Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu?

Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini?

30:26 Za 82:5; Yer 8:15Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia;

nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja.

30:27 Za 38:8; Mao 2:11Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii;

siku za mateso zinanikabili.

30:28 Mao 4:8; Za 38:6; Ay 19:7; 24:12Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua;

ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada.

30:29 Isa 34:13; Yer 9:11; Za 102:6; Mik 1:8Nimekuwa ndugu wa mbweha,

rafiki wa mabundi.

30:30 Mao 3:4; 4:8; 5:10; Kum 28:35Ngozi yangu imekuwa nyeusi nayo inachunika;

mifupa yangu inaungua kwa homa.

30:31 Mwa 8:8; Za 137:2Kinubi changu kimegeuka kuwa maombolezo,

nayo filimbi yangu imekuwa sauti ya kilio.

Read More of Ayubu 30

Ayubu 31:1-40

31:1 Kum 5:18; Mt 5:18“Nimefanya agano na macho yangu

yasimtazame msichana kwa kumtamani.

31:2 Ay 16:19; 20:29Kwa kuwa fungu la mwanadamu ni gani kutoka kwa Mungu juu,

urithi wake kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu Aliye juu?

31:3 Ay 21:30; 34:22; Rum 2:9Je, si uharibifu kwa watu waovu,

maangamizi kwa wale watendao mabaya?

31:4 2Nya 16:9; Mit 5:21; Yer 32:19; Dan 4:37Je, yeye hazioni njia zangu

na kuihesabu kila hatua yangu?

31:5 Ay 15:31; Mik 2:11“Kama nimeishi katika uongo

au mguu wangu umekimbilia udanganyifu,

31:6 Law 19:36; Ay 6:2Mungu na anipime katika mizani za uaminifu,

naye atajua kwamba sina hatia:

31:7 Ay 9:30; Hes 15:39; Eze 6:9; Mt 5:29; Mhu 11:9kama hatua zangu zimepotoka kutoka kwenye njia,

kama moyo wangu umeongozwa na macho yangu,

au kama mikono yangu imetiwa unajisi,

31:8 Law 26:16; Yn 4:37; Mik 6:15basi wengine na wale nilichokipanda,

nayo yale yote niliyootesha na yangʼolewe.

31:9 Kum 11:16; Yak 1:14“Kama moyo wangu umeshawishiwa na mwanamke,

au kama nimevizia mlangoni mwa jirani yangu,

31:10 Kum 28:30; Yer 8:16; Mit 14:31basi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine,

nao wanaume wengine walale naye.

31:11 Law 20:10; Yn 8:4-5Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu,

naam, dhambi ya kuhukumiwa.

31:12 Ay 15:30; 26:6Ni moto uwakao kwa Uharibifu;31:12 Kwa Kiebrania ni Abadon (Ay 26:6; Mit 15:11).

ungekuwa umengʼoa mavuno yangu.

31:13 Kut 21:2-11; Law 25:39-46“Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu,

walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu,

31:14 Ay 33:5; Hos 9:7; Za 10:13, 15; Isa 10:3; Yer 5:31nitafanya nini Mungu atakaponikabili?

Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu?

31:15 Ay 10:3; Efe 6:9Je, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu,

si ndiye aliwaumba?

Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sote

ndani ya mama zetu?

31:16 Law 25:17; Ay 20:19; Yak 1:27“Ikiwa nimewanyima maskini haja zao,

au kuyaacha macho ya wajane yadhoofike,

31:17 Ay 6:27; 29:12kama nimekula chakula changu mwenyewe,

bila kuwashirikisha yatima;

31:18 Isa 51:18lakini tangu ujana wangu nimemlea yatima kama ambavyo baba angefanya,

nami tangu kuzaliwa kwangu nimewaongoza wajane:

31:19 Ay 22:6; 24:4; Isa 58:7kama nilimwona yeyote akiteseka kwa kukosa nguo,

au mtu mhitaji asiye na mavazi

31:20 Ay 29:13; Amu 6:37ambaye wala moyo wake haukunibariki

kwa kumpatia joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo zangu,

31:21 Ay 22:7-9; Yak 1:27na kama nimeinua mkono wangu dhidi ya yatima,

nikijua kuwa nina ushawishi mahakamani,

31:22 Hes 15:30; Za 10:15basi mkono wangu na unyofoke toka begani mwangu,

nao na uvunjike kutoka kiungio chake.

31:23 Ay 10:3; 13:11; Mwa 20:11Kwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu,

nami kwa kuuogopa utukufu wake sikuweza kufanya mambo kama hayo.

31:24 Ay 22:25; Mk 10:24; Lk 12:15“Kama nimeweka tumaini langu kwenye dhahabu,

au kuiambia dhahabu safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’

31:25 Mwa 12:16; Isa 10:14kama nimefurahia wingi wa utajiri wangu,

ustawi ambao mikono yangu ilikuwa imepata,

31:26 Hes 11:20; Kum 4:19; Eze 8:16kama nimelitazama jua katika kungʼaa kwake

au mwezi ukienda kwa fahari yake,

31:27 Ay 24:15; Yak 1:14; Yer 8:2; 16:11hivyo moyo wangu kushawishiwa kwa siri,

au kubusu mkono wangu kwa kuviheshimu,

31:28 Mwa 38:24; Kum 17:2-7; Yos 24:23-27; Mit 30:9basi hiyo pia ingekuwa dhambi ya kuhukumiwa,

kwa kuwa ningekuwa si mwaminifu kwa Mungu aishiye juu sana.

31:29 Za 35:15; Mt 5:44; Mit 17:5; 24:17-18“Kama nimeshangilia msiba wa adui yangu,

au kutazama kwa furaha taabu iliyomjia,

lakini sikuruhusu kinywa changu kufanya dhambi

kwa kuomba laana dhidi ya maisha yake;

kama watu wa nyumbani mwangu kamwe hawakusema,

‘Ni nani ambaye hajashibishwa na nyama ya Ayubu?’

31:32 Amu 19:20; Mt 25:35; Ebr 13:2; 1Pet 4:9Lakini hakuna mgeni aliyelala njiani,

kwa maana mlango wangu ulikuwa wazi kwa msafiri;

31:33 Za 32:5; Mit 28:13; Mwa 3:8kama nimeifunika dhambi yangu kama wanadamu wengine wafanyavyo,

kwa kuficha hatia yangu moyoni mwangu,

31:34 Kut 23:2; Mit 29:25kwa sababu ya kuogopa umati wa watu,

na hivyo kuwa na hofu ya kudharauliwa na jamaa,

nikanyamaza kimya nisitoke nje ya mlango:

(“Laiti kama angekuwepo mtu wa kunisikia!

Tazama sasa ninatia sahihi kwenye utetezi wangu:

Mwenyezi na anijibu;

mshtaki wangu na aweke mashtaka yake kwenye maandishi.

Hakika ningeyavaa begani mwangu,

ningeyavaa kama taji.

31:37 Ay 1:3; 21:28Ningempa hesabu ya kila hatua yangu,

ningemwendea kama mwana wa mfalme.)

31:38 Mwa 4:10“Kama nchi yangu inalia dhidi yangu,

na mifereji yake yote imelowana kwa machozi,

31:39 1Fal 21:19; Law 19:13; Yak 5:4kama nimekula mazao yake bila malipo,

au kuvunja mioyo ya wapangaji wake,

31:40 Mwa 3:18; Mit 13:7basi miiba na iote badala ya ngano,

na magugu badala ya shayiri.”

Mwisho wa maneno ya Ayubu.

Read More of Ayubu 31

Ayubu 32:1-22

Sehemu Ya Tatu: Mazungumzo Ya Elihu

(Ayubu 32–37)

Elihu Awakemea Rafiki Za Ayubu

32:1 Ay 2:3; 10:7Basi watu hawa watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa kuwa alikuwa mwadilifu machoni pake mwenyewe. 32:2 Mwa 22:21; Ay 13:19; 35:2Lakini Elihu mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi wa jamaa ya Ramu, akamkasirikia sana Ayubu, kwa sababu ya kujihesabia haki mwenyewe badala ya Mungu. 32:3 Ay 42:7; 32:12-13; 15:13Pia aliwakasirikia hao rafiki watatu wa Ayubu, kwa sababu hawakuweza kupata njia ya kuthibitisha ya kuwa hayo maneno ya Ayubu hayakuwa ya kweli, nao bado walikuwa wamemlaumu. 32:4 Law 19:32Basi Elihu alikuwa amesubiri kwanza waongee na Ayubu kwa sababu walikuwa na umri mkubwa kumliko yeye. Lakini alipoona watu hao watatu hawakuwa na kitu zaidi cha kusema, hasira yake ikaamka.

32:6 Ay 15:10Basi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema:

“Mimi ni mdogo kwa umri,

nanyi ni wazee;

ndiyo sababu niliogopa,

sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua.

32:7 1Nya 29:15; 2Nya 10:6Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme,

nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’

32:8 Ay 27:3; 33:4; Mit 2:6; 1Fal 3:9Lakini ni Roho iliyoko ndani ya mwanadamu,

pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo yeye ufahamu.

32:9 1Kor 1:21-26Sio wazee peke yao walio na hekima,

sio wenye umri mkubwa peke yao wanaofahamu lililo sawa.

32:10 Ay 33:1; 31:33; Za 34:11; Ay 5:27“Kwa hiyo nasema: Nisikilizeni mimi;

mimi nami nitawaambia lile ninalojua.

Nilingojea mlipokuwa mnaongea,

nilizisikiliza hoja zenu;

mlipokuwa mkitafuta maneno ya kusema,

32:12 Ay 32:3niliwasikiliza kwa makini.

Lakini hakuna hata mmoja wenu

aliyethibitisha kwamba Ayubu amekosa;

hakuna hata mmoja wenu

aliyeweza kujibu hoja zake.

32:13 Mhu 9:11; Yer 9:23Msiseme, ‘Tumepata hekima;

Mungu na amthibitishe kuwa mwongo,

wala si mwanadamu.’

32:14 Ay 23:4Lakini Ayubu hajayapanga maneno yake dhidi yangu,

nami sitamjibu kwa kutumia hoja zenu.

32:15 Ay 32:1“Wametiwa hofu na hawana la zaidi la kusema;

maneno yamewaishia.

Je, ningoje sasa kwa sababu wamekuwa kimya,

kwa vile sasa wanasimama bila kuwa na la kujibu?

32:17 Ay 5:27; 33:3; 36:4Mimi nami nitakuwa na la kusema;

mimi nami nitasema lile nilijualo.

32:18 Mdo 4:20; 1Kor 9:16; 2Kor 5:14Kwa kuwa nimejawa na maneno,

nayo Roho iliyomo ndani yangu yanisukuma;

32:19 Yer 20:9; Amo 3:8; Mt 9:17ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai,

kama kiriba kipya cha divai kilicho tayari kupasuka.

32:20 Ay 4:2; Yer 6:11Ni lazima niseme ili niweze kutulia;

ni lazima nifumbue midomo yangu nipate kujibu.

32:21 Law 19:15; 2Nya 19:7; Mt 22:16Sitampendelea mtu yeyote,

wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote;

32:22 Ay 4:17; 9:9; Za 12:2-4kwa kuwa kama ningekuwa stadi wa kujipendekeza,

Muumba wangu angeniondolea mbali kwa upesi.

Read More of Ayubu 32