Ayubu 15:1-35
Elifazi Anaongea: Ayubu Anadhoofisha Imani
15:1 Ay 4:1Kisha Elifazi Mtemani akajibu:
15:2 Mwa 41:6; Ay 6:26“Je, mtu mwenye hekima hujibu kwa mawazo matupu,
au kujaza tumbo lake kwa upepo wenye joto wa mashariki?
15:3 Neh 4:2-3; Ay 6:26Je, aweza kubishana juu ya maneno yasiyofaa,
kwa hotuba zisizo na maana?
15:4 Ay 25:6Lakini unadhoofisha hata uchaji wa Mungu
na kuzuia ibada mbele za Mungu.
15:5 Ay 11:6; 22:5; 5:13; Mt 16:23Dhambi yako inasukuma kinywa chako,
nawe umechagua ulimi wa hila.
15:6 Za 10:2; Mt 12:37; Lk 19:22; Ay 7:15; 18:7Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si changu;
midomo yako mwenyewe inashuhudia dhidi yako.
15:7 Ay 38:21; 1Sam 2:8; Mit 8:25; Za 90:2“Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa?
Ulizaliwa kabla ya vilima?
15:8 Yer 23:18; 1Kor 2:11Je, wewe husikiliza mashauri ya siri ya Mungu?
Je, wewe unaizuia hekima iwe yako mwenyewe?
15:9 Ay 12:3Wewe unajua kitu gani tusichokijua sisi?
Unafahamu kitu gani tusichokifahamu sisi?
15:10 Ay 12:12; 32:6-7; 8:8-10Wale wenye mvi na wazee wako upande wetu,
watu ambao ni wazee hata kuliko baba yako.
15:11 Mwa 37:35; 2Kor 1:3-4; Kum 8:3; Yer 15:16Je, faraja za Mungu hazikutoshi,
au maneno yaliyosemwa kwako kwa upole si kitu?
15:12 Ay 11:13; 36:13Kwa nini moyo wako unakudanganya,
na kwa nini macho yako yanangʼaa,
15:13 Mit 29:11; Dan 11:30; Za 94:4; Ay 11:8; 22:5; 30:2ili kwamba upate kutoa hasira yako dhidi ya Mungu,
na kumwaga maneno kama hayo kutoka kinywani mwako?
15:14 Ay 14:1; 4:17; 2Nya 6:36; Mhu 7:18, 20“Mwanadamu ni kitu gani, hata aweze kuwa safi,
au yeye aliyezaliwa na mwanamke, hata aweze kuwa mwadilifu?
15:15 Ay 5:1; 4:18Kama Mungu hawaamini watakatifu wake,
kama hata mbingu zenyewe si safi machoni pake,
15:16 Law 5:2; Ay 12:4; 20:12; Mit 19:28; Za 14:1sembuse mwanadamu ambaye ni mwovu na mpotovu,
ambaye hunywa uovu kama anywavyo maji!
15:17 Ay 4:8“Nisikilize mimi nami nitakueleza,
acha nikuambie yale niliyoyaona,
15:18 Kum 32:7; Ay 8:8; Mwa 18:19ambayo watu wenye hekima wameyanena,
bila kuficha lolote walilopokea toka kwa baba zao
15:19 Mwa 12:1; Ay 22:8(wakati ambao wao peke yao ndio walipewa nchi,
hakuna mgeni aliyepita miongoni mwao):
15:20 Oba 1:15; Sef 1:17Mtu mwovu siku zake zote hupata mateso,
miaka yote aliwekewa mkorofi.
15:21 1Sam 3:11; Yer 6:25; Isa 13:3; 1The 5:3Sauti za kutisha hujaa masikioni mwake;
katika kufanikiwa kwake, wanyangʼanyi humshambulia.
15:22 Hos 9:13; Amo 5:19Hukata tamaa kuokoka gizani;
amewekwa kwa ajili ya upanga.
15:23 Za 59:15; 109:10; Ay 18:12Hutangatanga, akitafuta chakula;
anajua kwamba siku ya giza iko karibu.
15:24 Isa 8:22; 9:1; Ay 15:20; 18:14Taabu na maumivu makuu vinamtia hofu;
humshinda kama mfalme aliye tayari kwa vita,
15:25 Za 2:2-3; Mit 21:30kwa sababu amemkunjia Mungu ngumi yake
na kujigamba dhidi ya Mwenyezi,
15:26 Yer 44:16kwa kiburi akishambulia dhidi ya Mungu
akiwa na ngao nene, iliyo imara.
15:27 Amu 3:17; Za 17:10“Ingawa uso wake umefunikwa na mafuta kwa unene
na kiuno chake kimevimba kwa kunenepa,
15:28 Isa 5:9; Ay 3:14ataishi katika miji ya magofu,
na katika nyumba ambazo haziishi mwanadamu yeyote,
nyumba zinazokuwa vifusi.
15:29 Ay 3:15; 7:8; Isa 5:8Hatatajirika tena, nao utajiri wake hautadumu,
wala mali zake hazitakuwa nyingi juu ya nchi.
15:30 Ay 4:9, 15; 16:7; 20:26; Kut 15:10Hatatoka gizani;
mwali wa moto utanyausha machipukizi yake,
nayo pumzi ya kinywa cha Mungu itamwondolea mbali.
15:31 Yer 7:4-8; Mt 6:19; Za 62:1015:31 Ay 31:5; Mit 1:16; 6:18; Isa 44:20; 59:7; Mik 2:11; Mk 13:5Asijidanganye mwenyewe kutumainia ubatili,
kwa kuwa hatapata malipo yoyote.
15:32 Mhu 7:17; Za 109:8; Mit 10:27; Ay 18:16Atakuwa amelipwa kikamilifu kabla ya wakati wake,
nayo matawi yake hayatastawi.
15:33 Hab 3:17Atafanana na mzabibu uliopukutishwa matunda yake kabla hayajaiva,
kama mzeituni unaodondosha maua yake.
15:34 Kut 23:8; Ay 8:22; Isa 33:14Kwa kuwa jamii ya wasiomcha Mungu watakuwa tasa,
nao moto utateketeza hema za wale wanaopenda rushwa.
15:35 Hos 10:13; Gal 6:7; Za 7:14Hutunga mimba ya madhara na kuzaa uovu;
matumbo yao huumba udanganyifu.”
Ayubu 16:1-22
Hotuba Ya Tano Ya Ayubu
Ayubu Anathibitisha Tena Hali Yake Ya Kutokuwa Na Hatia
Kisha Ayubu akajibu:
16:2 Ay 6:15; 13:4; Za 69:20“Nimepata kusikia mambo mengi kama haya,
nanyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha!
16:3 Ay 6:26; 11:2; 18:2Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho?
Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno?
16:4 Mt 27:29; Yer 18:16; Mao 2:15Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi,
kama mngekuwa katika hali yangu;
ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu,
na kuwatikisia ninyi kichwa changu.
16:5 Ay 29:25; Mwa 37:35Lakini kinywa changu kingewatia moyo;
faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu.
16:6 Ay 6:3; 7:21“Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi;
nami kama nikijizuia, wala hayaondoki.
16:7 Amu 8:5; Ay 7:3; 1:19Ee Mungu, hakika umenichakaza;
umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote.
16:8 Mao 5:17; Ay 10:17; 17:7; 19:20; Za 22:17; 88:9; 6:7Umenikunjakunja, nalo limekuwa ushahidi;
nako kukonda kwangu kumeongezeka sana na kushuhudia dhidi yangu.
16:9 Ay 12:14; 13:24; Mao 2:16; Mdo 7:54; Hos 6:1; Ay 30:21; 9:5; 18:4; 19:11Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake,
na kunisagia meno yake;
adui yangu hunikazia macho yake makali.
16:10 Za 22:13; Mao 3:30; Mdo 7:57; 23:2; Za 27:3; Mik 5:1Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki;
hunipiga shavuni mwangu kwa dharau,
na kuungana pamoja dhidi yangu.
16:11 Ay 9:24Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya,
na kunitupa katika makucha ya waovu.
16:12 Ay 9:17; 6:4; Mao 3:12Mambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja;
amenikamata shingo na kuniponda.
Amenifanya mimi kuwa shabaha yake;
16:13 Mit 7:23; Mao 3:13wapiga upinde wake wananizunguka.
Bila huruma, huchoma figo zangu,
na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi.
16:14 Ay 9:17; 10:3; Yoe 2:7Huniponda tena na tena;
hunishambulia kama shujaa wa vita.
16:15 Mwa 37:34; Ay 2:8“Nimejishonea nguo ya gunia juu ya mwili wangu
nami nimekizika kipaji cha uso wangu kwenye vumbi.
16:16 Ay 16:20; 2:7; 17:7; 30:17, 30; Isa 52:14; Za 6:6Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia,
macho yangu yamepigwa na giza kuu.
16:17 Yer 18:11; Yon 3:8Hata hivyo mikono yangu haijafanya jeuri,
na maombi yangu ni safi.
16:18 Mwa 4:10; Ay 27:9; Isa 26:21; Za 66:18-19; Ebr 11:4“Ee nchi, usiifunike damu yangu,
nacho kilio changu kisinyamazishwe kamwe.
16:19 Mwa 31:50; Rum 1:9; 1The 2:5; Ay 22:12; 19:27; Za 113:5; Isa 33:5Hata sasa shahidi wangu yuko mbinguni;
wakili wangu yuko juu.
16:20 Mao 2:19; Rum 8:34; Yn 15:15; Ay 16:16Mwombezi wangu ni rafiki yangu
macho yangu yamwagapo machozi kwa Mungu;
16:21 1Fal 8:45; Za 140:12kwa niaba ya mtu anamsihi Mungu
kama mtu anavyosihi kwa ajili ya rafiki yake.
16:22 Ay 10:21; Mhu 12:5“Ni miaka michache tu itapita
kabla sijaenda safari ambayo sitarudi.
Ayubu 17:1-16
17:1 Za 88:3-4; Mhu 12:1-7Moyo wangu umevunjika,
siku zangu zimefupishwa,
kaburi linaningojea.
17:2 1Sam 1:6-7; Ay 11:3Hakika wenye mizaha wamenizunguka;
macho yangu yamebaki kutazama uadui wao.
Ayubu Anaomba Msaada
17:3 Za 35:27; 40:17; Mit 6:1; Isa 38:14“Ee Mungu, nipe dhamana unayodai.
Ni nani mwingine atakayeweka dhamana kwa ajili yangu?
17:4 Ay 12:12Umezifunga akili zao zisipate ufahamu,
kwa hiyo hutawaacha wapate ushindi.
17:5 Kut 22:15; Ay 11:20Kama mtu akiwashutumu rafiki zake ili apate ujira,
macho ya watoto wake yatashindwa kuona.
17:6 1Fal 9:7; Yer 15:4“Mungu amenifanya kitu cha dhihaka kwa kila mtu,
mtu ambaye watu humtemea mate usoni.
17:7 Ay 16:8; 2:12; 16:16Macho yangu yamefifia kwa ajili ya majonzi;
umbile langu lote ni kama kivuli.
17:8 Kut 4:14; Ay 22:19Watu wanyofu wanatishwa na hili;
watu wasio na hatia wanasimama dhidi ya wasiomcha Mungu.
17:9 Mit 4:18; 2Sam 22:21; Ay 22:30Hata hivyo, waadilifu watazishika njia zao,
nao wale wenye mikono safi wataendelea kupata nguvu.
17:10 Ay 12:3“Lakini ninyi njooni, ninyi nyote, jaribuni tena!
Sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu.
17:11 Ay 17:15; Isa 38:10; Ay 7:6Siku zangu zimepita, mipango yangu imevunjika,
vivyo hivyo shauku za moyo wangu.
17:12 Isa 50:11; Ay 5:17-26; 11:17Watu hawa hufanya usiku kuwa mchana,
kwenye giza wao husema, ‘Mwanga u karibu.’
17:13 2Sam 14:14; Ay 3:13; Za 139:8; 88:18Kama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi,17:13 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
kama nikikitandika kitanda changu gizani,
17:14 Ay 13:28; 30:28, 30; 4:19; 7:5; Za 16:10; 49:9; 17:15; Ay 7:6; Za 31:23; Mao 3:18; Eze 37:11kama nikiuambia uharibifu, ‘Wewe u baba yangu,’
na kuliambia buu, ‘Wewe u mama yangu’ au ‘Dada yangu,’
liko wapi basi tarajio langu?
Ni nani awezaye kuona tarajio lolote kwa ajili yangu?
17:16 Mwa 2:7; Yon 2:6; Ay 3:17Je, litashuka chini hadi kwenye malango ya mauti?17:16 Malango ya mauti hapa ina maana ya Kuzimu.
Je, tutashuka pamoja mavumbini?”
Ayubu 18:1-21
Bildadi Anasema: Mungu Huwaadhibu Waovu
18:1 Ay 8:1Bildadi Mshuhi akajibu:
18:2 Ay 8:2; 16:3“Je, ni lini utafika mwisho wa maneno haya?
Uwe mwenye busara, nasi ndipo tutakapoweza kuongea.
18:3 Za 73:22; Ay 12:7Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama,
na kuonekana wajinga machoni pako?
18:4 Ay 13:14; 16:9; 14:18Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande
katika hasira yako,
je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe?
Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake?
18:5 Yer 25:10; Yn 8:12; Mit 13:9“Taa ya mwovu imezimwa,
nao mwali wa moto wake umezimika.
18:6 Ay 8:22; 5:14; 11:17; 12:25Mwanga hemani mwake umekuwa giza;
taa iliyo karibu naye imezimika.
18:7 Za 18:36; Mit 4:12; Ay 5:13; 15:6Nguvu za hatua zake zimedhoofishwa;
shauri lake baya litamwangusha.
18:8 Mik 7:2; Hab 1:15Miguu yake imemsukumia kwenye wavu,
naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu.
18:9 Ay 22:10; 30:12; Isa 24:18; Yer 48:44; Amo 5:14; Mit 7:22Tanzi litamkamata kwenye kisigino;
mtego utamshikilia kwa nguvu.
18:10 Mit 7:22; Isa 51:20; 1Sam 28:9; Za 140:5Kitanzi kimefichwa ardhini kwa ajili yake;
mtego uko kwenye njia yake.
18:11 Ay 15:21; 20:8; Za 31:13; Isa 22:18; Yer 6:25Vitisho vimemtia hofu kila upande,
na adui zake humwandama kila hatua.
18:12 Isa 9:20; 65:13; 8:21; Ay 21:17; 31:3; 15:25Janga linamwonea shauku;
maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo.
18:13 Zek 14:12; Hes 12:12Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake;
mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake.
18:14 Ay 8:22; 15:24; 18:11Atangʼolewa kutoka usalama wa hema lake,
na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.
18:15 Mwa 19:24; Za 11:6; Ay 18:18; 20:26Moto utakaa katika hema lake;
moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake.
18:16 Hos 5:12; Amo 2:9; Mwa 27:28Mizizi yake chini itakauka
na matawi yake juu yatanyauka.
18:17 Mit 2:22; 10:7; Isa 49:15; Kum 32:26; 9:14; Za 9:5; 69:28Kumbukumbu lake litatoweka katika dunia,
wala hatakuwa na jina katika nchi.
18:18 Ay 5:14; 18:11; 11:20; 30:8Ameondolewa nuruni na kusukumiwa gizani,
naye amefukuzwa mbali atoke duniani.
18:19 Za 37:28; 21:10; Isa 14:22; Ay 27:14-15Hana mtoto wala mzao miongoni mwa watu wake,
wala aliyenusurika mahali alipoishi.
18:20 Yer 46:21; Eze 7:7Watu wa magharibi watashangaa yaliyompata;
watu wa mashariki watapatwa na hofu.
18:21 Ay 21:28; Yer 9:3; 1The 4:5Hakika ndivyo yalivyo makao ya mtu mwovu;
ndivyo palivyo mahali pake mtu asiyemjua Mungu.”