Ayubu 11:1-20, Ayubu 12:1-25, Ayubu 13:1-28, Ayubu 14:1-22 NEN

Ayubu 11:1-20

Sofari Anasema: Hatia Ya Ayubu Inastahili Adhabu

11:1 Ay 2:11Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu:

11:2 Ay 8:2; 16:3; Mwa 41:6“Je, maneno haya yote yapite bila kujibiwa?

Je, huyu mnenaji athibitishwe kuwa na haki?

11:3 Efe 4:29; 5:4; Ay 12:4; 16:10; 17:2; 21:3Je, maneno yako ya upuzi yawafanye watu wanyamaze kimya?

Je, mtu asikukemee unapofanya dhihaka?

11:4 Ay 6:10; 9:21; 10:7; 1Pet 3:15Unamwambia Mungu, ‘Imani yangu ni kamili

nami ni safi mbele zako.’

Aha! Laiti kwamba Mungu angesema,

kwamba angefungua midomo yake dhidi yako,

11:6 Ay 9:4; 1Kor 2:10; Mao 3:22; Ezr 9:13naye akufunulie siri za hekima,

kwa kuwa hekima ya kweli ina pande mbili.

Ujue hili: Mungu amesahau hata baadhi ya dhambi zako.

11:7 Mhu 3:11; Rum 11:33; Isa 40:28; Ay 5:9; Mt 11:27; Efe 3:8“Je, waweza kujua siri za Mungu?

Je, waweza kuyachunguza mambo yote kumhusu Mwenyezi?

11:8 Za 57:10; Isa 55:9; Efe 3:18; Mwa 15:5; Ay 22:12; 25:2; Za 57:10; 139:8; Isa 55:9; Ay 7:9; 15:13, 25; 33:13; 40:2Ni juu mno kuliko mbingu: waweza kufanya nini?

Kina chake ni kirefu kuliko kuzimu:

wewe waweza kujua nini?

11:9 Efe 3:19-20; Ay 22:12; 35:5; 36:26; 37:5, 23; Isa 40:26Kipimo chake ni kirefu kuliko dunia,

nacho ni kipana kuliko bahari.

11:10 Ay 9:12; Ufu 3:7“Kama akija na kukufunga gerezani,

na kuitisha mahakama, ni nani awezaye kumpinga?

11:11 Ay 10:4; 31:37; 34:11, 25; 36:7; Za 10:14Hakika anawatambua watu wadanganyifu;

naye aonapo uovu, je, haangalii?

11:12 Mwa 12:16; 2Nya 6:36Mpumbavu aweza kuwa mwenye hekima,

endapo mtoto wa punda-mwitu atazaliwa mwanadamu.

11:13 1Sam 7:3; Za 78:8; 88:9; Kut 9:29; Ay 5:8, 27“Hata sasa ukiutoa moyo wako kwake

na kumwinulia mikono yako,

11:14 Yos 24:14; Za 101:4; 22:23ukiiondolea mbali ile dhambi iliyo mkononi mwako

wala usiuruhusu uovu ukae hemani mwako,

11:15 Ay 22:26; 1Yn 3:21; 1Tim 2:8; 1Sam 2:9; Za 20:8; 37:23; 40:2; Efe 6:14; Mwa 4:7ndipo utainua uso wako bila aibu;

utasimama imara bila hofu.

11:16 Isa 26:16; 37:3; 65:16; Eze 21:7; Yos 7:5; Za 58:7; 112:10; Ay 22:11Hakika utaisahau taabu yako,

utaikumbuka tu kama maji yaliyokwisha kupita.

11:17 Ay 22:28; Za 37:6; Isa 58:8, 10; 62:1; Ay 17:12; Za 18:28Maisha yako yatangʼaa kuliko adhuhuri,

nalo giza litakuwa kama alfajiri.

11:18 Mhu 5:12; Isa 11:10; Zek 3:10; Za 127:2Utakuwa salama, kwa kuwa lipo tumaini;

utatazama pande zote na kupumzika kwa salama.

11:19 Law 26:6; Isa 45:14Utalala, wala hakuna atakayekuogofya,

naam, wengi watajipendekeza kwako.

11:20 Kum 28:65; Yer 11:11; Amo 2:14; Ay 8:13; 17:5Bali macho ya waovu hayataona,

wokovu utawaepuka;

tarajio lao litakuwa ni hangaiko

la mtu anayekata roho.”

Read More of Ayubu 11

Ayubu 12:1-25

Hotuba Ya Nne Ya Ayubu

Ayubu Anajibu: Mimi Ni Mtu Wa Kuchekwa

Ndipo Ayubu akajibu:

12:2 Ay 15:8; 17:10“Bila shaka ninyi ndio watu,

nayo hekima itakoma mtakapokufa!

12:3 Ay 13:2; 15:9Lakini mimi ninao ufahamu kama ninyi;

mimi si duni kwenu.

Ni nani asiyejua mambo haya yote?

12:4 Mwa 6:9; 38:23; Ay 21:3; 15:16; Za 91:15“Nimekuwa mtu wa kuchekwa na rafiki zangu,

ingawa nilimwita Mungu naye akanijibu:

mimi ni mtu wa kuchekwa tu,

ingawa ni mwadilifu na nisiye na hatia!

12:5 Za 123:4; 17:5; 37:31; 38:16; 66:9; 73:2; 94:18; Mit 14:2Wanadamu wakiwa katika utulivu huwa na dharau kwa wale wenye msiba

kana kwamba ndiyo haki ya wale ambao miguu yao inateleza.

12:6 Ay 5:24; 22:18; 9:24Hema za wanyangʼanyi hazisumbuliwi,

wale wanaomghadhibisha Mungu wako salama:

wale wamchukuao mungu wao mikononi mwao.

12:7 Ay 35:11; 18:3; Mt 6:26; Rum 1:20“Lakini ulizeni wanyama, nao watawafundisha,

au ndege wa angani, nao watawaambia;

au zungumzeni na dunia, nayo itawafundisha,

au acheni samaki wa baharini wawape taarifa.

12:9 Isa 41:20; 1:3; Ay 9:24Ni nani miongoni mwa hawa wote asiyejua

kwamba mkono wa Bwana ndio uliofanya hili?

12:10 Hes 16:22; Mdo 17:28; Dan 5:23Mkononi mwake kuna uhai wa kila kiumbe,

na pumzi ya wanadamu wote.

12:11 Ay 34:3Je, sikio haliyajaribu maneno

kama vile ulimi uonjavyo chakula?

12:12 1Fal 4:2; Ay 15:10; 17:4; 32:7, 9; 34:4, 10Je, hekima haipatikani katikati ya wazee?

Je, maisha marefu hayaleti ufahamu?

12:13 Mit 21:30; Isa 45:9; Yer 32:19; 1Kor 1:24; Dan 1:17“Hekima na nguvu ni vya Mungu;

shauri na ufahamu ni vyake yeye.

12:14 Ay 16:9; 9:3; Kum 13:16; Eze 26:14; Ufu 3:7; Za 127:1; Isa 24:20; 25:2Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena;

mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa.

12:15 1Fal 8:35; Isa 40:12; Kum 28:22; Mwa 7:11, 14Akizuia maji, huwa pana ukame;

akiyaachia maji, huharibu nchi.

12:16 2Nya 18:22; Rum 2:11; Ay 9:4; 13:7, 9; 27:4Kwake kuna nguvu na ushindi;

adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake.

12:17 Ay 12:19; 19:9; Isa 20:4; Ay 3:14; 1Kor 1:20Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara,

naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi.

12:18 Za 107:14; 116:16; Nah 1:13; Ay 12:21; 34:18Huondoa pingu zilizofungwa na wafalme,

na kuwafunga mishipi ya kiunoni.

12:19 Dan 2:21, 34; Kum 24:15; Ay 9:24; 14:20; 22:8; 24:12, 22; 12:17; Isa 2:22Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara,

na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu.

12:20 Yer 32:9; Kum 4:33-34; Ay 12:12, 24; Dan 4:33-34Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika,

na kuondoa busara ya wazee.

12:21 Ay 12:18; 3:15; Isa 34:12Huwamwagia dharau wanaoheshimika,

na kuwavua silaha wenye nguvu.

12:22 1Kor 4:5; Ay 3:5; Za 139:12; Dan 2:22Hufunua mambo ya ndani ya gizani,

na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana.

12:23 Isa 13:4; 54:3; Kut 34:24; Mt 10:26Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza;

hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya.

Huwaondolea viongozi wa nchi akili zao;

huwapeleka watangetange nyikani pasipo na njia.

12:25 Kum 28:29; Ay 5:14; Za 107:27; Isa 24:20Hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga;

huwafanya wapepesuke kama walevi.

Read More of Ayubu 12

Ayubu 13:1-28

13:1 Ay 9:24“Macho yangu yameona hili lote,

masikio yangu yamesikia na kulielewa.

13:2 Ay 12:3Hayo mnayoyajua mimi pia ninayajua;

mimi si mtu duni kuliko ninyi.

13:3 Ay 5:8; 23:3-4; 5:17; 40:2Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi

na kuhojiana shauri langu na Mungu.

13:4 Isa 9:15; Yer 23:32; Za 119:69; Yer 8:22; Ay 6:15Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo;

ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote!

13:5 Mit 17:28; Amo 5:13; Ay 13:13; Amu 18:19; Mhu 5:3; Yak 1:19Laiti wote mngenyamaza kimya!

Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima.

13:6 Ay 33:1; 36:4Sikieni sasa hoja yangu;

sikilizeni kusihi kwangu.

13:7 Ay 16:17; 36:4; 17:5; Rum 3:5-8Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu?

Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake?

13:8 Law 19:15; Mit 24:23Mtamwonyesha upendeleo?

Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake?

13:9 Ay 12:16; 9:3; Gal 6:7Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi?

Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu?

13:10 Law 19:15; 2Nya 19:7Hakika angewakemea

kama mkiwapendelea watu kwa siri.

13:11 Ay 31:23; Kut 3:6Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi?

Je, hofu yake isingewaangukia ninyi?

13:12 Neh 4:2-3Maneno yenu ni mithali za majivu;

utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi.

13:13 Ay 13:5; 7:11; 9:21“Nyamazeni kimya nipate kusema;

kisha na yanipate yatakayonipata.

13:14 Amu 9:17; Za 119:109Kwa nini nijiweke mwenyewe kwenye hatari

na kuyaweka maisha yangu mikononi mwangu?

13:15 Za 27:1; Dan 3:28; Ay 5:8; 27:5; Mit 14:32; Rum 8:38-39Ingawa ataniua, bado nitamtumaini;

hakika nitazitetea njia zangu mbele zake.

13:16 Hos 14:4; Flp 1:19; Isa 12:1-2Naam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu,

kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu

atakayethubutu kuja mbele yake!

13:17 Ay 21:2Sikilizeni maneno yangu kwa makini;

nayo masikio yenu yaingize kile nisemacho.

13:18 Ay 13:3; 23:4; 37:19; 2:3; 9:21Sasa kwamba nimekwisha kutayarisha mambo yangu,

ninajua mimi nitahesabiwa kuwa na haki.

13:19 Isa 50:8; Rum 8:33; Ay 3:13; 40:4; 9:15Je, kuna yeyote anayeweza kuleta mashtaka dhidi yangu?

Kama ndivyo, nitanyamaza kimya na nife.

“Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili,

nami sitajificha uso wako:

13:21 Za 39:10; Ebr 10:31; Kut 9:3; Ay 6:4Ondoa mkono wako uwe mbali nami,

nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu.

13:22 Ay 9:35; 14:15Niite kwenye shauri nami nitajibu,

au niache niseme, nawe upate kujibu.

13:23 1Sam 26:18; Ay 7:21; 9:21; 14:17; 33:9Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda?

Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu.

13:24 Isa 8:17; Za 88:14-15; Yer 30:14Kwa nini kuuficha uso wako

na kunihesabu mimi kuwa adui yako?

13:25 Law 26:36; Isa 43:17; Hos 13:3Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo?

Je, utayasaka makapi makavu?

13:26 Ay 21:23; Za 25:7Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu

na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu.

13:27 Mwa 40:15; Mdo 16:24Umeifunga miguu yangu kwenye pingu.

Unazichunga kwa makini njia zangu zote

kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu.

13:28 Hos 5:12; Yak 5:2“Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza,

kama vazi lililoliwa na nondo.

Read More of Ayubu 13

Ayubu 14:1-22

14:1 Mhu 2:23; Mwa 3:17; Ay 15:14; 10:20; Mt 11:11; Za 51:5“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke

siku zake ni chache nazo zimejaa taabu.

14:2 Za 103:15; Yak 1:10; 1Pet 1:24; Isa 40:6-8; Mhu 6:12Huchanua kama ua kisha hunyauka;

huwa kama kivuli kipitacho upesi, wala hadumu.

14:3 Za 144:3; 8:4; 143:2; Ay 7:18Je, unamwekea jicho lako mtu kama huyo?

Je, utamleta mbele yako katika hukumu?

14:4 Mwa 5:3; Ay 4:17; Za 51:10; Rum 5:12; Efe 2:1-3; Yn 3:6Ni nani awezaye kutoa kitu safi kutoka kitu najisi?

Hakuna awezaye!

14:5 Ay 24:1; 21:21; Za 31:15; 139:16; 39:4; 90:12; Mdo 17:26Siku za mwanadamu zimewekewa mpaka;

umekwisha kutangaza idadi ya miezi yake

na kuweka mpaka ambao hawezi kuuvuka.

14:6 Ay 7:19; 7:1, 2; Za 39:13; Isa 16:14; 21:16Hivyo angalia mbali umwache,

hadi awe amekamilisha muda wake

kama mtu aliyeajiriwa.

14:7 Ay 19:10; 24:20; Za 52:5; Isa 11:1; 53:2; 60:21; 6:13“Kwa maana lipo tumaini kwa mti;

kama ukikatwa utachipuka tena,

nayo machipukizi yake mapya hayatakoma.

14:8 Isa 6:13; 11:1; 53:2Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini

na kisiki chake kufa udongoni,

14:9 Ay 29:9; Zek 10:1; Za 1:3; Yer 17:8; Eze 31:7; Law 26:4; Eze 34:27lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua

na kutoa machipukizi kama mche.

14:10 Ay 14:12; 10:21; 13:19Lakini mwanadamu hufa, na huo ndio mwisho wake;

hutoa pumzi ya mwisho, naye hayuko tena!

14:11 2Sam 14:14; Isa 19:5Kama vile maji yatowekavyo katika bahari,

au mkondo wa mto ukaushwavyo na kuwa mkavu,

14:12 Za 102:26; Ufu 21:1; Mdo 3:21; Ay 14:10; Ufu 20:11ndivyo mwanadamu alalavyo chini asiamke;

hadi mbingu zitakapokuwa hazipo tena,

wanadamu hawataamka au kuamshwa

kutoka kwenye usingizi wao.

14:13 Za 30:5; Isa 54:7; Ay 6:8; 7:9; Isa 26:20; 54:7; Mwa 8:1“Laiti kama ungenificha kaburini,14:13 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

na kunisitiri hadi hasira yako ipite!

Laiti ungeniwekea wakati,

na kisha ukanikumbuka!

14:14 Ay 7:1; 2Fal 6:33; Za 16:10; 1Kor 15:42-58; Flp 3:21Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena?

Siku zote za kazi zangu ngumu

nitangojea kufanywa upya kwangu.

14:15 Ay 13:22; Yn 5:28; 1The 4:16; Za 50:4Utaniita nami nitakuitika;

utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba.

14:16 Mit 5:21; Yer 16:17; 32:19; Hos 13:12; 1Kor 13:5Hakika ndipo utakapozihesabu hatua zangu,

lakini hutazifuatia dhambi zangu.

14:17 Kum 32:34; Ay 13:23; 9:30; Yer 32:10Makosa yangu yatafungiwa kwa lakiri kwenye mfuko,

nawe utazifunika dhambi zangu.

14:18 Eze 38:20; Ay 18:4“Lakini kama mlima umomonyokavyo na kufikichika

na kama vile mwamba uondolewavyo mahali pake,

14:19 Eze 13:13; Mwa 7:23; Ay 7:8kama maji yamalizavyo mawe,

na mafuriko yachukuavyo udongo,

ndivyo unavyoharibu tegemeo la mwanadamu.

14:20 Ay 4:20; 7:10; 8:18; 12:19; 27:19; Yak 1:10Humshinda mara moja kwa daima, naye hutoweka;

waibadilisha sura yake na kumwondoa.

14:21 Mhu 9:5; Isa 63:16; 1Sam 4:20Kama wanawe wakipewa heshima, yeye hafahamu;

kama wakidharauliwa, yeye haoni.

14:22 Za 38:7; Isa 21:3; Yer 4:19; Ay 21:21Yeye hasikii kingine isipokuwa maumivu ya mwili wake mwenyewe,

naye huomboleza kwa ajili yake mwenyewe.”

Read More of Ayubu 14