Ayubu 1:1-22, Ayubu 2:1-13, Ayubu 3:1-26 NEN

Ayubu 1:1-22

Sehemu Ya Kwanza: Habari Za Awali

(Ayubu 1–2)

Ayubu Na Jamaa Yake

1:1 Mwa 22:21; Yak 5:11; Eze 14:14, 20; Mit 8:13; Mwa 10:23; 6:9; 22:12; Ay 23:7, 10; 2:3; Za 11:7; 107:42; Mit 21:29; Mik 7:2; Kum 4:6; 1The 5:22Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu. 1:2 Za 127:3; Rut 4:15; Ay 1:13, 18; 42:13; Za 144:12Alikuwa na wana saba na binti watatu, 1:3 Ay 29:25; Mwa 13:2; 12:16; Ay 1:8; Mwa 25:6; Ay 42:10; Za 103:10naye alikuwa na kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia tano za maksai, na punda mia tano, tena alikuwa na idadi kubwa ya watumishi. Alikuwa mtu mkuu sana miongoni mwa watu wa Mashariki.

1:4 Ay 1:13, 18Wanawe walikuwa na desturi ya kufanya karamu katika nyumba zao kwa zamu, nao wangewaalika umbu zao watatu ili kula na kunywa pamoja nao. 1:5 Mwa 8:20; Ay 42:8; 1Fal 21:10-13; Za 74:10; Neh 12:30; Ay 8:4; Za 10:3Wakati kipindi cha karamu kilimalizika, Ayubu angetuma waitwe na kuwafanyia utakaso. Angetoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya kila mmoja wao asubuhi na mapema, akifikiri, “Pengine wanangu wametenda dhambi na kumlaani Mungu mioyoni mwao.” Hii ilikuwa ndiyo desturi ya kawaida ya Ayubu.

Jaribu La Kwanza La Ayubu

1:6 1Fal 22:19; Ay 38:7; 2:1; Dan 7:10; Mwa 6:2; 2Sam 24:1; 2Nya 18:21; Za 109:6; Lk 22:31Siku moja wana wa Mungu1:6 Wana wa Mungu hapa ina maana malaika au viumbe vya mbinguni. walikwenda kujionyesha mbele za Bwana. Shetani1:6 Shetani hapa ina maana ya mshtaki wa watakatifu. naye akaja pamoja nao. 1:7 Mwa 3:1; 1Pet 5:8; Mt 12:43Bwana akamwambia Shetani, “Umetoka wapi?”

Shetani akamjibu Bwana, “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”

1:8 Ay 42:7-8; Kut 20:20; Yos 1:7; Za 25:16; 26:12; 112:1; 128:4Ndipo Bwana akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuepukana na uovu.”

1:9 1Tim 6:5Shetani akamjibu Bwana, “Je, Ayubu anamcha Mungu bure? 1:10 Za 34:7; 128:1-2; Ay 8:7; 1Sam 25:16; Ay 2:4; 29:6; 42:12, 17Je, wewe hukumjengea boma pande zote yeye na wa nyumbani mwake pamoja na kila kitu alicho nacho? Kazi za mikono yake umezibariki na hivyo makundi yake ya kondoo na mbuzi pamoja na ya wanyama yameenea katika nchi nzima. 1:11 Ay 19:21; Law 24:11; Ufu 12:9-10; Lk 22:31; Isa 3:8; 65:3; Ay 2:5Lakini nyoosha mkono wako na kupiga kila kitu alicho nacho, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.”

1:12 Ay 2:6; 1Kor 10:13Bwana akamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, kila kitu alicho nacho kiko mikononi mwako, lakini juu ya huyo mtu mwenyewe usimguse hata kwa kidole.”

Ndipo Shetani akatoka mbele za Bwana.

1:13 Ay 1:2, 4; Mhu 9:12; Lk 12:19, 20Siku moja watoto wa Ayubu walipokuwa wakifanya karamu wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, 1:14 Mwa 36:24akaja mjumbe kwa Ayubu na kusema, “Maksai walikuwa wakilima na punda walikuwa wakilisha karibu nao, 1:15 Mwa 10:7; Ay 6:19; 9:26Waseba wakawashambulia na kuchukua mifugo. Kisha wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!”

1:16 1Fal 18:38; 2Fal 1:12; Ay 20:26; Mwa 18:17; Law 10:2; Hes 11:1-3Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Moto wa Mungu ulishuka kutoka mbinguni na kuteketeza kondoo na watumishi, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!”

1:17 Mwa 11:28-31; Ay 9:24Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wakaldayo waliunda vikosi vitatu vya uvamizi na kuwaangukia ngamia wako na kuwachukua wakaondoka nao. Wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari.”

1:18 Ay 1:2, 4Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wana wako na binti zako walipokuwa wakifanya karamu, wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, 1:19 Isa 21:1; Mk 7:25; Za 11:6; Isa 5:28; Yer 4:11; 13:24; 18:17; Eze 17:10; Hos 13:15ghafula upepo wenye nguvu ukavuma kutoka jangwani, nao ukaipiga nyumba hiyo pembe zake nne. Ikawaangukia hao watoto nao wamekufa, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!”

1:20 Mwa 37:29; Mk 14:63; Isa 3:24; 15:2; 22:12; Yer 7:29; 16:6; Eze 27:31; 29:18; Mik 1:16; 1Pet 5:6Ndipo Ayubu akasimama, akararua joho lake na kunyoa nywele zake. Kisha akaanguka chini katika kuabudu 1:21 Mhu 5:15; Rut 1:21; Amu 10:15; Efe 5:20; Mwa 45:5; 1Tim 6:7; 1Sam 2:7; Mhu 7:14; Yak 5:11; Amo 3:6; Efe 5:20; Mwa 45:5na kusema:

“Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi,

nami nitaondoka uchi,1:21 Au: nitarudi huko uchi.

Bwana alinipa, naye Bwana ameviondoa,

jina la Bwana litukuzwe.”

1:22 Mit 10:19; Rum 9:20; Ay 2:10; Za 39:1; Isa 53:7Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa kumlaumu Mungu kwa kufanya ubaya.

Read More of Ayubu 1

Ayubu 2:1-13

Jaribu La Pili La Ayubu

2:1 Ay 1:6; Mwa 6:2Siku nyingine wana wa Mungu walikuja kujionyesha mbele za Bwana. Shetani naye akaja pamoja nao kujionyesha mbele zake. 2:2 Mwa 3:1Bwana akamuuliza Shetani, “Umetoka wapi?”

Shetani akamjibu Bwana “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”

2:3 Kut 20:20; Ay 6:29; 9:17; 13:18; Yak 1:12; Za 44:17; Ay 13:18; 27:5, 6; 1Pet 1:7; Mt 7:11; Yn 9:2Bwana akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, mtu asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Naye bado anadumisha uadilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.”

2:4 Ay 1:10Shetani akamjibu Bwana, “Ngozi kwa ngozi! Mwanadamu atatoa vyote alivyo navyo kwa ajili ya uhai wake. 2:5 Za 102:5; Ay 19:20; Mao 4:8; Za 32:3, 4; Ay 16:8; 1:11Lakini nyoosha mkono wako na kuipiga nyama yake na mifupa yake, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.”

2:6 Ay 1:12; 2Kor 12:7Bwana akamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, yeye yumo mikononi mwako, lakini lazima umwachie uhai wake.”

2:7 Kum 28:35; Ay 7:5; 16:16Basi Shetani akatoka mbele za Bwana naye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa. 2:8 2Sam 13:19; Za 7:5; Mt 11:21; Mwa 18:27; Es 4:3; Ay 16:15; 19:9; 42:6; Isa 5:8; 6:13; Yer 6:26; Mao 3:29; Eze 26:16; Yon 3:5-8Ndipo Ayubu akachukua kigae na kujikuna nacho huku akiketi kwenye majivu.

2:9 Ay 1:21; 13:15; 27:5; 33:9; 35:2; 1The 5:8; Kut 20:7; 2Fal 6:33Mke wake akamwambia, “Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!”

2:10 Mhu 2:24; Mao 3:38-41; Yak 5:11; Za 39:1Akamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu2:10 Mpumbavu hapa ina maana ya kupungukiwa maadili. yeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?”

Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake.

Marafiki Watatu Wa Ayubu

2:11 Mwa 25:2; 36:11; 37:35; Yer 49:7; Rum 12:15; Ay 11:1; 20:1; Yn 11:19Basi marafiki watatu wa Ayubu, ndio Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi, waliposikia juu ya taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga toka manyumbani mwao, nao wakakutana pamoja kwa makubaliano kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji. 2:12 2Sam 1:2; Neh 9:1; Eze 27:30; Ay 17:7; Isa 52:14; Mwa 37:29; Mk 14:63; Yos 7:6Walipomwona kwa mbali, ilikuwa vigumu kumtambua. Wakaanza kulia kwa sauti kubwa, wakayararua majoho yao na kujirushia mavumbi juu ya vichwa vyao. 2:13 Mwa 50:10-12; Eze 3:15; Isa 3:26; 47:1; Eze 26:16; Yn 3:6; Hag 2:22; Mit 17:28; Isa 23:2; 47:5Kisha wakaketi chini kwenye udongo pamoja na Ayubu kwa siku saba usiku na mchana. Hakuna yeyote aliyesema naye neno, kwa sababu waliona jinsi mateso yake yalivyokuwa makubwa.

Read More of Ayubu 2

Ayubu 3:1-26

Sehemu Ya Pili: Mazungumzo Ya Ayubu Na Rafiki Zake Watatu

(Ayubu 3–31)

Hotuba Ya Kwanza Ya Ayubu

Ayubu Anazungumza

3:1 Yer 15:10; 20:14Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake.

Kisha akasema:

3:3 Mhu 6:3; Ay 10:18-19; Yer 15:10; Ay 3:11, 16; Mit 26:24“Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali,

nao usiku ule iliposemekana,

‘Mtoto wa kiume amezaliwa!’

Siku ile na iwe giza;

Mungu juu na asiiangalie;

nayo nuru isiiangazie.

3:5 Za 44:19; Yer 13:16; Ay 16:16; Isa 9:2; Za 23:4; Mt 4:16; Lk 1:79; Mhu 4:2Giza na kivuli kikuu kiikalie tena;

wingu na likae juu yake;

weusi na uifunike nuru yake.

3:6 Ay 23:17; 30:26; Za 20:5; 33:3; 65:13; Isa 26:19Usiku ule na ushikwe na giza kuu;

usihesabiwe katika siku za mwaka,

wala usihesabiwe katika siku za mwezi wowote.

3:7 Za 20:5; 33:3; Isa 26:19; Yer 51:48Usiku ule na uwe tasa;

sauti ya furaha na isisikike ndani yake.

3:8 Yer 9:17Wale wazilaanio siku wailaani hiyo siku,

wale walio tayari kumwamsha Lewiathani.3:8 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.

3:9 Ay 41:18; Hab 3:4Nyota zake za alfajiri na ziwe giza;

nao ungojee mwanga bila mafanikio,

wala usiuone mwonzi wa kwanza

wa mapambazuko,

kwa sababu huo usiku haukunifungia

mlango wa tumbo la mama yangu,

ili kuyaficha macho yangu

kutokana na taabu.

3:11 Ay 3:3“Kwa nini sikuangamia wakati wa kuzaliwa?

Kwa nini sikufa nilipokuwa ninatoka tumboni?

3:12 Mwa 30:3; 48:12; Isa 66:12Kwa nini pakawa na magoti ya kunipokea

na matiti ili nipate kunyonyeshwa?

3:13 Ay 17:13; 30:23; 3:17; 7:8-10, 21; 3:19; 14:10-12; Za 139:11; Isa 8:22Kwa maana sasa ningekuwa nimepumzika kwa amani.

Ningekuwa nimelala na kupumzika

3:14 Isa 14:9; Eze 32:28-32; Yer 51:37; Nah 3:7; Ay 9:24; 12:17; 15:28pamoja na wafalme na washauri wa dunia,

waliojijengea mahali ambapo sasa ni magofu,

3:15 Ay 12:21; 15:29; 20:10; 27:17; Mit 13:22; Sef 1:11; Isa 45:1; Za 49:16-17; 45:1; Mit 13:22pamoja na watawala waliokuwa na dhahabu,

waliozijaza nyumba zao kwa fedha.

3:16 Mhu 6:3; 4:3; Za 58:8; 71:6Au kwa nini sikufichwa ardhini kama mtoto aliyezaliwa mfu,

kama mtoto mchanga ambaye kamwe hakuuona mwanga?

3:17 Ay 3:26; 30:26; 17:16; Mhu 4:2; Isa 14:3Huko waovu huacha kusumbua

na huko waliochoka hupumzika.

3:18 Ay 38:7; 39:7; Isa 51:14; Mwa 15:13Wafungwa nao hufurahia utulivu wao,

hawasikii tena sauti ya kukemea ya kiongozi wa watumwa.

3:19 Ay 9:22; 17:16; 21:33; 24:24; 30:23; Mhu 12:5Wadogo na wakubwa wamo humo,

na mtumwa ameachiwa huru kutoka kwa bwana wake.

3:20 Yer 20:18; Eze 27:30-31; 1Sam 1:10“Mbona nuru inawaangazia wale walio taabuni,

na hao wenye uchungu kupewa uhai,

3:21 Ufu 9:6; Mit 2:4; Za 119:127wale wanaotamani kifo ambacho hakiji,

wale watafutao kufa zaidi ya kutafuta hazina iliyofichwa,

3:22 Ay 7:16; Mhu 4:3; Yer 8:3ambao hujawa na furaha,

na hushangilia wafikapo kaburini?

3:23 Mao 2:4; 3:7; Hos 2:6; Mt 4:19; Isa 59:10; Yer 13:16; 23:12; Ay 6:4; 16:13; Za 88:8Kwa nini uhai hupewa mtu

ambaye njia yake imefichika,

ambaye Mungu amemzungushia boma?

3:24 Ay 33:20; Mao 2:12; 1Sam 1:15; Isa 35:10; 53:12; Za 6:6; 22:1; 32:3; 107:18Kwa maana kulia kwangu kwa uchungu kwanijia badala ya chakula;

kusononeka kwangu kunamwagika kama maji.

3:25 Hos 13:3; Ay 7:9; 30:15; 9:28; Mwa 42:36Lile nililokuwa naliogopa limenijia;

lile nililokuwa ninalihofia limenipata.

3:26 Dan 4:5; Mt 11:28; Isa 48:22; Yn 14:27Sina amani, wala utulivu;

sina pumziko, bali taabu tu.”

Read More of Ayubu 3