Yeremia 9:17-26, Yeremia 10:1-25, Yeremia 11:1-17 NEN

Yeremia 9:17-26

9:17 2Nya 35:25; Amo 5:15-16; Mhu 12:5Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“Fikiri sasa! Waite wanawake waombolezao waje,

waite wale walio na ustadi kuliko wote.

9:18 Za 119:136; Mao 3:48; Yer 14:17Nao waje upesi

na kutuombolezea,

mpaka macho yetu yafurike machozi

na vijito vya maji vitoke kwenye kope zetu.

9:19 Law 18:29; Yer 4:13Sauti ya kuomboleza imesikika kutoka Sayuni:

‘Tazama jinsi tulivyoangamizwa!

Tazama jinsi aibu yetu ilivyo kubwa!

Ni lazima tuihame nchi yetu

kwa sababu nyumba zetu zimekuwa magofu.’ ”

9:20 Isa 32:9-13; Yer 23:16Basi, enyi wanawake, sikieni neno la Bwana;

fungueni masikio yenu msikie maneno ya kinywa chake.

Wafundisheni binti zenu kuomboleza;

fundishaneni kila mmoja na mwenzake maombolezo.

9:21 2Nya 36:17; Isa 40:30; Yoe 2:9; Yer 16:6Mauti imeingia ndani kupitia madirishani,

imeingia kwenye majumba yetu ya fahari;

imewakatilia mbali watoto katika barabara

na vijana waume kutoka viwanja vya miji.

9:22 2Fal 9:37; Yer 8:2Sema, “Hili ndilo asemalo Bwana:

“ ‘Maiti za wanaume zitalala

kama mavi katika mashamba,

kama malundo ya nafaka nyuma ya mvunaji,

wala hakuna anayekusanya.’ ”

9:23 Ay 4:12; Isa 5:21; Mhu 9:11; Za 62:10; 1Fal 20:11; Mit 11:28; Eze 28:4-5; Yer 48:7Hili ndilo asemalo Bwana:

“Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake,

au mwenye nguvu ajisifu katika nguvu zake,

wala tajiri ajisifu katika utajiri wake,

9:24 Gal 6:14; 2Kor 10:17; Za 34:2; Mik 6:8; Za 36:6; 1Kor 1:31lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kwa sababu hili:

kwamba ananifahamu na kunijua mimi,

kwamba mimi ndimi Bwana, nitendaye wema,

hukumu na haki duniani,

kwa kuwa napendezwa na haya,”

asema Bwana.

9:25 Law 26:41; Rum 2:8-9; Amo 3:2“Siku zinakuja, nitakapowaadhibu wale wote ambao wametahiriwa kimwili tu, asema Bwana, 9:26 Yer 25:23; 49:32; Mdo 7:51; Rum 2:28; Eze 31:18; 1Sam 14:6yaani Misri, Yuda, Edomu, Amoni, Moabu na wote wanaoishi jangwani sehemu za mbali. Kwa maana mataifa haya yote hayakutahiriwa mioyo yao, nayo nyumba yote ya Israeli haikutahiriwa.”

Read More of Yeremia 9

Yeremia 10:1-25

Mungu Na Sanamu

Sikieni lile ambalo Bwana, anena nanyi ee nyumba ya Israeli. 10:2 Kut 23:24; Law 20:23; Mwa 1:14Hili ndilo asemalo Bwana:

“Usijifunze njia za mataifa

wala usitishwe na ishara katika anga,

ingawa mataifa yanatishwa nazo.

10:3 Isa 40:19; Kum 9:21; Eze 7:20; Yer 44:8; 1Fal 8:36Kwa maana desturi za mataifa hazina maana,

wanakata mti msituni,

na fundi anauchonga kwa patasi.

10:4 1Sam 5:3; Isa 41:7; Za 135:15; Hos 13:2; Hab 2:19Wanaparemba kwa fedha na dhahabu,

wanakikaza kwa nyundo na misumari ili kisitikisike.

10:5 1Fal 18:26; 1Kor 12:2; Isa 45:20; Hab 2:19; Isa 44:9-20; Mdo 19:26Sanamu zao ni kama sanamu

iliyowekwa shambani la matango kutishia ndege

nazo haziwezi kuongea;

sharti zibebwe

sababu haziwezi kutembea.

Usiziogope; haziwezi kudhuru,

wala kutenda lolote jema.”

10:6 2Sam 7:22; Kut 8:9-10; Za 48:1Hakuna aliye kama wewe, Ee Bwana;

wewe ni mkuu,

jina lako ni lenye nguvu katika uweza.

10:7 Isa 12:4; Ufu 15:4; Za 22:28; Yer 5:22Ni nani ambaye haimpasi kukuheshimu wewe,

Ee Mfalme wa mataifa?

Hii ni stahili yako.

Miongoni mwa watu wote wenye hekima

katika mataifa na katika falme zao zote,

hakuna aliye kama wewe.

10:8 Isa 40:19; Yer 4:22; Isa 44:18; Kum 32:21Wote hawana akili, tena ni wapumbavu,

wanafundishwa na sanamu za miti zisizofaa lolote.

10:9 Dan 10:5; Za 115:4; Isa 40:19; Mwa 10:4Huleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi

na dhahabu kutoka Ufazi.

Kile ambacho fundi na sonara wametengeneza

huvikwa mavazi ya rangi ya samawi na urujuani:

vyote vikiwa vimetengenezwa

na mafundi stadi.

10:10 1Tim 6:17; Za 76:7; Yos 3:10; Mt 16:16; Mwa 21:33; Dan 6:26; Amu 5:4; Ay 9:6Lakini Bwana ni Mungu wa kweli,

yeye ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele.

Anapokasirika, dunia hutetemeka,

mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.

10:11 Za 96:5; Isa 2:18“Waambie hivi: ‘Miungu hii, ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia kutoka dunia na kutoka chini ya mbingu.’ ”

10:12 Ay 9:9; 38:4; Isa 40:22-28; Mdo 14:15; 1Sam 2:8; Mwa 1:1, 8, 31Lakini Mungu aliiumba dunia kwa uweza wake,

akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake,

na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake.

10:13 Ay 36:29; Za 135:7; 104:13; Kum 28:12Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma;

huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia.

Hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua,

naye huuleta upepo kutoka ghala zake.

Kila mmoja ni mjinga na hana maarifa,

kila sonara ameaibishwa na sanamu zake.

Vinyago vyake ni vya udanganyifu,

havina pumzi ndani yavyo.

10:15 Isa 41:21; Yer 14; 22Havifai kitu, ni vitu vya kufanyia mzaha tu,

hukumu yavyo itakapowadia, vitaangamia.

10:16 Kum 32:9; Yer 32:17; Kut 34:9; Za 73:26; Yer 31:35; Za 74:2Yeye aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo,

kwani ndiye Muumba wa vitu vyote,

pamoja na Israeli, kabila la urithi wake:

Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.

Maangamizi Yajayo

10:17 Eze 12:12Kusanyeni mali na vitu vyenu mwondoke nchi hii,

enyi mnaoishi katika hali ya kuzingirwa na jeshi.

10:18 1Sam 25:29; Isa 22:17; Eze 6:10; Kum 28:52Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:

“Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu

wote waishio katika nchi hii;

nitawataabisha

ili waweze kutekwa.”

10:19 Mik 7:9; Nah 3:19; Ay 34:6; Yer 14:17; 15:18; Mao 2:13; Yer 30:12, 15Ole wangu mimi kwa ajili ya kuumia kwangu!

Jeraha langu ni kubwa!

Lakini nilisema,

“Kweli hii ni adhabu yangu,

nami sharti niistahimili.”

10:20 Yer 4:20; 31:15; Mao 1:5Hema langu limeangamizwa;

kamba zake zote zimekatwa.

Wana wangu wametekwa na hawapo tena;

hakuna hata mmoja aliyebaki wa kusimamisha hema langu

wala wa kusimamisha kibanda changu.

10:21 Yer 23:2; Eze 34:6; Yer 6:22; 25:34; 50:6; Isa 56:10; Yer 22:30Wachungaji hawana akili

wala hawamuulizi Bwana,

hivyo hawastawi

na kundi lao lote la kondoo limetawanyika.

10:22 Isa 34:13; Yer 9:11; 6:22; 27:6; Eze 12:19Sikilizeni! Taarifa inakuja:

ghasia kubwa kutoka nchi ya kaskazini!

Hii itafanya miji ya Yuda ukiwa,

makao ya mbweha.

Maombi Ya Yeremia

10:23 Ay 33:29; Yer 9:11; 6:22; 27:6; Eze 12:19Ninajua, Ee Bwana, kwamba maisha ya mwanadamu si yake mwenyewe;

hawezi kuziongoza hatua zake mwenyewe.

10:24 Yer 7:20; 18:23; 46:28; 30:11Unirudi, Ee Bwana, lakini kwa kipimo cha haki:

si katika hasira yako,

usije ukaniangamiza.

10:25 Ay 15:21; Yer 8:16; Za 69:24; 79:6-7; Sef 3:8; Yer 2:3Umwage ghadhabu yako juu ya mataifa

wasiokujua wewe,

juu ya mataifa wasioliitia jina lako.

Kwa kuwa wamemwangamiza Yakobo;

wamemwangamiza kabisa

na kuiharibu nchi yake.

Read More of Yeremia 10

Yeremia 11:1-17

Agano Limevunjwa

Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana: “Sikia maneno ya agano hili, nawe uwaambie watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu. 11:3 Kum 11:26-28; 27:26; Gal 3:10; Kum 28:15-68Waambie kwamba hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Amelaaniwa mtu ambaye hatayatii maneno ya agano hili, 11:4 Law 26:3; Kum 4:20; 1Fal 8:51; Kut 24:8; Yer 7:23; Eze 11:20maneno niliyowaamuru baba zenu nilipowatoa katika nchi ya Misri, kutoka tanuru la kuyeyushia vyuma.’ Nilisema, ‘Nitiini mimi na mfanye kila kitu ninachowaamuru, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. 11:5 Kum 7:12; Kut 6:8; 13:5; Za 105:8-11; Kut 3:8; Kum 27:26Kisha nitatimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi itiririkayo maziwa na asali,’ nchi ambayo mnaimiliki leo.”

Nikajibu, “Amen, Bwana.”

11:6 Kut 15:26; Yn 13:17; Rum 2:13; Yak 1:22; Yer 4:5; Kum 15:5Bwana akaniambia, “Tangaza maneno haya yote katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu: ‘Sikilizeni maneno ya agano hili na kuyafuata. 11:7 2Nya 36:15Tangu wakati ule niliwapandisha baba zenu kutoka Misri mpaka leo, niliwaonya tena na tena, nikisema “Nitiini mimi.” 11:8 Yer 7:26; Law 26:14-43; Yos 23:15; Mhu 9:3; Yer 3:17; 2Nya 7:19; Za 78:10Lakini hawakusikiliza wala kujali. Badala yake, walifuata ukaidi wa mioyo yao miovu. Hivyo nikaleta juu yao laana zote za agano nililokuwa nimewaamuru wao kulifuata, lakini wao hawakulishika.’ ”

11:9 Hos 6:9; Eze 1:28; 22:25Kisha Bwana akaniambia, “Kuna shauri baya linaloendelea miongoni mwa watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalemu. 11:10 Eze 20:18; Kum 9:7; 2Nya 30:7; Amu 2:11-13; 10:13; Zek 7:11; Yer 16:11; 34:18Wamerudia dhambi za baba zao, waliokataa kusikiliza maneno yangu. Wameifuata miungu mingine kuitumikia. Nyumba zote mbili za Israeli na Yuda zimelivunja agano nililofanya na baba zao. 11:11 Eze 8:8-18; Ay 27:9; Za 66:18; 2Fal 22:16; Zek 7:13; Ay 11:20; Yer 14:12Kwa hivyo, hili ndilo asemalo Bwana: ‘Nitaleta juu yao maafa ambayo hawawezi kuyakimbia. Hata kama wakinililia, sitawasikiliza. 11:12 Kum 32:37-38; Amu 10:14; Yer 44:17; Isa 45:20Miji ya Yuda na watu wa Yerusalemu watakwenda kuililia miungu ambayo wameifukizia uvumba, lakini haitawasaidia kamwe wakati maafa yatakapowapiga. 11:13 Yer 44:21; 3:24; Kut 20:3; Yer 19:4; 2Fal 17:29; Yer 7:9Mnayo miungu mingi kama miji mliyo nayo, ee Yuda, nazo madhabahu mlizozijenga za kufukizia uvumba huyo mungu wa aibu Baali ni nyingi kama barabara za Yerusalemu.’

11:14 Kut 32:10; Yer 7:16“Wewe usiwaombee watu hawa wala kufanya maombezi yoyote au kunisihi kwa ajili yao, kwa sababu sitawasikiliza watakaponiita wakati wa taabu yao.

11:15 Eze 16:25; Hag 2:12; Yer 7:9-10“Mpenzi wangu anafanya nini hekaluni mwangu,

anapofanya mashauri yake maovu na wengi?

Je, nyama iliyowekwa wakfu yaweza

kuondolea mbali adhabu yako?

Unapojiingiza katika ubaya wako,

ndipo unashangilia.”

11:16 Yer 7:20; 21:14; Rum 11:17-24; Hos 14:6; Isa 27:11Bwana alikuita mti wa mzeituni uliostawi

ulio na matunda mazuri kwa sura.

Lakini kwa ngurumo ya mawimbi makuu

atautia moto,

nayo matawi yake yatavunjika.

11:17 Kut 15:17; Isa 5:2; Yer 7:9; 12:2; 7:18Bwana Mwenye Nguvu Zote, aliyekupanda, ametamka maafa kwa ajili yako, kwa sababu nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda mmefanya maovu na kunikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba.

Read More of Yeremia 11