Yeremia 7:30-34, Yeremia 8:1-22, Yeremia 9:1-16 NEN

Yeremia 7:30-34

Bonde La Machinjo

7:30 Yer 2:7; 32:34; Eze 7:20-22; Law 20:3“ ‘Watu wa Yuda wamefanya maovu machoni pangu, asema Bwana. Wameziweka sanamu zao za machukizo ndani ya nyumba iitwayo kwa Jina langu, na wameitia unajisi. 7:31 2Fal 23:10; Law 18:21; Za 106:38; Eze 20:31; Mik 6:7; Yos 15:8; 2Nya 33:6Wamejenga mahali pa juu pa kuabudia sanamu pa Tofethi kwenye Bonde la Ben-Hinomu ili kuwateketeza wana wao na binti zao kwenye moto, kitu ambacho sikuamuru, wala hakikuingia akilini mwangu. 7:32 Yer 19:6; 19:11Kwa hiyo mjihadhari, siku zinakuja, asema Bwana, wakati watu watakapokuwa hawapaiti Tofethi au Bonde la Ben-Hinomu, lakini watapaita Bonde la Machinjo, kwa sababu watawazika wafu huko Tofethi mpaka pasiwe tena nafasi. 7:33 Kum 28:26; Eze 29:5; Mwa 15:11; Yer 6:11; 14:16Ndipo mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwepo na yeyote wa kuwafukuza. 7:34 Hos 2:11; Isa 24:8; Eze 26:13; Ufu 18:23; Zek 7:14; Mt 23:38; Isa 24:7-12Nitazikomesha sauti za shangwe na furaha, na sauti za bwana arusi na bibi arusi katikati ya miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu, kwa sababu nchi itakuwa ukiwa.

Read More of Yeremia 7

Yeremia 8:1-22

8:1 Isa 14:19; Za 53:5“ ‘Wakati huo, asema Bwana, mifupa ya wafalme na maafisa wa Yuda, mifupa ya makuhani na manabii, na mifupa ya watu wa Yerusalemu itaondolewa kutoka makaburi yao. 8:2 Yer 44:19; Mdo 7:42; Za 83:10; 2Fal 23:5; Yer 19:13; Ay 31:27; Yer 14:16Itawekwa wazi kwa jua, na mwezi, na nyota zote za mbingu, ambazo walizipenda na kuzitumikia, na ambazo wamezifuata kutafuta ushauri na kuziabudu. Hawatakusanywa pamoja au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyotapakaa juu ya ardhi. 8:3 Ay 3:22; Ufu 9:6; Kum 29:28Popote nitakapowafukuzia, mabaki wote wa kizazi hiki kiovu watatamani kufa kuliko kuishi, asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.’

Dhambi Na Adhabu

8:4 Mik 7:8; Mit 24:16; Yer 31:19; Za 119:67“Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana:

“ ‘Je, watu wanapoanguka hawainuki?

Je, mtu anapopotea harudi?

8:5 Yer 5:27; Isa 1:20; Yer 7:24; Zek 7:11Kwa nini basi watu hawa walipotea?

Kwa nini Yerusalemu inapotea kila mara?

Wanangʼangʼania udanganyifu

na wanakataa kurudi.

8:6 2Pet 3:9; Ufu 9:20; Za 14:1-3; Mal 3:16Nimewasikiliza kwa makini,

lakini hawataki kusema lililo sawa.

Hakuna anayetubia makosa yake

akisema, “Nimefanya nini?”

Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewe

kama farasi anayekwenda vitani.

8:7 Kum 32:28; Wim 2:12; Yer 4:22Hata korongo aliyeko angani

anayajua majira yake yaliyoamriwa,

nao njiwa, mbayuwayu na koikoi

hufuata majira yao ya kurudi.

Lakini watu wangu hawajui

Bwana anachotaka kwao.

8:8 Rum 2:17; Hos 8:12“ ‘Mwawezaje kusema, “Sisi tuna busara

kwa sababu tunayo sheria ya Bwana,”

wakati ambapo kwa hakika kalamu ya uongo ya waandishi

imeandika kwa udanganyifu?

8:9 Isa 29:14; Yer 5:16-19; 2Fal 19:26; Ay 5:13; Yer 6:19; 1Kor 1:20Wenye hekima wataaibika,

watafadhaika na kunaswa.

Kwa kuwa wamelikataa neno la Bwana,

hiyo hekima waliyo nayo ni ya namna gani?

8:10 Yer 6:12; Isa 56:11; Mao 4:13; Isa 28:7; Yer 14:14; Mao 2:14; Yer 23:11-15Kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao,

na mashamba yao kwa wamiliki wengine.

Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,

wote wana tamaa ya kupata zaidi;

manabii na makuhani wanafanana,

wote wanafanya udanganyifu.

8:11 Yer 6:14; Eze 13:10; 7:25; Yer 4:10Wanafunga majeraha ya watu wangu

bila uangalifu.

Wanasema, “Amani, amani,”

wakati hakuna amani.

8:12 Za 52:5-7; Yer 3:3; Isa 3:9; Yer 6:15Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno?

Hapana, hawana aibu hata kidogo,

hawajui hata kuona haya.

Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka,

watashushwa chini watakapoadhibiwa,

asema Bwana.

8:13 Hos 2:12; Mt 21:19; Yer 5:17; Lk 13:6“ ‘Nitayaondoa mavuno yao,

asema Bwana.

Hapatakuwepo zabibu kwenye mzabibu.

Hapatakuwepo na tini kwenye mtini,

majani yake yatanyauka.

Kile nilichowapa

watanyangʼanywa.’ ”

8:14 Yos 10:20; Yer 23:15; Kum 29:18; Dan 9:5; Yer 35:11; 9:15; 14:7, 20“Kwa nini tunaketi hapa?

Kusanyikeni pamoja!

Tukimbilie kwenye miji yenye maboma,

tukaangamie huko!

Kwa kuwa Bwana, Mungu wetu

ametuhukumu kuangamia,

na kutupa maji yenye sumu tunywe,

kwa sababu tumemtenda dhambi.

8:15 Ay 19:8; Yer 14:19Tulitegemea amani,

lakini hakuna jema lililokuja,

tulitegemea wakati wa kupona,

lakini kulikuwa hofu tu.

8:16 Mwa 30:6; Yer 4:15, 29; 51:29; 5:17Mkoromo wa farasi za adui

umesikika kuanzia Dani,

kwa mlio wa madume yao ya farasi,

nchi yote inatetemeka.

Wamekuja kuangamiza nchi na vyote vilivyomo,

mji na wote waishio ndani yake.”

8:17 Hes 21:6; Kum 32:24; Isa 3:3; Za 58:5“Tazama, nitatuma nyoka wenye sumu kali katikati yenu,

fira ambao hawawezi kulogwa,

nao watawauma,”

asema Bwana.

8:18 Mao 5:17Ee Mfariji wangu katika huzuni,

moyo wangu umezimia ndani yangu.

8:19 Kum 28:64; Yer 9:16; Mik 4:9; Yer 44:3; Isa 41:24; Kum 32:21Sikia kilio cha watu wangu

kutoka nchi ya mbali:

“Je, Bwana hayuko Sayuni?

Je, Mfalme wake hayuko tena huko?”

“Kwa nini wamenikasirisha kwa vinyago vyao,

kwa sanamu zao za kigeni zisizofaa?”

“Mavuno yamepita,

kiangazi kimekwisha,

nasi hatujaokolewa.”

8:21 Nah 2:10; Mao 2:13; Eze 6:9; Za 94:5; Isa 43:24; Yer 4:19Kwa kuwa watu wangu wamepondwa, nami nimepondeka pia;

ninaomboleza, nayo hofu kuu imenishika.

8:22 Mwa 37:25; Yer 30:12; Ay 13:4; Isa 1:6Je, hakuna zeri ya kuponya katika Gileadi?

Je, hakuna tabibu huko?

Kwa nini basi hakuna uponyaji

wa majeraha ya watu wangu?

Read More of Yeremia 8

Yeremia 9:1-16

9:1 Mao 3:48; Isa 22:4; Za 119:136; Yer 13:17; 14:17; Mao 2:11Laiti kichwa changu kingekuwa chemchemi ya maji

na macho yangu yangekuwa kisima cha machozi!

Ningelia usiku na mchana

kwa kuuawa kwa watu wangu.

9:2 Hes 25:1; Hos 4:2; Za 55:7; Yer 23:10; Hos 7:4; 1Fal 19:10; Isa 24:16Laiti ningekuwa na nyumba

ya kukaa wasafiri jangwani,

ningewaacha watu wangu

na kwenda mbali nao,

kwa kuwa wote ni wazinzi,

kundi la watu wadanganyifu.

9:3 Kut 20:16; Mik 6:12; Amu 2:10; 1Sam 2:12; Za 64:3; Isa 44; 20; Yer 18:18“Huweka tayari ndimi zao kama upinde,

ili kurusha uongo;

wamekuwa na nguvu katika nchi

lakini si katika ukweli.

Wanatoka dhambi moja hadi nyingine,

hawanitambui mimi,”

asema Bwana.

9:4 Mik 7:5-6; Mwa 27:35; 2Sam 15:12; Kut 20:16; Law 19:16“Jihadhari na rafiki zako;

usiwaamini ndugu zako.

Kwa kuwa kila ndugu ni mdanganyifu,

na kila rafiki ni msingiziaji.

9:5 Za 15:2; Law 6:2; Isa 59:15Rafiki humdanganya rafiki,

hakuna yeyote asemaye kweli.

Wamefundisha ndimi zao kudanganya,

wanajichosha wenyewe katika kutenda dhambi.

9:6 Yer 5:27; Mit 1:24Unakaa katikati ya udanganyifu;

katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,”

asema Bwana.

9:7 Ay 28:1; Isa 1:28; Hos 11:8; Yer 6:27Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“Tazama, nitawasafisha na kuwajaribu,

kwani ni nini kingine niwezacho kufanya

kwa sababu ya dhambi ya watu wangu?

9:8 Za 35:20; Yer 5:26; Isa 3:5Ndimi zao ni mshale wenye sumu,

hunena kwa udanganyifu.

Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake,

lakini moyoni mwake humtegea mtego.

9:9 Kum 32:43; Isa 10:3Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya jambo hili?”

asema Bwana.

“Je, nisijilipizie kisasi

kwa taifa kama hili?”

9:10 Hos 4:3; Yoe 1:18; Yer 31:35; 32:18; 23:10; 4:25; 12:4Nitalia na kuomboleza kwa ajili ya milima

na kuomboleza kuhusu malisho ya jangwani.

Yamekuwa ukiwa, wala hakuna apitaye humo,

milio ya ngʼombe haisikiki.

Ndege wa angani wametoroka

na wanyama wamekimbia.

9:11 Ay 30:29; Isa 34:13; Law 26:31; Mao 1:4; Yer 26:18; Isa 25:2“Nitaifanya Yerusalemu lundo la magofu,

makao ya mbweha;

nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa

ili asiwepo atakayeishi humo.”

9:12 Za 107:43; Hos 14:9Ni mtu yupi aliye na hekima ya kutosha ayaelewe haya? Ni nani aliyefundishwa na Bwana awezaye kuyaeleza haya? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa ukiwa kama jangwa ambapo hakuna awezaye kupita?

9:13 2Nya 7:19; Za 89:30-32Bwana akasema, “Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu, niliyoiweka mbele yao: hawajaniheshimu mimi wala kufuata sheria yangu. 9:14 Amo 2:4; Yer 3:17; 7:24; 2:8Badala yake wamefuata ukaidi wa mioyo yao, wamefuata Mabaali, kama vile baba zao walivyowafundisha.” 9:15 Mao 3:15; Yer 8:14; Za 80:5Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: “Tazama, nitawafanya watu hawa wale chakula kichungu na kunywa maji yenye sumu. 9:16 Law 26:33; Kum 28:64; 4:32; Eze 5:12; Yer 44:27; 8:19Nitawatawanya katika mataifa ambayo wao wala baba zao hawakuwajua, nikiwafuata kwa upanga mpaka niwe nimewaangamiza kabisa.”

Read More of Yeremia 9