Yeremia 6:1-30, Yeremia 7:1-29 NEN

Yeremia 6:1-30

Yerusalemu Imezingirwa Na Jeshi

6:1 Yos 18:28; Neh 3:14; Yer 4:6; Hes 10:7; Yer 4:21; 2Nya 11:6“Kimbieni kwa usalama wenu, enyi watu wa Benyamini!

Kimbieni kutoka Yerusalemu!

Pigeni tarumbeta katika Tekoa!

Inueni ishara juu ya Beth-Hakeremu!

Kwa kuwa maafa yanaonekana yakitoka kaskazini,

na uharibifu wa kutisha.

6:2 Za 9:14; Mao 4:5Nitamwangamiza Binti Sayuni,

aliye mzuri sana na mwororo.

6:3 Yer 12:10; 2Fal 25:4; Lk 19:43Wachungaji pamoja na makundi yao

watakuja dhidi yake;

watapiga mahema yao kumzunguka,

kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.”

6:4 Yer 15:8; 22:7“Jiandaeni kwa vita dhidi yake!

Inukeni tumshambulie mchana!

Lakini, ole wetu, mchana unaisha,

na vivuli vya jioni vinazidi kuwa virefu.

Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku,

na kuharibu ngome zake!”

6:6 Kum 20:19-20; 2Sam 20:15; Eze 26:6-8; Kum 28:33; Yer 25:38; Sef 3:1Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“Kateni miti mjenge boma

kuzunguka Yerusalemu.

Mji huu ni lazima uadhibiwe,

umejazwa na uonevu.

6:7 Isa 58:4; Yer 20:8; Mik 7:2-3; Za 55:9-11Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake,

ndivyo anavyomwaga uovu wake.

Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake,

ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima.

6:8 Eze 23:18; Hos 9:12Pokea onyo, ee Yerusalemu,

la sivyo nitageukia mbali nawe

na kuifanya nchi yako kuwa ukiwa,

asiweze mtu kuishi ndani yake.”

Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“Wao na wayakusanye mabaki ya Israeli

kwa uangalifu kama kwenye mzabibu;

pitisha mkono wako kwenye matawi tena,

kama yeye avunaye zabibu.”

6:10 Kut 6:12; Yer 15:10-15; Mdo 7:51; Yer 20:8; 7:13; 35:15; Isa 42:20Niseme na nani na kumpa onyo?

Ni nani atakayenisikiliza mimi?

Masikio yao yameziba,6:10 Masikio yameziba kwa Kiebrania ina maana kwamba masikio yao hayajatahiriwa.

kwa hiyo hawawezi kusikia.

Neno la Bwana ni chukizo kwao,

hawalifurahii.

6:11 Yer 7:20; Ay 32:20; 2Nya 36:17; Isa 40:30; Yer 15:17; Mao 2:21Lakini nimejaa ghadhabu ya Bwana,

nami siwezi kuizuia.

“Wamwagie watoto walioko barabarani,

na juu ya vijana waume waliokusanyika;

mume na mke watakumbwa pamoja ndani yake,

hata nao wazee waliolemewa na miaka.

6:12 Kum 28:30; Yer 8:10; Mik 2:4; Yer 43:6; Sef 1:4; Eze 6:14; Yer 43:6; 38:22Nyumba zao zitapewa watu wengine,

pamoja na mashamba yao na wake zao,

nitakapounyoosha mkono wangu

dhidi ya wale waishio katika nchi,”

asema Bwana.

6:13 Isa 56:11; Yer 8:10; Mao 4:13; Yer 2:29“Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,

wote wana tamaa ya kupata faida zaidi;

manabii na makuhani wanafanana,

wote wanafanya udanganyifu.

6:14 Eze 13:10; Isa 30:10; Yer 4; 10Wanafunga majeraha ya watu wangu

bila uangalifu.

Wanasema, ‘Amani, amani,’

wakati hakuna amani.

6:15 Mik 3:7; Zek 13:7; Yer 3:3; 8:10-12; 2Nya 25:16; Yer 27:15Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao

inayochukiza mno?

Hapana, hawana aibu hata kidogo;

hawajui hata kuona haya.

Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka,

watashushwa chini nitakapowaadhibu,”

asema Bwana.

6:16 Yer 18:15; Lk 16:29; Yos 1:13; Mt 11:29; 1Fal 8:36; Isa 11:10Hivi ndivyo asemavyo Bwana:

“Simama kwenye njia panda utazame,

ulizia mapito ya zamani,

ulizia wapi ilipo njia nzuri, uifuate hiyo,

nanyi mtapata raha nafsini mwenu.

Lakini ninyi mlisema, ‘Hatutaipita hiyo.’

6:17 Yer 25:4; Isa 52:8; Eze 3:17; 33:4; Kut 20:18; Yer 11:7-8Niliweka walinzi juu yenu na kusema,

‘Sikieni sauti ya tarumbeta!’

Lakini mkasema, ‘Hatutasikiliza.’

6:18 Mit 1:31; Eze 20:13; Kum 4:26; Amo 2:4; Yer 22:29; Yos 23:15; Yer 11:11; 29:19Kwa hiyo sikilizeni, enyi mataifa,

angalieni, enyi mashahidi,

lile litakalowatokea.

Sikia, ee nchi:

Ninaleta maafa juu ya watu hawa,

matunda ya mipango yao,

kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu

na wameikataa sheria yangu.

6:20 Kut 30:23; Isa 60:6; Amo 5:22; Za 50:8-10; Hos 8:13; Mik 6:6-8; Mwa 10:7Unanifaa nini uvumba kutoka Sheba,

au udi wa harufu nzuri kutoka nchi ya mbali?

Sadaka zako za kuteketezwa hazikubaliki,

dhabihu zako hazinifurahishi mimi.”

6:21 Isa 8:14; Ay 5:12; Yer 13:16; Law 26:37Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyo Bwana:

“Nitaweka vikwazo mbele ya watu hawa.

Baba na wana wao watajikwaa juu yake,

majirani na marafiki wataangamia.”

6:22 Yer 4:6; Kum 28:49Hivi ndivyo asemavyo Bwana:

“Tazama, jeshi linakuja

kutoka nchi ya kaskazini,

taifa kubwa linaamshwa

kutoka miisho ya dunia.

6:23 Isa 5:30; 13:18; Yer 4:29; Za 18:4; 93:3; Isa 10:32Wamejifunga pinde na mkuki,

ni wakatili na hawana huruma.

Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma

wanapoendesha farasi zao.

Wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita

ili kukushambulia, ee Binti Sayuni.”

6:24 Za 48:6; Yer 4:19, 31; 50:41-43; Isa 13:7Tumesikia taarifa zao,

nayo mikono yetu imelegea.

Uchungu umetushika,

maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.

6:25 Ay 15:21; Za 31:13; Amo 5:6; Yer 49:29Usitoke kwenda mashambani

au kutembea barabarani,

kwa kuwa adui ana upanga,

na kuna vitisho kila upande.

6:26 Yer 4:8; Ay 2:8; Yon 3:6; Zek 12:10; Mwa 12:16; Yer 25:34; Eze 27:30; Kut 12:23Enyi watu wangu, vaeni magunia

mjivingirishe kwenye majivu,

ombolezeni kwa kilio cha uchungu

kama amliliaye mwana pekee,

kwa maana ghafula

mharabu atatujia.

6:27 Yer 9:7; Zek 13:9“Nimekufanya wewe kuwa kitu cha kujaribu chuma,

nao watu wangu kama mawe yenye madini,

ili upate kuzijua na kuzijaribu njia zao.

6:28 Yer 5:23; Eze 22:18; Yer 9:4; Law 19:16Wote ni waasi sugu,

wakienda huku na huko kusengenya.

Wao ni shaba na chuma,

wote wanatenda upotovu.

Mivuo inavuma kwa nguvu,

kinachoungua kwa huo moto ni risasi,

lakini pamoja na kusafisha kote huku ni bure;

waovu hawaondolewi.

6:30 Za 53:5; Mao 5:22; Hos 9:17; Mit 17:3; Eze 22; 18; Yer 7:29Wanaitwa fedha iliyokataliwa,

kwa sababu Bwana amewakataa.”

Read More of Yeremia 6

Yeremia 7:1-29

Dini Za Uongo Hazina Maana

Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana: 7:2 Yer 17:19; 19:2-3“Simama kwenye lango la nyumba ya Bwana, na huko upige mbiu ya ujumbe huu:

“ ‘Sikieni neno la Bwana, enyi watu wote wa Yuda mliokuja kupitia malango haya ili kumwabudu Bwana. 7:3 Yer 26:13; 35:13; 18:11Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Tengenezeni njia zenu na matendo yenu, nami nitawaacha mkae mahali hapa. 7:4 Yer 28:15; Mik 3:11; Ay 15:31Msitumainie maneno ya udanganyifu na kusema, “Hili ni Hekalu la Bwana, Hekalu la Bwana, Hekalu la Bwana!” 7:5 Kut 22:22; Law 25:17; Isa 1:17; Yer 26:13Kama kweli mkibadili njia zenu na matendo yenu, mkatendeana haki kila mmoja na mwenzake, 7:6 2Fal 21:16; Kum 8:19; Yer 22:3; Kut 20:3; Yer 5:28; Eze 22:7; Yer 2:34kama msipomwonea mgeni, yatima wala mjane, na kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa, nanyi kama msipofuata miungu mingine kwa madhara yenu wenyewe, 7:7 Kum 4:40; Yos 1:16ndipo nitawaacha mkae mahali hapa, katika nchi niliyowapa baba zenu milele na milele. Lakini tazama, mnatumainia maneno ya udanganyifu yasiyo na maana.

7:9 Yer 11:13-17; Kut 20:3; Hos 2:13; Kut 20:13-15; Law 19:12; Zek 8:17; Yer 32:29“ ‘Je, mtaiba na kuua, mtazini na kuapa kwa uongo, na kufukiza uvumba kwa Baali, na kufuata miungu mingine ambayo hamkuijua, 7:10 2Fal 21:4-5; Eze 23:38-39; Yer 23:11; 32:34; Eze 33:25kisha mje na kusimama mbele yangu katika nyumba hii inayoitwa kwa Jina langu, mkisema, “Tuko salama.” Salama kwa kufanya mambo haya yote ya kuchukiza? 7:11 Isa 56:7; Mt 21:13; Mk 11:17; Mwa 31:50; Amu 11:10; Hes 11:29; Lk 19:40; Yer 42:5Je, nyumba hii, iitwayo kwa Jina langu, imekuwa pango la wanyangʼanyi kwenu? Lakini nimekuwa nikiona yanayotendeka! asema Bwana.

7:12 1Sam 4:10; Yos 18:1; Za 78:60-64; 1Sam 2:32; Kut 40:2; Yos 18:10; Dan 9:18“ ‘Nendeni sasa mahali pangu palipokuwa huko Shilo, mahali ambapo nilipafanya pa kwanza kuwa makao ya Jina langu, nanyi mwone lile nililopafanyia kwa ajili ya uovu wa watu wangu Israeli. 7:13 2Nya 36:15; Isa 65:12; Yer 35:17; Za 71:17; Isa 48:17; Yer 32:33; Mit 1:24Mlipokuwa mnafanya yote haya, asema Bwana, nilisema nanyi tena na tena, lakini hamkusikiliza; niliwaita, lakini hamkujibu. Kwa hiyo, nililolifanyia Shilo, nitalifanya sasa kwa nyumba hii iitwayo kwa Jina langu, Hekalu mnalolitumainia, mahali nilipowapa ninyi na baba zenu. 7:15 Mwa 4:14; Kut 33; 15; 2Fal 17:20; Za 78:67; Yer 23:39Nitawafukuza mbele yangu, kama nilivyowafanyia ndugu zenu, watu wa Efraimu.’

7:16 Kut 32:10; Kum 9:14; Hes 23:19“Kwa hiyo usiombe kwa ajili ya watu hawa, wala usinililie, na usifanye maombi kwa ajili yao; usinisihi, kwa sababu sitakusikiliza. Je, huyaoni hayo wanayoyatenda katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu? 7:18 Yer 44:17; 19:13; Kum 31:17; 1Fal 14:9; Isa 57:6Watoto wanakusanya kuni, baba zao wanawasha moto, na wanawake wanakanda unga na kuoka mikate kwa ajili ya Malkia wa Mbinguni. Wanamimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha. 7:19 Ay 7:20; 1Kor 10:22; Yer 22:22; Kum 32:21; Yer 44:3; 9:19Lakini je, mimi ndiye wanayenikasirisha? asema Bwana. Je, hawajiumizi wenyewe na kujiaibisha?

7:20 Ay 40:11; Mao 2:3-5; Isa 30:15; Yer 42:18; 6:11-12; Mao 4:11; Eze 20:47-48“ ‘Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenyezi: Hasira yangu na ghadhabu yangu itamwagwa mahali hapa, juu ya mwanadamu na mnyama, juu ya miti ya shambani na juu ya matunda ya ardhini, nayo itaungua pasipo kuzimwa.

7:21 Isa 1:11; Amo 5:21-22; 1Sam 2:12-17; Hos 8:13; Yer 6:20; 7:22; Isa 43:23; 1Sam 15:22“ ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Endeleeni, ongezeni sadaka zenu za kuteketezwa juu ya dhabihu zenu nyingine, mle nyama hiyo wenyewe! Kwa kuwa nilipowaleta baba zenu kutoka Misri na kusema nao, sikuwapa amri kuhusu sadaka za kuteketezwa na dhabihu tu, 7:23 Kut 15:26; 19:5; Law 26:12; Kum 5:33; 1Yn 3:23; Isa 51:16; 1Fal 8:36; 7:24; Za 81:11-12; Kum 29:19; Yer 34:14; 6:10; 11:8; 17:23; 3:17; 2:19lakini niliwapa amri hii nikisema: Nitiini mimi, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Enendeni katika njia zote ninazowaamuru ili mpate kufanikiwa. Lakini hawakusikiliza wala kujali. Badala yake, walifuata ukaidi wa mioyo yao miovu. Walirudi nyuma badala ya kusonga mbele. 7:25 Neh 9:30; Yer 25:4; 2Nya 36:15; Isa 20:3; Hes 11:29; Yer 35:15Tangu wakati ule baba zenu walipotoka Misri hadi sasa, siku baada ya siku, tena na tena nimewatumia watumishi wangu manabii. 7:26 Za 81:11; Kut 32:9; Mdo 7:51; Yer 16:12; Lk 11:27Lakini hawakunisikiliza wala hawakujali. Walikuwa na shingo ngumu na kufanya maovu kuliko baba zao.’

7:27 Eze 2:7; Zek 7:13; Eze 3:7; Isa 65:12“Utakapowaambia haya yote, hawatakusikiliza; utakapowaita, hawatajibu. Kwa hiyo waambie, ‘Hili ni taifa ambalo halimtii Bwana, Mungu wao, wala kukubali maonyo. Kweli imekufa, imetoweka midomoni mwao. 7:29 Isa 15:2; Hos 11:8; Mik 5:3; Law 21:5; Ay 1:20; Yer 4:8; 6:30; 12:7Nyoeni nywele zenu na kuzitupa, ombolezeni katika miinuko iliyo kame, kwa kuwa Bwana amekikataa na kukiacha kizazi hiki kilichomkasirisha.

Read More of Yeremia 7