Yeremia 43:1-13, Yeremia 44:1-30, Yeremia 45:1-5 NEN

Yeremia 43:1-13

Yeremia Apelekwa Misri

43:1 Yer 26:8; 42:9-22Yeremia alipomaliza kuwaambia watu maneno yote ya Bwana Mungu wao, yaani kila kitu Bwana alichokuwa amemtuma kuwaambia, 43:2 Yer 40:16; 42:1-2; 41:16; Za 12:4; 2The 2:10-12; Neh 9:29; 1Kor 4:18-21; Mwa 19:14; 2Kor 11:31; Kum 13:3; Kut 24:7; Eze 37:18Azaria mwana wa Hoshaya, na Yohanani mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakamwambia Yeremia, “Wewe unasema uongo! Bwana Mungu wetu hajakutuma kusema, ‘Kamwe msiende Misri kukaa huko.’ 43:3 Yer 38:4; 52:30; 32:12; 41:18Lakini Baruku mwana wa Neria anakuchochea dhidi yetu ili ututie mikononi mwa Wakaldayo, ili watuue au watuchukue uhamishoni Babeli.”

43:4 2Nya 25:16; Yer 42:5-6, 10; 41:16Basi Yohanani mwana wa Karea, na maafisa wote wa jeshi, na watu wote wakakataa kutii amri ya Bwana ya kukaa katika nchi ya Yuda. 43:5 Yer 40:12Badala yake, Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi wakawaongoza mabaki yote ya Yuda waliokuwa wamerudi kuishi katika nchi ya Yuda kutoka mataifa yote ambayo walikuwa wametawanywa. 43:6 Yer 6:12; 32:12Pia wakawaongoza wanaume wote, wanawake na watoto, na binti za mfalme ambao Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme alikuwa amewaacha na Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, na nabii Yeremia, na Baruku mwana wa Neria. 43:7 2Fal 25:26; Yer 2:16; 46:14; Eze 30:18Kwa hiyo wakaingia Misri kwa kutokumtii Bwana, wakaenda mpaka Tahpanhesi.

43:8 Za 139:7; Yer 2:16Huko Tahpanhesi neno la Bwana likamjia Yeremia kusema: 43:9 Mwa 31:45-53; Yos 4:1-7; 1Fal 18:31-32; Mwa 47:14“Wayahudi wakiwa wanaona, chukua baadhi ya mawe makubwa na kuyazika katika udongo wa mfinyanzi katika njia iliyojengwa kwa matofali katika ingilio la jumba la kifalme la Farao huko Tahpanhesi. 43:10 Dan 2:21; Isa 44:22; Eze 29:18-20; Yer 25:9; 27:6; 46:13; 49:38; Za 18; 11Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Nitamtumania mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nami nitakiweka kiti chake cha enzi juu ya haya mawe niliyoyazika hapa, naye atatandaza hema yake ya ufalme juu yake. 43:11 Yer 46:13-26; Zek 11:9; Eze 32:11; 2Tim 1:7; Eze 29:19-20; Mit 11:19; Rum 6:23; Za 49:14Atakuja na kuishambulia Misri, akiwaua wale waliokusudiwa kuuawa, awateke mateka wale waliokusudiwa kutekwa, na upanga kwa wale waliokusudiwa upanga. 43:12 Kut 12:12; Zek 13:2; Za 109:18-19; 104:2; Yos 7:15; 1Fal 16:32; Isa 2:18; Yer 46:25; Eze 30:13; Dan 11:8Atachoma moto mahekalu yao ya miungu ya Misri, atachoma mahekalu yao na kuteka miungu yao. Kama vile mchungaji ajizungushiavyo vazi lake ndivyo atakavyojizungushia Misri na kuondoka mahali hapo bila kudhurika. Humo ndani ya hekalu la jua43:13 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua). nchini ya Misri atabomoa nguzo za ibada, na kuteketeza kwa moto mahekalu ya miungu wa Misri.’ ”

Read More of Yeremia 43

Yeremia 44:1-30

Maafa Kwa Sababu Ya Ibada Za Sanamu

44:1 Kut 14:2; Yer 43:7-8; Isa 19:13; 11:11; Yer 46:14; Kum 32:42; Yer 24:8Neno hili lilimjia Yeremia kuhusu Wayahudi wote waishio Misri, huko Migdoli, Tahpanhesi na Memfisi,44:1 Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu. katika nchi ya Pathrosi44:1 Pathrosi ina maana Misri ya Juu. kusema: 44:2 Law 26:31; Kum 29:23; Mik 3:12; Yer 6:11; 40:5; 2Nya 34:24“Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Mliona maangamizi makubwa niliyoyaleta juu ya Yerusalemu na juu ya miji yote ya Yuda. Leo imeachwa ukiwa na magofu 44:3 Hes 25:3; Isa 19:1; Kum 32:17; Yer 19:4; Amu 2:19; Kut 32:22; Hes 11:33; 16:40kwa sababu ya uovu waliokuwa wameufanya. Walinikasirisha kwa kufukiza uvumba na kwa kuabudu miungu mingine ambayo kamwe wao, wala ninyi, wala baba zenu hawakuifahamu. 44:4 Yer 7:13, 25; Hes 11:29; Kum 18; 9; 1Fal 14:24; 1Pet 4:3Tena na tena, niliwatuma watumishi wangu manabii ambao walisema, ‘Msifanye jambo hili la kuchukiza ambalo nalichukia!’ 44:5 Yer 11:8-10; 25:4; Dan 9; 6; Mwa 6:5; 2Tim 2:19; Eze 8:18; 16:18; 23:41Lakini hawakusikiliza wala hawakujali, hawakugeuka ili kuuacha uovu wao, wala hawakuacha kufukiza uvumba kwa miungu mingine. 44:6 Eze 8:18; 20:34; Law 26:31-34; Zek 7:14Kwa hiyo hasira yangu kali ilimwagika, ikawaka dhidi ya miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu, na kuifanya ukiwa na magofu kama ilivyo leo.

44:7 Yer 26:19; 51:22; Hes 16:36; Rum 1:23; 2Fal 21:14“Basi hili ndilo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Kwa nini kujiletea maafa makubwa kama haya juu yenu kwa kujikatilia mbali kutoka Yuda wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, hata kujiacha bila mabaki? 44:8 Isa 40:18-20; Rum 1:23; Yer 44:18; 1Kor 10:22; Za 44:13; Yer 41:5; Kut 12:12Kwa nini kuichochea hasira yangu kwa kile ambacho mikono yenu imekitengeneza, mkaifukizia uvumba miungu mingine huko Misri, mahali mlipokuja kuishi? Mtajiangamiza wenyewe na kujifanya kitu cha kulaania na shutumu miongoni mwa mataifa yote duniani. 44:9 Yer 11:12; 32:32; Amu 2:19; 2Fal 23:11; Mit 31:10; Yer 6:12; 1Fal 21:25Je, mmesahau uovu uliotendwa na baba zenu, na wafalme na malkia wa Yuda, na uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na barabara za Yerusalemu? 44:10 Mit 28:14; Gal 3:19; 2Fal 17:17; 1Fal 9:6-9; Mt 23:12; Flp 2:9; Kum 6:13; Mt 5:17-20Mpaka leo hawajajinyenyekeza au kuonyesha heshima, wala hawajafuata sheria yangu na amri nilizoweka mbele yenu na baba zenu.

44:11 2Nya 34:24; Amo 9:4; Yer 21:10; Ufu 4:8“Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Mimi nimekusudia kuleta maafa juu yenu, na kuiangamiza Yuda yote. 44:12 Yer 40:15; Isa 1:28; Zek 8:13; Yer 42:15-18; Kum 28:25; Yer 29:18Nitawaondoa mabaki ya Yuda waliokusudia kwenda Misri kukaa humo. Wote wataangamia huko Misri, wataanguka kwa upanga au kufa kwa njaa. Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana, watakufa kwa upanga au njaa. Watakuwa kitu cha kulaania na cha kutisha, cha laumu na shutumu. 44:13 Yer 42:17; Kut 32:34; Law 26:14-17; Yer 15:2Nitawaadhibu wale waishio Misri kwa upanga, njaa na tauni kama nilivyoiadhibu Yerusalemu. 44:14 Mao 4:15; Rum 9:27; Yer 22:24-27; 49:5; Eze 6:8Hakuna hata mmoja wa mabaki ya Yuda ambaye amekwenda kuishi Misri atakayeepuka au kunusurika ili kurudi katika nchi ya Yuda, ambayo wanaitamani sana kurudi na kuishi ndani yake, hakuna hata mmoja atakayerudi isipokuwa wakimbizi wachache.”

44:15 Mit 31:10; Yer 6:12; 18:15Kisha wanaume wote ambao walijua kwamba wake zao walikuwa wakifukiza uvumba kwa miungu mingine, pamoja na wanawake wote waliokuwako, yaani, kusanyiko kubwa na watu wote walioishi nchi ya Misri na Pathrosi, wakamwambia Yeremia, 44:16 1Sam 8; 19; Ay 15:25-26; Mit 1:24-27; Lk 19; 14; Yer 11:8-11; 42:19“Hatutausikiliza ujumbe uliotuambia katika jina la Bwana! 44:17 Kum 23:23; Yer 7:18; Hes 30:12; Ay 21:15; Isa 3:9; 65:3; Neh 9:34; Yer 2:26; Hes 11:4-6; Kut 16:3; Hos 2:5-13Hakika tutafanya kila kitu tulichosema tutakifanya: Tutafukiza uvumba kwa Malkia wa Mbinguni na tutammiminia sadaka zetu za kinywaji kama vile sisi na baba zetu, wafalme wetu na maafisa wetu tulivyofanya katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu. Wakati ule tulikuwa na chakula tele, tulikuwa matajiri wala hatukupata dhara lolote. 44:18 Mal 3:13-15; Law 23:18; Yer 42:16Lakini tangu tulipoacha kumfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka za kinywaji, hatupati chochote, na tumekuwa tukiangamizwa kwa upanga na njaa.”

44:19 Yer 7:18; 18:15; Efe 5:22; Mwa 3:6; Law 7:12; Mdo 17:29Wanawake wakaongeza kusema, “Wakati tulipomfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka zetu za kinywaji, je, waume zetu hawakujua kwamba tulikuwa tukitengeneza maandazi kwa mfano wake, na kummiminia yeye sadaka za kinywaji?”

Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake waliokuwa wakimjibu, 44:21 Isa 64:5; Hos 8:13; Yer 11:13; Za 79:8; Yer 14:10; 2:26“Je, Bwana hakukumbuka na kufikiri juu ya uvumba uliofukizwa katika miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu na ninyi pamoja na baba zenu, wafalme wenu, maafisa wenu na watu wa nchi? 44:22 Mwa 19:13; Yer 25:18; Eze 33:28-29; Amo 2:13; Isa 1:14; Za 107:33-34Bwana alipokuwa hawezi kuendelea kuvumilia matendo yenu maovu na mambo ya machukizo mliyoyafanya, nchi yenu ilikuwa kitu cha kulaania na kuachwa ukiwa pasipo wakazi, kama ilivyo leo. 44:23 Yer 40:2; Law 26:33; Dan 9:11-12; 1Fal 9:6; Law 18:4; Yer 7:13-15; Eze 39:23Kwa sababu mmefukiza uvumba na kufanya dhambi dhidi ya Bwana, nanyi hamkumtii wala kufuata sheria yake au amri zake au maagizo yake, maafa haya yamekuja juu yenu, kama mnavyoona sasa.”

44:24 Mwa 3:6; Yer 43:7Kisha Yeremia akawaambia watu wote, pamoja na wanawake, “Sikieni neno la Bwana, enyi watu wote wa Yuda mlioko Misri. 44:25 Kum 32:28; Mit 20:25; Yak 1:13-15; Mit 31:10; Eze 20:29Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Ninyi na wake zenu mmeonyesha kwa matendo yenu kile mlichoahidi mliposema, ‘Hakika tutatimiza nadhiri tulizoziweka za kumfukizia uvumba na kummiminia sadaka za kinywaji Malkia wa Mbinguni.’

“Endeleeni basi, fanyeni yale mliyoahidi! Timizeni nadhiri zenu! 44:26 Mwa 22:16; Mdo 19:13; Za 50:16; Kum 32:40; Yer 24:8; Ebr 6:13-17; Mwa 15:2Lakini sikieni neno la Bwana, enyi Wayahudi wote mnaoishi Misri: ‘Ninaapa kwa Jina langu lililo kuu,’ asema Bwana, ‘kwamba hakuna hata mmoja atokaye Yuda anayeishi popote Misri ambaye kamwe ataomba tena kwa Jina langu au kuapa, akisema, “Hakika kama Bwana Mwenyezi aishivyo.” 44:27 Yer 21:10; 31:28; Eze 7:6; Yer 1:12; Ay 15:22; 2Pet 3:8-9; Dan 9:14; Amo 9:8Kwa maana ninawaangalia kwa ajili ya madhara, wala sio kwa mema. Wayahudi walioko Misri wataangamia kwa upanga na njaa, hadi wote watakapoangamizwa. 44:28 Isa 27:13; 10:19; Hab 3:2; Yer 45:5; Eze 6:8; Yer 39:16; 42:15-18Wale watakaonusurika upanga na kurudi katika nchi ya Yuda kutoka Misri watakuwa wachache sana. Ndipo mabaki wote wa Yuda waliokuja kuishi Misri watakapojua ni neno la nani litakalosimama, kwamba ni langu au lao.

44:29 Mwa 24:14; Kut 3:12; Hes 16:38; Mt 12:38; Mit 19:21“ ‘Hii itakuwa ndiyo ishara kwenu kwamba nitawaadhibu mahali hapa, asema Bwana, ili mpate kujua kuwa onyo langu la madhara dhidi yenu hakika litatimizwa.’ 44:30 Eze 29:3; Yer 25:19; Eze 32:32; Yer 24:8; 43:9-13; 2Fal 25:1-7Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Nitamtia Farao Hofra mfalme wa Misri mikononi mwa adui zake wanaoutafuta uhai wake, kama vile nilivyomtia Sedekia mfalme wa Yuda mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, adui aliyekuwa akiutafuta uhai wake.’ ”

Read More of Yeremia 44

Yeremia 45:1-5

Ujumbe Kwa Baruku

45:1 Yer 32:12; 36:18, 32; Isa 50:4; Yer 51:59; Kut 17:14; Za 40:7; 2Nya 36:5Hili ndilo nabii Yeremia alilomwambia Baruku mwana wa Neria katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, baada ya Baruku kuandika katika kitabu maneno ambayo yalitoka kinywani mwa Yeremia wakati ule: “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, akuambialo wewe Baruku: 45:3 Ay 23:2; Za 69:3; Isa 24:16; 1Kor 9:16; Mk 14:34; Rum 9:2; Ay 6:10; Ebr 4:3; Mt 11:24Ulisema, ‘Ole wangu! Bwana ameongeza huzuni juu ya maumivu yangu, nimechoka kwa kulia kwa uchungu wala sipati pumziko.’ ”

45:4 Isa 5:5; Yer 11:17; Kum 30:9; Yer 42:10; 18:7-10; Kum 28:63Bwana akasema, “Mwambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Nitakibomoa kile nilichokijenga, na kungʼoa kile nilichokipanda katika nchi yote. 45:5 Mt 6:25-27, 33; Yer 21:9; 32:8; 11:11; 40:2; 2:35; Za 68:20Je, utajitafutia mambo makubwa kwa ajili yako mwenyewe? Usiyatafute hayo. Kwa kuwa nitaleta maangamizi juu ya watu wote, asema Bwana, lakini popote utakapokwenda, nitayaokoa maisha yako.’ ”

Read More of Yeremia 45