Yeremia 4:10-31, Yeremia 5:1-31 NEN

Yeremia 4:10-31

4:10 Eze 14:9; Kut 5:23; 2The 2:11; Isa 63:17; Yer 6:14; 8:11; Eze 13:10; Mik 3:5Ndipo niliposema, “Aa, Bwana Mwenyezi, umewadanganyaje kabisa watu hawa na Yerusalemu kwa kusema, ‘Mtakuwa na amani,’ wakati upanga uko kwenye koo zetu!”

4:11 Mwa 41:6; Hos 13:15; Eze 17:10; Law 26:33; Ay 1:19Wakati huo watu hawa na Yerusalemu wataambiwa, “Upepo wa moto kutoka miinuko iliyo kame katika jangwa unavuma kuelekea watu wangu, lakini sio kupepeta au kutakasa, 4:12 Isa 64:6; Yer 1:16upepo wenye nguvu sana kuliko wa kupepeta na kutakasa utakuja kwa amri yangu. Sasa natangaza hukumu zangu dhidi yao.”

4:13 Isa 5:28; 2Sam 22:10; Eze 26:10; Kum 28:49; Mao 4:19; Isa 66:15Tazama! Anakuja kama mawingu,

magari yake yanakuja kama upepo wa kisulisuli,

farasi wake wana mbio kuliko tai.

Ole wetu! Tunaangamia!

4:14 Rut 3; 3; Yak 4:8; Za 51:2; Isa 45:22; Za 6:3Ee Yerusalemu, usafishe uovu kutoka moyoni mwako na uokolewe.

Utaendelea kuficha mawazo mapotovu mpaka lini?

4:15 Yer 8:16; Mwa 30:6; Yer 31:6Sauti inatangaza kutoka Dani,

ikipiga mbiu ya maafa kutoka vilima vya Efraimu.

“Waambie mataifa jambo hili,

piga mbiu hii dhidi ya Yerusalemu:

‘Jeshi la kuzingira linakuja kutoka nchi ya mbali,

likipiga kelele ya vita dhidi ya miji ya Yuda.

4:17 2Fal 25:1-4; 1Sam 12:15; Yer 5:23Wamemzunguka kama watu walindao shamba,

kwa sababu amefanya uasi dhidi yangu,’ ”

asema Bwana.

4:18 Za 107:17; Ay 20:6-11; Yer 2:17-19; Isa 1:28; Yer 5:25“Mwenendo wako na matendo yako mwenyewe

yameleta haya juu yako.

Hii ndiyo adhabu yako.

Tazama jinsi ilivyo chungu!

Tazama jinsi inavyochoma moyo!”

4:19 Isa 16:11; Mao 1:20; Hes 10:9; Yer 20:9; Sef 1:16; Isa 22:4; Yer 6:24Ee mtima wangu, mtima wangu!

Ninagaagaa kwa maumivu.

Ee maumivu makuu ya moyo wangu!

Moyo wangu umefadhaika ndani yangu,

siwezi kunyamaza.

Kwa sababu nimesikia sauti ya tarumbeta,

nimesikia kelele ya vita.

4:20 Kum 31:17; Za 42:7; Hes 24:5; Mao 2:4; Yer 10:20Maafa baada ya maafa,

nchi yote imekuwa magofu.

Kwa ghafula mahema yangu yameangamizwa,

makazi yangu kwa muda mfupi.

4:21 Hes 2:2; Isa 18:3; Yos 6:20; Hos 5:8Hata lini nitaendelea kuona bendera ya vita

na kusikia sauti za tarumbeta?

4:22 1Kor 14:20; Yer 5:21; 13:23; Za 36:3; Rum 16:19; Yer 5:21; 10:8; Za 14:4“Watu wangu ni wapumbavu,

hawanijui mimi.

Ni watoto wasio na akili,

hawana ufahamu.

Ni hodari kutenda mabaya,

hawajui kutenda yaliyo mema.”

4:23 Ay 9:7; 30:26; Isa 5:30; 59:9; Mao 3:2Niliitazama dunia,

nayo haikuwa na umbo tena ni tupu;

niliziangalia mbingu,

mianga ilikuwa imetoweka.

4:24 Eze 38:20; Ay 9:6; Isa 5:25; Kut 19:18Niliitazama milima, nayo ilikuwa ikitetemeka,

vilima vyote vilikuwa vikiyumbayumba.

4:25 Hos 4:3; Sef 1:3; Yer 7:20Nilitazama, wala watu hawakuwepo;

kila ndege wa angani alikuwa ameruka zake.

Nilitazama, hata nchi iliyokuwa imestawi vizuri imekuwa jangwa,

miji yake yote ilikuwa magofu

mbele za Bwana,

mbele ya hasira yake kali.

4:27 Amo 9:8; Yer 5:10; 12:12; Eze 20:17; Yer 46:28Hivi ndivyo Bwana asemavyo:

“Nchi yote itaharibiwa,

ingawa sitaiangamiza kabisa.

4:28 Yer 14:2; Hos 4:3; Hes 23:19; Isa 5:30; Yer 30:24; 23:20; 12:4-11Kwa hiyo dunia itaomboleza

na mbingu zilizo juu zitakuwa giza,

kwa sababu nimesema nami sitarudi nyuma,

nimeamua na wala sitageuka.”

4:29 Yer 8:16; Isa 6:12; 2Fal 25:4; Yer 6:23; 1Sam 26:20; Kut 33:22Kwa sauti ya wapanda farasi na wapiga upinde

kila mji unakimbia.

Baadhi wanakimbilia vichakani,

baadhi wanapanda juu ya miamba.

Miji yote imeachwa,

hakuna aishiye ndani yake.

4:30 Isa 10:3-4; Eze 16:11; 23:40; 2Fal 9:30; Ay 19:14; Eze 23:9; Za 35:4Unafanya nini, ewe uliyeharibiwa?

Kwa nini unajivika vazi jekundu

na kuvaa vito vya dhahabu?

Kwa nini unapaka macho yako rangi?

Unajipamba bure.

Wapenzi wako wanakudharau,

wanautafuta uhai wako.

4:31 Mwa 3:16; Mik 4:10; Isa 42:14; Mao 1:17; Yer 6:24; 13:21; 22:23; Za 9:14; Isa 42:14; Kum 32:25; Mao 2:21Nasikia kilio kama cha mwanamke

katika utungu wa kuzaa,

kilio cha uchungu kama cha anayemzaa

mtoto wake wa kwanza:

kilio cha Binti Sayuni akitweta ili aweze kupumua,

akiinua mikono yake, akisema,

“Ole wangu! Ninazimia;

maisha yangu yamekabidhiwa kwa wauaji.”

Read More of Yeremia 4

Yeremia 5:1-31

Hakuna Hata Mmoja Aliye Mkamilifu

5:1 Eze 22:30; Mwa 18:24; Mik 7:2; Yer 2:29; 2Nya 16:9; Za 45:10“Pandeni na kushuka katika mitaa ya Yerusalemu,

tazameni pande zote na mtafakari,

tafuteni katika viwanja vyake.

Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja tu

atendaye kwa uaminifu na kutafuta kweli,

nitausamehe mji huu.

5:2 Tit 1:16; Yer 4:2; Law 19:12Ingawa wanasema, ‘Kwa hakika kama Bwana aishivyo,’

bado wanaapa kwa uongo.”

5:3 2Nya 16:9; Yer 7:28; Isa 9:13; Sef 3:2; Zek 7:2; Eze 36:26; 3:8-9; Amo 4:6Ee Bwana, je, macho yako hayaitafuti kweli?

Uliwapiga, lakini hawakusikia maumivu,

uliwapondaponda, lakini walikataa maonyo.

Walifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko jiwe

nao walikataa kutubu.

5:4 Yer 8:7; Mit 10:21; Yer 4:22Ndipo nikasema, “Hawa ni maskini tu;

wao ni wapumbavu,

kwa maana hawaijui njia ya Bwana,

sheria ya Mungu wao.

5:5 Mik 3:1, 9; Za 2:3; Yer 2:20Kwa hiyo nitakwenda kwa viongozi

na kuzungumza nao,

hakika wao wanaijua njia ya Bwana,

sheria ya Mungu wao.”

Lakini kwa nia moja nao pia walikuwa wameivunja nira

na kuvivunja vifungo.

5:6 Hos 13:7; Yer 4:7; 30:14; Za 7:12; Law 26:22Kwa hiyo simba kutoka mwituni atawashambulia,

mbwa mwitu kutoka jangwani atawaangamiza,

chui atawavizia karibu na miji yao,

ili kumrarua vipande vipande yeyote atakayethubutu kutoka nje,

kwa maana maasi yao ni makubwa,

na kukengeuka kwao kumekuwa ni kwingi.

5:7 Yos 23:7; Yer 12:16; Gal 4:8; Amo 8:14; Kum 32:21; Hes 25:1; Yer 2:11; 13:27“Kwa nini niwasamehe?

Watoto wenu wameniacha na kuapa kwa miungu ambayo si miungu.

Niliwapatia mahitaji yao yote,

lakini bado wamefanya uzinzi na kusongana katika nyumba za makahaba.

5:8 Eze 22:11; 2Sam 11:2-4; Eze 33:26; Yer 29:23Wamelishwa vizuri, kama farasi waume wenye tamaa nyingi,

kila mmoja akimlilia mke wa mwanaume mwingine.

5:9 Yer 44:22; Eze 7:9; Isa 1:24; 57:6Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?”

asema Bwana.

“Je, nisijilipizie kisasi

juu ya taifa kama hili?

5:10 Yer 39:8; 4:27; Amo 9:8“Piteni katika mashamba yake ya mizabibu na kuyaharibu,

lakini msiangamize kabisa.

Pogoeni matawi yake,

kwa kuwa watu hawa sio wa Bwana.

5:11 1Fal 19:10; Yer 3:20; Za 73:27; Isa 24:16Nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda

wamekuwa si waaminifu kwangu kamwe,”

asema Bwana.

5:12 Yer 23:17; 2Nya 36:16; Yer 28:7; Isa 28:15; Yer 14:13Wamedanganya kuhusu Bwana.

Wamesema, “Yeye hatafanya jambo lolote!

Hakuna dhara litakalotupata;

kamwe hatutaona upanga wala njaa.

5:13 Yer 14:15; 2Nya 36:16; Ay 6:26Manabii ni upepo tu, wala neno halimo ndani yao,

kwa hiyo hayo wayasemayo na yatendeke kwao.”

5:14 Hos 6:5; Yer 1:9; 23:9; Za 39:3Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote:

“Kwa sababu watu hawa wamesema maneno haya,

nitayafanya maneno yangu vinywani mwenu kuwa moto,

na watu hawa wawe kuni

zinazoliwa na huo moto.

5:15 Kum 28:49; Isa 5:26; 2Fal 24:2; Isa 28:11; Mwa 11:7Ee nyumba ya Israeli,” asema Bwana,

“Ninaleta taifa toka mbali dhidi yako,

taifa la kale na linaloendelea kudumu,

taifa ambalo lugha yao huijui,

wala msemo wao huwezi kuuelewa.

5:16 Ay 39:23Podo zao ni kama kaburi lililo wazi,

wote ni mashujaa hodari wa vita.

5:17 Yer 30:16; Law 26:16; Yer 50:7-17; Kum 28:31-33; Yer 8:16; Hes 16:14; Hos 2:12Watayaangamiza mazao yenu na chakula chenu,

wataangamiza wana wenu na mabinti zenu;

wataangamiza makundi yenu ya kondoo na ya ngʼombe,

wataangamiza mizabibu yenu na mitini yenu.

Kwa upanga wataangamiza

miji yenye maboma mliyoitumainia.

“Hata hivyo katika siku hizo, sitakuangamiza kabisa,” asema Bwana. 5:19 Kum 29:24-26; 4:28; Yer 15:4; 13:22; 1Fal 9; 9; Yer 16:13“Nao watu watakapouliza, ‘Kwa nini Bwana, Mungu wetu ametufanyia mambo haya yote?’ utawaambia, ‘Kama vile mlivyoniacha mimi na kutumikia miungu migeni katika nchi yenu wenyewe, ndivyo sasa mtakavyowatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.’

“Itangazie nyumba ya Yakobo hili

na ulipigie mbiu katika Yuda:

5:21 Isa 6:10; Eze 12:2; Mdo 28:26; Isa 42:20; Mk 8:18; Kum 32:6; Yer 4:22; Hes 2:18Sikieni hili, enyi watu wapumbavu, msio na akili,

mlio na macho lakini hamwoni,

mlio na masikio lakini hamsikii:

5:22 Kum 28:58; Ay 4:14; Isa 64:2; Za 46:3Je, haiwapasi kuniogopa mimi?” asema Bwana.

“Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu?

Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari,

kizuizi cha milele ambacho haiwezi kupita.

Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita;

yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka.

5:23 Kum 21:18; Za 14:3Lakini watu hawa wana mioyo ya ukaidi na ya uasi,

wamegeukia mbali na kwenda zao.

5:24 Mt 5:45; Yoe 2:23; Mwa 8:22; Mdo 14:17; Kum 6:24; Yak 5:7Wao hawaambiani wenyewe,

‘Sisi na tumwogope Bwana Mungu wetu,

anayetupatia mvua za masika na za vuli kwa majira yake,

anayetuhakikishia majuma ya mavuno kwa utaratibu.’

Matendo yenu mabaya yamezuia haya yote,

dhambi zenu zimewazuia msipate mema.

5:26 Za 10:8; Mit 1:11; Mt 7; 15; Mhu 9:12; Yer 9:8; Mik 7:2“Miongoni mwa watu wangu wamo walio waovu

wanaovizia kama watu wanaotega ndege,

na kama wale wanaoweka mitego

kuwakamata watu.

Kama vitundu vilivyojaa ndege,

nyumba zao zimejaa udanganyifu;

wamekuwa matajiri na wenye nguvu,

5:28 Kum 32:15; Zek 7:10; Kut 22:21-24; Amo 5:12; Za 73:12; 82:3wamenenepa na kunawiri.

Matendo yao maovu hayana kikomo;

hawatetei mashauri ya yatima wapate kushinda,

hawatetei haki za maskini.

Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?”

asema Bwana.

“Je, nisijilipizie kisasi

juu ya taifa kama hili?

5:30 Yer 18:13; Hos 6:10; Yer 23:14“Jambo la kutisha na kushtusha

limetokea katika nchi hii:

5:31 Eze 13:6; Isa 30:10; Mik 2:11; Mao 4:13; Hos 9:5Manabii wanatabiri uongo,

makuhani wanatawala kwa mamlaka yao wenyewe,

nao watu wangu wanapenda hivyo.

Lakini mtafanya nini mwisho wake?

Read More of Yeremia 5