Yeremia 32:26-44, Yeremia 33:1-26, Yeremia 34:1-22 NEN

Yeremia 32:26-44

Ndipo neno la Bwana likamjia Yeremia kusema: 32:27 Hes 16:22; Mwa 18:14; 2Fal 3:18“Mimi ndimi Bwana, Mungu wa wote wenye mwili. Je, kuna jambo lolote lililo gumu nisiloliweza? 32:28 2Nya 36:17; Yer 21:10Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa Wakaldayo, na mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ambaye atauteka. 32:29 Yer 19:13; 52:13; 44:18; 7:9Wakaldayo ambao wanaushambulia mji huu watakuja na kuuchoma moto na kuuteketeza, pamoja na nyumba ambamo watu wamenikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba katika mapaa na kumimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine.

32:30 Za 25:7; Yer 22:21; 8:19; 25:7“Watu wa Israeli na wa Yuda hawakufanya kitu kingine ila uovu mbele zangu tangu ujana wao. Naam, watu wa Israeli hawakufanya kitu kingine ila kunikasirisha kwa kazi ambazo mikono yao imetengeneza, asema Bwana. 32:31 2Fal 23:27; 24:3; Sef 3:1; Mt 23:37; 2Fal 21:4-5; 1Fal 11:7-8Tangu siku ulipojengwa hadi sasa, mji huu umenikasirisha na kunighadhibisha kiasi kwamba ni lazima niuondoe machoni pangu. 32:32 Isa 1:4-6; Dan 9:8; 1Fal 14:9; Yer 2:26; 44:9Watu wa Israeli na wa Yuda wamenikasirisha kwa uovu wote waliofanya: wao, wafalme wao na maafisa wao, makuhani wao na manabii wao, watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu. 32:33 1Fal 14:9; Za 14:3; Kum 4:5; Isa 28:9; Yer 7:13, 28; 2:27; Eze 8:16; Zek 7:11Walinigeuzia visogo vyao, wala si nyuso zao. Ingawa niliwafundisha tena na tena, hawakupenda kusikiliza wala kuitikia adhabu. 32:34 Yer 7:30; Eze 8:3-16Waliweka miungu yao ya kuchukiza sana katika nyumba iitwayo kwa Jina langu na kuinajisi. 32:35 Law 18:21; Yer 7:31; 2Fal 23:10; Yer 19:5; 25:7Wakajenga mahali pa juu pa kuabudia miungu kwa ajili ya Baali katika Bonde la Ben-Hinomu, ambapo walitoa wana wao na binti zao kafara kwa Moleki, ingawa kamwe sikuamuru, wala halikuingia akilini mwangu, kwamba watafanya chukizo kama hilo na kumfanya Yuda atende dhambi.

“Mnasema kuhusu mji huu, ‘Kwa upanga, njaa na tauni, mji utatiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli,’ lakini hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli asemalo: 32:37 Isa 11:12; Yer 23:3-6; Law 25:18; Kum 30:3; Eze 34:28; 39:26; Yer 21:5Hakika nitawakusanya kutoka nchi zote nilizowafukuzia katika hasira yangu kali na ghadhabu yangu kuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwaruhusu waishi kwa salama. 32:38 Yer 24:7; 2Kor 6:16Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao. 32:39 Eze 11:19; Yn 17:21; 2Nya 30:12; Mdo 4:32; Kum 6:24; 10:16; Za 86:11Nitawapa moyo mmoja na kutenda pamoja, ili kwamba waniche daima kwa mema yao wenyewe na kwa mema ya watoto wao baada yao. 32:40 Mwa 9:16; Isa 55:3; Yer 24; 7; Isa 42:6; Kum 4:10Nitafanya nao agano la milele: Kamwe sitaacha kuwatendea mema, nami nitawavuvia kunicha mimi, ili kamwe wasigeukie mbali nami. 32:41 Kum 28:3-12; Yer 24:6; Kum 30; 9; Amo 9:15; Yer 31:28; Isa 62:4; Mik 7:18Nitafurahia kuwatendea mema, na kwa hakika nitawapanda katika nchi hii kwa moyo wangu wote na roho yangu yote.

32:42 Yer 29:10; 31:28; Mao 3:38“Hili ndilo asemalo Bwana: Kama nilivyoleta maafa haya makubwa kwa watu hawa, ndivyo nitakavyowapa mafanikio niliyowaahidi. Kwa mara nyingine tena mashamba yatanunuliwa katika nchi hii ambayo mlisema, ‘Imekuwa ukiwa, isiyofaa, isiyo na watu wala wanyama, kwa sababu imetiwa mikononi mwa Wakaldayo.’ 32:44 Yer 17:26; Ezr 9:9; Yer 33:7, 11, 26; Rut 4:9; Isa 8:2; Za 14:7Mashamba yatanunuliwa kwa fedha, na hati zitatiwa sahihi, zitatiwa muhuri na kushuhudiwa katika nchi ya Benyamini, katika vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu, katika miji ya Yuda na katika miji ya nchi ya vilima, sehemu za magharibi katika miji ya tambarare na katika Negebu, kwa sababu nitarudisha tena mafanikio yao,32:44 Au: nitawarudisha tena kutoka utumwani. asema Bwana.”

Read More of Yeremia 32

Yeremia 33:1-26

Ahadi Ya Kurudishwa

33:1 Yer 32:2; 37:21; 38:28; Za 88:8; Yer 13:3Wakati Yeremia alipokuwa angali amefungwa kwenye ua wa walinzi, neno la Bwana lilimjia mara ya pili kusema: 33:2 Yer 10:16; Za 136:6; Kut 3:15; 15:3“Hili ndilo Bwana asemalo, yeye aliyeumba dunia, Bwana aliyeifanya na kuithibitisha, Bwana ndilo jina lake: 33:3 Mwa 18:17; Yer 29:12; Isa 55:6; Ay 28:11‘Niite nami nitakuitika na kukuambia mambo makuu na yasiyochunguzika, usiyoyajua.’ 33:4 2Fal 25:1; Eze 4:2; 26:8; Hab 1:10; Yer 32:24Kwa maana hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu nyumba katika mji huu na majumba ya kifalme ya Yuda yaliyobomolewa ili yatumiwe dhidi ya kule kuzungukwa na jeshi na upanga 33:5 Yer 21:4-7; Kum 31:17; Isa 8:17katika kupigana na Wakaldayo: ‘Zitajazwa na maiti za watu nitakaowachinja katika hasira na ghadhabu yangu. Nitauficha uso wangu kwa sababu ya maovu yake yote.

33:6 Kum 32:39; Isa 30:26; 9:6“ ‘Hata hivyo, nitauletea afya na uponyaji, nitawaponya watu wangu na kuwafanya wafurahie amani tele na salama. 33:7 Yer 32:44; Eze 39:25; Amo 9:14; Isa 1:26; Yer 24:6; 30:3Nitawarudisha Yuda na Israeli kutoka nchi ya kutekwa kwao, na kuwajenga tena kama walivyokuwa hapo awali. 33:8 Law 16:30; Ebr 9:13-14; 2Sam 24:14; Mik 7:18; Yer 31:34Nitawatakasa dhambi zote walizofanya dhidi yangu, na nitawasamehe dhambi zote za uasi dhidi yangu. 33:9 Isa 60:18; Yer 13:11; Isa 64:2; Yer 3:17; 1Yn 1:7-9; Isa 55:13Kisha mji huu utaniletea utukufu, furaha, sifa na heshima mbele ya mataifa yote ya dunia yatakayosikia mambo yote mazuri ninayoufanyia. Nao watashangaa na kutetemeka kwa ajili ya wingi wa mafanikio na amani nitakayoupatia.’

33:10 Yer 32:43; 9:11“Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Mnasema kuhusu mahali hapa kwamba, “Ni mahali palipoachwa ukiwa, pasipo na wanadamu wala wanyama.” Lakini katika miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu ambazo zimeachwa, ambazo hazikaliwi na wanadamu wala wanyama, huko kutasikika kwa mara nyingine 33:11 Za 51:8; 24:8; Law 7:12; 2Nya 5:13; Za 25:8; 100:4-5; 14:7sauti za shangwe na furaha, sauti za bibi na bwana arusi, na sauti za wale waletao sadaka za shukrani katika nyumba ya Bwana, wakisema,

“ ‘ “Mshukuruni Bwana Mwenye Nguvu Zote,

kwa maana Bwana ni mwema;

upendo wake wadumu milele.”

Kwa kuwa nitairudishia nchi baraka kama zilivyokuwa hapo awali,’ asema Bwana.

33:12 Yer 32:43; Isa 65:10; Eze 34:11-15“Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Mahali hapa, ambapo ni ukiwa, pasipo na wanadamu wala wanyama: katika miji yake, patakuwepo tena malisho kwa ajili ya wachungaji kupumzisha makundi yao ya kondoo. 33:13 Yer 32:43; Isa 65:10; Eze 34:11-15Katika miji ya nchi ya vilima, ya vilima vya magharibi na ya Negebu, katika nchi ya Benyamini, katika vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu na katika miji ya Yuda, makundi ya kondoo yatapita tena chini ya mkono wa yeye ayahesabuye,’ asema Bwana.

33:14 Kum 28:1-14; Yos 23:15; Yer 29:10“ ‘Siku zinakuja,’ asema Bwana, ‘wakati nitakapotimiza ahadi yangu ya rehema niliyoifanya kwa nyumba ya Israeli na kwa nyumba ya Yuda.

33:15 Isa 4:2; Za 72:2; Isa 11:1; 2Sam 7:12“ ‘Katika siku hizo na wakati huo

nitalifanya Tawi la haki lichipuke kutoka ukoo wa Daudi,

naye atafanya lile lililo haki na sawa

katika nchi.

33:16 Isa 45:17; 1Kor 1:30; Zek 8:3, 16; Sef 3:13; Eze 48:35; Yer 3:17; Isa 59:14; Yer 32:37Katika siku hizo, Yuda ataokolewa

na Yerusalemu ataishi salama.

Hili ndilo jina atakaloitwa:

Bwana Haki Yetu.’

33:17 2Sam 7:13; 2Nya 7:18; Za 89:29-37Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana: ‘Daudi kamwe hatakosa mtu wa kukalia kiti cha enzi cha nyumba ya Israeli, 33:18 Kum 18:1; Ebr 13:15; Hes 25:11-13; Ebr 7:17-22wala hata makuhani, ambao ni Walawi, kamwe hawatakosa mtu wa kusimama mbele zangu daima ili kutoa sadaka za kuteketezwa, ili kuteketeza sadaka ya nafaka na kutoa dhabihu.’ ”

Neno la Bwana likamjia Yeremia kusema: 33:20 Za 89:36; Mwa 8:22; Isa 54:9; Mwa 1:14“Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Ikiwa mtaweza kuvunja agano langu kuhusu usiku na mchana, ili usiku na mchana visiwepo kwa nyakati zake, 33:21 Za 89:34; 2Sam 7:13-18; 2Nya 7:18basi agano langu na Daudi mtumishi wangu, na agano langu na Walawi ambao ni makuhani wanaohudumu mbele zangu, linaweza kuvunjwa, na Daudi hatakuwa tena na mzao wa kutawala katika kiti chake cha enzi. 33:22 Mwa 15:5; Hos 1:10; Mwa 13:16; Yer 30:19; Mwa 12:2Nitawafanya wazao wa Daudi mtumishi wangu na Walawi wanaohudumu mbele zangu wengi, wasioweza kuhesabika kama nyota za angani, tena wasiopimika kama mchanga wa ufuoni mwa bahari.’ ”

Neno la Bwana likamjia Yeremia kusema: 33:24 Eze 37:22; Neh 4:4; Yer 30:17; Eze 36:20“Je, hujasikia kwamba watu hawa wanasema, ‘Bwana amezikataa zile falme mbili alizozichagua?’ Kwa hiyo wamewadharau watu wangu, na hawawaoni tena kama taifa. 33:25 Mwa 1:18; Yer 31:35-36; Za 74:16-17; 148:6Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Kama sijathibitisha agano langu na usiku na mchana, na kuziweka wakfu sheria za mbingu na nchi, 33:26 Law 26:44; Yer 31:37; Isa 14:1; Zek 10:6; Za 14:7; Yer 30:18basi nitawakataa wazao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na sitachagua mmoja wa wanawe kutawala juu ya wazao wa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha kutoka nchi ya kutekwa kwao na kuwaonea huruma.’ ”

Read More of Yeremia 33

Yeremia 34:1-22

Onyo Kwa Sedekia

34:1 Yer 27:7; 2Fal 25:1; Yer 39:1; Dan 2:37Wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli na jeshi lake lote, pamoja na falme zote na mataifa katika himaya aliyotawala walipokuwa wakipigana dhidi ya Yerusalemu pamoja na miji yote inayoizunguka, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwa Bwana: 34:2 2Nya 36:11; Yer 32:29; 37:8“Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli, kusema: Nenda kwa Sedekia mfalme wa Yuda umwambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto. 34:3 Yer 32:4; 21:7; 2Fal 25:7Hutaweza kuepuka mkono wake, bali hakika utatekwa na kukabidhiwa kwake. Utamwona mfalme wa Babeli kwa macho yako mwenyewe, naye atazungumza nawe ana kwa ana. Nawe utakwenda Babeli.

34:4 Yer 52:11“ ‘Lakini sikia ahadi ya Bwana, ee Sedekia mfalme wa Yuda. Hili ndilo asemalo Bwana kukuhusu: Hutakufa kwa upanga, 34:5 2Nya 16:14utakufa kwa amani. Kama vile watu walivyowasha moto wa maziko kwa heshima ya baba zako, wafalme waliokutangulia, ndivyo watu watakavyowasha moto kwa heshima yako na kuomboleza, wakisema: “Ole, Ee Bwana!” Mimi mwenyewe ninaweka ahadi hii, asema Bwana.’ ”

Ndipo nabii Yeremia akamwambia Sedekia mfalme wa Yuda mambo haya yote huko Yerusalemu, 34:7 Yos 10:3-10; 2Nya 11:9; 2Fal 18:13wakati jeshi la mfalme wa Babeli lilipokuwa likipigana dhidi ya Yerusalemu na miji mingine ya Yuda ambayo bado ilikuwa imara, yaani Lakishi na Azeka. Hii ilikuwa miji pekee yenye ngome iliyobaki katika Yuda.

Uhuru Kwa Watumwa

34:8 2Fal 11:17; Kut 21:2; Neh 5:5-8; Law 25:39-41Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana, baada ya Mfalme Sedekia kufanya agano na watu wote huko Yerusalemu ili kutangaza uhuru kwa watumwa. 34:9 Law 25:39-46; Kum 15:12-18; Neh 5:11Kila mmoja alipaswa kuwaacha huru watumwa wake wa Kiebrania, wanawake na wanaume. Hakuna yeyote aliyeruhusiwa kumshikilia Myahudi mwenzake kama mtumwa. Kwa hiyo maafisa wote na watu walioingia katika agano hili wakakubali kwamba watawaacha huru watumwa wao wa kiume na wa kike, na hawatawashikilia tena kama watumwa. Wakakubali na wakawaacha huru. Lakini baadaye wakabadili mawazo yao, na kuwarudisha wale watumwa waliokuwa wamewaacha huru, wakawafanya tena watumwa.

Ndipo neno la Bwana likamjia Yeremia kusema: 34:13 Kut 24:8; Kum 15:15“Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: Nilifanya agano na baba zenu nilipowatoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. Nilisema, 34:14 Kut 21:2; Law 25:39; Kum 15:12; 2Fal 17:14; Yer 7:26‘Kila mwaka wa saba, kila mmoja wenu ni lazima amwache huru mtumwa ambaye ni Mwebrania mwenzenu aliyejiuza kwenu. Baada ya kukutumikia kwa miaka sita, ni lazima umwache huru aende zake.’ Hata hivyo baba zenu hawakunisikiliza wala kunijali. 34:15 Yer 7:10-11; 32:34; Neh 10:29Hivi karibuni tu mlitubu na kufanya yaliyo sawa machoni pangu: Kila mmoja wenu aliwatangazia uhuru Waebrania wake. Hata mlifanya agano mbele zangu ndani ya nyumba iitwayo kwa Jina langu. 34:16 Eze 3:20; 18:24; Kut 20:7; Law 19:12Lakini sasa mmegeuka na kulinajisi jina langu. Kila mmoja wenu amemrudisha mtumwa wa kiume na wa kike ambao mlikuwa mmewaacha huru waende zao walikotaka. Mmewalazimisha kuwa watumwa wenu tena.

34:17 Mt 7:2; Gal 6:7; Yer 15:4; Kum 28:25, 64; Yer 21:7; 14:12; 29:18; 24:9“Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana: Hamkunitii mimi. Hamkutangaza uhuru kwa ndugu zenu. Hivyo sasa, ninawatangazia ninyi ‘uhuru,’ asema Bwana: ‘uhuru’ ili kuanguka kwa upanga, tauni na njaa. Nitawafanya mwe chukizo kwa falme zote za dunia. 34:18 Mwa 15:10; Rum 2:8; Yer 11:10Watu waliovunja agano langu, na ambao hawakutunza masharti ya agano walilofanya mbele zangu, nitawafanya kama ndama waliyemkata vipande viwili, kisha wakatembea kati ya vile vipande vya huyo ndama. 34:19 Yer 26:10; Sef 3:3-4Viongozi wa Yuda na Yerusalemu, maafisa wa mahakama, makuhani na watu wote wa nchi waliopita kati ya vile vipande vya ndama, 34:20 Eze 16:27; 23:28; Yer 11:21; 7:33; 21:7; Kum 28:25, 64nitawatia mikononi mwa adui zao wanaotafuta uhai wao. Maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi.

34:21 Yer 32:4; 52:24-27; 37:5; 39:6; 2Fal 25:21“Nitamtia Sedekia mfalme wa Yuda na maafisa wake mikononi mwa adui zao wanaotafuta uhai wao, kwa jeshi la mfalme wa Babeli, lililokuwa limeondoka kwenu. 34:22 Yer 39:1-2; 37:8; 38:18; Neh 2:17; Mik 7:13; Eze 23:47Nitatoa amri, asema Bwana, nami nitawarudisha tena katika mji huu. Watapigana dhidi yake, wautwae na kuuteketeza kwa moto. Nami nitaiangamiza miji ya Yuda hivyo pasiwe na yeyote atakayeweza kuishi humo.”

Read More of Yeremia 34