Yeremia 25:15-38, Yeremia 26:1-24 NEN

Yeremia 25:15-38

Kikombe Cha Ghadhabu Ya Mungu

25:15 Za 75:8; Ufu 14:10; Ay 21:20; Isa 51:17; Yer 49:12; Mao 4:21; Eze 23:31Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, aliloniambia: “Chukua kutoka mkononi mwangu kikombe hiki kilichojaa divai ya ghadhabu yangu, na kuyanywesha mataifa yote ambayo ninakutuma kwao. 25:16 Za 60:3; Nah 3:11; Yer 51:7Watakapoinywa, watapepesuka na kukasirika sana kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka katikati yao.”

25:17 Yer 1:10; 27:3Hivyo nikakichukua kikombe kutoka mkononi mwa Bwana, na kuyafanya mataifa yote aliyonituma kwao kukinywa: 25:18 Yer 24; 9; Mwa 19:13; Yer 44:22; 13:13; Ay 12:19; 2Nya 29:8Yaani Yerusalemu na miji ya Yuda, wafalme wake na maafisa wake, kuwafanya magofu na kuwa kitu cha kuchukiza, cha dhihaka na laana, kama walivyo leo; 25:19 2Fal 18:21; Isa 20:3; Eze 29:2; Yer 44:30pia Farao mfalme wa Misri, watumishi wake, maafisa wake na watu wake wote, 25:20 Mwa 10:23; Yer 47:5; Amo 1:7-8; Yos 13:3; Sef 2:4-7; Mwa 10:19pia wageni wote walioko huko; wafalme wote wa nchi ya Usi; wafalme wote wa Wafilisti (wale wa Ashkeloni, Gaza, Ekroni na watu walioachwa huko Ashdodi); 25:21 Mwa 19:38; Yer 27:3; Mwa 25:30; Kum 23:6Edomu, Moabu na Amoni; 25:22 Mwa 10:15; Yer 47:4; Dan 11:18; Isa 11:11; Yos 19:29; Isa 48:20; Yer 31:10wafalme wote wa Tiro na Sidoni; wafalme wa nchi za pwani ngʼambo ya bahari; 25:23 Mwa 25:3, 15; 22:21; Yer 9:26; 49:32Dedani, Tema, Buzi na wote walio maeneo ya mbali; 25:24 2Nya 9:14; Yer 50:37wafalme wote wa Arabuni na wafalme wote wa watu wageni wanaoishi katika jangwa; 25:25 Mwa 25:2; 10:22; Isa 21:2wafalme wote wa Zimri, Elamu na Umedi; 25:26 Yer 51:41; 50:3-9; Isa 23:17na wafalme wote wa pande za kaskazini, wa karibu na wa mbali, mmoja baada ya mwingine; yaani falme zote juu ya uso wa dunia. Baada ya hao wote, mfalme wa Sheshaki25:26 Sheshaki ni Babeli kwa fumbo. atakunywa pia.

25:27 Isa 29:9; Nah 3:18; Hab 2:16; Eze 14:17; 21:4; Yer 51:57; Eze 23:32-34“Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Kunyweni, mlewe na mtapike; angukeni, wala msiinuke tena kwa sababu ya upanga nitakaotuma miongoni mwenu.’ Lakini kama wakikataa kupokea kikombe kutoka mikononi mwako na kunywa, waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: Ni lazima mnywe! 25:29 Mit 11:31; 1Pet 4:17; Isa 10:12; 2Sam 5:7; Eze 38:21; Yer 13:12-14; Isa 34:2Tazama, nimeanza kuleta maafa juu ya mji ulio na Jina langu, na je, kweli ninyi mtaepuka kuadhibiwa? Hamwezi kuepuka kuadhibiwa, kwa maana nitaleta vita juu ya wote waishio duniani, asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.’

25:30 Isa 42:13; 16:10; Yoe 3:16; Za 46:6; Isa 63:3; Ufu 14:19-20“Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie:

“ ‘Bwana atanguruma kutoka juu;

atatoa sauti ya ngurumo

kutoka makao yake matakatifu

na kunguruma kwa nguvu sana

dhidi ya nchi yake.

Atapiga kelele kama wao wakanyagao zabibu,

atapiga kelele dhidi ya wote waishio duniani.

25:31 Hos 4:1; Mik 6:2; Yer 23:19; 1Sam 12:7; Yer 2:9, 35; Eze 36:5; Yer 15:9Ghasia zitasikika hadi miisho ya dunia,

kwa maana Bwana ataleta mashtaka dhidi ya mataifa;

ataleta hukumu juu ya wanadamu wote

na kuwaua waovu wote,’ ”

asema Bwana.

25:32 Isa 34:2; Yer 23:19; Isa 30:25; Kum 28:49Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:

“Tazama! Maafa yanaenea

kutoka taifa moja hadi jingine;

tufani kubwa inainuka

kutoka miisho ya dunia.”

25:33 Eze 39:17-20; Isa 66:16; Yer 16:4; Isa 34:2-8; Yer 8:2; Za 79:3Wakati huo, hao waliouawa na Bwana watatapakaa kila mahali, kuanzia mwisho mmoja wa dunia hadi mwisho mwingine. Hawataombolezewa wala kukusanywa au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyoenea juu ya ardhi.

25:34 Yer 6:26; Za 44:22; Zek 11:4-7; Yer 2:8; Zek 10:3; Isa 34:6; Yer 50:27Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji,

mgaagae mavumbini,

ninyi viongozi wa kundi.

Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia;

mtaanguka na kuvunjavunjwa

kama vyombo vizuri vya udongo.

25:35 Ay 11:20Wachungaji hawatakuwa na mahali pa kukimbilia,

viongozi wa kundi hawatapata mahali pa kutorokea.

25:36 Yer 6:26; 23:1; Zek 11:3Sikia kilio cha wachungaji, maombolezo ya viongozi wa kundi,

kwa maana Bwana anayaharibu malisho yao.

Makao yao ya amani yataharibiwa

kwa sababu ya hasira kali ya Bwana.

25:38 Ay 10:16; Yer 4:7; 44:22; 4:26; 46:16; 50:16; Kut 15:7Kama simba ataacha pango lake,

nchi yao itakuwa ukiwa

kwa sababu ya upanga wa mdhalimu,

na kwa sababu ya hasira kali ya Bwana Mungu.

Read More of Yeremia 25

Yeremia 26:1-24

Yeremia Atishiwa Kuuawa

26:1 2Fal 23:36Mwanzoni mwa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilikuja kutoka kwa Bwana: 26:2 Yer 19:14; Kut 23:14; Mdo 20:27; Kum 12:5; Yer 17:19; Mt 28:20; Kum 4:2“Hili ndilo Bwana asemalo: Simama katika ua wa nyumba ya Bwana na useme na watu wote wa miji ya Yuda wanaokuja kuabudu katika nyumba ya Bwana. Waambie kila kitu nitakachokuamuru, usipunguze neno. 26:3 Kum 30:2; Isa 55:7; Yer 18:8; 2Nya 33:12-13; Yer 35:15; 36:7Huenda watasikiliza, na kila mmoja akageuka kutoka njia yake mbaya. Kisha nitawahurumia na kuacha kuwaletea maafa niliyokuwa ninapanga kwa sababu ya maovu waliyofanya. 26:4 Law 26:14; Yer 25:3; 1Fal 9:6; Yer 11:8Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Ikiwa hamtanisikiliza na kuifuata sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu, 26:5 Mit 1:24; Isa 65:12; Yer 7:13; 25:4; 44:5nanyi ikiwa hamtayasikiliza maneno ya watumishi wangu manabii, ambao nimewatuma kwenu tena na tena (ijapokuwa hamkuwasikiliza), 26:6 Yos 18:1; Amu 18:31; Kum 28:25; 2Fal 22:19ndipo nitaifanya nyumba hii kama Shilo na mji huu kuwa kitu cha kulaaniwa na mataifa yote ya dunia.’ ”

Makuhani, manabii na watu wote wakamsikia Yeremia akiyasema maneno haya ndani ya nyumba ya Bwana. 26:8 Mdo 6:12; 21:27; Law 24:15-16; Neh 9:26; Yer 11:21Lakini mara tu Yeremia alipomaliza kuwaambia watu kila kitu Bwana alichomwamuru kukisema, basi makuhani, manabii na watu wote walimkamata wakisema, “Ni lazima ufe! 26:9 Law 26:32; Yer 9:11; Mdo 21:32Kwa nini unatoa unabii katika jina la Bwana kwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa na kuachwa tupu?” Nao watu wote wakamkusanyikia na kumzunguka Yeremia ndani ya nyumba ya Bwana.

26:10 Yer 34:19; Eze 22:27; Mwa 23:10Maafisa wa Yuda waliposikia kuhusu mambo haya, wakapanda kutoka jumba la kifalme, wakaenda katika nyumba ya Bwana na kushika nafasi zao kwenye ingilio la Lango Jipya la nyumba ya Bwana. 26:11 Yer 38:4; Kum 18:20; Mdo 6:11; Kum 18:20Kisha makuhani na manabii wakawaambia maafisa pamoja na watu wote, “Mtu huyu anastahili ahukumiwe kifo kwa sababu ametoa unabii mbaya dhidi ya mji huu. Mmesikia kwa masikio yenu wenyewe!”

26:12 Yer 1:18; Isa 6:8; Mdo 5:29; Amo 7:15; Mdo 4:18-20Kisha Yeremia akawaambia maafisa wote na watu wote: “Bwana amenituma kutoa unabii dhidi ya nyumba hii na mji huu mambo yote mliyoyasikia. 26:13 Yoe 2:12; Yer 7:5; 35:15; 11:4; 18:8Sasa tengenezeni njia zenu na matendo yenu, na kumtii Bwana Mungu wenu. Ndipo Bwana atawahurumia na kuacha kuleta maafa aliyokuwa ameyatamka dhidi yenu. 26:14 Yos 9:15; Yer 38:5Lakini kwa habari yangu mimi, niko mikononi mwenu, nifanyieni lolote mnaloona kuwa ni jema na la haki. 26:15 Kum 19:10; Yer 1:17Hata hivyo, jueni kwa hakika, ikiwa mtaniua, mtakuwa mmejipatia dhambi kwa damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe, na juu ya mji huu na wote wanaoishi ndani yake, kwa maana ni kweli Bwana amenituma kwenu ili niseme maneno haya yote masikioni mwenu.”

26:16 Mdo 23:9; 5:34-39; 23:29Kisha maafisa na watu wote wakawaambia makuhani na manabii, “Mtu huyu asihukumiwe kifo! Amesema nasi katika jina la Bwana, Mungu wetu.”

Baadhi ya wazee wa nchi wakasogea mbele, wakaliambia kusanyiko lote la watu, 26:18 Isa 2:3; 2Fal 25:9; Neh 4:2; Mik 1:4; Zek 8:3; Yer 17:3; 9:11“Mika Mmoreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“ ‘Sayuni italimwa kama shamba,

Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto,

na kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu

kilichofunikwa na vichaka.’

26:19 1Nya 3:13; Kut 32:14; Isa 37:14-20; 2Sam 24:16; Hab 2:10; 2Nya 32:24-26Je, Hezekia mfalme wa Yuda au mtu mwingine yeyote katika Yuda alimhukumu Mika kufa? Je, Hezekia hakumcha Bwana na kuhitaji msaada wake? Je, Bwana hakuwahurumia na akaacha kuleta maafa aliyokuwa ametamka dhidi yao? Tunakaribia sana kujiletea maangamizo ya kutisha sisi wenyewe!”

26:20 Yos 9:17(Wakati huu, Uria mwana wa Shemaya kutoka mji wa Kiriath-Yearimu alikuwa mtu mwingine aliyetoa unabii kwa jina la Bwana. Alitoa unabii juu ya mambo yaliyofanana na haya dhidi ya mji huu na nchi hii kama alivyofanya Yeremia. 26:21 Mwa 31:21; Mt 10:23; 1Fal 19:2-3; Yer 2:30; Mt 23:37Mfalme Yehoyakimu na wakuu wake wote na maafisa waliposikia maneno yake, mfalme alitafuta kumuua. Lakini Uria alipata habari, na kwa kuogopa akakimbilia Misri. 26:22 Yer 36:12, 25; Mit 29:12Hata hivyo, Mfalme Yehoyakimu alimtuma Elnathani mwana wa Akbori huko Misri, pamoja na watu wengine ili kwenda kumkamata Uria. 26:23 2Fal 23:6; Ebr 11:37Wakamrudisha Uria kutoka Misri na kumpeleka kwa Mfalme Yehoyakimu, ambaye alimuua kwa upanga, na mwili wake kutupwa kwenye eneo la makaburi ya watu wasio na cheo.)

26:24 2Fal 22:12; Yer 39:14Zaidi ya hayo, Ahikamu mwana wa Shafani akamuunga mkono Yeremia, kwa hiyo hakutiwa tena mikononi mwa watu ili auawe.

Read More of Yeremia 26