Yeremia 2:31-37, Yeremia 3:1-25, Yeremia 4:1-9 NEN

Yeremia 2:31-37

2:31 Isa 45:19; Ay 21:14“Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la Bwana:

“Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli

au nchi ya giza kuu?

Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura,

hatutarudi kwako tena’?

Je, mwanamwali husahau vito vyake,

au bibi arusi mapambo yake ya arusi?

Lakini watu wangu wamenisahau mimi,

tena kwa siku zisizo na hesabu.

Je, wewe una ustadi kiasi gani katika kufuatia mapenzi!

Hata wale wanawake wabaya kuliko wote

wanaweza kujifunza kutokana na njia zako.

2:34 Yer 19:4; Mit 6:17; Kut 22:2; 2Fal 21:16Katika nguo zako watu huona

damu ya uhai ya maskini wasio na hatia,

ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba.

Lakini katika haya yote

2:35 Mit 28:13; Eze 17:20; 2Sam 12:13; 1Yn 1:8-10; Mit 30:12; Isa 66:16; Yer 25:31unasema, ‘Sina hatia;

Mungu hajanikasirikia.’

Lakini nitakuhukumu kwa sababu unasema,

‘Mimi sijatenda dhambi.’

2:36 Yer 31:22; Hos 5:13; Za 108:12; Isa 30:2-7; Yer 37:7Kwa nini unatangatanga sana,

kubadili njia zako?

Utakatishwa tamaa na Misri

kama ulivyokatishwa na Ashuru.

2:37 2Sam 13:19; Yer 37:7Pia utaondoka mahali hapo

ukiwa umeweka mikono kichwani,

kwa kuwa Bwana amewakataa wale unaowatumainia;

hutasaidiwa nao.

Read More of Yeremia 2

Yeremia 3:1-25

Israeli Asiye Mwaminifu

3:1 Kum 24:1-4; Lk 15:16, 24; Mwa 3; 17; 2Fal 16; 7; Yer 2:25; Eze 16:26; Hos 2:5, 12“Kama mtu akimpa talaka mkewe,

naye akamwacha na akaolewa na mtu mwingine,

je, huyo mume aweza kumrudia tena?

Je, hiyo nchi haitanajisika kabisa?

Lakini umeishi kama kahaba na wapenzi wengi:

je, sasa utanirudia tena?”

asema Bwana.

3:2 Mwa 38:14; Eze 16:25; Kum 12:2; Hes 15:39; Isa 1:21“Inua macho utazame miinuko iliyo kame na uone.

Je, pana mahali ambapo hawajalala nawe?

Uliketi kando ya barabara ukiwasubiri wapenzi,

ukakaa kama yeye ahamahamaye jangwani.

Umeinajisi nchi

kwa ukahaba wako na uovu wako.

3:3 Law 26:19; Kum 11:14; Amo 4; 7; Sef 3:5; Yer 5:25; 14:4; Yoe 1:10; Eze 16:30Kwa hiyo mvua imezuiliwa,

nazo mvua za vuli hazikunyesha.

Hata hivyo, una uso usio na haya kama wa kahaba;

unakataa kutahayari kwa aibu.

3:4 Kum 32:6; Hos 2:15; Za 89:26; Isa 63:16; Yer 31:9Je, wewe hujaniita hivi punde tu:

‘Baba yangu, rafiki yangu tangu ujana wangu,

3:5 Isa 57:19; Za 103:9je, utakasirika siku zote?

Je, ghadhabu yako itaendelea milele?’

Hivi ndivyo unavyozungumza,

lakini unafanya maovu yote uwezayo.”

Wito Kwa Ajili Ya Toba

3:6 Kum 12:2; Hos 4:13; Yer 2:20; 1Nya 3:14; Isa 24:16; Yer 31:22; Eze 20:28Wakati wa utawala wa Mfalme Yosia, Bwana aliniambia, “Umeona kile Israeli asiye mwaminifu amekifanya? Amepanda juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti uliotanda na amefanya uzinzi huko. 3:7 Eze 16:46; 2Fal 17:13; Amo 4:8Mimi nilifikiri kuwa baada ya kuyafanya yote haya angelinirudia, lakini hakurudi, naye dada yake Yuda mdanganyifu aliona hili. 3:8 Eze 16:47; 23:11; Yer 11:10; Kum 4:27Nilimpa Israeli asiye mwaminifu hati yake ya talaka, na kumfukuza kwa ajili ya uzinzi wake wote. Hata hivyo nikaona kuwa Yuda dada yake mdanganyifu hakuogopa. Yeye pia alitoka na kufanya uzinzi. 3:9 Law 17:7; Isa 1:21; 57:6; Yer 7:22Kwa sababu uasherati wa Israeli haukuwa kitu kwake, Yuda aliinajisi nchi kwa kuzini na mawe na miti. 3:10 Yer 12:2; Eze 33:31; Hos 7:14; Isa 31:6; Amo 4:9; Hag 2:17; 2Fal 17:19Pamoja na hayo yote, Yuda dada yake mdanganyifu hakunirudia kwa moyo wake wote, bali kwa kujifanya tu,” asema Bwana.

3:11 Eze 16:52; 23:11; Yer 2:19Bwana akaniambia, “Israeli asiye mwaminifu ana haki kuliko Yuda mdanganyifu. 3:12 Isa 44:22; 2Fal 17:3-6; Kum 4:30; Za 86:15; Yer 31:21; Eze 14:6; 1Fal 3:26Nenda, ukatangaze ujumbe huu kuelekea kaskazini:

“ ‘Rudi, Israeli usiye mwaminifu,’ asema Bwana,

‘sitakutazama tena kwa uso uliokunjamana,

kwa kuwa mimi ni mwenye huruma,’ asema Bwana,

‘Sitashika hasira yangu milele.

3:13 Law 26:40-44; Yer 31:18-20; Lk 15:18-21; 1Yn 1:9; Yer 2:2, 5; Kum 12:2; Yer 14; 20Ungama dhambi zako tu:

kwamba umemwasi Bwana Mungu wako,

umetapanya wema wako kwa miungu ya kigeni

chini ya kila mti unaotanda,

nawe hukunitii mimi,’ ”

asema Bwana.

3:14 Rum 11:5; Ay 22:23; Hos 2:19; Isa 54:5“Rudini, enyi watu msio waaminifu, kwa kuwa mimi ni mume wenu,” asema Bwana. “Nitawachagua ninyi, mmoja kutoka kwenye mji, na wawili kutoka kwenye ukoo, nami nitawaleta Sayuni. 3:15 Isa 31:4; Mdo 20:28; Efe 4:10; Mdo 13:22Kisha nitawapeni wachungaji wanipendezao moyo wangu, ambao watawaongoza kwa maarifa na ufahamu. 3:16 Isa 65:17; Yn 4:21-24; Hes 3:31; 1Nya 15:25Katika siku hizo, idadi yenu itakapokuwa imeongezeka sana katika nchi, watu hawatasema tena, ‘Sanduku la Agano la Bwana,’ ” asema Bwana. “Halitaingia tena kwenye mawazo yao wala kukumbukwa, hawatalihitaji wala halitatengenezwa jingine. 3:17 Za 47:8; Eze 43:7; Za 22:23; 81:12; Yer 18:12; 17:12; 33:16Wakati huo, wataita Yerusalemu kuwa Kiti cha Enzi cha Bwana, nayo mataifa yote watakusanyika Yerusalemu kuliheshimu jina la Bwana. Hawatafuata tena ukaidi wa mioyo yao miovu. 3:18 Amo 9:15; Eze 37:19; Yer 16:15; Isa 11:13; Hos 1:11; Yer 30:3; 50:4; Kum 31:7; Kut 4:22Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaungana na nyumba ya Israeli, wao kwa pamoja watakuja kutoka nchi ya kaskazini hadi nchi niliyowapa baba zenu kama urithi.

3:19 Kut 4:22; Isa 63:16; 2Sam 7:14; Za 106:24; Eze 20:6“Mimi mwenyewe nilisema,

“ ‘Tazama jinsi nitakavyowatunza kwa furaha kama wana

na kuwapa nchi nzuri,

urithi ulio mzuri kuliko wa taifa jingine lolote.’

Nilidhani mngeniita ‘Baba,’

na msingegeuka, mkaacha kunifuata.

Lakini kama mwanamke asiye mwaminifu kwa mumewe,

vivyo hivyo mmekosa uaminifu kwangu pia, ee nyumba ya Israeli,”

asema Bwana.

3:21 Yer 31:18; Isa 57:11Kilio kinasikika juu ya miinuko iliyo kame,

kulia na kuomboleza kwa watu wa Israeli,

kwa sababu wamepotoka katika njia zao

na wamemsahau Bwana Mungu wao.

3:22 Hos 14:4; Ay 22:23; Isa 30:26; Hos 6:1; Yer 33:6; 2:19“Rudini, enyi watu msio waaminifu,

nami nitawaponya ukengeufu wenu.”

“Naam, tutakuja kwako,

kwa maana wewe ni Bwana Mungu wetu.

3:23 Yer 17:14; Za 3:8; Yer 2:20Hakika zile ghasia za kuabudu sanamu kwenye vilima

na milimani ni udanganyifu;

hakika katika Bwana, Mungu wetu,

uko wokovu wa Israeli.

3:24 Yer 11:13; Hos 9:10Tangu ujana wetu miungu ya aibu imeyala

matunda ya kazi za baba zetu:

makundi yao ya kondoo na ngʼombe,

wana wao na binti zao.

3:25 Eze 6:9; Dan 9:7; Za 25:7; Yer 22:21; 31:19; Amu 10:10; 1Fal 8:47; Yer 14:20Sisi na tulale chini katika aibu yetu,

na fedheha yetu itufunike.

Tumetenda dhambi dhidi ya Bwana Mungu wetu,

sisi na mababa zetu;

tangu ujana wetu hadi leo

hatukumtii Bwana Mungu wetu.”

Read More of Yeremia 3

Yeremia 4:1-9

4:1 Yoe 2:12; Ezr 8:5; 2Fal 7:13; 21:4; Kum 4:30; Hos 12:6; Yer 16:18; 35:15“Ikiwa utataka kurudi, ee Israeli,

nirudie mimi,”

asema Bwana.

“Ikiwa utaondoa sanamu zako za kuchukiza mbele ya macho yangu

na usiendelee kutangatanga,

4:2 Kum 10:20; Hes 14:21; Gal 3:8; Hos 4:15; Mwa 12:2; Isa 19:18; 65:16; Yer 12:16ikiwa kwa kweli, kwa haki na kwa unyofu utaapa,

‘Kwa hakika kama vile Bwana aishivyo,’

ndipo mataifa yatakapobarikiwa naye

na katika yeye watajitukuza.”

4:3 Hos 10:12; Mk 4:18Hili ndilo asemalo Bwana kwa watu wa Yuda na kwa Yerusalemu:

“Vunjeni mabonge kwenye mashamba yenu,

wala msipande katikati ya miiba.

4:4 Law 26:41; Rum 2:28-29; Sef 2:2; Amo 5:6; Ay 41:21; Kut 32:22; Yer 8:14; Yos 10:20; Yer 5:20; Hes 10:2-7; Ay 39:24Jitahirini katika Bwana,

tahirini mioyo yenu,

enyi wanaume wa Yuda

na watu wa Yerusalemu,

la sivyo ghadhabu yangu itatoka kwa nguvu

na kuwaka kama moto

kwa sababu ya uovu mliotenda,

ikiwaka pasipo wa kuizima.

Maafa Kutoka Kaskazini

“Tangaza katika Yuda na upige mbiu katika Yerusalemu na kusema:

‘Piga tarumbeta katika nchi yote!’

Piga kelele na kusema:

‘Kusanyikeni pamoja!

Tukimbilie katika miji yenye maboma!’

4:6 Yer 1:13-15; Isa 14:31; Za 74:4; Isa 31:9; Yer 50:2; 11:11; 18:11Onyesheni ishara ili kwenda Sayuni!

Kimbilieni usalama pasipo kuchelewa!

Kwa kuwa ninaleta maafa kutoka kaskazini,

maangamizi ya kutisha.”

4:7 Dan 7:4; Eze 12:20; Yer 2:15; Isa 6:11; Yer 25:38; Hos 5:14; Nah 2:12; Yer 6:26Simba ametoka nje ya pango lake,

mharabu wa mataifa amejipanga.

Ametoka mahali pake

ili aangamize nchi yenu.

Miji yenu itakuwa magofu

pasipo mtu wa kuishi humo.

4:8 1Fal 21:27; Yer 30:24; Isa 22:12; 3:24; Yer 6:26; Eze 7:18; Yer 7:29; 9:20Hivyo vaeni nguo za magunia,

ombolezeni na kulia kwa huzuni,

kwa kuwa hasira kali ya Bwana

haijaondolewa kwetu.

“Katika siku ile,” asema Bwana

“mfalme na maafisa watakata tamaa,

makuhani watafadhaika,

na manabii watashangazwa mno.”

Read More of Yeremia 4