Yeremia 18:1-23, Yeremia 19:1-15, Yeremia 20:1-18 NEN

Yeremia 18:1-23

Katika Nyumba Ya Mfinyanzi

Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana: “Shuka uende mpaka nyumba ya mfinyanzi, nami huko nitakupa ujumbe wangu.” Kwa hiyo nikashuka mpaka kwenye nyumba ya mfinyanzi, nikamkuta akifinyanga kwa gurudumu lake. Lakini chombo alichokuwa akikifinyanga kutokana na udongo kilivunjika mikononi mwake, hivyo mfinyanzi akakifanya kuwa chombo kingine, umbo jingine kama vile ilivyoonekana vyema kwake yeye.

Kisha neno la Bwana likanijia kusema: 18:6 Isa 29:16; 45:9; Rum 9:20-21; Mwa 2:7“Ee nyumba ya Israeli, je, siwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?” asema Bwana. “Kama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, ee nyumba ya Israeli. 18:7 Yer 1:10Ikiwa wakati wowote nikitangaza kuwa taifa au ufalme utangʼolewa, utaangushwa na kuangamizwa, 18:8 Kut 32:14; Eze 18:21; Yn 3:8-10; Dan 9:14; Amu 10:15-16; Za 25:11; Yer 26:13; 31:28; 42:10; Hos 11:8-9; Yoe 2:13ikiwa lile taifa nililolionya litatubia uovu wake, ndipo nitakapokuwa na huruma, wala sitawapiga kwa maafa niliyokuwa nimewakusudia. 18:9 Yer 1:10; 31:28Ikiwa wakati mwingine nitatangaza kuwa taifa ama utawala ujengwe na kuwekwa wakfu, 18:10 Eze 33:18; 1Sam 2:29-30; 13:13; Yer 1:10ikiwa utafanya maovu mbele zangu na hukunitii, ndipo nitakapoghairi makusudio yangu mema niliyokuwa nimeyakusudia.

18:11 2Fal 22:16; Yer 4:6; Kum 4:30; 2Fal 17:13; Isa 1:16-19; Ay 16:17; Yer 7:3“Basi kwa hiyo waambie watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Tazama! Ninaandaa maafa kwa ajili yenu, nami ninabuni mabaya dhidi yenu. Kwa hiyo geukeni kutoka njia zenu mbaya, kila mmoja wenu, tengenezeni njia zenu na matendo yenu.’ 18:12 Isa 57:10; Yer 2:25; 3:17Lakini wao watajibu, ‘Hakuna faida. Tutaendelea na mipango yetu wenyewe, kila mmoja wetu atafuata ukaidi wa moyo wake mbaya.’ ”

18:13 Isa 66:8; Yer 2:10; 5:30; 2Fal 19:21Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana:

“Ulizia miongoni mwa mataifa:

Ni nani alishasikia jambo kama hili?

Jambo la kutisha sana limefanywa

na Bikira Israeli.

Je, barafu ya Lebanoni iliwahi kutoweka

kwenye miteremko yake ya mawe wakati wowote?

Je, maji yake baridi yatokayo katika vyanzo vilivyo mbali

yaliwahi kukoma kutiririka wakati wowote?

18:15 Yer 51:18; Hos 11:12; Yer 6:16; Isa 57:14; 62:10; 17:10; 1:13; Eze 44:12Lakini watu wangu wamenisahau mimi,

wanafukizia uvumba sanamu zisizofaa kitu,

zilizowafanya wajikwae katika njia zao

na katika mapito ya zamani.

Zimewafanya wapite kwenye vichochoro

na kwenye barabara ambazo hazikujengwa.

18:16 Eze 33:28-29; Yer 49:13; 42:18; Ay 16:4; 2Fal 19:21; Kum 28:37; Yer 25:9Nchi yao itaharibiwa,

itakuwa kitu cha kudharauliwa daima;

wote wapitao karibu nayo watashangaa

na kutikisa vichwa vyao.

18:17 Ay 7:10; Yer 13:24; 2Nya 29:6; Yer 2:27Kama upepo utokao mashariki,

nitawatawanya mbele ya adui zao;

nitawapa kisogo wala sio uso,

katika siku ya maafa yao.”

18:18 Yer 11:19; Hag 2:11; Yer 5:13; Za 64:2-8; Yer 9:3; 2:8; Mao 2:7; Ay 5:13Wakasema, “Njooni, tutunge hila dhidi ya Yeremia; kwa kuwa kufundisha sheria kwa kuhani hakutapotea, wala shauri litokalo kwa mwenye hekima, wala neno la manabii. Hivyo njooni, tumshambulie kwa ndimi zetu na tusijali chochote asemacho.”

Nisikilize, Ee Bwana,

sikia wanayosema washtaki wangu!

18:20 Mwa 20:7; Kum 9:19; Za 119:85; 35:7; 109:23; Mwa 44:4; Yer 14:7-9Je, mema yalipwe kwa mabaya?

Lakini wao wamenichimbia shimo.

Kumbuka kwamba nilisimama mbele yako

na kunena mema kwa ajili yao,

ili wewe ugeuze hasira yako kali mbali nao.

18:21 Yer 11:22; 14:16; 1Sam 15:33; Mao 5:3; Za 63:10; Isa 47:9; 9:17Kwa hiyo uwaache watoto wao waone njaa;

uwaache wauawe kwa makali ya upanga.

Wake zao wasiwe na watoto, na wawe wajane;

waume wao wauawe,

nao vijana wao waume

wachinjwe kwa upanga vitani.

18:22 Yer 6:26; Za 35:15; Yer 5:26; Za 119:85; Yer 20:10Kilio na kisikike kutoka kwenye nyumba zao

ghafula uwaletapo adui dhidi yao,

kwa kuwa wamechimba shimo ili kunikamata

na wameitegea miguu yangu mitego.

18:23 Yer 11:21; 37:15; Neh 4:5; Za 109:14; 59:5; Yer 10:24Lakini unajua, Ee Bwana,

hila zao zote za kuniua.

Usiyasamehe makosa yao

wala usifute dhambi zao

mbele za macho yako.

Wao na waangamizwe mbele zako;

uwashughulikie wakati wa hasira yako.

Read More of Yeremia 18

Yeremia 19:1-15

Gudulia La Udongo Lililovunjika

19:1 Hes 11:17; Yer 18:2Hili ndilo asemalo Bwana: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kutoka kwa mfinyanzi. Wachukue baadhi ya wazee wa watu na wa makuhani 19:2 Yos 15:8; 2Fal 23:10na mtoke mwende mpaka kwenye Bonde la Ben-Hinomu, karibu na ingilio la Lango la Vigae. Huko tangaza maneno ninayokuambia, 19:3 Yer 17:20; 6:19; 1Sam 3:11nawe useme, ‘Sikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda na watu wa Yerusalemu. Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Sikilizeni! Nitaleta maafa mahali hapa, ambayo yatafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yawashe. 19:4 Kum 28:20; 31:16; Law 18:21; 2Fal 21:16; Isa 65:11; Kut 20:3; Yer 1:16Kwa kuwa wameniacha na kupafanya mahali hapa kuwa pa miungu ya kigeni. Wameiteketezea sadaka miungu ambayo wao wala baba zao wala wafalme wa Yuda kamwe hawakuijua, nao wamelijaza eneo hili kwa damu isiyo na hatia. 19:5 2Fal 3:27; Za 106:37-38; Yer 32:35; Eze 16:36; Yer 7:31Wamejenga mahali pa juu pa kuabudia miungu pa Baali ili kuteketeza wana wao katika moto kama sadaka kwa Baali, kitu ambacho sikukiamuru wala kukitaja, wala hakikuingia akilini mwangu. 19:6 Yos 15:8; Yer 7:32; 2Fal 23:10Hivyo jihadharini, siku zinakuja, asema Bwana, wakati watu hawatapaita tena mahali hapa Tofethi ama Bonde la Ben-Hinomu, bali Bonde la Machinjo.

19:7 Law 26:17; Kum 28:25-26; Yer 16:4; Za 79:2; 33:10-11; Yer 34:20“ ‘Nitaiharibu mipango ya Yuda na Yerusalemu mahali hapa. Nitawafanya waanguke kwa upanga mbele ya adui zao, katika mikono ya wale watafutao uhai wao, nami nitaitoa mizoga yao kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi. 19:8 Kum 28:37; Yer 25:9; Mao 2:15-16; Sef 2:15; Yer 18:16; Law 26:32Nitauharibu mji huu na kuufanya kitu cha kudharauliwa. Wote wapitao karibu watashangaa na kuudhihaki kwa sababu ya majeraha yake yote. 19:9 Law 26:29; Mao 4:10; Isa 9:20; Kum 28:49-57; Yer 21:7Nitawafanya wao kula nyama ya wana wao na binti zao; kila mmoja atakula nyama ya mwenzake wakati wa dhiki ya kuzungukwa na jeshi lililowekwa juu yao na adui wanaotafuta uhai wao.’

19:10 Yer 13:14; 51:63; Za 2:9“Kisha livunje lile gudulia wale walio pamoja nawe wakiwa wanaangalia, 19:11 Yer 7:32; Za 2:9; Isa 30:14uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: Nitalivunja taifa hili na mji huu kama gudulia hili la mfinyanzi lilivyovunjwa, nalo haliwezi kutengenezeka tena. Watawazika waliokufa huko Tofethi hata isiwepo nafasi zaidi. Hivi ndivyo nitakavyopafanya mahali hapa na kwa wale waishio ndani yake, asema Bwana. Nitaufanya mji huu kama Tofethi. 19:13 Yer 52:13; Eze 16:41; Ay 38:32; Mdo 7:42; Eze 20:28; Yer 7:18; 32:29; Eze 20:28Nyumba zilizoko Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, Tofethi: yaani nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani, na kumimina dhabihu za vinywaji kwa miungu mingine.’ ”

19:14 2Nya 20:5; Yer 7:2; 26:2Kisha Yeremia akarudi kutoka Tofethi, mahali ambapo Bwana alikuwa amemtuma kutoa unabii, akasimama katika ua wa Hekalu la Bwana na kuwaambia watu wote, 19:15 Zek 7:11-14; Mdo 7:51-52; Neh 9:16; Yer 11:11; 22:21“Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Sikilizeni! Nitaleta juu ya mji huu pamoja na vijiji vinavyouzunguka kila maafa niliyosema dhidi yake, kwa sababu wamekuwa na shingo ngumu, na hawakuyasikiliza maneno yangu.’ ”

Read More of Yeremia 19

Yeremia 20:1-18

Yeremia Ateswa Na Pashuri

20:1 1Nya 24:14; 2Fal 25:18; Lk 22:52Ikawa kuhani Pashuri mwana wa Imeri, mkuu wa maafisa wa Hekalu la Bwana, alipomsikia Yeremia akitoa unabii juu ya mambo haya, 20:2 Kum 25:2-3; 2Kor 11:24; Ay 13:27; Zek 14:10; Ay 29:7; Yer 15:15; 37:15; 29:26; Mdo 16:24; Ebr 11:36akaamuru Yeremia nabii apigwe na kufungwa kwenye mkatale katika Lango la Juu la Benyamini huko Hekaluni la Bwana. Siku ya pili Pashuri alipomwachia kutoka kwenye mkatale, Yeremia akamwambia, “Bwana hakukuita jina lako kuwa Pashuri bali Magor-Misabibu.20:3 Magor-Misabibu maana yake hapa ni Vitisho pande zote. 20:4 Ay 18:11; Yer 29:21; 25:9; 52:27; 39:9; 21:10; 13:19Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: ‘Nitakufanya kuwa hofu kuu kwako wewe mwenyewe na rafiki zako wote, na kwa macho yako mwenyewe utawaona wakianguka kwa upanga wa adui zao. Nitawatia Yuda wote mikononi mwa mfalme wa Babeli, ambaye atawachukua na kuwapeleka Babeli, ama awaue kwa upanga. 20:5 2Fal 25:15; Yer 17:3; 3:24; 2Fal 20:17Nitatia utajiri wote wa mji huu kwa adui zao: yaani mazao yao yote, vitu vyao vyote vya thamani, na hazina zote za wafalme wa Yuda. Watavitwaa kwa nyara na kuvipeleka Babeli. 20:6 Yer 14:15; Mao 2:14; Yer 28:15Nawe Pashuri pamoja na wote waishio katika nyumba yako mtakwenda uhamishoni Babeli. Mtafia humo na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ”

Malalamiko Ya Yeremia

20:7 Kut 5:23; 22:16; Isa 8:11; 1Kor 9:16; Ay 12:4Ee Bwana, umenidanganya,

nami nikadanganyika;

wewe una nguvu kuniliko,

nawe umenishinda.

Ninadharauliwa mchana kutwa,

kila mmoja ananidhihaki.

20:8 Yer 28:8; 2Nya 36:16; Yer 6:7-10Kila ninenapo, ninapiga kelele

nikitangaza ukatili na uharibifu.

Kwa hiyo neno la Bwana limeniletea matukano

na mashutumu mchana kutwa.

20:9 Za 39:3; Yer 4:19; Amo 3:8; Mdo 4:20; 18:5; Yer 44:16Lakini kama nikisema, “Sitamtaja

wala kusema tena kwa jina lake,”

neno lake linawaka ndani ya moyo wangu kama moto,

moto uliofungwa ndani ya mifupa yangu.

Nimechoka sana kwa kulizuia ndani mwangu;

kweli, siwezi kujizuia.

20:10 Yer 6:25; Neh 6:6-13; Ay 19:14; Lk 11:54; Za 57:4Ninasikia minongʼono mingi,

“Hofu iko pande zote!

Mshtakini! Twendeni tumshtaki!”

Rafiki zangu wote wananisubiri niteleze,

wakisema,

“Labda atadanganyika;

kisha tutamshinda

na kulipiza kisasi juu yake.”

20:11 Rum 8:31; Yer 15:15; 17:18; 23:40; 7:19; Za 129:2Lakini Bwana yu pamoja nami

kama shujaa mwenye nguvu;

hivyo washtaki wangu watajikwaa

na kamwe hawatashinda.

Watashindwa, nao wataaibika kabisa;

kukosa adabu kwao hakutasahauliwa.

20:12 Yer 17:10; Za 54:7; Rum 12:19; Za 62:8; Yer 11:20; Za 7:9; Kum 32:35Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,

wewe umjaribuye mwenye haki

na kupima moyo na nia,

hebu nione ukilipiza kisasi juu yao,

kwa maana kwako

nimeliweka shauri langu.

20:13 Za 35:10; Yak 2:5-6; Isa 12:6; Za 34:6; 97:10Mwimbieni Bwana!

Mpeni Bwana sifa!

Yeye huokoa uhai wa mhitaji

kutoka mikononi mwa waovu.

20:14 Yer 15:10; Ay 3:8, 16Ilaaniwe siku niliyozaliwa!

Nayo isibarikiwe ile siku

mama yangu aliyonizaa!

Alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari,

yule aliyemfanya afurahi sana, akisema,

“Mtoto amezaliwa kwako,

tena mtoto wa kiume!”

20:16 Mwa 19:25; Yer 18:22; 6:26Mtu huyo na awe kama miji ile

ambayo Bwana Mungu

aliiangamiza bila huruma.

Yeye na asikie maombolezo asubuhi

na kilio cha vita adhuhuri.

20:17 Ay 3:10-16; 10:18-19Kwa sababu hakuniua nikiwa tumboni,

hivyo mama yangu angekuwa kaburi langu,

nalo tumbo lake la uzazi

lingebaki kuwa kubwa daima.

20:18 1Fal 19:4; Za 102:3; Ay 3:20; 3:10-11; Mhu 4:2; Mwa 3:17; Ay 5:7; Za 90:9Kwa nini basi nilitoka tumboni

ili kuona taabu na huzuni,

na kuzimaliza siku zangu katika aibu?

Read More of Yeremia 20