Isaya 8:11-22, Isaya 9:1-21, Isaya 10:1-19 NEN

Isaya 8:11-22

Mwogope Mungu

8:11 Eze 3:14; 2:8; 1:3Bwana alisema nami mkono wake wenye nguvu ukiwa juu yangu, akinionya nisifuate njia za taifa hili. Akasema:

8:12 Isa 36:6; 7:2; 20:5; 1Pet 3:14; Mt 10:28“Usiite fitina kila kitu ambacho watu hawa hukiita fitina,

usiogope kile wanachokiogopa,

wala usikihofu.

8:13 Hes 20:12; Isa 29:23; Kut 20:20Bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye peke yake

ikupasaye kumheshimu kuwa mtakatifu,

ndiye peke yake utakayemwogopa,

ndiye peke yake utakayemhofu,

8:14 Rum 9:33; Eze 11:16; Isa 24:17-18; Za 118:22; Yer 6:21; Lk 2:34; Isa 4:6; Lk 20:18; Eze 3:20naye atakuwa mahali patakatifu;

lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa

jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa

na mwamba wa kuwaangusha.

Kwa watu wa Yerusalemu,

atakuwa mtego na tanzi.

8:15 Lk 20:18; Isa 28:13; 59:10; Rum 9:32; Mt 4:19; Lk 20:18; Isa 59:10Wengi wao watajikwaa;

wataanguka na kuvunjika,

watategwa na kunaswa.”

8:16 Dan 8:26; 12:4; Yer 32:14; Rut 4:7; Isa 29:11-12Funga ushuhuda na kutia muhuri sheria

miongoni mwa wanafunzi wangu.

8:17 Kum 31:17; Za 27:14; 22:5; Ebr 2:13Nitamngojea Bwana,

ambaye ameificha nyumba ya Yakobo uso wake.

Nitaliweka tumaini langu kwake.

8:18 Mwa 33:5; Ebr 2:13; Kut 3:12; Lk 2:34; Eze 12:6; 24:24; 4:3; Kum 28:46; Eze 12:11; Za 9:11Niko hapa, pamoja na watoto ambao Bwana amenipa. Sisi ni ishara na mfano wake katika Israeli, kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayeishi juu ya Mlima Sayuni.

8:19 1Sam 28:8; Isa 29:4; Hes 27:21; Law 19:31Wakati watu wanapowaambia ninyi kutafuta ushauri kwa waaguzi na wenye kuongea na mizimu, ambao hunongʼona na kunungʼunika, je, watu wasingeuliza kwa Mungu wao? Kwa nini watake shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai? 8:20 Mik 3:6; Isa 60:2; 1:10; Rut 4:7; Lk 16:29; Isa 9:2; 59:9; 9:2Kwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko. 8:21 Ay 18:12; Kut 22:28; Ay 30:3; Ufu 16:11Watazunguka katika nchi yote, wakiwa na dhiki na njaa. Watakapotaabika kwa njaa, watapatwa na hasira kali, nao, wakiwa wanatazama juu, watamlaani mfalme wao na Mungu wao. 8:22 Ay 15:24; 3:13; Isa 5:30; Ufu 16:10; Mt 25:30Kisha wataangalia duniani na kuona tu dhiki na giza, hofu na huzuni tupu, nao watasukumiwa kwenye giza nene kabisa.

Read More of Isaya 8

Isaya 9:1-21

Kwa Ajili Yetu Mtoto Amezaliwa

9:1 2Fal 15:29; 1Nya 5:26; Law 26:24; Ay 15:24Hata hivyo, hapatakuwepo huzuni tena kwa wale waliokuwa katika dhiki. Wakati uliopita aliidhili nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, lakini katika siku zijazo ataiheshimu Galilaya ya Mataifa, karibu na njia ya bahari, kando ya Yordani:

9:2 Mt 4:15-16; Eze 5:8; Mal 4:2; Yn 8:12; Za 82:5; 107:10-14; 36:9; Isa 8:20; Efe 5:8Watu wanaotembea katika giza

wameona nuru kuu,

wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti,

nuru imewazukia.

9:3 Ay 12:23; Isa 25:9; Kut 15:9; Za 119:162; 4:7; Yos 22:8Umelikuza taifa,

na kuzidisha furaha yao,

wanafurahia mbele zako,

kama watu wanavyofurahia wakati wa mavuno,

kama watu wafurahivyo

wagawanyapo nyara.

9:4 Amu 7:22-25; Nah 1:13; Isa 10:26-27; Mt 11:30; Isa 60:18; Ay 34:24; Isa 37:36-38; 14:24; Yer 2:20; Za 81:6Kama vile siku ya kushindwa kwa Wamidiani,

umevunja nira iliyowalemea,

ile gongo mabegani mwao na

fimbo yake yeye aliyewaonea.

9:5 Isa 2:4Kila kiatu cha askari kilichotumiwa vitani,

na kila vazi lililovingirishwa katika damu

vitawekwa kwa ajili ya kuchomwa,

vitakuwa kuni za kuwasha moto.

9:6 Ebr 13:20; Mwa 3:15; Ay 15:8; Amu 13:18; Mt 28:18; Za 24:8; Lk 2:14; Mwa 3:15Kwa maana, kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,

tumepewa mtoto mwanaume,

nao utawala utakuwa mabegani mwake.

Naye ataitwa

Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,

Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.

9:7 Dan 2:44; Yn 12:34; Yer 23:5; 2Fal 19:31; Za 85:8; 1Kor 15:25; 2Sam 7:13Kuongezeka kwa utawala wake na amani

hakutakuwa na mwisho.

Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi

na juu ya ufalme wake,

akiuthibitisha na kuutegemeza

kwa haki na kwa adili,

tangu wakati huo na hata milele.

Wivu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote

utatimiza haya.

Hasira Ya Bwana Dhidi Ya Israeli

Bwana ametuma ujumbe dhidi ya Yakobo,

utamwangukia Israeli.

9:9 Isa 7:9; Eze 2:4; Zek 7:11; Isa 2:4Watu wote watajua hili:

Efraimu na wakazi wa Samaria,

wanaosema kwa kiburi

na majivuno ya mioyo,

9:10 Mwa 11:3; Amo 7:14; Lk 19:14; 1Fal 7:2-3“Matofali yameanguka chini,

lakini tutajenga tena kwa mawe yaliyochongwa,

mitini imeangushwa,

lakini tutapanda mierezi badala yake.”

9:11 Isa 7:8Lakini Bwana amemtia nguvu adui wa Resini dhidi yao

na kuchochea watesi wao.

9:12 Za 79:7; Isa 5:25; 2Fal 16:6; Ay 40:11Waashuru kutoka upande wa mashariki

na Wafilisti kutoka upande wa magharibi

wameila Israeli kwa kinywa kilichopanuliwa.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,

mkono wake bado umeinuliwa juu.

9:13 Yer 5:3; Amo 4:6-10; Sef 1:16; 2Nya 28:22; Hag 2:17; Dan 9:13; Yer 50:4; Isa 17:7Lakini watu hawajamrudia yeye aliyewapiga,

wala hawajamtafuta Bwana Mwenye Nguvu Zote.

9:14 Isa 19:15; Ufu 18:8Kwa hiyo Bwana atakatilia mbali kutoka Israeli kichwa na mkia,

tawi la mtende na tete katika siku moja.

9:15 Isa 3:2-3; 5:13; 28:7; Ay 13:4; Eze 13:2, 22; Mt 24:24Wazee na watu mashuhuri ndio vichwa,

nao manabii wanaofundisha uongo ndio mkia.

9:16 Mt 15:14; 23:16, 24; Isa 3:12Wale wanaowaongoza watu hawa wanawapotosha,

nao wale wanaoongozwa wamepotoka.

9:17 Amo 8:13; Rum 3:13-14; Yer 13:14; Isa 32:6; Mik 7:2; Isa 5:25; Yer 9:21; 11:22; Isa 27:11; 5:25; Mt 12:34; Yer 48:15; 49:26Kwa hiyo Bwana hatawafurahia vijana,

wala hatawahurumia yatima na wajane,

kwa kuwa kila mmoja wao hamchi Mungu, nao ni waovu,

na kila kinywa kinanena upotovu.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,

mkono wake bado umeinuliwa juu.

9:18 Za 83:14; Kum 29:23; Isa 1:31; 5:6Hakika uovu huwaka kama moto;

huteketeza michongoma na miiba,

huwasha moto vichaka vya msituni,

hujiviringisha kuelekea juu kama nguzo ya moshi.

9:19 Mik 7:2-6; Isa 13:9-13; Ay 40:11; Za 97:3; Isa 1:31; Yer 17:27; Isa 3:5Kwa hasira ya Bwana Mwenye Nguvu Zote

nchi itachomwa kwa moto,

nao watu watakuwa kuni za kuchochea moto.

Hakuna mtu atakayemhurumia ndugu yake.

9:20 Law 26:26; Ay 18:12; Isa 49:26; Zek 11:9Upande wa kuume watakuwa wakitafuna,

lakini bado wataona njaa;

upande wa kushoto watakuwa wakila,

lakini hawatashiba.

Kila mmoja atajilisha kwa nyama ya mtoto wake mwenyewe:

9:21 Amu 7:22; 12:4; 2Nya 28:6; Isa 5:25Manase atamla Efraimu,

naye Efraimu atamla Manase;

nao pamoja watakuwa kinyume na Yuda.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,

mkono wake bado umeinuliwa juu.

Read More of Isaya 9

Isaya 10:1-19

10:1 Za 58:2; Isa 5:8Ole wao wawekao sheria zisizo za haki,

kwa wale watoao amri za kuonea,

10:2 Isa 3:14; 5:23; Kum 10:18; Ay 6:27; Isa 1:17kuwanyima maskini haki zao

na kuzuilia haki za watu wangu walioonewa,

kuwafanya wajane mawindo yao

na kuwanyangʼanya yatima.

10:3 Isa 31:3; Hes 9:7; Lk 19:44; Ay 31:14; Za 59:5; Isa 13:6Mtafanya nini siku ya kutoa hesabu,

wakati maafa yatakapokuja kutoka mbali?

Mtamkimbilia nani awape msaada?

Mtaacha wapi mali zenu?

10:4 Mao 1:12; Yer 39:6; Isa 24:22; Nah 3:3; Zek 9:11; Isa 5:25; 63:10; Yer 30:24Hakutasalia kitu chochote,

isipokuwa kujikunyata miongoni mwa mateka,

au kuanguka miongoni mwa waliouawa.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,

mkono wake bado umeinuliwa juu.

Hukumu Ya Mungu Juu Ya Ashuru

10:5 Sef 2:13; Yer 50:23; 51:20; Isa 37:7; Eze 30:24-25; 2Fal 19:21; Isa 7:20; 14:25“Ole kwa Ashuru, fimbo ya hasira yangu,

ambaye mkononi mwake ana rungu ya ghadhabu yangu!

10:6 Isa 9:17-19; 2Nya 28:9; Amu 6:4; Isa 5:29; 2Sam 22:43; Isa 37:26-27; Za 7:5Ninamtuma dhidi ya taifa lisilomjua Mungu,

ninamtuma dhidi ya taifa linalonikasirisha,

kukamata mateka na kunyakua nyara,

pia kuwakanyaga chini kama matope ya barabarani.

10:7 Mwa 50:20; Mdo 4:23-28; Mik 4:12Lakini hili silo analokusudia,

hili silo alilo nalo akilini;

kusudi lake ni kuangamiza,

kuyakomesha mataifa mengi.

10:8 2Fal 18:24Maana asema, ‘Je, wafalme wote

si majemadari wangu?

10:9 2Nya 35:20; Mwa 14:15; 2Fal 17:6; Yer 49:24; Hes 13:21; 34:8; Amo 6:2; Mwa 10:10Je, Kalno hakutendwa kama Karkemishi?

Hamathi si kama Arpadi,

nayo Samaria si kama Dameski?

10:10 2Fal 19:18Kama vile mkono wangu ulivyotwaa falme za sanamu,

falme ambazo vinyago vyao vilizidi vile vya Yerusalemu na Samaria:

10:11 2Fal 19:13; Isa 36:18-20; 37:10-13je, nisiishughulikie Yerusalemu na sanamu zake

kama nilivyoshughulikia Samaria na vinyago vyake?’ ”

10:12 2Fal 19:7, 31; Isa 28:21; 2:8; Yer 50:18; 5:29; Isa 2:11; Eze 28:17; Za 18:27Bwana atakapokuwa amemaliza kazi yake yote dhidi ya Mlima Sayuni na Yerusalemu, atasema, “Nitamwadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya majivuno ya ukaidi wa moyo wake na kutazama kwa macho yenye dharau.” 10:13 Kut 15:9; Eze 28:4; Dan 4:30; Kum 32:26-27; 8:17; Isa 47:7; 14:13-14Kwa kuwa anasema:

“ ‘Kwa nguvu za mkono wangu nimefanya hili,

kwa hekima yangu, kwa sababu nina ufahamu.

Niliondoa mipaka ya mataifa,

niliteka nyara hazina zao,

kama yeye aliye shujaa

niliwatiisha wafalme wao.

10:14 Oba 1:4; Hab 2:6-11; Ay 31:25; Yer 49:16; Isa 37:24-25; 2Fal 19:22-24Kama mtu atiavyo mkono kwenye kiota,

ndivyo mkono wangu ulivyochukua utajiri wa mataifa;

kama watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa,

ndivyo nilivyokusanya nchi zote;

wala hakuna hata mmoja aliyepiga bawa

au kufungua kinywa chake kutoa mlio.’ ”

10:15 Rum 9:20-21; Isa 7:20; 45:9Je, shoka laweza kujigamba kuwa na nguvu zaidi

kuliko yule anayelitumia,

au msumeno kujisifu

dhidi ya yule anayeutumia?

Ni kana kwamba fimbo ingeweza kumwinua yeye aichukuaye,

au mkongojo ungemwinua mwenye kuutumia!

10:16 Hes 11:33; Isa 17:14; Za 78:31; Isa 8:7; Yer 21:14Kwa hiyo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,

atatuma ugonjwa wa kudhoofisha kwa askari wake walio hodari,

katika fahari yake moto utawaka

kama mwali wa moto.

10:17 Ay 41:21; Isa 37:23; 2Sam 23:6; Isa 9:18; 31:9; Zek 2:5Nuru ya Israeli itakuwa moto,

Aliye Mtakatifu wao mwali wa moto;

katika siku moja utaunguza na kuteketeza miiba

na michongoma yake.

10:18 2Fal 19:23Fahari ya misitu yake na mashamba yenye rutuba

utateketeza kabisa,

kama vile mtu mgonjwa adhoofikavyo.

10:19 Isa 21:12; 32:19; 17:6; 21:17; 27:13; Yer 44:28Nayo miti inayobaki katika misitu yake itakuwa michache sana

hata mtoto mdogo angeweza kuihesabu.

Read More of Isaya 10