Isaya 65:17-25, Isaya 66:1-24 NEN

Isaya 65:17-25

Mbingu Mpya Na Dunia Mpya

65:17 2Kor 5:17; 2Pet 3:13; Yer 3:16; Ufu 7:17; Isa 41:22; 43:18“Tazama, nitaumba

mbingu mpya na dunia mpya.

Mambo ya zamani hayatakumbukwa,

wala hayatakuja akilini.

65:18 Kum 32:43; Za 98:1-9; Isa 25:9; Ufu 21:2Lakini furahini na kushangilia daima

katika hivi nitakavyoumba,

kwa kuwa nitaumba Yerusalemu uwe wa kupendeza,

nao watu wake wawe furaha.

65:19 Isa 35:10; 62:5; Ufu 7:17; Kum 30:9; Isa 25:8Nami nitaifurahia Yerusalemu

na kuwafurahia watu wangu;

sauti ya maombolezo na ya kilio

haitasikika humo tena.

65:20 Mwa 15:15; Mhu 8:12; Zek 8:4; Isa 11:8; Mwa 5:1-32“Kamwe hatakuwepo tena ndani yake

mtoto mchanga atakayeishi siku chache tu,

au mzee ambaye hataishi akatimiza miaka yake.

Yeye atakayekufa akiwa na umri wa miaka mia moja

atahesabiwa kwamba ni kijana tu,

yeye ambaye hatafika miaka mia moja,

atahesabiwa kuwa amelaaniwa.

65:21 Isa 32:18; 2Fal 19:29; Eze 28:26; Isa 61:4; 37:30; Amo 9:14Watajenga nyumba na kuishi ndani yake;

watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake.

65:22 Za 92:12-14; 21:4; 91:16; Kum 28:30; Isa 14:1Hawatajenga nyumba, nao watu wengine waishi ndani yake,

au kupanda mazao na wengine wale.

Kwa kuwa kama zilivyo siku za mti,

ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu,

wateule wangu watafurahia kwa siku nyingi

kazi za mikono yao.

65:23 Mwa 12:2; Kum 28:3-12; Mdo 2:39; Hos 9:12; Isa 49:4; 1Kor 15:58; Yer 3:4Hawatajitaabisha kwa kazi bure,

wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga,

kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na Bwana,

wao na wazao wao pamoja nao.

65:24 Dan 9:20-23; 10:12; Mt 6:8; Isa 55:6; Ay 8:6; Zek 10:6; Isa 30:19Kabla hawajaita, nitajibu,

nao wakiwa katika kunena, nitasikia.

65:25 Mwa 3:14; Rum 16:20; Mik 7:17; Isa 11:6; Dan 2:35; Ay 40:15; 5:23; Isa 2:4Mbwa mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja,

naye simba atakula nyasi kama maksai,

lakini mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka.

Hawatadhuru wala kuharibu

katika mlima wangu mtakatifu wote,”

asema Bwana.

Read More of Isaya 65

Isaya 66:1-24

Hukumu Na Matumaini

66:1 2Nya 6:18; Mt 23:22; Mdo 17:24; 1Fal 8:27; Mt 5:34-35; Za 2:4; 2Sam 7:7Hili ndilo asemalo Bwana,

“Mbingu ni kiti changu cha enzi,

nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.

Iko wapi nyumba mtakayoijenga kwa ajili yangu?

Mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?

66:2 Isa 40:26; Mdo 17:24; Ezr 9:4; Mit 28:14; Mdo 7:50; Isa 57:15; Mt 5:3-4; Lk 18:13-14Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote,

hivyo vikapata kuwepo?”

asema Bwana.

“Mtu huyu ndiye ninayemthamini:

yeye ambaye ni mnyenyekevu

na mwenye roho yenye toba,

atetemekaye asikiapo neno langu.

66:3 Isa 1:11; Law 2:2; Isa 57:17; Kum 27:15; Eze 8:9-13Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali

ni kama yeye auaye mtu,

na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo,

ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa.

Yeyote atoaye sadaka ya nafaka,

ni kama yule aletaye damu ya nguruwe,

na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu,

ni kama yule aabuduye sanamu.

Wamejichagulia njia zao wenyewe,

nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao.

66:4 Mit 10:24; 1Sam 8:19; Mit 1:24; 2Fal 21:2-6; Isa 10:12; 41:28; 65:12Hivyo, mimi pia nitawachagulia mapigo makali,

nami nitaleta juu yao kile wanachokiogopa.

Kwa maana nilipoita, hakuna yeyote aliyejibu,

niliposema, hakuna yeyote aliyesikiliza.

Walifanya maovu machoni pangu

na kuchagua lile linalonichukiza.”

66:5 Za 38:20; Yn 15:18-21; Lk 13:17; Tit 2:13; Ezr 9:4; Isa 60:15; 44:9Sikieni neno la Bwana,

ninyi mtetemekao kwa neno lake:

“Ndugu zenu wanaowachukia ninyi

na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema,

Bwana na atukuzwe,

ili tupate kuona furaha yenu!’

Hata sasa wataaibika.

66:6 1Sam 2:10; Za 68:33; Law 26:28; Isa 65:6; Yoe 3:7Sikieni hizo ghasia kutoka mjini,

sikieni hizo kelele kutoka hekaluni!

Ni sauti ya Bwana ikiwalipa adui zake

yote wanayostahili.

66:7 Isa 54:1; Ufu 12:5“Kabla hajasikia utungu, alizaa;

kabla hajapata maumivu,

alizaa mtoto mwanaume.

66:8 Isa 64:4; Yer 18:13; Isa 49:20, 21Ni nani amepata kusikia jambo kama hili?

Ni nani amepata kuona mambo kama haya?

Je, nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja,

au taifa laweza kutokea mara?

Mara Sayuni alipoona utungu,

alizaa watoto wake.

66:9 Isa 37:3Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwa

na nisizalishe?” asema Bwana.

“Je, nifunge tumbo la uzazi

wakati mimi ndiye nizalishaye?”

asema Mungu wako.

66:10 Kum 32:43; Rum 15:10; Za 26:8; Isa 25:9; 57:19; 61:2“Shangilieni pamoja na Yerusalemu na mfurahi kwa ajili yake,

ninyi nyote mnaompenda,

shangilieni kwa nguvu pamoja naye,

ninyi nyote mnaoomboleza juu yake.

66:11 Hes 11:12; Isa 60:16; Mwa 49:25; Isa 25:6; Hes 25:1Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka

katika faraja ya matiti yake;

mtakunywa sana,

na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.”

66:12 Isa 33:21; 48:18; Hes 11:12; Isa 60:4-5; Za 72:3; 119:165; Isa 9:6Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:

“Nitamwongezea amani kama mto,

nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho;

utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwake

na kubembelezwa magotini pake.

66:13 Isa 40:1; 2Kor 1:4; 1The 2:7; Isa 49:15Kama mama anavyomfariji mtoto wake,

ndivyo nitakavyokufariji wewe,

nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.”

66:14 Eze 37:1; Isa 10:5; 30:27; 25:9; Za 72:16; Isa 54:17; 41:20Wakati mtakapoona jambo hili, mioyo yenu itashangilia,

nanyi mtastawi kama majani;

mkono wa Bwana utajulikana kwa watumishi wake,

bali ghadhabu yake kali

itaonyeshwa kwa adui zake.

66:15 2Fal 2:11; Za 68:17; Kum 28:20; Za 39:11; Isa 1:31; 42:25Tazama, Bwana anakuja na moto,

magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli,

atateremsha hasira yake kwa ghadhabu kali,

na karipio lake pamoja na miali ya moto.

66:16 Amo 7:4; Eze 24:21; Isa 1:20; 30:30; 13:9-11; Yer 2:35; Eze 36:5; Isa 10:4Kwa maana kwa moto na kwa upanga wake

Bwana atatekeleza hukumu juu ya watu wote,

nao wengi watakuwa ni wale

waliouawa na Bwana.

66:17 Isa 65:3; Za 37:20; Isa 1:28-29; Law 11:7, 29“Watu wote wanaojiweka wakfu na kujitakasa wenyewe ili kwenda bustanini, wakimfuata aliye katikati ya wale ambao hula nyama za nguruwe na panya pamoja na vitu vingine vilivyo machukizo, watafikia mwisho wao pamoja,” asema Bwana.

66:18 Mit 24:2; Isa 65:2; 2:3; Zek 12:3; Kut 16:17; Isa 59:19“Nami, kwa sababu ya matendo yao na mawazo yao, niko karibu kuja na kukusanya mataifa yote na lugha zote, nao watakuja na kuuona utukufu wangu.

66:19 Lk 2:34; Isa 11:10-11; Mt 24:30; Eze 27:10; 1Nya 16:24; Isa 24:15; Yer 46:9“Nitaweka ishara katikati yao, nami nitapeleka baadhi ya hao walionusurika kwa mataifa, hadi Tarshishi, kwa Puli66:19 Puli hapa inamaanisha Libya. na Waludi (wanaojulikana kama wapiga upinde), kwa Tubali na Uyunani, hadi visiwa vya mbali ambavyo havijasikia juu ya sifa zangu au kuuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa. 66:20 Isa 52:11; Rum 15:16; Yer 31:23; Eze 34:13; Kum 33:19; Yer 25:22Nao watawaleta ndugu zenu wote, kutoka mataifa yote, mpaka kwenye mlima wangu mtakatifu katika Yerusalemu kama sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, katika magari ya vita na magari makubwa, juu ya nyumbu na ngamia,” asema Bwana. “Watawaleta, kama Waisraeli waletavyo sadaka zao za nafaka, katika Hekalu la Bwana, katika vyombo safi kwa kufuata desturi za ibada. 66:21 Kut 19:6; 1Pet 2:5-9Nami nitachagua baadhi yao pia wawe makuhani na Walawi,” asema Bwana.

66:22 2Pet 3:13; Isa 65:17; 1Pet 1:4-5; Isa 48:19; Ebr 12:26-27; Yn 10:27-29“Kama vile mbingu mpya na nchi mpya ninazozifanya zitakavyodumu mbele zangu,” asema Bwana, “ndivyo jina lenu na wazao wenu watakavyodumu. 66:23 Eze 46:1-3; Ufu 15:4; Za 22:29; Zek 14:16; Isa 19:21; 44:5Kutoka Mwezi Mpya hata mwingine, na kutoka Sabato hadi nyingine, wanadamu wote watakuja na kusujudu mbele zangu,” asema Bwana. 66:24 Isa 14:11; 1:31; Mt 25:41; Mk 9:48; Za 110:6; Isa 1:2“Nao watatoka nje na kuona maiti za wale walioniasi mimi. Funza wao hawatakufa, wala moto wao hautazimika, nao watakuwa kitu cha kuchukiza sana kwa wanadamu wote.”

Read More of Isaya 66