Isaya 60:1-22, Isaya 61:1-11, Isaya 62:1-12 NEN

Isaya 60:1-22

Utukufu Wa Sayuni

60:1 Isa 52:2; Yn 8:12; Mal 4:2; Za 36:9; Efe 5:14; Za 118:27; Ufu 21:11; Kut 16:7“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja

na utukufu wa Bwana umezuka juu yako.

60:2 Yer 13:16; Kol 1:13; 1Sam 2:9; Za 82:5; Isa 8:20; Za 107:14Tazama, giza litaifunika dunia

na giza kuu litayafunika mataifa,

lakini Bwana atazuka juu yako

na utukufu wake utaonekana juu yako.

60:3 Mt 2:1-11; Isa 49:23; Ufu 21:24; Isa 44:5; 45:14; 42:6Mataifa watakuja kwenye nuru yako

na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako.

60:4 Isa 11:12; 43:6; 49:20-22; Yer 30:10; Isa 43:6“Inua macho yako na utazame pande zote:

Wote wanakusanyika na kukujia,

wana wako wanakuja toka mbali,

nao binti zako wanabebwa mikononi.

60:5 Rum 11:25; Kut 34:29; Isa 35:2; 65:13; 66:14; Zek 10:7; Kum 33:19; Amu 3:15; Ufu 21; 6Ndipo utatazama na kutiwa nuru,

moyo wako utasisimka na kujaa furaha,

mali zilizo baharini zitaletwa kwako,

utajiri wa mataifa utakujilia.

60:6 Mwa 25:2-4; Yer 6:20; Za 72:10; Mt 2:11; Amu 6:5; Isa 42:10Makundi ya ngamia yatajaa katika nchi yako,

ngamia vijana wa Midiani na Efa.

Nao wote watokao Sheba watakuja,

wakichukua dhahabu na uvumba

na kutangaza sifa za Bwana.

60:7 Mwa 25:13; Hag 2:3-9; Isa 18:7; Sef 3:10; Eze 20:40; 43:27; Isa 19:21Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako,

kondoo dume wa Nebayothi watakutumikia,

watakubalika kama sadaka juu ya madhabahu yangu,

nami nitalipamba Hekalu langu tukufu.

60:8 Isa 49:21; 19:1“Ni nani hawa warukao kama mawingu,

kama hua kuelekea kwenye viota vyao?

60:9 Mwa 10:4; Isa 2:16; 14:2; Yer 30:19; Isa 43:6; Gal 4:26; 1Fal 10:22Hakika visiwa vinanitazama,

merikebu za Tarshishi60:9 Au: za biashara (ona pia 1Fal 10:22; 22:48; 2Nya 9:21; 20:36; Isa 2:16). ndizo zinazotangulia,

zikiwaleta wana wenu kutoka mbali,

wakiwa na fedha na dhahabu zao,

kwa heshima ya Bwana, Mungu wenu,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,

kwa maana amekujalia utukufu.

60:10 Ezr 1:2; Ufu 21:24; Za 102:13; Isa 54:8; Kut 1:11; Isa 14:1-2; 56:6“Wageni watazijenga upya kuta zako,

na wafalme wao watakutumikia.

Ingawa katika hasira nilikupiga,

lakini katika upendeleo wangu

nitakuonyesha huruma.

60:11 Mik 2:13; Ufu 21:25-26; Isa 2:12; 61:6; Za 24:7Malango yako yatakuwa wazi siku zote,

kamwe hayatafungwa, mchana wala usiku,

ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa:

wafalme wao wakiongoza maandamano ya ushindi.

60:12 Isa 11:14; Zek 14:17; Za 2:12; Dan 2:34; Mwa 27:29Kwa maana taifa au ufalme ule ambao hautakutumikia utaangamia;

utaharibiwa kabisa.

60:13 Isa 35:2; Ezr 3:7; 1Nya 28:2; Isa 41:19“Utukufu wa Lebanoni utakujilia,

msunobari, mvinje pamoja na mteashuri,

ili kupapamba mahali pangu patakatifu,

nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu.

60:14 Mwa 27:29; Ufu 3:9; Ebr 12:22; Isa 14:9; 1:12Wana wa wale waliokuonea watakuja wakisujudu mbele yako,

wote wanaokudharau watasujudu kwenye miguu yako,

nao watakuita Mji wa Bwana,

Sayuni ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.

60:15 Isa 6:12; 54:6; Za 126:5; Isa 65:18; 1:7-9; Kut 14:30; Isa 33:8“Ingawa umeachwa na kuchukiwa,

bila yeyote anayesafiri ndani yako,

nitakufanya kuwa fahari ya milele,

na furaha ya vizazi vyote.

60:16 Eze 34:30; Kut 6:2; Isa 66:11-12; Ay 19:25; Isa 59:20; Kut 14:30Utanyonya maziwa ya mataifa,

na kunyonyeshwa matiti ya wafalme.

Ndipo utakapojua kwamba Mimi, Bwana, ni Mwokozi wako,

Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.

60:17 1Fal 10:21; Za 85:8; Isa 66:12; 9:7; Hag 2:9Badala ya shaba nitakuletea dhahabu,

na fedha badala ya chuma.

Badala ya mti nitakuletea shaba,

na chuma badala ya mawe.

Nitafanya amani kuwa mtawala wako,

na haki kuwa mfalme wako.

60:18 Law 26:6; 2Sam 7:10; Yer 33:9; Sef 3:20; Isa 9:4; 49:19; 33:6; 61:11; 62:7Jeuri hazitasikika tena katika nchi yako,

wala maangamizi au uharibifu ndani ya mipaka yako,

lakini utaita kuta zako Wokovu,

na malango yako Sifa.

60:19 Zek 2:5; Za 36:9; Ufu 21:23; 22:5; Za 118:27Jua halitakuwa tena nuru yako mchana,

wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia,

kwa maana Bwana atakuwa nuru yako ya milele,

naye Mungu wako atakuwa utukufu wako.

60:20 Amo 8:9; Isa 30:19, 26; Ufu 7:17; Isa 35:10Jua lako halitazama tena,

nao mwezi wako hautafifia tena;

Bwana atakuwa nuru yako milele,

nazo siku zako za huzuni zitakoma.

60:21 Efe 2:10; Law 10:3; Za 37:11, 22; Zek 8:12; Amo 9:15; Isa 4:3; Yer 32:41; Mt 15:13Ndipo watu wako wote watakuwa waadilifu,

nao wataimiliki nchi milele.

Wao ni chipukizi nililolipanda,

kazi ya mikono yangu,

ili kuonyesha utukufu wangu.

60:22 Mwa 12:2; Kum 1:10; Isa 5:19Aliye mdogo kwenu atakuwa elfu,

mdogo kuliko wote atakuwa taifa lenye nguvu.

Mimi ndimi Bwana;

katika wakati wake nitayatimiza haya upesi.”

Read More of Isaya 60

Isaya 61:1-11

Mwaka Wa Upendeleo Wa Bwana

61:1 Isa 11:2; Mdo 4:26; Lk 4:18-19; Zek 9:12; 2Kor 3:17; Isa 50:4; Dan 9:24-26; Ay 5:16Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu,

kwa sababu Bwana amenitia mafuta

kuwahubiria maskini habari njema.

Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo,

kuwatangazia mateka uhuru wao,

na hao waliofungwa

habari za kufunguliwa kwao;

61:2 Isa 49:8; Mal 4:1-3; Mt 5:4; Isa 1:24; Lk 4:18-19; Ay 5:1; Lk 6:21kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa,

na siku ya kisasi ya Mungu wetu,

kuwafariji wote waombolezao,

61:3 Isa 60:20-21; 3:23; Ay 2:8; Rut 3:3; Ebr 1:9; Yer 31:13; Za 92:12-13; Mt 15:13na kuwapa mahitaji

wale wanaohuzunika katika Sayuni,

ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu,

mafuta ya furaha badala ya maombolezo,

vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa.

Nao wataitwa mialoni ya haki,

pando la Bwana,

ili kuonyesha utukufu wake.

61:4 Amo 9:14; Yn 15:8; Zek 1:16-17; Isa 44:26; Eze 36:33Watajenga upya magofu ya zamani

na kupatengeneza mahali palipoachwa ukiwa zamani;

watafanya upya miji iliyoharibiwa,

iliyoachwa ukiwa kwa vizazi vingi.

61:5 Isa 14:1-2; Eze 36:33; Isa 56:6Wageni watayachunga makundi yenu,

wageni watafanya kazi katika mashamba yenu,

na kutunza mashamba yenu ya mizabibu.

61:6 Kut 19:6; Kum 33:19; 1Pet 2:5; Isa 60:1Nanyi mtaitwa makuhani wa Bwana,

mtaitwa watumishi wa Mungu wetu.

Mtakula utajiri wa mataifa,

nanyi katika utajiri wao mtajisifu.

61:7 Kum 21:17; Zek 9:12; Isa 29:22; 41:11; 60:21; Za 126:5; Isa 25:9Badala ya aibu yao

watu wangu watapokea sehemu maradufu,

na badala ya fedheha

watafurahia katika urithi wao;

hivyo watarithi sehemu maradufu katika nchi yao,

nayo furaha ya milele itakuwa yao.

61:8 Mwa 9:16; Isa 1:17; 55:3; 5:16; Za 11:7; Ebr 13:20; Isa 42:6“Kwa maana Mimi, Bwana, napenda haki,

na ninachukia unyangʼanyi na uovu.

Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao

na kufanya agano la milele nao.

61:9 Isa 43:5; 48:19; Mwa 12:2; Kum 28:3-12Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa,

na uzao wao miongoni mwa kabila za watu.

Wale wote watakaowaona watatambua

kuwa ni taifa ambalo Bwana amelibariki.”

61:10 Hab 3:18; Ay 27:6; Isa 49:18; Ufu 21:2; Za 2:11; Isa 7:13; Lk 1:47; Ufu 19:8Ninafurahia sana katika Bwana,

nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu.

Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu,

na kunipamba kwa joho la haki,

kama vile bwana arusi apambavyo

kichwa chake kama kuhani,

na kama bibi arusi ajipambavyo

kwa vito vyake vya thamani.

61:11 Za 85:11; Isa 45:8; Mwa 47:23; Isa 58:11Kwa maana kama vile ardhi ifanyavyo chipukizi kuota,

na bustani isababishavyo mbegu kuota,

ndivyo Bwana Mwenyezi atafanya haki na sifa

zichipuke mbele ya mataifa yote.

Read More of Isaya 61

Isaya 62:1-12

Jina Jipya La Sayuni

Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza,

kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia,

mpaka haki yake itakapoangaza kama mapambazuko,

wokovu wake kama mwanga wa moto.

62:2 Isa 1:26; Za 67:2; Ufu 3:12; Mwa 32:28; Ufu 2:7; Es 4:14; Za 50:12Mataifa wataona haki yako,

nao wafalme wote wataona utukufu wako;

wewe utaitwa kwa jina jipya

lile ambalo kinywa cha Bwana kitatamka.

62:3 Zek 9:16; 1The 2:19; Isa 28:5Utakuwa taji ya fahari mkononi mwa Bwana,

taji ya kifalme mkononi mwa Mungu wako.

62:4 Law 26:43; 1Pet 2:10; Hos 2:19; Yer 3:14; Sef 3:17; Mal 3:12; Isa 6:12; 54:6Hawatakuita tena Aliyeachwa,

wala nchi yako kuiita Ukiwa.

Bali utaitwa Hefsiba,62:4 Hefsiba maana yake Yeye ninayemfurahia.

nayo nchi yako itaitwa Beula,62:4 Beula maana yake Aliyeolewa.

kwa maana Bwana atakufurahia,

nayo nchi yako itaolewa.

62:5 Kum 28:63; Wim 3:11; Isa 65:19; Yer 31:12; Sef 3:17Kama vile kijana aoavyo mwanamwali,

ndivyo wanao62:5 Au: wajenzi wako. watakavyokuoa wewe;

kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake,

ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.

62:6 Eze 3:17; Ebr 13:17; Isa 52:8; Za 132:4Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, ee Yerusalemu,

hawatanyamaza mchana wala usiku.

Ninyi wenye kumwita Bwana,

msitulie,

62:7 Mt 15:21-28; Sef 3:20; Lk 18:1-8; Isa 60:18; Kum 26:19msimwache apumzike hadi atakapoufanya imara Yerusalemu

na kuufanya uwe sifa ya dunia.

62:8 Kum 28:30-33; Yer 5:17; Mwa 22:16; Isa 14:25; 49:18Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume

na kwa mkono wake wenye nguvu:

“Kamwe sitawapa tena adui zenu

nafaka zenu kama chakula chao;

kamwe wageni hawatakunywa tena

divai mpya ambayo mmeitaabikia,

lakini wale waivunao nafaka wataila

na kumsifu Bwana,

nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yake

katika nyua za patakatifu pangu.”

62:10 Isa 11:10-16; 57:14; Za 24:7; Isa 60:11Piteni, piteni katika malango!

Tengenezeni njia kwa ajili ya watu.

Jengeni, jengeni njia kuu!

Ondoeni mawe.

Inueni bendera kwa ajili ya mataifa.

62:11 Amo 9:14; Kum 12:7; Yoe 2:26; Isa 1:10Bwana ametoa tangazo

mpaka miisho ya dunia:

“Mwambie Binti Sayuni,

‘Tazama, mwokozi wako anakuja!

Tazama ujira wake uko pamoja naye,

na malipo yake yanafuatana naye!’ ”

62:12 Za 9:14; Mt 21:5; Isa 35:4; Ufu 22:12; Kum 30:4; Zek 9:9; Isa 40:10Wataitwa Watu Watakatifu,

Waliokombolewa na Bwana;

nawe utaitwa Aliyetafutwa,

Mji Usioachwa Tena.

Read More of Isaya 62