Isaya 57:14-21, Isaya 58:1-14, Isaya 59:1-21 NEN

Isaya 57:14-21

Faraja Kwa Wenye Majuto

57:14 Isa 62:10; Yer 18:15; Isa 11:16Tena itasemwa:

“Jengeni, jengeni, itengenezeni njia!

Ondoeni vikwazo katika njia ya watu wangu.”

57:15 Kum 33:27; Ay 6:10; Mik 6:8; Za 90:2; 2Fal 22:19; Zek 2:13; Isa 52:13; Ay 16:19Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu, yeye aliyeinuliwa sana,

yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu:

“Ninaishi mimi mahali palipoinuka na patakatifu,

lakini pia pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu

na mwenye roho ya unyenyekevu,

ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu

na kuihuisha mioyo yao waliotubu.

57:16 Za 85:5; Mik 7:18; Ebr 12:9; Isa 3:13-14; 54:9; Zek 12:1Sitaendelea kulaumu milele,

wala sitakasirika siku zote,

kwa kuwa roho ya mwanadamu

ingezimia mbele zangu:

yaani pumzi ya mwanadamu niliyemuumba.

57:17 Isa 56:11; Yer 8:10; Isa 30:15; 53:6; 66:3Nilighadhibika na tamaa yake ya dhambi;

nilimwadhibu, nikauficha uso wangu kwa hasira,

na bado aliendelea katika njia zake za tamaa.

57:18 Kum 32:39; 2Nya 7:14; Isa 49:13; Za 48:14; Isa 42:16; 48:17Nimeziona njia zake, lakini nitamponya,

nitamwongoza na kumrudishia upya faraja,

57:19 Isa 51:16; Ebr 13:15; Efe 2:17; Mdo 2:39; Lk 2:14; Isa 32:17; 26:3nikiumba sifa midomoni ya waombolezaji

katika Israeli.

Amani, amani, kwa wale walio mbali

na kwa wale walio karibu,”

asema Bwana. “Nami nitawaponya.”

57:20 Ay 18:5-21; Mwa 49:4; Efe 4:14; Yud 13; Za 69:14Bali waovu ni kama bahari ichafukayo,

ambayo haiwezi kutulia,

mawimbi yake hutupa takataka na matope.

57:21 Isa 26:3; Eze 13:16; Isa 59:8; 48:22Mungu wangu asema,

“Hakuna amani kwa waovu.”

Read More of Isaya 57

Isaya 58:1-14

Mfungo Wa Kweli

58:1 Isa 24:20; 40:6; 48:8; Eze 3:17; Isa 57:12“Piga kelele, usizuie.

Paza sauti yako kama tarumbeta.

Watangazieni watu wangu uasi wao,

na kwa nyumba ya Yakobo dhambi zao.

58:2 Isa 29:13; Yak 4:8Kwa maana kila siku hunitafuta,

wanaonekana kutaka kujua njia zangu,

kana kwamba walikuwa taifa linalotenda lililo sawa,

na ambalo halijaziacha amri za Mungu wake.

Hutaka kwangu maamuzi ya haki,

nao hutamani Mungu awakaribie.

58:3 Law 16:29; Mal 3:14; Zek 7:5-6; Kut 10:3; 2Nya 6:37; Yer 44:10; Isa 22:13Wao husema, ‘Mbona tumefunga, nawe hujaona?

Mbona tumejinyenyekeza, nawe huangalii?’

“Lakini katika siku ya kufunga kwenu, mnafanya mnavyotaka

na kuwadhulumu wafanyakazi wenu wote.

58:4 Mal 2:16; Mao 3:44; Mik 3:4; 1Fal 21:9-13; Isa 59:6; Eze 7:11; 8:18; 1Sam 8:18Kufunga kwenu huishia kwenye magomvi na mapigano,

na kupigana ninyi kwa ninyi kwa ngumi za uovu.

Hamwezi kufunga kama mnavyofanya leo

na kutazamia sauti zenu kusikiwa huko juu.

58:5 Zek 7:5; 1Fal 21:27; Mt 6:16; Ay 2:8; Isa 36:6Je, hii ndiyo aina ya mfungo niliouchagua,

siku moja tu ya mtu kujinyenyekeza?

Je, ni kwa kuinamisha kichwa chini kama tete,

na kwa kujilaza juu ya nguo ya gunia na majivu?

Je, huo ndio mnaouita mfungo,

siku iliyokubalika kwa Bwana?

58:6 Neh 5:10-11; Kum 14:29; Lk 4:19; Yoe 2:12-13; Yer 34:9; Amo 4:1; Isa 9:4“Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua:

kufungua minyororo ya udhalimu,

na kufungua kamba za nira,

kuwaweka huru walioonewa,

na kuvunja kila nira?

58:7 Ay 22:7; Dan 4:27; Ebr 13:12; Ay 31:19-20; Mwa 29:14; Mt 25:36; Eze 18:16Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaa

na kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi,

unapomwona aliye uchi, umvike,

wala si kumkimbia mtu wa nyama na damu yako mwenyewe?

58:8 Isa 9:2; 30:26; Kut 14:19; Ay 11:17; Isa 26:2Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko

na uponyaji wako utatokea upesi;

ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako,

na utukufu wa Bwana utakuwa mlinzi nyuma yako.

58:9 Mit 6:13; Za 50:12; 12:2; Isa 59:13; Ay 8:6; Dan 9:20; Zek 10:6Ndipo utaita, naye Bwana atajibu,

utalia kuomba msaada,

naye atasema: Mimi hapa.

“Kama ukiiondoa nira ya udhalimu,

na kunyoosha kidole na kuzungumza maovu,

58:10 Kum 15:7-8; Ay 11:17; Isa 42:16nanyi kama mkimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi zenu

na kutosheleza mahitaji ya walioonewa,

ndipo nuru yenu itakapongʼaa gizani,

nao usiku wenu utakuwa kama adhuhuri.

58:11 Za 104:28; Wim 4:15; Yn 4:14; Za 48:14; Isa 42:16; 48:7; Za 68:1; 72:6Bwana atakuongoza siku zote,

atayatosheleza mahitaji yako katika nchi kame,

naye ataitia nguvu mifupa yako.

Utakuwa kama bustani iliyonyweshwa vizuri,

kama chemchemi ambayo maji yake hayakauki kamwe.

Watu wako watajenga tena magofu ya zamani

na kuinua misingi ya kale;

utaitwa Mwenye Kukarabati Kuta Zilizobomoka,

Mwenye Kurejeza Barabara za Makao.

58:13 Law 19:20; Kut 20:8; Za 37:4; Isa 56:2“Kama ukitunza miguu yako isivunje Sabato,

na kutokufanya kama vile upendavyo katika siku yangu takatifu,

kama ukiita Sabato siku ya furaha

na siku takatifu ya Bwana ya kuheshimiwa,

kama utaiheshimu kwa kutoenenda

katika njia zako mwenyewe,

na kutokufanya yakupendezayo

au kusema maneno ya upuzi,

58:14 Ay 22:26; Kum 32:13; Isa 1:20; Za 105:10-11ndipo utakapojipatia furaha yako katika Bwana,

nami nitakufanya upande juu ya miinuko ya nchi

na kusherehekea urithi wa Yakobo baba yako.”

Kinywa cha Bwana kimenena haya.

Read More of Isaya 58

Isaya 59:1-21

Dhambi, Toba Na Ukombozi

59:1 Hes 11:23; Isa 50:2; 30:19; 41:20; 58:9; 65:24Hakika mkono wa Bwana si mfupi hata usiweze kuokoa,

wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia.

59:2 Za 18:41; Yn 9:31; Yer 11:11; Isa 58:4; Eze 39:23; Yer 5:25Lakini maovu yenu yamewatenga

ninyi na Mungu wenu,

dhambi zenu zimewaficha ninyi uso wake,

ili asisikie.

59:3 2Fal 21:16; Eze 22:9; Rum 3:15; Isa 1:15; Za 7:3; Isa 3:8Kwa maana mikono yenu imetiwa mawaa kwa damu

na vidole vyenu kwa hatia.

Midomo yenu imenena uongo,

nazo ndimi zenu zimenongʼona mambo maovu.

59:4 Za 7:14; Yak 1:15; Isa 5:23; Ay 15:31; Isa 44:20; 29:20; Ay 4:8Hakuna hata mmoja anayedai kwa haki;

hakuna hata mmoja anayetetea shauri lake kwa haki.

Wanategemea mabishano matupu na kusema uongo,

huchukua mimba ya magomvi na kuzaa uovu.

59:5 Ay 8:14; Mt 3:7; Isa 11:8Huangua mayai ya nyoka wenye sumu kali

na kutanda wavu wa buibui.

Yeyote alaye mayai yao atakufa,

na wakati moja lianguliwapo, nyoka hutoka humo.

59:6 Isa 28:20; Mit 4:17; Za 55:9; Isa 58:4Utando wao wa buibui haufai kwa nguo;

hawawezi kujifunika kwa kile walichokitengeneza.

Matendo yao ni matendo maovu,

vitendo vya jeuri vipo mikononi mwao.

59:7 2Fal 21:16; Mik 3:10; Mit 6:17; Rum 3:15-17; Mk 7:21-22Miguu yao hukimbilia kwenye dhambi,

ni myepesi kumwaga damu isiyo na hatia.

Mawazo yao ni mawazo maovu;

uharibifu na maangamizi huonekana katika njia zao.

59:8 Mit 2:15; Isa 57:21; Lk 1:79; Amu 5:6; Rum 3:15-17Hawajui njia ya amani,

hakuna haki katika mapito yao.

Wameyageuza kuwa njia za upotovu,

hakuna apitaye njia hizo atakayeifahamu amani.

59:9 Yer 8:15; Ay 19:8; Za 107:14; Isa 5:30; 8:20; Lk 1:79Hivyo uadilifu uko mbali nasi,

nayo haki haitufikii.

Tunatazamia nuru, kumbe! Yote ni giza,

tunatazamia mwanga, lakini tunatembea katika giza kuu.

59:10 Mao 4:14; Sef 1:17; Ay 3:23; Yn 11:10; Kum 28:29; Isa 6:9-10; Mao 3:6Tunapapasa ukuta kama kipofu,

tunapapasa katika njia zetu kama watu wasio na macho.

Adhuhuri tunajikwaa kama wakati wa gizagiza;

katikati ya wenye nguvu, tuko kama wafu.

59:11 Eze 7:16Wote tunanguruma kama dubu;

tunalia kwa maombolezo kama hua.

Tunatafuta haki, kumbe hakuna kabisa;

tunatafuta wokovu, lakini uko mbali.

59:12 Ezr 9:6; Yer 2:19; Mwa 4:7; Isa 57; 12; 3:9; Yer 51:3Kwa sababu makosa yetu ni mengi machoni pako,

na dhambi zetu zinashuhudia dhidi yetu.

Makosa yetu yako pamoja nasi daima,

nasi tunayatambua maovu yetu:

59:13 Hes 11:20; Za 12:5; Mt 12:34; Mk 7:21-22; Mit 30; 9; Tit 1:16; Isa 48:8Uasi na udanganyifu dhidi ya Bwana,

kumgeuzia Mungu wetu kisogo,

tukichochea udhalimu na maasi,

tukinena uongo ambao mioyo yetu imeuhifadhi.

59:14 Neh 8:1; Isa 48:1; Yer 33:16; Isa 29:21; 1:21Hivyo uadilifu umerudishwa nyuma,

nayo haki inasimama mbali,

kweli imejikwaa njiani,

uaminifu hauwezi kuingia.

59:15 Yer 7:28; Dan 8:12; Isa 5:7Kweli haipatikani popote,

na yeyote aepukaye uovu huwa mawindo.

Bwana alitazama naye akachukizwa

kwamba hapakuwepo haki.

59:16 Isa 41:28; 65:3; Za 98:1; Isa 53:12; 46:13Aliona kuwa hakuwepo hata mtu mmoja,

akashangaa kwamba hakuwepo hata mmoja wa kuingilia kati;

hivyo mkono wake mwenyewe

ndio uliomfanyia wokovu,

nayo haki yake mwenyewe

ndiyo iliyomtegemeza.

59:17 Efe 6:14; 1The 5:8; Ay 27:6; Eze 5:13; Efe 6:17; Isa 63:3Alivaa haki kama dirii kifuani mwake,

na chapeo ya wokovu kichwani mwake,

alivaa mavazi ya kisasi

naye akajifunga wivu kama joho.

59:18 Hes 10:35; Isa 34:8; Mt 16:27Kulingana na kile walichokuwa wametenda,

ndivyo atakavyolipa

ghadhabu kwa watesi wake

na kisasi kwa adui zake,

atavilipa visiwa sawa na wanavyostahili.

59:19 Isa 49:12; Za 113:3; Ufu 12:15; Mt 8:11; Za 97:6Kuanzia magharibi, watu wataliogopa jina la Bwana

na kuanzia mawio ya jua, watauheshimu utukufu wake.

Wakati adui atakapokuja kama mafuriko,

Roho wa Bwana atainua kiwango dhidi yake na kumshinda.

59:20 Yer 35:15; Mdo 2:38-39; Rum 11:26; Ay 19:25; Isa 52:8; Yoe 3:21; Yer 35:15“Mkombozi atakuja Sayuni,

kwa wale wa Yakobo

wanaozitubu dhambi zao,”

asema Bwana.

59:21 Isa 44:3; Ebr 8:10; Eze 36:37; Mwa 9:16; Kum 29:14; Isa 42:6; Kut 4:15“Kwa habari yangu mimi, hili ndilo agano langu nao,” asema Bwana. “Roho wangu, aliye juu yenu, na maneno yangu ambayo nimeyaweka katika vinywa vyenu, havitaondoka vinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwa watoto wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao, kuanzia sasa na hata milele,” asema Bwana.

Read More of Isaya 59