Isaya 55:1-13, Isaya 56:1-12, Isaya 57:1-13 NEN

Isaya 55:1-13

Mwaliko Kwa Wenye Kiu

55:1 Mao 5:4; Mit 9:5; Ufu 3:18; Yer 2:31; Isa 35:7; Mt 5:6; Lk 5:21; Yn 4:14; Zek 14:8; Hos 14:4; Eze 47:1, 12“Njooni, ninyi nyote wenye kiu,

njooni kwenye maji;

nanyi ambao hamna fedha,

njooni, nunueni na mle!

Njooni, nunueni divai na maziwa

bila fedha na bila gharama.

55:2 Yer 12:13; Hag 1:6; Za 22:26; Mhu 6:2; Isa 49:4; Hos 4:10; 8:7Kwa nini kutumia fedha kwa kitu ambacho si chakula,

na kutaabikia kitu kisichoshibisha?

Sikilizeni, nisikilizeni mimi na mle kilicho kizuri,

nazo nafsi zenu zitafurahia utajiri wa unono.

55:3 Law 18:5; Yn 6:27; Mwa 9:16; Ebr 13:20; Mdo 13:34; Rum 10:5; Isa 54:10Tegeni sikio mje kwangu,

nisikieni mimi, ili nafsi zenu zipate kuishi.

Nitafanya agano la milele nanyi,

pendo la uaminifu nililomwahidi Daudi.

55:4 1Tim 6:13; 1Sam 13:14; Eze 34:23-24; Ebr 2:10; 2Nya 7:18Tazama, nimemfanya kuwa shahidi wa mataifa,

kiongozi na jemadari wa mataifa.

Hakika utaita mataifa usiyoyajua,

nayo mataifa yale yasiyokujua yataharakisha kukujia,

kwa sababu ya Bwana Mungu wako,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,

kwa maana amekutukuza.”

55:6 Mdo 17:27; Za 32:6; Amo 5:14; Yer 33:3; Isa 9:13; Kum 4:29; 2Nya 15:2Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana;

mwiteni maadamu yu karibu.

55:7 Yer 3:12; 26:3; Isa 32:7; Eze 18:32; 2Nya 6:21; 30:6; Eze 18:27-28Mtu mwovu na aiache njia yake,

na mtu mbaya na ayaache mawazo yake.

Yeye na amrudie Bwana, naye atamrehemu,

arudi kwa Mungu wetu, kwa kuwa atamsamehe bure kabisa.

55:8 Isa 53:6; Mik 4:12; Flp 2:5; 4:8“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu,

wala njia zenu si njia zangu,”

asema Bwana.

55:9 Ay 11:8; Za 103:11; Hes 23:19; Isa 40:13-14“Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia,

ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu

na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

55:10 2Kor 9:10; Isa 30:23; Mwa 47:23; Za 67:6; Ay 14:9; Law 25:19Kama vile mvua na theluji

ishukavyo kutoka mbinguni,

nayo hairudi tena huko

bila kunywesha dunia

na kuichipusha na kuistawisha,

hivyo hutoa mbegu kwa mpanzi

na mkate kwa mlaji,

55:11 Isa 54:10-13; 1Nya 16:33; Za 98:4; Isa 35:2; Za 65:12-13; 96:12-13; 98:8ndivyo lilivyo neno langu lile litokalo kinywani mwangu:

Halitanirudia tupu,

bali litatimiliza lile nililokusudia

na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma.

Mtatoka nje kwa furaha

na kuongozwa kwa amani;

milima na vilima

vitapaza sauti kwa nyimbo mbele yenu,

nayo miti yote ya shambani

itapiga makofi.

55:13 Hes 33:55; Za 102:12; Yer 32:20; Isa 5:6; 41:19; 63:12; Yer 33:9Badala ya kichaka cha miiba

itaota miti ya misunobari,

na badala ya michongoma

utaota mhadasi.55:13 Mhadasi ni aina ya mti ambao huota milimani karibu na Yerusalemu, hutoa harufu nzuri itumikayo kutengeneza manukato; kwa Kiebrania ni “hadas”, na ilikuwa inatumika kujenga vibanda wakati wa Sikukuu ya Vibanda (ona pia Neh 8:15).

Hili litakuwa jambo la kumpatia Bwana jina,

kwa ajili ya ishara ya milele,

ambayo haitaharibiwa.”

Read More of Isaya 55

Isaya 56:1-12

Wokovu Kwa Ajili Ya Wengine

56:1 Yer 22:3; Rum 13:11; Za 85:9; Dan 9:24; Yer 23:6; Isa 26:8Hili ndilo asemalo Bwana:

“Dumisheni haki

na mkatende lile lililo sawa,

kwa maana wokovu wangu u karibu

na haki yangu itafunuliwa upesi.

56:2 Kut 20:8-10; Isa 58:3; Za 119:2Amebarikiwa mtu yule atendaye hili,

mtu yule alishikaye kwa uthabiti,

yeye ashikaye Sabato bila kuinajisi,

auzuiaye mkono wake usifanye uovu wowote.”

56:3 Law 21:20; Mdo 8:27; Kut 12:43; 1Fal 8:41; Zek 8:20-23; Yer 38:7; Kum 23:3Usimwache mgeni aambatanaye na Bwana aseme,

“Hakika Bwana atanitenga na watu wake.”

Usimwache towashi yeyote alalamike akisema,

“Mimi ni mti mkavu tu.”

56:4 Yer 38:7; Kut 31:13Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa matowashi washikao Sabato zangu,

ambao huchagua kile kinachonipendeza

na kulishika sana agano langu:

56:5 1Tim 5:13; Isa 60:18; 48:19; 55:13; Ufu 3:12; Hes 32:42; 1Sam 15:12; Isa 47:3hao nitawapa ndani ya Hekalu langu na kuta zake

kumbukumbu na jina bora

kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike:

nitawapa jina lidumulo milele,

ambalo halitakatiliwa mbali.

56:6 1Nya 22:2; Isa 61:5; Kut 12:43; 1Fal 8:41; Isa 60:7-10Wageni wanaoambatana na Bwana

ili kumtumikia,

kulipenda jina la Bwana,

na kumwabudu yeye,

wote washikao Sabato bila kuinajisi

na ambao hushika sana agano langu:

56:7 Eze 20:40; Rum 12:1; Isa 19:21; Flp 4:18; Mt 21:13; Mk 11:17; Isa 19:21; Lk 19:46hawa nitawaleta kwenye mlima wangu mtakatifu

na kuwapa furaha ndani ya nyumba yangu ya sala.

Sadaka zao za kuteketeza na dhabihu zao

zitakubalika juu ya madhabahu yangu;

kwa maana nyumba yangu itaitwa

nyumba ya sala kwa mataifa yote.”

56:8 Eze 34:12; Yn 10:16; Efe 1:10; Kum 30:4; Isa 11:12; 60:3-11Bwana Mwenyezi asema, yeye awakusanyaye

Waisraeli waliohamishwa:

“Bado nitawakusanya wengine kwao

zaidi ya hao ambao wamekusanywa tayari.”

Mashtaka Ya Mungu Dhidi Ya Waovu

56:9 Yer 12:9; Eze 34:5-8; Isa 18:6; Eze 39:17-20Njooni, enyi wanyama wote wa kondeni,

njooni mle, ninyi wanyama wote wa mwituni!

56:10 Mt 15:14; Eze 3:17; Nah 3:18; Isa 52:8; 62:6; Yer 6:17; 31:6; 14:13-14Walinzi wa Israeli ni vipofu,

wote wamepungukiwa na maarifa;

wote ni mbwa walio bubu,

hawawezi kubweka;

hulala na kuota ndoto,

hupenda kulala.

56:11 Yer 23:1; 8:10; Eze 34:2; Mik 3:11; Isa 53:6; Hos 4:7-8; Isa 57:17Ni mbwa wenye tamaa kubwa,

kamwe hawatosheki.

Wao ni wachungaji waliopungukiwa na ufahamu;

wote wamegeukia njia yao wenyewe,

kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.

56:12 Za 10:6; Lk 12:18-19; Law 10:9; Mit 23:20; Isa 42:25Kila mmoja hulia, “Njooni, tupate mvinyo!

Tunywe kileo sana!

Kesho itakuwa kama leo,

au hata bora zaidi.”

Read More of Isaya 56

Isaya 57:1-13

Ibada Ya Sanamu Ya Israeli Iliyo Batili

57:1 Eze 21:3; 2Fal 22:20; Za 12:1; Isa 42:25Mwenye haki hupotea,

wala hakuna hata mmoja awazaye hilo moyoni mwake;

watu wanaomcha Mungu huondolewa,

wala hakuna hata mmoja anayeelewa

kuwa wenye haki wameondolewa

ili wasipatikane na maovu.

57:2 Isa 26:7; Kum 12:13Wale waendao kwa unyofu

huwa na amani;

hupata pumziko walalapo mautini.

57:3 Mal 3:5; Yak 4:4; Yer 2:20; Kut 22:18; Mt 16:4; Isa 1:20“Lakini ninyi:

Njooni hapa, ninyi wana wa wachawi,

ninyi wazao wa wazinzi na makahaba!

57:4 Isa 1:2Mnamdhihaki nani?

Ni nani mnayemcheka kwa dharau,

na kumtolea ndimi zenu?

Je, ninyi si watoto wa waasi,

uzao wa waongo?

57:5 Kum 12:2; 2Fal 16:4; Eze 16:20; Kum 18:10; Isa 1:29; Law 18:21; 18:2; Za 106:37-38Mnawaka tamaa katikati ya mialoni

na chini ya kila mti uliotanda matawi;

mnawatoa kafara watoto wenu kwenye mabonde

na chini ya majabali yenye mianya.

57:6 2Fal 17:10; Hab 2:19; Yer 44:18; 19:13; 7:18; 3:9; 7:18; 5:9-29; 9:9; 2:19“Sanamu zilizo katikati ya mawe laini ya mabondeni ndizo fungu lenu;

hizo ndizo sehemu yenu.

Naam, kwa hizo mmemimina sadaka za vinywaji,

na kutoa sadaka za nafaka.

Katika haya yote,

niendelee kuona huruma?

57:7 Yer 3:6; Eze 6:3; 23:41; 20:29; 20:27-28Umeweka kitanda chako juu kwenye kilima kirefu kilichoinuka,

huko ulikwenda kutoa dhabihu zako.

57:8 Eze 16:26; 23:7, 18; 23:18Nyuma ya milango yako na miimo yako

umeweka alama zako za kipagani.

Kwa kuniacha mimi, ulifunua kitanda chako,

umepanda juu yake na kukipanua sana;

ulifanya patano na wale ambao unapenda vitanda vyao,

nawe uliangalia uchi wao.

57:9 Law 18:21; 1Fal 11:5; Wim 4:10; Eze 23:16, 40Ulikwenda kwa Moleki57:9 Moleki alikuwa mungu aliyekuwa anaabudiwa na Waamoni; pia alijulikana kama Malkomu, Maloki au Kemoshi wa Moabu. ukiwa na mafuta ya zeituni,

na ukaongeza manukato yako.

Ukawatuma wajumbe wako mbali sana,

ukashuka kwenye kaburi57:9 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. lenyewe!

57:10 Yer 18:12; Mal 3:14; Isa 47:13; Yer 2:25; 1Sam 2:4Ulikuwa umechoshwa na njia zako zote,

lakini hukusema, ‘Hakuna tumaini.’

Ulipata uhuisho wa nguvu zako,

kwa sababu hiyo hukuzimia.

57:11 Mit 29:25; Eze 22:12; Yer 18:15; Es 4:14; Za 50:21; Yer 3:21; 1Fal 1:15; Isa 17:10“Ni nani uliyemhofu hivyo na kumwogopa

hata ukawa mwongo kwangu,

wala hukunikumbuka

au kutafakari hili moyoni mwako?

Si ni kwa sababu nimekuwa kimya muda mrefu

hata huniogopi?

57:12 Eze 16:2; Mik 2:2-8; Isa 29:15; 66:18Nitaifunua haki yako na matendo yako,

nayo hayatakufaidi.

57:13 Za 37:3-9; Yer 30:15; Isa 2:2-3; Yer 22:20; Amu 10:14; Za 118:8; Isa 65:9-11Utakapolia kwa kuhitaji msaada,

sanamu zako ulizojikusanyia na zikuokoe!

Upepo utazipeperusha zote,

pumzi peke yake itazipeperusha,

Lakini mtu atakayenifanya kimbilio lake,

atairithi nchi

na kuumiliki mlima wangu mtakatifu.”

Read More of Isaya 57