Isaya 51:17-23, Isaya 52:1-15, Isaya 53:1-12, Isaya 54:1-17 NEN

Isaya 51:17-23

Kikombe Cha Ghadhabu Ya Bwana

51:17 Amu 5:12; Ay 21:20; Ufu 16:19; Za 60:3; 16:5; Mt 20:22; Isa 42:25Amka, amka!

Simama, ee Yerusalemu,

wewe uliyekunywa kutoka mkono wa Bwana

kikombe cha ghadhabu yake,

wewe uliyekunywa mpaka kufikia machujo yake,

kikombe kile cha kunywea

kiwafanyacho watu kuyumbayumba.

51:18 Ay 31:18; Za 88:18; Isa 49:21; 41:13Kati ya wana wote aliowazaa

hakuwepo hata mmoja wa kumwongoza,

kati ya wana wote aliowalea

hakuwepo hata mmoja wa kumshika mkono.

51:19 Isa 40:2; 47:9; 49:13; Yer 14:12; 24:10Majanga haya mawili yamekuja juu yako:

ni nani awezaye kukufariji?

Maangamizi, uharibifu, njaa na upanga:

ni nani awezaye kukutuliza?

51:20 Yer 14:16; Mao 2:19; Isa 5:25; Ay 18:10; Yer 44:6; Ay 40:11; Kum 28:20Wana wako wamezimia,

wamelala kwenye mwanzo wa kila barabara,

kama swala aliyenaswa kwenye wavu.

Wamejazwa na ghadhabu ya Bwana

na makaripio ya Mungu wako.

51:21 Isa 14:32; 29:9; Mao 3:15Kwa hiyo sikiliza hili, wewe uliyeteswa,

uliyelewa, lakini si kwa mvinyo.

51:22 Yer 50:34; Hab 2:16; Isa 49:25; Yer 25:15; Mt 20:2251:22 Yer 50:34; Hab 2:16; Isa 49:25; Yer 25:15; Mt 20:22Hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi wako,

Mungu wako, yeye ambaye huwatetea watu wake:

“Tazama, nimeondoa mkononi mwako

kikombe kilichokufanya uyumbayumbe;

kutoka kikombe hicho,

kikombe cha kunywa cha ghadhabu yangu,

kamwe hutakunywa tena.

51:23 Yer 49:12; Zek 12:3; Yos 10:24; Isa 14:4; 49:26; Yer 25:15-17, 26; Mik 7:1051:23 Yer 49:12; Zek 12:3; Yos 10:24; Isa 14:4; 49:26; Yer 25:15-17, 26; Mik 7:10Nitakiweka mikononi mwa watesi wako,

wale waliokuambia,

‘Anguka kifudifudi

ili tuweze kutembea juu yako.’

Ukaufanya mgongo wako kama ardhi,

kama njia yao ya kupita.”

Read More of Isaya 51

Isaya 52:1-15

52:1 Isa 51:9; Es 6:8; Ufu 21:2; Yoe 3:17; Zek 3:4; Isa 49:18; Kut 28:2, 40; Neh 1:1Amka, amka, ee Sayuni,

jivike nguvu.

Vaa mavazi yako ya fahari,

ee Yerusalemu, mji mtakatifu.

Asiyetahiriwa na aliye najisi

hataingia kwako tena.

52:2 Zek 2:7; Isa 29:4; 10:27; Za 81:9; 9:14Jikungʼute mavumbi yako,

inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, ee Yerusalemu.

Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako,

ee Binti Sayuni uliye mateka.

52:3 Za 44:12; Isa 45:13; 1:27; 1Pet 1:18Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:

“Mliuzwa pasipo malipo,

nanyi mtakombolewa bila fedha.”

52:4 Mwa 46:6; Isa 10:24Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:

“Hapo kwanza watu wangu walishuka Misri kuishi,

hatimaye, Ashuru wakawaonea.

52:5 Eze 36:20; Rum 2:24; Isa 37:23“Basi sasa nina nini hapa?” asema Bwana.

“Kwa kuwa watu wangu wamechukuliwa pasipo malipo,

nao wale wanaowatawala wanawadhihaki,”

asema Bwana.

“Mchana kutwa

jina langu limetukanwa bila kikomo.

52:6 Isa 49:23; Kut 6:3; Isa 41:26; 10:20Kwa hiyo watu wangu watalijua Jina langu;

kwa hiyo katika siku ile watajua

kwamba ndimi niliyetangulia kulisema.

Naam, ni mimi.”

52:7 2Sam 18:26; Rum 10:15; 1Kor 15:24-25; Lk 2:14; Isa 42:11; 40:9; Efe 6:15Tazama jinsi miguu ya wale waletao habari njema

ilivyo mizuri juu ya milima,

wale wanaotangaza amani,

wanaoleta habari njema,

wanaotangaza wokovu,

wauambiao Sayuni,

“Mungu wako anatawala!”

52:8 Sef 3:9; Eze 3:17; 1Sam 14:16; Isa 56:10; Yer 6:17; Hes 10:36; Zek 8:3Sikiliza! Walinzi wako wanapaza sauti zao,

pamoja wanapaza sauti zao kwa furaha.

Wakati Bwana atakaporejea Sayuni,

wataliona kwa macho yao wenyewe.

52:9 Za 98:4; Isa 35:2; Za 74:3; Isa 48:20; Ezr 9:9; Lk 2:25; Isa 51:3Pazeni sauti ya nyimbo za furaha pamoja,

enyi magofu ya Yerusalemu,

kwa maana Bwana amewafariji watu wake,

ameikomboa Yerusalemu.

52:10 Lk 2:30; Za 67:2; Isa 66:18; 2Nya 32:8; Za 44:3; Isa 30:30; Yos 4:24Mkono mtakatifu wa Bwana umefunuliwa

machoni pa mataifa yote,

nayo miisho yote ya dunia itaona

wokovu wa Mungu wetu.

52:11 Yer 50:8; 2Kor 6:17; Hes 8:6; 2Tim 2:9; Isa 1:16; 2Nya 36:10; Isa 48:20Ondokeni, ondokeni, tokeni huko!

Msiguse kitu chochote kilicho najisi!

Tokeni kati yake mwe safi,

ninyi mchukuao vyombo vya Bwana.

52:12 Kut 14:19; 12:11; Mik 2:13; Yn 10:4Lakini hamtaondoka kwa haraka,

wala hamtakwenda kwa kukimbia;

kwa maana Bwana atatangulia mbele yenu,

Mungu wa Israeli atakuwa mlinzi nyuma yenu.

Mateso Na Utukufu Wa Mtumishi

52:13 Isa 53:3; Mdo 3:13; Yos 1:8; Isa 20:3; 57:15; Flp 2:9Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa hekima;

atatukuzwa, na kuinuliwa juu, na kukwezwa sana.

52:14 Law 26:32; Ay 2:12; 16:16; 18:20; 2Sam 10:4Kama walivyokuwa wengi

walioshangazwa naye,

kwani uso wake ulikuwa umeharibiwa sana

zaidi ya mtu yeyote

na umbo lake kuharibiwa

zaidi ya mfano wa mwanadamu:

52:15 Ebr 9:13; Rum 15:21; Efe 3:4-5; Za 107:42; Amu 18:19; Law 14:7; 16:14-15hivyo atayashangaza mataifa mengi,

nao wafalme watafunga vinywa vyao kwa sababu yake.

Kwa kuwa yale ambayo hawakuambiwa, watayaona,

nayo yale wasiyoyasikia, watayafahamu.

Read More of Isaya 52

Isaya 53:1-12

53:1 Isa 28:9; Yn 12:38; Rum 10:16; Za 98:1; Isa 30:30Ni nani aliyeamini ujumbe wetu,

na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani?

53:2 Mk 9:12; Isa 52:14; 2Fal 19:26; Ay 14:7; Isa 4:2; 11:10Alikua mbele yake kama mche mwororo

na kama mzizi katika nchi kavu.

Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvutia kwake,

hakuwa na chochote katika sura yake cha kutufanya tumtamani.

53:3 Ebr 4:15; Mt 16:21; 27:29; 1Sam 2:30; Za 69:29; Kut 1:10; Lk 18:31-33Alidharauliwa na kukataliwa na wanadamu,

mtu wa huzuni nyingi, ajuaye mateso.

Kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,

alidharauliwa, wala hatukumhesabu kuwa kitu.

53:4 Mt 8:17; Zek 13:7; Yn 19:7; Kum 5:24; Ay 4:5; Yer 23:5-6; Eze 34:23-24; Mik 5:2Hakika alichukua udhaifu wetu

na akajitwika huzuni zetu,

hata hivyo tulidhania kuwa amepigwa na Mungu,

akapigwa sana naye, na kuteswa.

53:5 Kum 32:39; Yn 3:17; 1Pet 2:24-25; 2Nya 7:14; Rum 4:25; 1Kor 15:3; Ebr 9:8; Kut 28:38Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu,

alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu;

adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake,

na kwa majeraha yake sisi tumepona.

53:6 Za 119:176; 1Pet 2:25Sisi sote, kama kondoo, tumepotea,

kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe,

naye Bwana aliweka juu yake

maovu yetu sisi sote.

53:7 Mdo 8:32; Mk 14:61; 1Pet 2:23; Isa 49:26; Mt 27:31; Yn 1:29; Za 44:22Alionewa na kuteswa,

hata hivyo hakufungua kinywa chake;

aliongozwa kama mwana-kondoo

apelekwaye machinjoni,

kama vile kondoo anyamazavyo mbele ya wao wamkataye manyoya,

hivyo hakufungua kinywa chake.

53:8 Za 88:5; Dan 9:26; Mdo 8:32-33; Za 39:8; Mk 14:49Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa.

Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake?

Kwa maana alikatiliwa mbali na nchi ya walio hai,

alipigwa kwa ajili ya makosa ya watu wangu.

53:9 Mk 15:43-46; Lk 23:50-53; Isa 42:1-3; Ay 16:17; Ufu 14:5; Yn 19:19, 38-41Wakamfanyia kaburi pamoja na waovu,

pamoja na matajiri katika kifo chake,

ingawa hakutenda jeuri,

wala hapakuwa na hila kinywani mwake.

53:10 2Kor 5:21; Mwa 12:17; Za 22:30; Mdo 2:23; Isa 46:10; Law 5:15; Yn 3:17Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Bwana

kumchubua na kumsababisha ateseke.

Ingawa Bwana amefanya maisha yake

kuwa sadaka ya hatia,

ataona uzao wake na kuishi siku nyingi,

nayo mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake.

53:11 Yn 10:14-18; Rum 5:18-19; Ay 33:30; Isa 20:3; Mdo 7:52; Yn 1:29; Rum 4:24; Mdo 10:43Baada ya maumivu ya nafsi yake,

ataona nuru ya uzima na kuridhika;

kwa maarifa yake, mtumishi wangu mwenye haki

atawafanya wengi kuwa wenye haki,

naye atayachukua maovu yao.

53:12 Flp 2:9; Mt 26:28, 38; 27:38; Lk 23:34; Kut 15:9; Za 119:162; Ebr 9:28; Isa 59:19; Rum 8:34; Mk 15:27; Lk 22:37Kwa hiyo nitamgawia sehemu miongoni mwa wakuu,

naye atagawana nyara pamoja na wenye nguvu,

kwa sababu aliyamimina maisha yake hadi mauti,

naye alihesabiwa pamoja na wakosaji.

Kwa kuwa alichukua dhambi za wengi,

na kuwaombea wakosaji.

Read More of Isaya 53

Isaya 54:1-17

Utukufu Wa Baadaye Wa Sayuni

54:1 Isa 49:20; Gal 4:27; Mwa 21:6; Za 98:4; Isa 66:7; 49:20“Imba, ewe mwanamke tasa,

wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto;

paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha,

wewe ambaye kamwe hukupata utungu;

kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi

kuliko wa mwanamke mwenye mume,”

asema Bwana.

54:2 Mwa 26:22; Isa 26:15; Kut 35:18; 39:40; Isa 49:19-20“Panua mahali pa hema lako,

tandaza mapazia ya hema lako uyaeneze mbali,

wala usiyazuie;

ongeza urefu wa kamba zako,

imarisha vigingi vyako.

54:3 Mwa 13:14; Isa 48:19; Ay 12:23; Isa 14:2; 60:4-11; 49:19Kwa maana utaenea upande wa kuume

na upande wa kushoto;

wazao wako watayamiliki mataifa

na kukaa katika miji yao iliyoachwa ukiwa.

54:4 Isa 30:10; Yoe 2:21; Isa 28:16; Mwa 30:23; Za 25:7; 119:39; Yer 22:21; Isa 47:8“Usiogope, wewe hutaaibika.

Usiogope aibu, wewe hutaaibishwa.

Wewe utasahau aibu ya ujana wako,

wala hutakumbuka tena mashutumu ya ujane wako.

54:5 Wim 3:3; Isa 41:14; 48:17; Rum 3:29; Hos 2:7-16; Za 149:2; Isa 51:13Kwa maana Muumba wako ndiye mume wako,

Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ni Mkombozi wako,

yeye anaitwa Mungu wa dunia yote.

54:6 Isa 49:14-21; 60:15; 62:4; Yer 44:2; Hos 1:10; Kut 20:14; Mal 2:14Bwana atakuita urudi

kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni;

kama mke aliyeolewa bado angali kijana

na kukataliwa,” asema Mungu wako.

54:7 Ay 14:13; Isa 26:20; 2Kor 4:17; Isa 27:8; Za 71:11; Isa 49:18“Kwa kitambo kidogo nilikuacha,

lakini kwa huruma nyingi nitakurudisha.

54:8 Isa 9:12; Yer 31:3; Za 92:2; Isa 26:20; Za 25:6; Isa 55:3; 63:7; Hos 2:19Katika ukali wa hasira

nilikuficha uso wangu kwa kitambo,

lakini kwa fadhili za milele

nitakuwa na huruma juu yako,”

asema Bwana Mkombozi wako.

54:9 Mwa 8:21; Mik 7:18; Eze 39:29; Isa 14:24; Kum 28:20; Isa 49:18“Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Noa,

nilipoapa kuwa maji ya Noa kamwe hayatafunika tena dunia.

Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi,

kamwe sitawakemea tena.

54:10 Za 46:2; Ebr 12:27; Mwa 9:16; Kut 34:10; Ufu 6:14; Hes 25:12; Isa 55:7Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe,

hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika,

wala agano langu la amani halitaondolewa,”

asema Bwana, mwenye huruma juu yenu.

54:11 Isa 14:32; 29:6; 1Nya 29:2; Ufu 21:18; 21:19-20; Isa 26:18; 28:16; Kut 24:10“Ewe mji uliyeteswa, uliyepigwa kwa dhoruba na usiyetulizwa,

nitakujenga kwa almasi, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi.

54:12 Ufu 21:21Nitafanya minara yako ya akiki,

malango yako kwa vito vingʼaavyo,

nazo kuta zako zote za vito vya thamani.

54:13 Mik 4:2; Ebr 8:11; Law 26:6; Isa 11:9; 28:9; 48:18; Yn 6:45Watoto wako wote watafundishwa na Bwana,

nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu.

54:14 2Sam 7:10; Isa 9:4; 17:14; 26:2; Yer 30:20; Sef 3:17; Zek 9:8Kwa haki utathibitika:

Kuonewa kutakuwa mbali nawe;

hutaogopa chochote.

Hofu itakuwa mbali nawe;

haitakukaribia wewe.

54:15 Isa 41:11-16Kama mtu yeyote akikushambulia,

haitakuwa kwa ruhusa yangu;

yeyote akushambuliaye

atajisalimisha kwako.

54:16 Isa 44:12; 10:5; 13:5“Tazama, ni mimi niliyemuumba mhunzi,

yeye afukutaye makaa kuwa moto,

na kutengeneza silaha inayofaa kwa kazi yake.

Tena ni mimi niliyemwambia mharabu

kufanya uharibifu mwingi.

54:17 Isa 29:8; Mdo 6:10; Isa 45:24-25; 41:11; 56:6-8; Zek 1:20-21; Isa 65:8-9Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako

itakayofanikiwa,

nawe utauthibitisha kuwa mwongo

kila ulimi utakaokushtaki.

Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana

na hii ndiyo haki yao itokayo kwangu,”

asema Bwana.

Read More of Isaya 54