Isaya 49:8-26, Isaya 50:1-11, Isaya 51:1-16 NEN

Isaya 49:8-26

Kurejezwa Kwa Israeli

49:8 Za 69:13; 2Kor 6:2; Law 25:10; Za 37:9; Isa 60:10; 41:10; 26:3; 5:249:8 Isa 44:28; Neh 2:17Hili ndilo asemalo Bwana:

“Wakati wangu uliokubalika nitakujibu,

nami katika siku ya wokovu nitakusaidia;

nitakuhifadhi, nami nitakufanya

kuwa agano kwa ajili ya watu,

ili kurudisha nchi

na kugawanyia urithi tena wale waliokuwa ukiwa,

49:9 Lk 4:19; Isa 41:18; Zek 9:12; Isa 42:7; Za 107:10kuwaambia mateka, ‘Tokeni nje,’

nao wale walio gizani, ‘Kuweni huru!’

“Watajilisha kando ya barabara

na kupata malisho yao juu ya kila kilima kilicho kitupu.

49:10 Isa 33:16; Ufu 7:16; Isa 35:7; Za 21:6; Isa 42:16; 33:21Hawataona njaa wala kuona kiu,

wala hari ya jangwani au jua halitawapiga.

Yeye mwenye huruma juu yao atawaonyesha njia,

na kuwaongoza kando ya chemchemi za maji.

49:11 Isa 11:6; Yer 31:9; Isa 40:4Nitaifanya milima yangu yote kuwa barabara,

na njia kuu zangu zitainuliwa.

49:12 Isa 2:3; 43:5-6; 59:19; Mt 8:11Tazama, watakuja kutoka mbali:

wengine kutoka kaskazini, wengine kutoka magharibi,

wengine kutoka nchi ya Sinimu.”49:12 Sinimu hapa ina maana ya Aswani.

49:13 Za 98:4; 71:21; 2Kor 1:4; Isa 48:20; Za 96:11; 65:12-13; 9:12Pigeni kelele kwa furaha, enyi mbingu;

furahi, ee dunia;

pazeni sauti kwa kuimba, enyi milima!

Kwa maana Bwana anawafariji watu wake,

naye atakuwa na huruma kwa watu wake walioumizwa.

49:14 Isa 40:9; Za 9:10; Isa 27:8; Za 71:11Lakini Sayuni alisema, “Bwana ameniacha,

Bwana amenisahau.”

49:15 Mt 7:11; Isa 44:21; 1Fal 3:26; Isa 66:13“Je, mama aweza kumsahau mtoto

aliyeko matitini mwake akinyonya,

wala asiwe na huruma

juu ya mtoto aliyemzaa?

Ingawa anaweza kusahau,

mimi sitakusahau wewe!

49:16 Wim 8:6; Kut 28:9; Za 48:12-13; Isa 62:6; Mwa 38:18Tazama, nimekuchora kama muhuri

katika vitanga vya mikono yangu,

kuta zako zi mbele yangu daima.

49:17 Isa 49:19Wana wako wanaharakisha kurudi,

nao wale waliokuteka wanaondoka kwako.

49:18 Mit 17:6; Rum 14:11; Hes 14:21; Yer 2:32; Isa 11:12; 43:5; 54:9; 45:23Inua macho yako ukatazame pande zote:

wana wako wote wanakusanyika na kukujia.

Kwa hakika kama vile niishivyo,

utawavaa wote kama mapambo,

na kujifunga nao kama bibi arusi,”

asema Bwana.

49:19 Law 26:33; Isa 62:4; Zek 10:10; Eze 36:10-11; Zek 2:4; Isa 60:18; 1:20“Ingawa uliangamizwa na kufanywa ukiwa,

na nchi yako ikaharibiwa,

sasa nafasi itakuwa finyu kwa ajili ya watu wako,

nao wale waliokuangamiza watakuwa mbali sana.

49:20 Mt 3:9; Rum 11:11, 12Watoto waliozaliwa wakati wa msiba wako

bado watakuambia,

‘Mahali hapa ni finyu sana kwetu,

tupe eneo kubwa zaidi la kuishi.’

49:21 Isa 5:13; Lk 15:5; Isa 60:4; 29:23; 66:7-8; 47:8; Yer 10:20; Mwa 15:2Ndipo utasema moyoni mwako,

‘Ni nani aliyenizalia hawa?

Nilikuwa nimefiwa, tena tasa;

nilikuwa nimehamishwa na kukataliwa.

Ni nani aliyewalea hawa?

Niliachwa peke yangu,

lakini hawa wametoka wapi?’ ”

49:22 Isa 60:10-11; Hes 11:12; Mwa 3:14; Za 72:9; Kut 6:2; Mik 7:17; Mwa 3:14Hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:

“Tazama, nitawaashiria watu wa Mataifa,

nitainua bendera yangu kwa mataifa;

watawaleta wana wako mikononi yao,

na kuwabeba binti zenu juu ya mabega yao.

Wafalme watakuwa baba zenu wa kuwalea,

na malkia wao watakuwa mama zenu wa kuwalea.

Watasujudu mbele yako nyuso zao zikigusa ardhi;

wataramba mavumbi yaliyo miguuni mwako.

Ndipo utajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana;

wale wanaonitumaini mimi hawataaibika.”

49:24 Mt 12:29; Mk 3:27; Lk 11:21Je, nyara zaweza kuchukuliwa kutoka kwa mashujaa wa vita,

au mateka kuokolewa kutoka kwa watu wakali?

49:25 Yer 50:33-34; Isa 14:2; 25:9; Mk 3:27; Isa 13:11; 25:4-9; 1Sam 24:15Lakini hili ndilo asemalo Bwana:

“Naam, mateka watachukuliwa kutoka kwa mashujaa,

na nyara zitapokonywa kutoka kwa watu wakali.

Nitashindana na wale wanaoshindana nawe,

nami nitawaokoa watoto wako.

49:26 Isa 9:4, 20; Nah 1:10; Ufu 16:6; Eze 39:7; Hes 23:24; Yer 25:27; Isa 11:9; Ay 19:25; Isa 48:17; Mwa 49:24; Za 132:2Nitawafanya wale wanaokuonea kula nyama yao wenyewe,

watalewa kwa damu yao wenyewe,

kama vile kwa mvinyo.

Ndipo wanadamu wote watajua

ya kuwa Mimi, Bwana, ni Mwokozi wako,

Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.”

Read More of Isaya 49

Isaya 50:1-11

Dhambi Ya Israeli Na Utii Wa Mtumishi

50:1 Kum 24:1; Mk 10:4; Mt 18:25; Amu 3:8; Hos 2:2; Mt 19:7; Neh 5:5; Isa 1:25Hili ndilo asemalo Bwana:

“Iko wapi hati ya talaka ya mama yako

ambayo kwayo niliachana naye?

Au nimewauza ninyi kwa nani

miongoni mwa watu wanaonidai?

Kwa ajili ya dhambi zenu mliuzwa,

kwa sababu ya makosa, mama yenu aliachwa.

50:2 Mwa 18:14; Kut 14:22; Hes 11:23; 1Sam 8:19; Isa 41:28; Za 68:35; Yer 14:9Nilipokuja, kwa nini hakuwepo hata mmoja?

Nilipoita, kwa nini hakuwepo hata mmoja wa kujibu?

Je, mkono wangu ni mfupi mno hata nisiweze kuwakomboa?

Je, mimi sina nguvu za kukuokoa?

Kwa kukemea tu naikausha bahari,

naigeuza mito ya maji kuwa jangwa;

samaki wake wanaoza kwa kukosa maji

na kufa kwa ajili ya kiu.

50:3 Isa 5:30; Ufu 6:12; Kut 10:21Ninalivika anga weusi na kufanya nguo ya gunia

kuwa kifuniko chake.”

50:4 Kut 4:11-12; Za 88:13; Mt 7:29; Isa 40:29; Mt 11:28Bwana Mwenyezi amenipa ulimi uliofundishwa,

ili kujua neno limtegemezalo aliyechoka.

Huniamsha asubuhi kwa asubuhi,

huamsha sikio langu lisikie kama mtu afundishwaye.

50:5 Isa 35:5; Eze 2:8; Ebr 10:5; Isa 48:16; Eze 24:3; Mdo 26:19; Mt 26:39Bwana Mwenyezi amezibua masikio yangu,

nami sikuwa mwasi,

wala sikurudi nyuma.

50:6 Mt 27:30; Isa 53:5; Mao 3:30; Hes 12:14; Mt 26:67; Mk 14:65Niliwapa mgongo wangu wale wanipigao,

mashavu yangu wale wangʼoao ndevu zangu;

sikuuficha uso wangu kutokana na fedheha

na kutemewa mate.

50:7 Isa 41:10; Rum 8:31; Eze 3:8-9; Isa 48:16; 28:16; 29:22Kwa sababu Bwana Mwenyezi ananisaidia,

sitatahayarika.

Kwa hiyo nimekaza uso wangu kama jiwe la gumegume,

nami ninajua sitaaibika.

50:8 Ay 13:19; Rum 8:32-34; 1Kor 4:4; Isa 26:2; 49:4Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu.

Ni nani basi atakayeleta mashtaka dhidi yangu?

Tukabiliane uso kwa uso!

Mshtaki wangu ni nani?

Ni nani aliye mshtaki wangu?

50:9 Ay 13:28; Isa 41:10; Ebr 1:11-12; Rum 8:1, 34; Isa 51:8Ni Bwana Mwenyezi anisaidiaye mimi.

Ni nani huyo atakayenihukumu?

Wote watachakaa kama vazi,

nondo watawala wawamalize.

50:10 2Nya 20:20; Isa 49:3; 26:4; 1:19; Hag 1:12; Mdo 26:18; Isa 10:20Ni nani miongoni mwenu amchaye Bwana,

na kulitii neno la mtumishi wake?

Yeye atembeaye gizani,

yeye asiye na nuru,

na alitumainie jina la Bwana,

na amtegemee Mungu wake.

50:11 Mit 26:18; Yak 3:6; Ay 15:20; Isa 65:13-15; Kum 21:22-23Lakini sasa, ninyi nyote mnaowasha mioto,

na kupeana mienge iwakayo ninyi kwa ninyi,

nendeni, tembeeni katika nuru ya moto wenu

na ya mienge mliyoiwasha.

Hili ndilo mtakalolipokea kutoka mkononi mwangu:

Mtalala chini kwa mateso makali.

Read More of Isaya 50

Isaya 51:1-16

Wokovu Wa Milele Kwa Sayuni

51:1 Isa 46:3; Kum 7:13; Mit 26:27; Kum 16:20; Za 94:15; Isa 63:8; Rum 9:30-31; Isa 17:10“Nisikilizeni, ninyi mnaofuatia haki

na mnaomtafuta Bwana:

Tazameni mwamba ambako mlichongwa,

na mahali pa kuvunjia mawe ambako mlichimbwa;

51:2 Mwa 17:6; Ebr 11:11; Mwa 12:2; Isa 29:22; Rum 4:16mwangalieni Abrahamu, baba yenu,

na Sara, ambaye aliwazaa.

Wakati nilipomwita alikuwa mmoja tu,

nami nikambariki na kumfanya kuwa wengi.

51:3 Isa 40:1; Mwa 13:10; Yer 16:9; Za 102:13; Isa 44:26; Za 51:18; Isa 61:4Hakika Bwana ataifariji Sayuni,

naye atayaangalia kwa huruma magofu yake yote;

atayafanya majangwa yake yawe kama Edeni,

nazo sehemu zake zisizolimika ziwe kama bustani ya Bwana.

Shangwe na furaha zitakuwako ndani yake,

shukrani na sauti za kuimba.

51:4 Kut 6:7; Isa 26:18; 42:4-6; Za 50:7; Isa 3:15; 63:8“Nisikilizeni, watu wangu;

nisikieni, taifa langu:

Sheria itatoka kwangu;

haki yangu itakuwa nuru kwa mataifa.

51:5 Isa 35:4; 46:13; Za 98:1; 85:9; Mwa 49:10; Isa 52:10Haki yangu inakaribia mbio,

wokovu wangu unakuja,

nao mkono wangu utaleta hukumu kwa mataifa.

Visiwa vitanitegemea

na kungojea mkono wangu kwa matumaini.

51:6 Za 37:20; Lk 21:33; Za 102:25-26; Ebr 1:10-12; Mt 24:35; Isa 54:10Inueni macho yenu mbinguni,

mkaitazame dunia chini;

mbingu zitatoweka kama moshi,

dunia itachakaa kama vazi,

na wakazi wake kufa kama mainzi.

Bali wokovu wangu utadumu milele,

haki yangu haitakoma kamwe.

51:7 Za 37:31; Mt 10:28; Mdo 5:41; Za 119:39; Lk 6:22; Isa 54:4; 50:7“Nisikieni, ninyi mnaojua lililo sawa,

ninyi watu ambao mna sheria yangu mioyoni mwenu:

Msiogope mashutumu ya wanadamu

wala msitiwe hofu na matukano yao.

51:8 Ay 13:28; Yak 5:2; Isa 14:11Kwa maana nondo atawala kama vazi,

nao funza atawatafuna kama sufu.

Lakini haki yangu itadumu milele,

wokovu wangu kwa vizazi vyote.”

51:9 Kut 32:7; Za 68:30; Ay 26:12; Eze 29:3; Amu 5:12; Mwa 18:14; Za 65:6; 74:13Amka, Amka! Jivike nguvu,

ewe mkono wa Bwana,

Amka, kama siku zilizopita,

kama vile vizazi vya zamani.

Si ni wewe uliyemkata Rahabu vipande vipande,

uliyemchoma yule joka?

51:10 Zek 10:11; Kut 14:21; Ufu 16:12; Kut 15:5, 8, 13; Ay 36:30Si ni wewe uliyekausha bahari,

maji ya kilindi kikuu,

uliyefanya barabara katika vilindi vya bahari

ili waliokombolewa wapate kuvuka?

51:11 Isa 35:9; 44:23; 48:20; Ufu 7:17; Yer 31:13; 30:19; Sef 3:17; Isa 30:19Wale waliolipiwa fidia na Bwana watarudi.

Wataingia Sayuni wakiimba;

furaha ya milele itakuwa taji juu ya vichwa vyao.

Furaha na shangwe zitawapata,

huzuni na kulia kwa uchungu kutatoweka.

51:12 Za 118:6; 2Kor 1:3-4; 1Pet 1:24; Isa 15:6; 2Fal 1:15; Isa 2:22; 40:6-7“Mimi, naam mimi,

ndimi niwafarijie ninyi.

Ninyi ni nani hata kuwaogopa

wanadamu wanaokufa,

wanadamu ambao ni majani tu,

51:13 Ay 8:13; 4:17; Isa 17:10; 7:4; Ay 20:7; Isa 45:11; 48:13; 9:4kwamba mnamsahau Bwana Muumba wenu,

aliyezitanda mbingu

na kuiweka misingi ya dunia,

kwamba mnaishi katika hofu siku zote

kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu,

ambaye nia yake ni kuangamiza?

Iko wapi basi ghadhabu ya mdhalimu?

51:14 Isa 49:10; Zek 9:11; Isa 42:7Wafungwa waliojikunyata kwa hofu

watawekwa huru karibuni;

hawatafia kwenye gereza lao,

wala hawatakosa chakula.

51:15 Kut 14:21; Isa 43:16; Za 74:13; Yer 31:35; Za 93:3; Isa 13:4Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,

ambaye huisukasuka bahari ili mawimbi yake yangurume:

Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.

51:16 Kut 4:12-15; 2Pet 3:13; Kum 18:18; 33:22; Zek 8:8; Eze 14:11; Yer 7:23; 24:7Nimeweka maneno yangu kinywani mwako

na kukufunika kwa uvuli wa mkono wangu:

Mimi niliyeweka mbingu mahali pake,

niliyeweka misingi ya dunia,

niwaambiaye Sayuni,

‘Ninyi ni watu wangu.’ ”

Read More of Isaya 51