Isaya 47:1-15, Isaya 48:1-22, Isaya 49:1-7 NEN

Isaya 47:1-15

Anguko La Babeli

47:1 Mao 2:10; Isa 21:9; 23:12; Yer 51:33; Zek 2:7; Ay 2:13; Isa 29:4“Shuka uketi mavumbini,

ee Bikira Binti Babeli;

keti chini pasipo na kiti cha enzi,

ee binti wa Wakaldayo.

Hutaitwa tena mwororo wala wa kupendeza.

47:2 Mt 24:41; Kut 11:5; Amu 16:21; Mwa 24:65; Isa 32:11Chukua mawe ya kusagia, usage unga,

vua shela yako.

Pandisha mavazi yako, ondoa viatu vyako,

vuka vijito kwa shida.

47:3 Mwa 2:25; Rum 12:19; Neh 3:5; Isa 13:18-19; 20:4; 34:8; Eze 16:37Uchi wako utafunuliwa

na aibu yako itaonekana.

Nitalipa kisasi;

sitamhurumia hata mmoja.”

47:4 Yer 50:34; Amo 4:13; Isa 48:2, 17; Ay 19:25Mkombozi wetu: Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake;

ndiye yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

47:5 Dan 2:37; Isa 13:10, 19; 9:2; 21:9; Ufu 17:18; Ay 2:13; Ufu 18:7“Keti kimya, ingia gizani,

Binti wa Wakaldayo,

hutaitwa tena malkia wa falme.

47:6 2Nya 28:9; Isa 10:13; Zek 1:15; Kum 13:15; Yer 50:11; Isa 14:6; 42:24Niliwakasirikia watu wangu

na kuaibisha urithi wangu;

niliwatia mikononi mwako,

nawe hukuwaonea huruma.

Hata juu ya wazee

uliweka nira nzito sana.

47:7 Ufu 18:7; Kum 32:29; Isa 10:13; Dan 4:30; Isa 42:23-25Ukasema, ‘Nitaendelea

kuwa malkia milele!’

Lakini hukutafakari mambo haya

wala hukuwaza juu ya kile kingeweza kutokea.

47:8 Isa 32:9; 45:6; 49:21; 54:4; Sef 2:15; Ufu 18:7“Sasa basi, sikiliza, ewe kiumbe mpenda anasa,

ukaaye mahali pako pa salama,

na kujiambia mwenyewe,

‘Mimi ndiye, wala hakuna mwingine zaidi yangu.

Kamwe sitakuwa mjane,

wala sitafiwa na watoto.’

47:9 1The 5:3; Isa 13:8; Nah 3:4; Za 55:15; Mal 3:5; Kum 18:10-11; Ufu 9:21; 18:8-10Haya mawili yatakupata, kufumba na kufumbua,

katika siku moja:

kufiwa na watoto, na ujane.

Yote yatakupata kwa kipimo kikamilifu,

ijapokuwa uchawi wako ni mwingi,

na uaguzi wako ni mwingi.

47:10 Ay 15:31; 2Fal 21:16; Isa 5:21; 29:15; Za 52:7; 62:10Umeutegemea uovu wako,

nawe umesema, ‘Hakuna yeyote anionaye.’

Hekima yako na maarifa yako vinakupoteza

unapojiambia mwenyewe,

‘Mimi ndiye, wala hakuna mwingine zaidi yangu.’

47:11 Dan 5:30; Za 55:15; 1The 5:3; Isa 10:3; 14:15; 21:9; Lk 17:27; Isa 17:14Maafa yatakujia,

nawe hutaweza kuyaondoa kwa uaguzi.

Janga litakuangukia,

wala hutaweza kulikinga kwa fidia;

msiba mkuu usioweza kuutabiri

utakujia ghafula.

47:12 Kut 7:11“Endelea basi na uaguzi wako,

na wingi wa uchawi wako,

ambao umeutumikia tangu utoto wako.

Labda utafanikiwa,

labda unaweza ukasababisha hofu kuu.

47:13 Yer 51:58; Hab 2:13; Isa 19:3; 5:29; 43:13; 57:10; 46:7; Dan 2:2Ushauri wote uliopokea umekuchosha bure!

Wanajimu wako na waje mbele,

wale watazama nyota watabiriao mwezi baada ya mwezi,

wao na wawaokoe na lile linalokuja juu yenu.

47:14 Isa 5:24; Nah 1:10; Yer 50:30-32; Isa 30:30; 10:17Hakika wako kama mabua makavu;

moto utawateketeza.

Hawawezi hata kujiokoa wao wenyewe

kutokana na nguvu za mwali wa moto.

Hapa hakuna makaa ya kumtia mtu yeyote joto;

hapa hakuna moto wa kuota.

47:15 Ufu 18:11; Isa 44:17Hayo ndiyo yote wanayoweza kuwatendea ninyi,

hawa ambao umetaabika nao

na kufanya nao biashara tangu utoto.

Kila mmoja atatoroka;

hakuna yeyote awezaye kukuokoa.

Read More of Isaya 47

Isaya 48:1-22

Israeli Mkaidi

48:1 Kum 6:13; Kut 23:13; Dan 8:12; Zek 8:3; Mwa 17:5; 29:35; Isa 19:18“Sikilizeni hili, ee nyumba ya Yakobo,

ninyi mnaoitwa kwa jina la Israeli,

na mnaotoka katika ukoo wa Yuda,

ninyi mnaoapa kwa jina la Bwana,

mnaomwomba Mungu wa Israeli,

lakini si katika kweli au kwa haki;

48:2 Neh 11:1; Rum 2:17; Mik 3:11; Isa 1:26; Mt 4:5; Isa 10:20; 47:4ninyi mnaojiita raiya wa mji mtakatifu,

na kumtegemea Mungu wa Israeli,

Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake:

48:3 Isa 40:21; 45:21; Yos 21:45; Isa 41:22; 17:14; 30:13Nilitoa unabii mambo ya kwanza tangu zamani,

kinywa changu kiliyatangaza na kuyafanya yajulikane;

kisha ghafula nikayatenda, nayo yakatokea.

48:4 Kum 9:27; 31:27; Mdo 5:21; Isa 9:9; Kut 32:9; Eze 3:9; Mdo 7:51Kwa kuwa nalijua jinsi ulivyokuwa mkaidi;

mishipa ya shingo yako ilikuwa chuma,

kipaji chako cha uso kilikuwa shaba.

48:5 Yer 44:15-18; Isa 42:9; 40:21Kwa hiyo nilikuambia mambo haya tangu zamani,

kabla hayajatokea nilikutangazia

ili usije ukasema,

‘Sanamu zangu zilifanya hayo;

kinyago changu cha mti na mungu wangu wa chuma aliyaamuru.’

48:6 Isa 41:22; Rum 16:25Umesikia mambo haya; yaangalie hayo yote.

Je, hutayakubali?

“Kuanzia sasa na kuendelea nitakueleza mambo mapya,

juu ya mambo yaliyofichika usiyoyajua.

48:7 Isa 65:18; 45:21; Kut 6:7Yameumbwa sasa, wala si tangu zamani;

hukupata kuyasikia kabla ya siku ya leo.

Hivyo huwezi kusema,

‘Naam, niliyajua hayo.’

48:8 Za 58:3; Kum 9:24; Isa 41:24; Mal 2:11-14; Isa 43:27Hujayasikia wala kuyaelewa,

tangu zamani sikio lako halikufunguka.

Ninafahamu vyema jinsi ulivyo mdanganyifu,

uliitwa mwasi tangu kuzaliwa kwako.

48:9 Yos 7:9; Ay 9:13; Za 78:38; 1Sam 12:22; Isa 37:35; 30:18Kwa ajili ya Jina langu mwenyewe

ninaichelewesha ghadhabu yangu,

kwa ajili ya sifa zangu nimeizuia isikupate,

ili nisije nikakukatilia mbali.

48:10 Za 66:10Tazama, nimekusafisha, ingawa si kama fedha,

nimekujaribu katika tanuru ya mateso.

48:11 1Sam 12:22; Law 18:21; Isa 42:8; Kum 32:26-27; Eze 20:9; Yer 14:7, 21Kwa ajili yangu mwenyewe,

kwa ajili yangu mwenyewe, nafanya hili.

Jinsi gani niliache Jina langu lichafuliwe?

Sitautoa utukufu wangu kwa mwingine.

Israeli Anawekwa Huru

48:12 Isa 46:3; 41:4; Ufu 22:13; Isa 43:13; 42:6“Ee Yakobo, nisikilize mimi,

Israeli, ambaye nimekuita:

Mimi ndiye;

mimi ndimi mwanzo na mwisho.

48:13 Ebr 1:10-12; Ay 9:8; Isa 34:16; 40:26; Kut 20:11; Isa 45:18Mkono wangu mwenyewe uliweka misingi ya dunia,

nao mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu;

niziitapo, zote husimama pamoja.

48:14 Isa 43:9; 46:10-11; 41:2, 22; Yer 50:45; Isa 21:9“Kusanyikeni, ninyi nyote, msikilize:

Ni ipi miongoni mwa hizo sanamu

ambayo imetabiri vitu hivi?

Watu wa Bwana waliochaguliwa na kuungana

watatimiza kusudi lake dhidi ya Babeli;

mkono wa Mungu utakuwa dhidi ya Wakaldayo.

48:15 Amu 4:10; Isa 45:1Mimi, naam, Mimi, nimenena;

naam, nimemwita yeye.

Nitamleta,

naye atafanikiwa katika lile nililomtuma.

48:16 Isa 45:19; Zek 2:8-11; Isa 33:13; 50:5-9; 11:2“Nikaribieni na msikilize hili:

“Tangu tangazo la kwanza sikusema kwa siri;

wakati litokeapo, nitakuwako hapo.”

Sasa Bwana Mwenyezi amenituma,

kwa Roho wake.

48:17 Ay 19:25; Za 32:4; Isa 54:8; 47:4; 28:9; Yer 7:13; Isa 49:10Hili ndilo asemalo Bwana,

Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:

“Mimi ni Bwana, Mungu wako,

nikufundishaye ili upate faida,

nikuongozaye katika njia ikupasayo kuiendea.

48:18 Kum 5:29; Isa 42:23; Za 147:14; 45:8; Isa 54:13; 33:21; 45:5Laiti ungesikiliza kwa makini maagizo yangu,

amani yako ingekuwa kama mto,

haki yako kama mawimbi ya bahari.

48:19 Mwa 22:17; Ay 5:25; Yer 35:19; Isa 43:5; 61:9; Mwa 12:2; Isa 56:5Wazao wako wangekuwa kama mchanga,

watoto wako kama chembe zake zisizohesabika;

kamwe jina lao lisingefutiliwa mbali,

wala kuangamizwa kutoka mbele zangu.”

48:20 Zek 2:6-7; Ufu 18:4; Isa 12:6; Mik 4:10; Isa 52:11; Yer 48:6; 50:8Tokeni huko Babeli,

kimbieni kutoka kwa Wakaldayo!

Tangazeni hili kwa kelele za shangwe

na kulihubiri.

Lipelekeni mpaka miisho ya dunia;

semeni, “Bwana amemkomboa

mtumishi wake Yakobo.”

48:21 Isa 41:17; 33:16; 30:25; Kut 17:6; Za 105:41; Hes 20:11Hawakuona kiu alipowaongoza kupita jangwani;

alifanya maji yatiririke kutoka kwenye mwamba kwa ajili yao;

akapasua mwamba

na maji yakatoka kwa nguvu.

48:22 Isa 3:11; 57:21; Ay 3:26“Hakuna amani kwa waovu,” asema Bwana.

Read More of Isaya 48

Isaya 49:1-7

Mtumishi Wa Bwana

49:1 Isa 44:24; Yer 1:5; Lk 1:15; Isa 33:13; 11:11; Mt 1:20; Isa 7:14; 9:6; Kut 33:12Nisikilizeni, enyi visiwa, sikieni hili,

ninyi mataifa mlio mbali:

Kabla sijazaliwa, Bwana aliniita,

tangu kuzaliwa kwangu, amelitaja jina langu.

49:2 Za 64:3; Hos 6:5; Efe 6:17; Ay 40:18; Ufu 1:16; Kut 33:22; Zek 9:13Akafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa,

katika uvuli wa mkono wake akanificha;

akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa,

na kunificha katika podo lake.

49:3 Isa 20:3; Zek 3:8; Law 10:3; Isa 44:23Akaniambia, “Wewe u mtumishi wangu,

Israeli, ambaye katika yeye

nitaonyesha utukufu wangu.”

49:4 Eze 3:19; Law 26:20; Isa 35:4; Ay 27:2; Isa 55:2; 65:23; 45:25; 54:17Lakini nilisema, “Nimetumika bure,

nimetumia nguvu zangu bure bila faida.

Hata hivyo linalonistahili liko mkononi mwa Bwana,

nao ujira wangu uko kwa Mungu wangu.”

49:5 Kum 30:4; Isa 11:12; 43:4; Za 139:13; Gal 1:15; Za 18:1Sasa Bwana asema:

yeye aliyeniumba tumboni kuwa mtumishi wake,

kumrudisha tena Yakobo kwake

na kumkusanyia Israeli,

kwa maana nimepata heshima machoni pa Bwana,

naye Mungu wangu amekuwa nguvu yangu;

49:6 Zek 8:22; Lk 2:32; Yn 11:52; Isa 9:2; Yon 1:9; Isa 26:18; Kum 30:4; Mdo 13:47yeye asema:

“Je, ni jambo dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu

ili kurejeza makabila ya Yakobo,

na kuwarudisha wale Waisraeli niliowahifadhi?

Pia nitakufanya uwe nuru kwa ajili ya watu wa Mataifa,

ili upate kuleta wokovu wangu hata miisho ya dunia.”

49:7 Isa 48:17; Za 69:7-9; Isa 52:15; Mwa 27:29; Za 22:6, 29; 86:9; Kum 7:9Hili ndilo asemalo Bwana,

yeye Mkombozi na Aliye Mtakatifu wa Israeli,

kwake yeye aliyedharauliwa na kuchukiwa na taifa,

kwa mtumishi wa watawala:

“Wafalme watakuona na kusimama,

wakuu wataona na kuanguka kifudifudi,

kwa sababu ya Bwana, aliye mwaminifu,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, aliyekuchagua wewe.”

Read More of Isaya 49