Isaya 44:24-28, Isaya 45:1-25, Isaya 46:1-13 NEN

Isaya 44:24-28

Yerusalemu Kukaliwa

44:24 Ay 19:25; Isa 43:15; 42:5; Za 139:13“Hili ndilo asemalo Bwana,

Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni:

“Mimi ni Bwana,

niliyeumba vitu vyote,

niliyezitanda mbingu peke yangu,

niliyeitandaza nchi mwenyewe,

44:25 Law 19:26; Ay 5:13; 2Sam 15:31; 1Kor 1:19-20, 27; Za 33:10; 1Sam 6:2; Isa 47:13“mimi huzipinga ishara za manabii wa uongo,

na kuwatia upumbavu waaguzi,

niyapinduaye maarifa ya wenye hekima,

na kuyafanya kuwa upuzi,

44:26 Zek 1:6; Isa 59:21; Mt 5:18; Ezr 9:9; Isa 46:10; Yer 23:20; 39:16niyathibitishaye maneno ya watumishi wake,

na kutimiza utabiri wa wajumbe wake,

“niambiaye Yerusalemu, ‘Itakaliwa na watu,’

niambiaye miji ya Yuda kuwa, ‘Itajengwa,’

na kuhusu magofu yake, ‘Mimi nitayatengeneza,’

44:27 Isa 11:15; 19:5; Ufu 16:12niambiaye kilindi cha maji, ‘Kauka,

nami nitakausha vijito vyako,’

44:28 2Nya 36:22-23; Ezr 1:2-4; Isa 14:32; 41:2; 28:16; 58:12nisemaye kuhusu Koreshi, ‘Yeye ni mchungaji wangu,

naye atatimiza yote yanipendezayo;

atauambia Yerusalemu, “Ukajengwe tena,”

na kuhusu Hekalu, “Misingi yake na iwekwe.” ’

Read More of Isaya 44

Isaya 45:1-25

Koreshi Chombo Cha Mungu

45:1 Za 73:23; Mik 4:13; Yer 50:20, 35; 51:20; Isa 48:14; 41:13; Za 45:7“Hili ndilo asemalo Bwana kwa mpakwa mafuta wake,

Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume

kutiisha mataifa mbele yake

na kuwavua wafalme silaha zao,

kufungua milango mbele yake

ili malango yasije yakafungwa:

45:2 Isa 40:4; Mao 2:9; Nah 3:13; Kut 23:20; Isa 13:2; Za 107:16; Yer 51:30Nitakwenda mbele yako

na kusawazisha milima;

nitavunjavunja malango ya shaba

na kukatakata mapingo ya chuma.

45:3 Kut 33:12; Isa 41:23; Yer 41:8; 2Fal 24:13; Yer 50:37; 51:13Nitakupa hazina za gizani,

mali zilizofichwa mahali pa siri,

ili upate kujua ya kwamba Mimi ndimi Bwana,

Mungu wa Israeli, akuitaye kwa jina lako.

45:4 Mdo 17:23; Isa 41:8-9; 14:1Kwa ajili ya Yakobo mtumishi wangu,

Israeli niliyemchagua,

nimekuita wewe kwa jina lako,

na kukupa jina la heshima,

ingawa wewe hunitambui.

45:5 Kum 32:12; Za 18:31, 39; Eze 30:24-25; Isa 44:8; 43:10Mimi ndimi Bwana, wala hakuna mwingine,

zaidi yangu hakuna Mungu.

Nitakutia nguvu,

ingawa wewe hujanitambua,

45:6 Za 113:3; Mal 1:11; Isa 14:13-14; Sef 2:15; Isa 43:5; 11:9ili kutoka mawio ya jua

mpaka machweo yake,

watu wapate kujua kwamba hakuna Mungu mwingine ila Mimi.

Mimi ndimi Bwana wala hakuna mwingine.

45:7 Mao 3:38; Amo 3:6; Kut 10:22; Isa 14:15; 31:2Mimi ninaumba nuru na kuhuluku giza,

ninaleta mafanikio na kusababisha maafa.

Mimi, Bwana, huyatenda haya yote.

45:8 Yoe 3:18; Hos 12:10; Mal 4:2; Za 85:9; 72:6; Isa 41:2; 46:13; Amu 5:24; Isa 60:21“Enyi mbingu juu, nyesheni haki,

mawingu na yaidondoshe.

Dunia na ifunguke sana,

wokovu na uchipuke,

haki na ikue pamoja nao.

Mimi, Bwana, ndiye niliyeiumba.

45:9 Ay 27:2; Yer 18:16; 1Kor 10:22; Rum 9:20-21; Ay 12:13; 15:25; 33:13; 9:12“Ole wake yeye ashindanaye na Muumba wake,

yeye ambaye ni kigae tu kati ya vigae juu ya ardhi.

Je, udongo wa kufinyangia humwambia mfinyanzi,

‘Unatengeneza nini wewe?’

Je, kazi yako husema,

‘Hana mikono’?

Ole wake amwambiaye baba yake,

‘Umezaa nini?’

Au kumwambia mama yake,

‘Umezaa kitu gani?’

45:11 Yer 31:9; Za 8:6; Isa 19:25; Za 149:2; Isa 51:13“Hili ndilo asemalo Bwana,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli na Muumba wake:

Kuhusu mambo yatakayokuja,

je, unaniuliza habari za watoto wangu,

au kunipa amri kuhusu kazi za mikono yangu?

45:12 Isa 42:5; Yer 27:5; Neh 9:6; Ay 38:32; Isa 48:13Mimi ndiye niliyeumba dunia

na kumuumba mwanadamu juu yake.

Mikono yangu mwenyewe ndiyo iliyozitanda mbingu,

nikayapanga majeshi yake yote ya angani.

45:13 Rum 3:24; Isa 52:3; 2Nya 36:22; Isa 41:2; 1Fal 8:36; Za 26:12Mimi nitamwinua Koreshi katika haki yangu:

nitazinyoosha njia zake zote.

Yeye atajenga mji wangu upya,

na kuwaweka huru watu wangu walio uhamishoni,

lakini si kwa kulipiwa fedha wala kupewa zawadi,

asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.”

45:14 2Sam 3:34; Isa 14:2; Zek 8:20-23; 2Sam 8:2; Isa 18:7; Mwa 27:29; Yer 16:19; 1Kor 14:25; Isa 43:10Hili ndilo asemalo Bwana:

“Mazao ya Misri na bidhaa za Kushi,

nao wale Waseba warefu,

watakujia na kuwa wako,

watakujia wakijikokota nyuma yako,

watakujia wamefungwa minyororo.

Watasujudu mbele yako

wakikusihi na kusema,

‘Hakika Mungu yu pamoja nawe,

wala hakuna mwingine;

hakuna Mungu mwingine.’ ”

45:15 Kum 31:17; Isa 8:17; Za 44:24; Isa 25:9; 1:15Hakika wewe u Mungu unayejificha,

Ee Mungu na Mwokozi wa Israeli.

45:16 Za 35:4; Isa 1:29Wote watengenezao sanamu wataaibika na kutahayarika;

wataenda kutahayarika pamoja.

45:17 Yer 23:6; Rum 11:26; Isa 26:4; Yer 33:16; Isa 12:2; Mwa 30:23; Isa 29:22Lakini Israeli ataokolewa na Bwana

kwa wokovu wa milele;

kamwe hutaaibika wala kutatahayarika,

milele yote.

45:18 Mwa 1:2, 26; Isa 42:5; Kum 4:25Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana,

yeye aliyeumba mbingu,

ndiye Mungu;

yeye aliyeifanya dunia na kuiumba,

yeye ndiye aliiwekea misingi imara,

hakuiumba ili iwe tupu,

bali aliiumba ikaliwe na viumbe vyake.

Anasema:

“Mimi ndimi Bwana,

wala hakuna mwingine.

45:19 Neh 9:13; Isa 48:16; 65:4, 9; Yer 31:36; Kum 30:11; Yer 2:31; Kum 4:49Sijasema sirini,

kutoka mahali fulani katika nchi ya giza;

sijawaambia wazao wa Yakobo,

‘Nitafuteni bure.’

Mimi, Bwana, nasema kweli;

ninatangaza lililo sahihi.

45:20 Yer 2:28; Isa 43:9; 44:19; Rum 1:22; Kum 32:37; Yer 10:5; Za 115:7“Kusanyikeni pamoja mje,

enyi wakimbizi kutoka mataifa.

Wale wabebao sanamu za mti ni watu wasio na akili,

wale waombao miungu isiyoweza kuokoa.

45:21 Za 46:10; Mk 12:32; Isa 41:22; 46:10; 25:9; Za 11:7Tangazeni litakalokuwepo, lisemeni hilo,

wao na wafanye shauri pamoja.

Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani,

aliyetangaza tangu zamani za kale?

Je, haikuwa Mimi, Bwana?

Wala hapana Mungu mwingine

zaidi yangu mimi,

Mungu mwenye haki na Mwokozi;

hapana mwingine ila mimi.

45:22 Zek 12:10; Hes 21:8-9; Mwa 49:10; Isa 11:9-12; 44:22; 2Nya 20:12“Nigeukieni mimi, nanyi mkaokolewe,

enyi miisho yote ya dunia;

kwa maana mimi ndimi Mungu,

wala hapana mwingine.

45:23 Mwa 22:16; Ebr 6:13; Flp 2:10-11; Isa 14:24; Za 63:11; Kum 6:13Nimeapa kwa nafsi yangu,

kinywa changu kimenena katika uadilifu wote

neno ambalo halitatanguka:

Kila goti litapigwa mbele zangu,

kwangu mimi kila ulimi utaapa.

45:24 Yer 33:16; Isa 41:11; Kum 33:29; Isa 40:26Watasema kuhusu mimi,

‘Katika Bwana peke yake

ndiko kuna haki na nguvu.’ ”

Wote ambao wamemkasirikia Mungu

watamjia yeye, nao watatahayarika.

45:25 Isa 24:23; 41:16; 49:4Lakini katika Bwana wazao wote wa Israeli

wataonekana wenye haki na watashangilia.

Read More of Isaya 45

Isaya 46:1-13

Miungu Ya Babeli

46:1 Yer 51:44; Isa 45:20; 21:9; Yer 50:2Beli anasujudu hadi nchi, Nebo anainama;

sanamu zao zabebwa na wanyama wa mizigo.

Vinyago hivi mnavyobeba kila mahali ni mzigo wa kulemea,

mzigo kwa waliochoka.

46:2 2Sam 5:21; Yer 51:47; Amu 18:17-18Vinyago pamoja na wale wanaovibeba wanainama chini;

hiyo miungu haiwezi kuwaokoa watu,

wote wanakwenda utumwani pamoja.

46:3 Isa 48:12; Kut 19:14; Isa 44:2; Kum 1:31; Za 28:9; 22:10“Nisikilizeni mimi, ee nyumba ya Yakobo,

ninyi nyote mliobaki wa nyumba ya Israeli,

ninyi ambao nimewategemeza tangu mlipotungwa mimba,

nami nimewabeba tangu kuzaliwa kwenu.

46:4 Mal 3:6; Za 71:18; Isa 43:13; Kum 32:39; Za 18:35; 119:117Hata mpaka wakati wa uzee wenu na mvi, Mimi ndiye,

Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi.

Nimewahuluku, nami nitawabeba,

nitawasaidia ninyi na kuwaokoa.

46:5 Kut 15:11; Ay 41:10; Isa 40:18, 25; Yer 49:19“Mtanilinganisha na nani, au mtanihesabu kuwa sawa na nani?

Ni nani mtakayenifananisha naye ili tuweze kulinganishwa?

46:6 Kut 20:5; Hos 13:2; Isa 40:19; 44:17Wengine humwaga dhahabu kutoka kwenye mifuko yao,

na kupima fedha kwenye mizani;

huajiri mfua dhahabu kutengeneza mungu,

kisha huisujudia na kuiabudu.

46:7 1Sam 5:3; Isa 41:7; 1Fal 16:26Huiinua mabegani na kuichukua;

huiweka mahali pake, papo hapo ndipo isimamapo.

Wala haiwezi kusogea kutoka mahali pale.

Ingawa mtu huililia, haimjibu;

haiwezi kumwokoa kwenye taabu zake.

46:8 Isa 44:21; 1:2“Kumbukeni hili, litieni akilini,

liwekeni moyoni, enyi waasi.

46:9 Kum 8:10; Kut 8:10; Mk 12:32; Isa 41:22; 45:21Kumbukeni mambo yaliyopita, yale ya zamani za kale;

mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine;

mimi ndimi Mungu,

wala hakuna mwingine aliye kama mimi.

46:10 Mit 19:21; Efe 1:11; Mdo 5:39; Isa 45:21; 41:22; 7:7-9; 44:26Ni mimi nitangazaye mwisho tangu mwanzo,

naam, tangu zamani za kale,

mambo ambayo hayajatendeka.

Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama,

nami nitatenda mapenzi yangu yote.

46:11 Mwa 41:25; Yer 44:28; Amu 4:10; Ezr 1:2; Isa 8:5Kutoka mashariki ninaita ndege awindaye;

kutoka nchi ya mbali,

mtu atakayetimiza kusudi langu.

Lile ambalo nimelisema, ndilo nitakalolitimiza;

lile nililolipanga, ndilo nitakalolitenda.

46:12 Yer 2:5; Za 119:150; Rum 10:3; Kut 32:9; Isa 9:9Nisikilizeni, ninyi wenye mioyo migumu,

ninyi mlio mbali na haki.

46:13 Isa 24:23; Mdo 13:36; Rum 1:17; Isa 1:26; 45:8; Rum 3:21; Yoe 2:32Ninaleta haki yangu karibu,

haiko mbali;

wala wokovu wangu hautachelewa.

Nitawapa Sayuni wokovu,

Israeli utukufu wangu.

Read More of Isaya 46