Isaya 41:1-29, Isaya 42:1-25 NEN

Isaya 41:1-29

Msaidizi Wa Israeli

41:1 Za 37:7; Isa 48:16; 50:8; Hab 2:20; Zek 2:13; Isa 11:11; 1Sam 2:4“Nyamazeni kimya mbele zangu, enyi visiwa!

Mataifa na wafanye upya nguvu zao!

Wao na wajitokeze, kisha waseme,

tukutane pamoja mahali pa hukumu.

41:2 2Sam 22:43; Isa 40:24; Yer 51:11; Ezr 1:2; Isa 44:28; Yer 50:3; 25:9“Ni nani aliyemchochea mmoja kutoka mashariki,

akimwita katika haki kwa utumishi wake?

Huyatia mataifa mikononi mwake,

na kuwatiisha wafalme mbele zake.

Huwafanya kuwa mavumbi kwa upanga wake,

huwafanya makapi yapeperushwayo na upepo kwa upinde wake.

41:3 Dan 8:4Huwafuatia na kuendelea salama,

katika njia ambayo miguu yake haijawahi kupita.

41:4 Isa 48:12; Ufu 22:13; Mdo 15:18; Isa 43:7; Kum 32:29Ni nani aliyefanya jambo hili na kulitimiliza,

akiita vizazi tangu mwanzo?

Mimi, Bwana, ni wa kwanza

nami nitakuwa pamoja na wa mwisho:

mimi Bwana ndiye.”

41:5 Eze 26:17-18; Kum 30:4; Isa 11:11-12Visiwa vimeliona na kuogopa,

miisho ya dunia inatetemeka.

Wanakaribia na kuja mbele,

41:6 Isa 1:6kila mmoja humsaidia mwingine

na kusema kwa ndugu yake, “Uwe hodari!”

41:7 Isa 40:19; 44:13; Yer 30:3-5Fundi humtia moyo sonara,

yeye alainishaye kwa nyundo

humhimiza yeye agongeaye kwenye fuawe,

Humwambia yeye aunganishaye, “Ni kazi njema.”

Naye huikaza sanamu kwa misumari ili isitikisike.

41:8 Mwa 18:19; Isa 29:22; Neh 9:7; 2Nya 20:7; Yak 2:23; Isa 63:16; Za 136:22“Lakini wewe, ee Israeli, mtumishi wangu,

Yakobo, niliyemchagua,

ninyi wazao wa Abrahamu rafiki yangu,

41:9 Isa 37:16; Kum 7:6; Isa 20:3; 11:12nilikuchukua toka miisho ya dunia,

nilikuita kutoka pembe zake za mbali.

Nilisema, ‘Wewe ni mtumishi wangu’;

nimekuchagua, wala sikukukataa.

41:10 Kum 3:22; Rum 8:3; Isa 49:8; Yer 30:10; 46:27-28; Ay 40:14; Za 18:35Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;

usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.

Nitakutia nguvu na kukusaidia;

nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

41:11 Isa 17:12; 54:17; Kut 23:22; Isa 29:8; Zek 12:3; Yer 2:3; Isa 29:23“Wote walioona hasira dhidi yako

hakika wataaibika na kutahayarika,

wale wakupingao

watakuwa kama vile si kitu, na kuangamia.

41:12 Za 37:35-36; Isa 34:12; Ay 7:8; Isa 29:20; 17:14Ingawa utawatafuta adui zako,

hutawaona.

Wale wanaopigana vita dhidi yako

watakuwa kama vile si kitu kabisa.

41:13 Za 73:23; Isa 42:6; 45:1; 51:18Kwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,

nikushikaye mkono wako wa kuume

na kukuambia, Usiwe na hofu,

nitakusaidia.

41:14 Ay 4:19; Za 22:6; Kut 15:13; Ay 19:23; Isa 1:27Usiogope, ee Yakobo uliye mdudu,

ee Israeli uliye mdogo,

kwa kuwa Mimi mwenyewe nitakusaidia,” asema Bwana,

Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

41:15 Ay 41:30; Mik 4:13; Isa 21:10; Kut 19:18; Yer 9:10; Eze 33:28“Tazama, nitakufanya chombo cha kupuria,

kipya na chenye makali, chenye meno mengi.

Utaipura milima na kuiponda

na kuvifanya vilima kuwa kama makapi.

41:16 Yer 51:2; Isa 45:25; 60:19; Dan 2:35; Yer 15:7; Isa 25:9; Mk 1:24Utaipepeta, nao upepo utaichukua,

dhoruba itaipeperushia mbali.

Bali wewe utajifurahisha katika Bwana

na katika utukufu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

41:17 Isa 43:20; 35:7; 30:19“Maskini na wahitaji wanatafuta maji,

lakini hayapo,

ndimi zao zimekauka kwa kiu.

Lakini Mimi Bwana nitawajibu,

Mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.

41:18 Isa 30:25; 43:19; Ay 38:26; Isa 35:7; 2Fal 3:17Nitaifanya mito itiririke juu ya vilima vilivyo kame,

nazo chemchemi ndani ya mabonde.

Nitaligeuza jangwa liwe mabwawa ya maji,

nayo ardhi iliyokauka kuwa chemchemi za maji.

41:19 Isa 60:13; Kut 25:10-13; Isa 37:24; 44:14Katika jangwa nitaotesha

mwerezi, mshita, mhadasi na mzeituni.

Nitaweka misunobari, mivinje na misanduku

pamoja huko nyikani,

41:20 Ay 12:9; Isa 4:5ili kwamba watu wapate kuona na kujua,

wapate kufikiri na kuelewa,

kwamba mkono wa Bwana umetenda hili,

kwamba yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ndiye alilifanya.”

41:21 Isa 43:14; 44:6Bwana asema, “Leta shauri lako.

Toa hoja yako,” asema Mfalme wa Yakobo.

41:22 Isa 48:14; 65:17; Yn 13:19; Isa 43:9; 45:21“Leteni sanamu zenu zituambie

ni nini kitakachotokea.

Tuambieni mambo ya zamani yalikuwa nini,

ili tupate kuyatafakari

na kujua matokeo yake ya mwisho.

Au tutangazieni mambo yatakayokuja,

41:23 Kum 18:22; Isa 44:7-8; Yer 10:5; Isa 43:5; 2Fal 19:26tuambieni ni nini kitakachotokea baadaye,

ili tupate kujua kuwa ninyi ni miungu.

Fanyeni jambo lolote zuri au baya,

ili tupate kutishika na kujazwa na hofu.

41:24 Isa 37:19; 1Kor 8:4; Za 115:8; 1Sam 12:21; Isa 48:8Lakini ninyi ni zaidi ya bure kabisa,

na kazi zenu hazifai kitu kabisa;

yeye awachaguaye ni chukizo sana.

41:25 Yer 51:48; Nah 3:14; 2Sam 22:43; Yer 50:9“Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini,

naye yuaja, mmoja toka mawio ya jua aliitaye Jina langu.

Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope,

kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia.

41:26 Hab 2:18-19; 1Fal 18:26; Isa 52:6Ni nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua,

au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa sawa’?

Hakuna aliyenena hili,

hakuna aliyetangulia kusema hili,

hakuna yeyote aliyesikia maneno kutoka kwenu.

41:27 Isa 48:3, 16; 40:9Nilikuwa wa kwanza kumwambia Sayuni,

‘Tazama, wako hapa!’

Nilimpa Yerusalemu mjumbe wa habari njema.

41:28 Eze 22:30; Za 22:11; Isa 40:13-14; 50:2; 59:16; 64:7; Yer 25:4Ninatazama, lakini hakuna yeyote:

hakuna yeyote miongoni mwao awezaye kutoa shauri,

hakuna yeyote wa kutoa jibu wakati ninapowauliza.

41:29 Yer 5:13; 1Sam 12:21; Isa 37:19Tazama, wote ni ubatili!

Matendo yao ni bure;

vinyago vyao ni upepo mtupu na machafuko.

Read More of Isaya 41

Isaya 42:1-25

Mtumishi Wa Bwana

42:1 Isa 49:3-6; 14:1; Yn 3:34; Lk 9:35; Mwa 49:10; Mt 3:16-17; 20:28“Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza,

mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye;

nitaweka Roho yangu juu yake,

naye ataleta haki kwa mataifa.

42:2 Za 8:1-4Hatapaza sauti wala kupiga kelele,

wala hataiinua sauti yake barabarani.

42:3 Za 72:2; Mt 12:17-21; Za 96:13; Isa 36:6; Ay 30:24; 13:25Mwanzi uliopondeka hatauvunja,

na utambi unaofuka moshi hatauzima.

Kwa uaminifu ataleta haki,

42:4 Mwa 49:10; Ebr 12:2; Rum 8:22-25; Kut 34:29; Isa 51:4; 11:11hatazimia roho wala kukata tamaa,

mpaka atakaposimamisha haki juu ya dunia.

Visiwa vitaweka tumaini lao katika sheria yake.”

42:5 Za 24:2; Mdo 17:24-25; Isa 44:24; 48:13; Za 102:25Hili ndilo asemalo Mungu, Bwana,

yeye aliyeziumba mbingu na kuzitanda,

aliyeitandaza dunia na vyote vitokavyo humo,

awapaye watu wake pumzi,

na uzima kwa wale waendao humo:

42:6 Kut 31:2; Amu 4:10; Yer 23:6; Mdo 13:47; Dan 9:7; Isa 26:18; Lk 22:20“Mimi, Bwana, nimekuita katika haki;

nitakushika mkono wako.

Nitakulinda na kukufanya

kuwa Agano kwa ajili ya watu

na nuru kwa Mataifa,

42:7 Zek 9:11; 2:7; 2Tim 2:26; Lk 4:19; Mt 11:5; Isa 32:3; 51:14; Za 146:8kuwafungua macho wale wasioona,

kuwaacha huru kutoka kifungoni waliofungwa jela,

na kuwafungua kutoka gerezani

wale wanaokaa gizani.

42:8 Kut 3:14-15; 6:3; Isa 48:11; Za 81:10; Ebr 2:14-15; Kut 8:10; Isa 46:9“Mimi ndimi Bwana; hilo ndilo Jina langu!

Sitampa mwingine utukufu wangu

wala sanamu sifa zangu.

42:9 Isa 41:22; 40:21; Eze 2:4Tazama, mambo ya kwanza yametokea,

nami natangaza mambo mapya;

kabla hayajatokea

nawatangazia habari zake.”

Wimbo Wa Kumsifu Bwana

42:10 Za 98:1; Kum 30:4; Za 96:11; 1Fal 10:9; 1Nya 16:32; Za 48:10; Isa 11:11Mwimbieni Bwana wimbo mpya,

sifa zake toka miisho ya dunia,

ninyi mshukao chini baharini,

na vyote vilivyomo ndani yake,

enyi visiwa na wote wakaao ndani yake.

42:11 Mwa 25:13; Isa 32:16; 52:7; Nah 1:15; Isa 60:7; Amu 1:36Jangwa na miji yake na vipaze sauti zao;

makao anamoishi Kedari na yashangilie.

Watu wa Sela waimbe kwa furaha,

na wapige kelele kutoka vilele vya milima.

42:12 Isa 24:15; 1Nya 16:24; 1Pet 2:9; Za 26:7; 66:2Wampe Bwana utukufu,

na kutangaza sifa zake katika visiwa.

42:13 Isa 9:6; Yos 6:5; Yoe 3:16; Isa 66:14; 26:11; Kut 14:14; Hos 11:10Bwana ataenda kama mtu mwenye nguvu,

kama shujaa atachochea shauku yake,

kwa kelele ataamsha kilio cha vita,

naye atashinda adui zake.

42:14 Es 4:14; Yer 4:31; Mwa 43:31; Lk 18:7“Kwa muda mrefu nimenyamaza kimya,

nimekaa kimya na kujizuia.

Lakini sasa, kama mwanamke wakati wa kujifungua,

ninapiga kelele, ninatweta na kushusha pumzi.

42:15 Eze 38:20; Za 107:33; Isa 11:15; 50:2; Nah 1:4-6Nitaharibu milima na vilima

na kukausha mimea yako yote;

nitafanya mito kuwa visiwa

na kukausha mabwawa.

42:16 Kum 4:31; Ebr 13:5; Yer 31:8-9; Isa 26:7; 29:24; 57:18; Mdo 26:18; Ebr 13:5Nitawaongoza vipofu kwenye njia ambayo hawajaijua,

kwenye mapito wasiyoyazoea nitawaongoza;

nitafanya giza kuwa nuru mbele yao,

na kufanya mahali palipoparuza kuwa laini.

Haya ndiyo mambo nitakayofanya;

mimi sitawaacha.

42:17 Kut 32:4; Za 97:7; Isa 1:26Lakini wale wanaotumaini sanamu,

wanaoviambia vinyago, ‘Ninyi ndio miungu yetu,’

watarudishwa nyuma kwa aibu kubwa.

Israeli Kipofu Na Kiziwi

“Sikieni, enyi viziwi;

tazameni, enyi vipofu, mpate kuona!

42:19 Isa 43:8; Eze 12:2; Isa 41:8-9; Hag 1:13; Isa 26:3Ni nani aliye kipofu isipokuwa mtumishi wangu,

na kiziwi kama mjumbe ninayemtuma?

Ni nani aliye kipofu kama yeye aliyejitoa kwangu,

aliye kipofu kama mtumishi wa Bwana?

42:20 Isa 6:9-10; Yer 5:21; Rum 2:21; Yer 6:10; Isa 48:21; 41:17Mmeona vitu vingi, lakini hamkuzingatia;

masikio yenu yako wazi, lakini hamsikii chochote.”

42:21 2Kor 3:7; Isa 43:25Ilimpendeza Bwana

kwa ajili ya haki yake

kufanya sheria yake kuwa kuu na tukufu.

42:22 Isa 24:18-22; Lk 19:41-44; Amu 6:4; 2Fal 24:13; Isa 5:29; Za 66:11; Yos 22:5; Isa 1:14; 30:11Lakini hili ni taifa lililoibwa na kutekwa nyara,

wote wamenaswa katika mashimo,

au wamefichwa katika magereza.

Wamekuwa nyara,

wala hapana yeyote awaokoaye.

Wamefanywa mateka,

wala hapana yeyote asemaye, “Warudishe.”

42:23 Kum 32:29; Za 81:13; Isa 47:7; 48:18; 57:11Ni nani miongoni mwenu atakayesikiliza hili,

au atakayezingatia kwa makini katika wakati ujao?

42:24 2Fal 17:6; Isa 43:28; 10:5-6Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka,

na Israeli kwa wateka nyara?

Je, hakuwa yeye, Bwana,

ambaye tumetenda dhambi dhidi yake?

Kwa kuwa hawakufuata njia zake,

hawakutii sheria zake.

42:25 Hos 7:9; Nah 1:6; 2Fal 22:13; Ay 40:11; Eze 7:19; 2Fal 25:9; Isa 29:13Hivyo akawamwagia hasira yake inayowaka,

ukali wa vita.

Iliwazunguka kwa miali ya moto, lakini hata hivyo hawakuelewa;

iliwateketeza, lakini hawakuyatia moyoni.

Read More of Isaya 42