Isaya 33:1-24, Isaya 34:1-17, Isaya 35:1-10 NEN

Isaya 33:1-24

Taabu Na Msaada

33:1 Hab 2:8; Yer 30:16; Eze 39:10; 2Fal 19:21; Isa 31:8; 21:2; Mt 7:2Ole wako wewe, ee mharabu,

wewe ambaye hukuharibiwa!

Ole wako, ee msaliti,

wewe ambaye hukusalitiwa!

Utakapokwisha kuharibu,

utaharibiwa;

utakapokwisha kusaliti,

utasalitiwa.

33:2 Za 13:5; Isa 59:16; 25:9; 5:30; Ezr 9:8; Mwa 43:29; Isa 40:10Ee Bwana, uturehemu,

tunakutamani.

Uwe nguvu yetu kila asubuhi

na wokovu wetu wakati wa taabu.

33:3 Za 12:5; Hes 10:35; Za 46:6; 68:33; Isa 59:16-18Kwa ngurumo ya sauti yako, mataifa yanakimbia;

unapoinuka, mataifa hutawanyika.

33:4 Hes 14:3; 2Fal 7:16; Isa 17:5; Yoe 3:13Mateka yenu, enyi mataifa, yamevunwa kama vile wafanyavyo madumadu,

kama kundi la nzige watu huvamia juu yake.

33:5 Za 97:9; Isa 5:16; 28:6; Ay 16:19; Isa 9:7; 1:26Bwana ametukuka, kwa kuwa anakaa mahali palipoinuka,

ataijaza Sayuni kwa haki na uadilifu.

33:6 Isa 12:2; Mt 6:33; Mit 1:7; Mwa 39:3; Ay 22:25; 1Sam 11:2-3Atakuwa msingi ulio imara kwa wakati wenu,

ghala za wokovu tele, hekima na maarifa;

kumcha Bwana ni ufunguo wa hazina hii.

33:7 Isa 10:34; 2Fal 18:37Angalia, watu wake mashujaa wanapiga kelele kwa nguvu barabarani,

wajumbe wa amani wanalia kwa uchungu.

33:8 Amu 5:6; Isa 30:21; 60:15; Zek 7:14; 2Fal 18:14Njia kuu zimeachwa,

hakuna wasafiri barabarani.

Mkataba umevunjika,

mashahidi wake wamedharauliwa,33:8 Au: miji yake imedharauliwa.

hakuna yeyote anayeheshimiwa.

33:9 Isa 3:26; 2Fal 19:23; Isa 24:4; 3:26; Yer 22:6; Kum 32:35-43; Mik 7:14Ardhi inaomboleza33:9 Au: Ardhi inakauka. na kuchakaa,

Lebanoni imeaibika na kunyauka,

Sharoni ni kama Araba,

nayo Bashani na Karmeli

wanapukutisha majani yao.

33:10 Isa 33:3; 2:21; 5:16“Sasa nitainuka,” asema Bwana.

“Sasa nitatukuzwa;

sasa nitainuliwa juu.

33:11 Za 7:14; Yak 1:5; Isa 26:18; 59:4Mlichukua mimba ya makapi,

mkazaa mabua,

pumzi yenu ni moto uwateketezao.

33:12 Amo 2:1; Isa 5:6; 10:17; 27:11Mataifa yatachomwa kama ichomwavyo chokaa,

kama vichaka vya miiba vilivyokatwa ndivyo watakavyochomwa.”

33:13 Za 48:10; Isa 48:16; 49:1Ninyi mlio mbali sana, sikieni lile nililofanya;

ninyi mlio karibu, tambueni uweza wangu!

33:14 Isa 32:11; Zek 13:9; Ebr 12:29; Isa 30:30; 1:28-31Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu,

kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu:

“Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao?

Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?”

33:15 Za 15:2; 119:37; Isa 58:8; Za 24:4; Eze 22:13; Mit 15:27Yeye aendaye kwa uadilifu

na kusema lililo haki,

yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma

na kuizuia mikono yake isipokee rushwa,

yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji,

na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu:

33:16 Isa 25:4; Za 18:1-2; Isa 65:13; Kum 32:13; Isa 48:21; 49:10huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu,

ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani.

Atapewa mkate wake,

na maji yake hayatakoma.

33:17 Isa 6:5; 4:2; 26:10Macho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake

na kuiona nchi inayoenea mbali.

33:18 1Kor 1:20; Isa 17:14; 2:15Katika mawazo yenu mtaifikiria hofu iliyopita:

“Yuko wapi yule afisa mkuu?

Yuko wapi yule aliyechukua ushuru?

Yuko wapi afisa msimamizi wa minara?”

33:19 Mwa 11:7; Yer 5:15; Isa 28:11Hutawaona tena wale watu wenye kiburi,

wale watu wenye usemi wa mafumbo,

wenye lugha ngeni, isiyoeleweka.

33:20 Isa 32:18; Za 46:5; 125:1-2; Mwa 26:22; Isa 41:18; 48:18Mtazame Sayuni, mji wa sikukuu zetu;

macho yenu yatauona Yerusalemu,

mahali pa amani pa kuishi, hema ambalo halitaondolewa,

nguzo zake hazitangʼolewa kamwe,

wala hakuna kamba yake yoyote itakayokatika.

33:21 Kut 17:6; Nah 3:8; Zek 2:5; Isa 10:34Huko Bwana atakuwa Mwenye Nguvu wetu.

Patakuwa kama mahali pa mito mipana na vijito.

Hakuna jahazi lenye makasia litakalopita huko,

wala hakuna meli yenye nguvu itakayopita huko.

33:22 Yak 4:12; Mt 21:5; Isa 11:4; Za 89:18; Isa 2:3Kwa kuwa Bwana ni mwamuzi wetu,

Bwana ndiye mtoa sheria wetu,

Bwana ni mfalme wetu,

yeye ndiye atakayetuokoa.

33:23 2Fal 7:8-16Kamba zenu za merikebu zimelegea:

Mlingoti haukusimama imara,

nalo tanga halikukunjuliwa.

Wingi wa mateka yatagawanywa,

hata yeye aliye mlemavu atachukua nyara.

33:24 Hes 23:21; Rum 11:27; 1Yn 1:7-9; Isa 30:26; 2Nya 6:21; Yer 31:34; 33:18Hakuna yeyote aishiye Sayuni atakayesema, “Mimi ni mgonjwa”;

nazo dhambi za wale waishio humo zitasamehewa.

Read More of Isaya 33

Isaya 34:1-17

Hukumu Dhidi Ya Mataifa

34:1 Isa 43:9; Kum 4:26; 32:1; Za 24:1; Isa 33:13Njooni karibu, enyi mataifa, nanyi msikilize;

sikilizeni kwa makini,

enyi kabila za watu!

Dunia na isikie, navyo vyote vilivyo ndani yake,

ulimwengu na vyote vitokavyo ndani yake!

34:2 Isa 13:5; Zek 5:3; Isa 10:25; 30:25Bwana ameyakasirikia mataifa yote;

ghadhabu yake ni juu ya majeshi yao yote.

Atawaangamiza kabisa,

atawatia mikononi mwa wachinjaji.

34:3 Yoe 2:20; Amo 4:10; Eze 38:22; Isa 5:25; Za 110:6; Eze 5:17; 14:19Waliouawa watatupwa nje,

maiti zao zitatoa uvundo,

milima itatota kwa damu zao.

34:4 2Pet 3:10; Yoe 2:31; Eze 32:7-8; Ay 9:7; Ufu 6:13; Isa 13:13; Mt 24:29; Ay 8:12; Mk 13:15; Isa 15:6; Ebr 1:12Nyota zote za mbinguni zitayeyuka

na anga litasokotwa kama kitabu,

jeshi lote la angani litaanguka

kama majani yaliyonyauka kutoka kwenye mzabibu,

kama tini iliyonyauka kutoka kwenye mtini.

34:5 Yer 49:7; 46:10; Zek 13:7; 2Sam 8:13-14; Yos 6:17; Kum 32:41-42; Amo 3:14-15; Yer 47:6; Eze 21:5; 2Nya 28:17; Amo 1:11-12; 6:11; Mal 1:4Upanga wangu umekunywa na kushiba huko mbinguni,

tazama, unashuka katika hukumu juu ya Edomu,

wale watu ambao nimeshawahukumu,

kuwaangamiza kabisa.

34:6 Kum 32:41; Law 3:9; Mwa 36:33; Isa 30:25; Yer 25:34; Ufu 19:17Upanga wa Bwana umeoga katika damu,

umefunikwa na mafuta ya nyama:

damu ya kondoo na mbuzi,

mafuta kutoka figo za kondoo dume.

Kwa maana Bwana ana dhabihu huko Bosra,

na machinjo makuu huko Edomu.

34:7 Hes 23:22; Za 68:30; 2Sam 1:22Nyati wataanguka pamoja nao,

ndama waume na mafahali wakubwa.

Nchi yao italowana kwa damu,

nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama.

34:8 Isa 2:12; 1:24; 59:18; Yoe 3:4; Eze 25:12-17; Amo 1:6-10Kwa sababu Bwana anayo siku ya kulipiza kisasi,

mwaka wa malipo,

siku ya kushindania shauri la Sayuni.

34:9 Mwa 19:24Vijito vya Edomu vitageuka kuwa lami,

mavumbi yake yatakuwa kiberiti kiunguzacho,

nchi yake itakuwa lami iwakayo!

34:10 Ufu 14:10-11; 19:3; Yer 49:18; Mal 1:3; Isa 13:20; Eze 29:12; 35:3Haitazimishwa usiku wala mchana,

moshi wake utapaa juu milele.

Kutoka kizazi hadi kizazi itakuwa ukiwa,

hakuna mtu yeyote atakayepita huko tena.

34:11 Law 11:16-18; Ufu 18:2; Mao 2:8; Amo 7:8; Kum 14:15-17; Yoe 3:19; 2Fal 21:13Bundi wa jangwani na bundi mwenye sauti nyembamba wataimiliki,

bundi wakubwa na kunguru wataweka viota humo.

Mungu atanyoosha juu ya Edomu

kamba ya kupimia ya machafuko matupu,

na timazi ya ukiwa.

34:12 Isa 41:11-12; Za 107:10; Ay 12:21; Isa 40:23; Eze 24:5; Yer 39:6Watu wake wa kuheshimiwa hawatakuwa na chochote

kitakachoitwa ufalme huko,

nao wakuu wao wote watatoweka.

34:13 Hos 9:6; Isa 32:13; 13:22; Yer 9:11; Isa 7:19; Za 44:19Miiba itaenea katika ngome za ndani,

viwawi na michongoma itaota

kwenye ngome zake.

Itakuwa maskani ya mbweha,

makao ya bundi.

34:14 Za 74:14; Isa 13:22; Ufu 18:2Viumbe vya jangwani vitakutana na fisi,

nao mbuzi-mwitu watalia wakiitana;

huko viumbe vya usiku vitastarehe pia

na kujitafutia mahali pa kupumzika.

34:15 Za 17:8; Kum 14:13Bundi wataweka viota huko na kutaga mayai,

atayaangua na kutunza makinda yake

chini ya uvuli wa mabawa yake;

pia huko vipanga watakusanyika,

kila mmoja na mwenzi wake.

34:16 Isa 30:8; Dan 7:10; Isa 1:20; 58:14; 48:13Angalieni katika gombo la Bwana na msome:

Hakuna hata mmoja katika hawa atakayekosekana,

hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzi wake.

Kwa kuwa ni kinywa chake Mungu kimeagiza,

na Roho wake atawakusanya pamoja.

34:17 Za 78:55; Isa 17:14; Yer 13:25Huwagawia sehemu zao,

mkono wake huwagawanyia kwa kipimo.

Wataimiliki hata milele

na kuishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.

Read More of Isaya 34

Isaya 35:1-10

Furaha Ya Waliokombolewa

35:1 Isa 27:10; 41:18-19; 51:3; 32:15-16; 27:6Jangwa na nchi kame vitafurahi;

nyika itashangilia na kuchanua maua.

Kama waridi, 35:2 Wim 7:5; Mwa 21:6; Ezr 3:7; Za 105:43; Isa 32:15; 12:6; 25:9; 1Nya 27:29litachanua maua,

litashangilia sana na kupaza sauti kwa furaha.

Litapewa utukufu wa Lebanoni,

fahari ya Karmeli na Sharoni;

wataona utukufu wa Bwana,

fahari ya Mungu wetu.

35:3 Ay 4:3-4; Ebr 12:12Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu,

yafanyeni imara magoti yaliyolegea,

35:4 Isa 40:2; 2Nya 32:6; Zek 1:13; Kum 20:3; Isa 21:4; Yos 1:9; Isa 7:4; 1:24; 34:8; 25:9; 40:1; 10:9, 10-11; 51:5; 62:11; Dan 10:19; Ufu 22:12waambieni wale wenye mioyo ya hofu,

“Kuweni hodari, msiogope;

tazama, Mungu wenu atakuja,

pamoja na malipo ya Mungu,

atakuja na kuwaokoa ninyi.”

35:5 Mt 9:27; 11:5; Isa 42:18; 29:18; 2Nya 32:6; Isa 40:2; Zek 1:13; Isa 21:4; Ufu 22:12Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa

na masikio ya viziwi yatazibuliwa.

35:6 Lk 7:22; Yn 5:8-9; Mk 7:35; Kut 17:6; Yn 7:38; Mdo 3:2; Mt 15:30; Mdo 3:8Ndipo kilema atarukaruka kama kulungu,

nao ulimi wa aliye bubu utapaza sauti kwa shangwe.

Maji yatatiririka kwa kasi katika nyika,

na vijito katika jangwa.

35:7 Za 68:6; Isa 41:17; 44:3; 55:1; 49:10; 58:11; 13:22; Za 107:35; Ay 8:11; 40:21Mchanga wa moto utakuwa bwawa la maji,

ardhi yenye kiu itabubujika chemchemi.

Maskani ya mbweha walikolala hapo awali

patamea majani, matete na mafunjo.

35:8 Yer 31:21; Yoe 3:17; Mt 7:13-14; 1Pet 1:15; Isa 52:1; 33:8Nako kutakuwa na njia kuu,

nayo itaitwa Njia ya Utakatifu.

Wasio safi hawatapita juu yake;

itakuwa ya wale watembeao katika Njia ile;

yeye asafiriye juu yake,

ajapokuwa mjinga, hatapotea.

35:9 Isa 30:9; 11:6-9; Law 25:47-55; Kut 6:6; Isa 13:22; 62:12Huko hakutakuwepo na simba,

wala mnyama mkali hatapita njia hiyo,

wala hawatapatikana humo.

Ila waliokombolewa tu ndio watakaopita huko,

35:10 Yn 16:22; Isa 51:11; 30:29; Ufu 21:4; Ay 19:25; Za 51:8waliokombolewa na Bwana watarudi.

Wataingia Sayuni wakiimba;

furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao.

Watapata furaha na shangwe;

huzuni na majonzi vitakimbia.

Read More of Isaya 35