Isaya 30:19-33, Isaya 31:1-9, Isaya 32:1-20 NEN

Isaya 30:19-33

30:19 Isa 61:3; Ay 22:27; Mt 7:7-11; Isa 25:8; Ay 24:12; Zek 13:9; Za 86:7; Isa 41:17Enyi watu wa Sayuni, mnaoishi Yerusalemu, hamtalia tena. Tazameni jinsi atakavyokuwa na huruma mtakapolia kwa kumwomba msaada! Mara asikiapo, atawajibu. 30:20 1Fal 22:27; Za 74:9; Isa 28:9; Amo 8:11Ingawa Bwana huwapa chakula cha shida na maji ya taabu, walimu wenu hawatafichwa tena, kwa macho yenu wenyewe mtawaona. 30:21 Kum 5:32; Mit 4:27; Isa 29:24; Ay 33:11Mkigeuka kuume au kushoto, masikio yenu yatasikia sauti nyuma yenu ikisema, “Hii ndiyo njia, ifuateni.” 30:22 Kut 32:4; Isa 2:20; Law 15:19-23; Eze 7:19-20Kisha mtanajisi sanamu zenu zilizofunikwa kwa fedha, na vinyago vyenu vilivyofunikwa kwa dhahabu. Mtazitupilia mbali kama vitambaa vya wakati wa hedhi na kuziambia, “Haya, tokeni hapa!”

30:23 1Tim 4:8; Za 65:13; Kum 28:12; Isa 65:21-22; Yer 31:14; Ay 36:31Pia atawapa mvua kwa ajili ya mbegu mnazootesha ardhini, chakula kinachotoka ardhini kitakuwa kizuri sana, tena tele. Katika siku ile, ngʼombe wenu watalisha katika shamba pana la majani. 30:24 Mt 3:12; Lk 3:17; Isa 32:14; Ay 6:5Maksai na punda walimao watakula majani makavu na vyakula vilivyotengenezwa, vinavyotandazwa kwa uma na sepeto. 30:25 Isa 13:5; Kut 17:6; Isa 32:2; Yoe 3:18Katika siku ile ya mauaji makuu, wakati minara itakapoanguka, vijito vya maji vitatiririka juu ya kila mlima mrefu na kila kilima kilichoinuka sana. 30:26 Zek 14:7-8; Ufu 21:23; 2Nya 7:14; Hos 14:4; Isa 60:19-20; Yer 3:22; 17:14Mwezi utaangaza kama jua, nao mwanga wa jua utangʼaa mara saba zaidi, kama nuru ya siku saba, wakati Bwana atakapoyafunga majeraha ya watu wake na kuwaponya vidonda alivyowatia.

30:27 1Fal 18:24; Isa 26:20; 60:14; Eze 22:31; Ay 41:21Tazama, Jina la Bwana linakuja kutoka mbali,

likiwa na hasira kali inayowaka

pamoja na wingu zito la moshi,

midomo yake imejaa ghadhabu

na ulimi wake ni moto ulao.

30:28 2The 2:8; Amo 9:9; 2Fal 19:28; Isa 37:29; 11:4; 28:15; Za 50:3Pumzi yake ni kama mkondo wa maji yaendayo kasi,

yakipanda hadi shingoni.

Hutikisa mataifa katika chekecheke ya uharibifu,

huweka lijamu katika mataya ya mataifa

ambayo huwaongoza upotevuni.

30:29 Mt 26:30; Za 42:4; Isa 25:9; 1Sam 10:5; Mwa 49:24Nanyi mtaimba kama usiku ule mnaadhimisha

sikukuu takatifu.

Mioyo yenu itashangilia

kama vile watu wanapokwea na filimbi

kwenye mlima wa Bwana,

kwa Mwamba wa Israeli.

30:30 Kut 19:18; Za 29:3; Kut 20:18; Isa 47:14; 9:12Bwana atawasababisha watu waisikie sauti yake ya utukufu,

naye atawafanya wauone mkono wake ukishuka

pamoja na hasira yake kali na moto ulao,

kukiwa na tufani ya mvua,

ngurumo za radi na mvua ya mawe.

30:31 Isa 10:5, 12; 11:4Sauti ya Bwana itaivunjavunja Ashuru,

kwa fimbo yake ya utawala atawapiga.

30:32 Isa 11:15; 10:26; Eze 32:10; Kut 15:20Kila pigo Bwana atakaloliweka juu yao

kwa fimbo yake ya kuadhibu,

litakuwa kwa wimbo wa matari na vinubi,

anapopigana nao katika vita

kwa mapigo ya mkono wake.

30:33 2Fal 23:10; Yer 7:31; Mwa 19:24; Ufu 9:17; 2Sam 22:16Tofethi imeandaliwa toka zamani,

imewekwa tayari kwa ajili ya mfalme.

Shimo lake la moto limetengenezwa kwa kina kirefu

na kwa upana mkubwa,

likiwa na moto na kuni tele;

pumzi ya Bwana,

kama kijito cha kiberiti,

huuwasha moto.

Read More of Isaya 30

Isaya 31:1-9

Ole Wa Wale Wanaotegemea Misri

31:1 Eze 17:15; Kum 17:16; 20:1; Yer 37:5; Dan 9:13; Hos 11:8; Isa 30:2-5; Ay 6:10Ole wao wale washukao Misri kwa ajili ya msaada,

wale wategemeao farasi,

wanaoweka tumaini katika wingi wa magari yao ya vita,

na katika nguvu nyingi za wapanda farasi,

lakini hawamwangalii yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,

wala hawatafuti msaada kwa Bwana.

31:2 Za 92:5; Rum 16:27; Hes 23:19; Mit 19:21; Isa 29:15; Amo 3:6; Isa 29:19; 32:6Hata hivyo yeye pia ana hekima na anaweza kuleta maafa,

wala hayatangui maneno yake.

Yeye atainuka dhidi ya nyumba ya mwovu,

dhidi ya wale ambao huwasaidia watenda mabaya.

31:3 Eze 28:9; Isa 20:5; Za 9:20; 2The 2:4; Ay 30:21; Yer 51:25; Isa 30:5-7; Neh 1:10Lakini Wamisri ni wanadamu, wala si Mungu,

farasi wao ni nyama, wala si roho.

Wakati Bwana atakaponyoosha Mkono wake,

yeye anayesaidia atajikwaa,

naye anayesaidiwa ataanguka,

wote wawili wataangamia pamoja.

31:4 Nah 3:18; Ay 30:21; Isa 30:5-7; Hes 24:9; 1Sam 17:34; Eze 34:23; Isa 42:13; Hos 11:10Hili ndilo Bwana analoniambia:

“Kama vile simba angurumavyo,

simba mkubwa juu ya mawindo yake:

hata ingawa kundi lote la wachunga mifugo

huitwa pamoja dhidi yake,

hatiwi hofu na kelele zao

wala kusumbuliwa na ghasia zao;

ndivyo Bwana Mwenye Nguvu Zote atakavyoshuka

kufanya vita juu ya Mlima Sayuni

na juu ya vilele vyake.

31:5 Za 91:4; Kum 32:11; Zek 9:15; Za 34:7; Mt 23:37; Kut 12:23Kama ndege warukao,

Bwana Mwenye Nguvu Zote ataukinga Yerusalemu;

ataukinga na kuuokoa,

atapita juu yake na kuufanya salama.”

31:6 Ay 22:23; Isa 1:5, 27Mrudieni yeye ambaye nyumba ya Israeli imemwasi sana. 31:7 Isa 2:20; 30:22; 1Fal 12:30; Za 135:5Kwa kuwa katika siku ile kila mmoja wenu atazikataa sanamu za fedha na za dhahabu zilizotengenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi.

31:8 Isa 10:12; Kut 12:12; Hab 2:8; Mwa 49:15; Isa 14:25; Yer 25:12; Kum 20:11“Ashuru itaanguka kwa upanga ambao si wa mwanadamu;

upanga usio wa kibinadamu utawaangamiza.

Watakimbia mbele ya upanga

na vijana wao wa kiume watafanyizwa kazi kwa lazima.

31:9 Kum 32:31-37; Isa 10:17; Law 6:13; Isa 18:3; Yer 4:6; 51:9; Za 21:9Ngome zao zitaanguka kwa sababu ya hofu;

kwa kuona bendera ya vita,

majemadari wao watashikwa na hofu ya ghafula,”

asema Bwana,

ambaye moto wake uko Sayuni,

nayo tanuru yake iko Yerusalemu.

Read More of Isaya 31

Isaya 32:1-20

Ufalme Wa Haki

32:1 2Nya 31:20; Eze 37:24; Za 72:1-4; Yer 23:5; Isa 28:6; Za 149:2; Isa 6:5Tazama, mfalme atatawala kwa uadilifu

na watawala watatawala kwa haki.

32:2 1Fal 18:4; Isa 4:6; Za 55:8; 23:2; Isa 49:10; Yer 31:9; Za 107:35Kila mtu atakuwa kama kivuli cha kujificha kutokana na upepo

na kimbilio kutokana na dhoruba,

kama vijito vya maji jangwani

na kivuli cha mwamba mkubwa katika ardhi yenye kiu.

32:3 Isa 29:18; 42:7, 16; Kum 29:4Ndipo macho ya wale wanaoona hayatafumbwa tena,

nayo masikio ya wale wanaosikia yatasikiliza.

32:4 Isa 6:10; 29:24; 35:6Moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu na kuelewa,

nao ulimi wenye kigugumizi utanena kwa ufasaha.

32:5 1Sam 25:25Mpumbavu hataitwa tena muungwana,

wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu.

32:6 Isa 3:15; Mit 19:3; Isa 9:16-17; Mit 24:2; Isa 26:10Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu,

moyo wake hushughulika na uovu:

Hutenda mambo yasiyo ya kumcha Mungu,

na hueneza habari za makosa kuhusu Bwana;

yeye huwaacha wenye njaa bila kitu,

na wenye kiu huwanyima maji.

32:7 Yer 5:26-28; Dan 12:10; Mik 7:3; Isa 29:19-20; Za 72:4; Isa 29:21Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu,

hufanya mipango miovu

ili kumwangamiza maskini kwa uongo,

hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki.

32:8 1Nya 29:9; Mit 11:25; Isa 14:24Lakini mtu muungwana hufanya mipango ya kiungwana,

na kwa matendo ya kiungwana yeye hufanikiwa.

Wanawake Wa Yerusalemu

32:9 Isa 28:23; Dan 4:4; Amo 6:1; Sef 2:15Enyi wanawake wenye kuridhika sana,

amkeni na mnisikilize.

Enyi binti mnaojisikia kuwa salama,

sikieni lile ninalotaka kuwaambia!

32:10 Isa 5:5-6; 24:7; 37:30Muda zaidi kidogo ya mwaka mmoja,

ninyi mnaojisikia salama mtatetemeka,

mavuno ya zabibu yatakoma

na mavuno ya matunda hayatakuwepo.

32:11 Nah 3:5; Mik 1:8; Isa 34:14; 47:2; 3:24Tetemekeni, enyi wanawake wenye kuridhika,

tetemekeni kwa hofu, enyi binti mnaojisikia salama!

Vueni nguo zenu,

vaeni nguo ya gunia viunoni mwenu.

32:12 Nah 2:7; Isa 16:9Pigeni matiti yenu kwa ajili ya mashamba mazuri,

kwa ajili ya mizabibu iliyozaa vizuri

32:13 Hos 9:6; 10:8; Isa 23:7; 24:11na kwa ajili ya nchi ya watu wangu,

nchi ambayo miiba na michongoma imemea:

naam, ombolezeni kwa ajili ya nyumba zote za furaha

na kwa ajili ya mji huu wenye kufanya sherehe.

32:14 Isa 13:22; 27:10; 2:15; 34:13; 6:11; 5:17; Za 104:11Ngome itaachwa,

mji wenye kelele nyingi utahamwa,

ngome ndani ya mji na mnara wa ulinzi vitakuwa ukiwa milele,

mahali pazuri pa punda na malisho ya makundi ya kondoo,

32:15 Yoe 2:28; Eze 37:9; Za 107:35; Isa 29:17; 11:2mpaka Roho amwagwe juu yetu kutoka juu,

nalo jangwa kuwa shamba lenye rutuba,

na shamba lenye rutuba kuwa kama msitu.

32:16 Isa 9:7; 28:6; 35:1, 6; 42:11; Za 48:1; Isa 1:26Haki itakaa katika jangwa,

na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba.

32:17 Za 85:10; 119:165; Rum 14:17; Ebr 12:11Matunda ya haki yatakuwa amani,

matokeo ya haki yatakuwa utulivu

na matumaini milele.

32:18 Yos 1:13; 11:18; Hos 2:18-23; Amo 9:14Watu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani,

katika nyumba zilizo salama,

katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu.

32:19 Isa 19:18; 24:10; 28:17; 30:30; Zek 11:2; Ay 40:11Hata kama mvua ya mawe iangushe msitu

na mji ubomolewe kabisa,

32:20 Mhu 11:1; Isa 30:24; Ay 39:8; Kum 28:12tazama jinsi utakavyobarikiwa,

ukipanda mbegu yako katika kila kijito,

na kuwaacha ngʼombe wako

na punda wajilishe kwa uhuru.

Read More of Isaya 32