Isaya 3:1-26, Isaya 4:1-6, Isaya 5:1-7 NEN

Isaya 3:1-26

Hukumu Juu Ya Yerusalemu Na Yuda.

3:1 Law 26:26; Eze 4:16; Amo 4:6; Yer 37:21; Za 18:18; Isa 5:13; 65:13Tazama sasa, Bwana,

Bwana Mwenye Nguvu Zote,

yu karibu kuwaondolea Yerusalemu na Yuda

upatikanaji wa mahitaji na misaada,

upatikanaji wote wa chakula na tegemeo lote la maji,

3:2 Eze 17:13; Isa 9:14-15; 2Fal 24:14; Kum 18:10shujaa na mtu wa vita,

mwamuzi na nabii,

mwaguzi na mzee,

3:3 Ay 22:8; 2Fal 24:14; Mhu 10:11; Yer 8:17; 2Fal 1:9jemadari wa kikosi cha watu hamsini

na mtu mwenye cheo, mshauri,

fundi stadi na mlozi mjanja.

3:4 Mhu 10:16Nitawafanya wavulana wawe maafisa wao,

watoto ndio watakaowatawala.

3:5 Za 28:3; Yer 9:8; Isa 9:19; Mik 7:2-6Watu wataoneana wao kwa wao:

mtu dhidi ya mtu, na jirani dhidi ya jirani yake.

Kijana atainuka dhidi ya mzee,

mtu mnyonge dhidi ya mtu mwenye heshima.

Mtu atamkamata mmoja wa ndugu zake

katika nyumba ya baba yake na kusema,

“Unalo joho, sasa uwe kiongozi wetu,

tawala lundo hili la magofu!”

3:7 Yer 30:12; Hos 5:13; Isa 2:11; 24:2; Eze 34:4; Yoe 1:16Lakini siku hiyo atapiga kelele akisema,

“Sina uponyaji.

Sina chakula wala mavazi katika nyumba yangu,

msinifanye niwe kiongozi wa watu.”

3:8 Isa 30:9; 9:15-17; 28:15; 1:7; Ay 1:11; Za 73:9-11; 2Nya 33:6; Isa 65:7Yerusalemu inapepesuka,

Yuda inaanguka;

maneno yao na matendo yao ni kinyume na Bwana,

wakiudharau uwepo wake uliotukuka.

3:9 Mwa 13:13; 2Nya 34:24; Rum 6:23; Hes 32:23; Isa 59:12; Yer 14:7; Mit 8:36; Hos 5:5Nyuso zao zinavyoonekana zinashuhudia dhidi yao,

hujivunia dhambi yao kama Sodoma,

wala hawaifichi.

Ole wao!

Wamejiletea maafa juu yao wenyewe.

3:10 Za 37:17; Yer 22:15; Mwa 15:1; Za 128:2; Kum 12:28; 5:33Waambie wanyofu itakuwa heri kwao,

kwa kuwa watafurahia tunda la matendo yao.

3:11 Kum 28:15-68; Ay 9:13; Isa 57:20; Kum 28:15-68; 2Nya 6:23; Yer 21:14; Mao 5:16; Eze 24:14Ole kwa watu waovu! Maafa yapo juu yao!

Watalipwa kwa ajili ya yale mikono yao iliyotenda.

3:12 Yer 25:16; Mik 3:5; Isa 9:16; 19:14; 28:7; Yer 23:13; 25:16Vijana wanawatesa watu wangu,

wanawake wanawatawala.

Enyi watu wangu, viongozi wenu wanawapotosha,

wanawapoteza njia.

3:13 Ay 10:2; Za 82:1; Isa 2:4Bwana anachukua nafasi yake mahakamani,

anasimama kuhukumu watu.

3:14 1Sam 12:7; Yak 2:6; Ay 22:4; 24:9; Isa 25:4; 11:4Bwana anaingia katika hukumu

dhidi ya wazee na viongozi wa watu wake:

“Ninyi ndio mlioharibu shamba langu la mizabibu,

mali zilizonyangʼanywa maskini zimo nyumbani mwenu.

3:15 Za 94:5; Ay 24:14; Isa 10:6; 26:6; 29:19; 32:6; 5:7Mnamaanisha nini kuwaponda watu wangu

na kuzisaga nyuso za maskini?”

asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.

3:16 Wim 3:11; Ay 15:25Bwana asema,

“Wanawake wa Sayuni wana kiburi,

wanatembea na shingo ndefu,

wakikonyeza kwa macho yao,

wanatembea kwa hatua za madaha,

wakiwa na mapambo ya njuga kwenye vifundo vya miguu yao.

3:17 Eze 27:31; Amo 8:10Kwa hiyo Bwana ataleta majipu kwenye vichwa vya wanawake wa Sayuni;

Bwana atazifanya ngozi za vichwa vyao kuwa vipara.”

3:18 Mwa 41:42; Amu 8:21; Isa 2:11Katika siku ile Bwana atawanyangʼanya uzuri wao: bangili, tepe za kichwani, mikufu yenye alama za mwezi mwandamo, 3:19 Mwa 24:47; Eze 16:11-12vipuli, vikuku, shela, 3:20 Kut 39:28; Eze 44:18; 24:17, 23vilemba, mikufu ya vifundo vya miguu, mshipi, chupa za manukato na hirizi, 3:21 Mwa 24:22; Kut 29:6pete zenye muhuri, pete za puani, 3:22 Rut 3:15majoho mazuri, mitandio, mavazi, kifuko cha kutilia fedha, 3:23 Eze 26:10; 23:26; Kut 29:6; Wim 3:11; Isa 61:3; 62:3vioo, mavazi ya kitani, taji na shali.

3:24 Es 2:12; Mit 31:24; Law 13:40; Yon 3:5-8; Isa 4:4; 20:2; Ay 1:20; 16:15; Mwa 37:34; Yer 4:8; Mao 2:10Badala ya harufu ya manukato kutakuwa na uvundo;

badala ya mishipi, ni kamba;

badala ya nywele zilizotengenezwa vizuri, ni upara;

badala ya mavazi mazuri, ni nguo za magunia;

badala ya uzuri, ni alama ya aibu kwa chuma cha moto.

3:25 Isa 1:20; Yer 15:8Wanaume wako watauawa kwa upanga,

nao mashujaa wako watauawa vitani.

3:26 Yer 14:2; 4:28; Mao 2:10; Ay 2:13; Isa 14:12, 31; 33:9; 24:4, 7; Za 137:1Malango ya Sayuni yataomboleza na kulia,

ataketi mavumbini akiwa fukara.

Read More of Isaya 3

Isaya 4:1-6

4:1 Mwa 30:23; 2The 3:12; Isa 13:12; 32:9; 2:11Katika siku ile wanawake saba

watamshika mwanaume mmoja

wakisema, “Tutakula chakula chetu wenyewe

na kuvaa nguo zetu wenyewe,

ila wewe uturuhusu tu tuitwe kwa jina lako.

Utuondolee aibu yetu!”

Tawi La Bwana

4:2 Zek 6:12; Yer 23:5; Eze 36:8; 17:22; Za 72:16; Isa 11:1-5; 52:13; Yer 33:15-16; Isa 2:11; Yer 23:6; Zek 3:8Katika siku ile Tawi la Bwana litakuwa zuri na lenye utukufu, nalo tunda la nchi litakuwa fahari na utukufu wa wale Waisraeli watakaonusurika. 4:3 Mao 1:17; Sef 3:13; Rum 11:5; Za 56:8; Lk 10:20; Isa 1:26; Kut 19:6; Yoe 3:1-7Wale watakaoachwa Sayuni, watakaobaki Yerusalemu, wataitwa watakatifu, wale wote ambao wameorodheshwa miongoni mwa walio hai huko Yerusalemu. 4:4 Zek 13:9; Isa 3:24; 28:6; 30:30; Mt 3:11; Ufu 7:15Bwana atausafisha uchafu wa wanawake wa Sayuni, atatakasa madoa ya damu kutoka Yerusalemu kwa Roho ya hukumu na Roho ya moto. 4:5 Isa 58:8; Kut 13:21-22; Isa 41:20; 65:18; Ufu 14:1; Isa 35:2; Za 18:11; Ufu 7:15Kisha Bwana ataumba juu ya Mlima wote wa Sayuni, na juu ya wale wote wanaokusanyika hapo, wingu la moshi wakati wa mchana, na kungʼaa kwa miali ya moto wakati wa usiku, nako juu ya huo utukufu wote kutatanda kifuniko cha ulinzi. 4:6 Law 23:34-43; Isa 25:4; 30:2; 57:13; 8:14; Za 27:5; 55:8; Eze 11:16; Isa 14:32Utakuwa sitara na kivuli kutokana na joto la mchana, na kuwa mahali pa kujificha kutokana na dhoruba na mvua.

Read More of Isaya 4

Isaya 5:1-7

Wimbo Wa Shamba La Mizabibu

5:1 Za 80:8-9; Yn 15:1; Isa 27:2Nitaimba wimbo kwa ajili ya mmoja nimpendaye,

kuhusu shamba lake la mizabibu:

Mpendwa wangu alikuwa na shamba la mizabibu

kwenye kilima chenye rutuba.

5:2 Kum 32:6; Kut 15:17; Yer 2:21; Mt 21:19; Mk 11:13; Isa 16:8; 27:3; 1Sam 2:9; Ay 24:11; Mt 21:33; Lk 13:6Alililima na kuondoa mawe

na akaliotesha mizabibu bora sana.

Akajenga mnara wa ulinzi ndani yake,

na kutengeneza shinikizo la kukamulia divai pia.

Kisha akatazamia kupata mazao ya zabibu nzuri,

lakini lilizaa matunda mabaya tu.

5:3 Mt 21:40“Basi enyi wakazi wa Yerusalemu na watu wa Yuda,

hukumuni kati yangu na shamba langu la mizabibu.

5:4 2Nya 36:15; Mt 23:37; Yer 2:5-7; 2:21; Mk 6:3-4; Yer 24:2; 29:17Ni nini zaidi ambacho kingeweza kufanyika kwa shamba langu la mizabibu

kuliko yale niliyofanya?

Nilipotazamia kupata zabibu nzuri,

kwa nini lilizaa zabibu mbaya tu?

5:5 Za 80:12; Lk 21:24; Yer 12:10; Isa 6:12; 27:10; 22:5; 10:6; 2Nya 36:21Sasa nitawaambia lile nitakalolitendea

shamba langu la mizabibu:

Nitaondoa uzio wake,

nalo litaharibiwa,

nitabomoa ukuta wake,

nalo litakanyagwa.

5:6 Hos 2:12; Ebr 6:8; Mwa 6:13; Isa 6:13; 49:17; 2Sam 23:6; Isa 7:23-24; Law 26:32; Eze 28:24; 2Sam 1:21; Amo 4:7Nitalifanya nchi ya ukiwa isiyokaliwa na watu,

halitakatiwa matawi wala kulimwa,

nayo michongoma na miiba itamea huko,

nitaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.”

5:7 Isa 37:30; Eze 9:9; 22:29; Za 80:8; Isa 17:10; 10:2; 29:21; 61:8; Za 12:5Shamba la mzabibu la Bwana Mwenye Nguvu Zote

ni nyumba ya Israeli,

na watu wa Yuda

ni bustani yake ya kumpendeza.

Alitazamia haki, lakini akaona umwagaji damu,

alitazamia uadilifu, lakini akasikia vilio vya taabu.

Read More of Isaya 5