Isaya 14:1-32, Isaya 15:1-9, Isaya 16:1-14 NEN

Isaya 14:1-32

Yuda Kufanywa Upya

14:1 Isa 54:7-8; Zek 10:6; Mwa 18:19; Eze 47:22; Efe 2:12-19; Kut 12:43; Eze 47:22; Zek 8:22-23; Isa 11:10; Yer 3:18; Zek 2:12Bwana atamhurumia Yakobo,

atamchagua Israeli tena,

na kuwakalisha katika nchi yao wenyewe.

Wageni wataungana nao

na kujiunga na nyumba ya Yakobo.

14:2 Isa 11:12; 26:15; 49:7; 49:23; 54:3; 60:9; Sef 3:19; Zek 2:9; Za 49:14Mataifa watawachukua

na kuwaleta mahali pao wenyewe.

Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa

kama watumishi na wajakazi katika nchi ya Bwana.

Watawafanya watekaji wao kuwa mateka,

na kutawala juu ya wale waliowaonea.

14:3 Isa 11:10-12; Ay 3:17; Kut 1:14Katika siku Bwana atakapokuondolea mateso, udhia na utumwa wa kikatili, 14:4 Hab 2:6; Mik 2:4; Isa 13:19; 9:4utaichukua dhihaka hii dhidi ya mfalme wa Babeli:

Tazama jinsi mtesi alivyofikia mwisho!

Tazama jinsi ghadhabu yake kali ilivyokoma!

14:5 Isa 10:15; Za 125:3; 110:2Bwana amevunja fimbo ya mwovu,

fimbo ya utawala ya watawala,

14:6 2Fal 15:29; Isa 10:14; Za 47:3; Isa 47:6ambayo kwa hasira waliyapiga mataifa

kwa mapigo yasiyo na kikomo,

nao kwa ghadhabu kali waliwatiisha mataifa

kwa jeuri pasipo huruma.

14:7 Za 126:1-3; Hes 6:26; Yer 50:34; Zek 1:11Nchi zote ziko kwenye mapumziko na kwenye amani,

wanabubujika kwa kuimba.

14:8 1Nya 16:33; Za 65:13; Eze 31:16; 2Fal 19:23; Isa 37:24Hata misunobari na mierezi ya Lebanoni

inashangilia mbele yako na kusema,

“Basi kwa sababu umeangushwa chini,

hakuna mkata miti atakayekuja kutukata.”

14:9 Mit 30:16; Eze 32:21; Ay 26:5; Zek 10:3; Ay 3:14Kuzimu kote kumetaharuki

kukulaki unapokuja,

kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea,

wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu,

kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme:

wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa.

14:10 Eze 26:20; 32:21Wote wataitikia,

watakuambia,

“Wewe pia umekuwa dhaifu, kama sisi tulivyo;

wewe umekuwa kama sisi.”

14:11 Ay 7:5; 24:20; Hes 16:30; Mit 30:16; Isa 5:12; Eze 26:13; Amo 6:5; Ay 21:26Majivuno yako yote yameshushwa mpaka kuzimu,

pamoja na kelele ya vinubi vyako,

mafunza yametanda chini yako,

na minyoo imekufunika.

14:12 Isa 34:4; 2Pet 1:19; Ufu 2:28; Lk 10:18; Eze 26:17; Ufu 2:28Tazama jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni,

ewe nyota ya asubuhi, mwana wa mapambazuko!

Umetupwa chini duniani,

wewe uliyepata kuangusha mataifa!

14:13 Mt 11:23; Eze 28:2; 2The 2:4; Dan 8:10; 5:23; Isa 37:24Ulisema moyoni mwako,

“Nitapanda juu hadi mbinguni,

nitakiinua kiti changu cha enzi

juu ya nyota za Mungu,

nitaketi nimetawazwa

juu ya mlima wa kusanyiko,

kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu.

14:14 Hes 24:16; 2The 2:4; Ay 20:6; Isa 47:8; Yer 50:29; Dan 11:38; Isa 10:13Nitapaa juu kupita mawingu,

nitajifanya kama Yeye Aliye Juu Sana.”

14:15 Mt 11:23; Lk 10:15; Mdo 12:23; Isa 13:6; 47:11; Ay 21:13; Eze 31:16Lakini umeshushwa chini hadi kuzimu,

hadi kwenye vina vya shimo.

14:16 Yer 50:23; Ufu 18:18; Isa 2:19; 13:13; Yoe 3:16Wale wanaokuona wanakukazia macho,

wanatafakari hatima yako:

“Je, huyu ndiye yule aliyetikisa dunia

na kufanya falme zitetemeke,

14:17 Isa 15:6; Za 52:7; 2Fal 15:29; Kut 7:14; Yer 50:33; Ufu 18:18yule aliyeifanya dunia kuwa jangwa,

aliyeipindua miji yake,

na ambaye hakuwaachia mateka wake

waende nyumbani?”

14:18 Ay 21:32Wafalme wote wa mataifa wamelala kwa heshima

kila mmoja katika kaburi lake.

14:19 Isa 22:16-18; Yer 36:30; Isa 34:3; 13:15; Yer 8:1; 41:7-9Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako

kama tawi lililokataliwa,

umefunikwa na waliouawa

pamoja na wale waliochomwa kwa upanga,

wale washukao mpaka

kwenye mawe ya shimo.

Kama mzoga uliokanyagwa chini ya nyayo,

14:20 Ay 18:19; Kum 32:16; Za 21:10; 1Fal 21:19Hutajumuika nao kwenye mazishi,

kwa kuwa umeharibu nchi yako

na kuwaua watu wako.

Mzao wa mwovu

hatatajwa tena kamwe.

14:21 Mwa 9:25; Kut 20:5; Hes 16:27; Law 26:39Andaa mahali pa kuwachinjia wanawe

kwa ajili ya dhambi za baba zao,

wasije wakainuka ili kuirithi nchi

na kuijaza dunia kwa miji yao.

14:22 2Sam 18:18; 1Fal 14:10; Za 94:16; Ay 18:17-19; Isa 13:18; Za 109:13Bwana Mwenye Nguvu Zote asema,

“Nitainuka dhidi yao,

nitalikatilia mbali jina lake kutoka Babeli pamoja na watu wake walionusurika,

watoto wake na wazao wake,”

asema Bwana.

14:23 Law 11:16-18; Sef 2:14; Isa 34:11-15; Yer 25:12; 50:3; 51:62“Nitaifanya kuwa mahali pa bundi,

na kuwa nchi ya matope;

nitaifagia kwa ufagio wa maangamizi,”

asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

Unabii Dhidi Ya Ashuru

14:24 Isa 62:8; Eze 12:25; Mdo 4:28; Isa 45:23; 23:8-9; Dan 4:35; Isa 46:10-11Bwana Mwenye Nguvu Zote ameapa,

“Hakika, kama vile nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa,

nami kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyosimama.

14:25 Isa 37:36-37; 10:27; 9:4Nitamponda Mwashuru katika nchi yangu,

juu ya milima yangu nitawakanyagia chini.

Nira yake itaondolewa kutoka kwa watu wangu,

nao mzigo wake utaondolewa kutoka mabegani mwao.”

14:26 Kut 15:12; Ay 30:21; Isa 23:9Huu ndio mpango uliokusudiwa kwa ajili ya ulimwengu wote,

huu ni mkono ulionyooshwa juu ya mataifa yote.

14:27 2Nya 20:6; Ay 40:8; Dan 4:35; Yer 49:20; Kut 14:21Kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amekusudia,

ni nani awezaye kumzuia?

Mkono wake umenyooshwa,

ni nani awezaye kuurudisha?

Unabii Dhidi Ya Wafilisti

Neno hili lilikuja mwaka ule Mfalme Ahazi alipofariki:

14:29 Yos 13:3; Isa 11:8; Kum 8:15; 2Nya 26:6Msifurahi, enyi Wafilisti wote,

kwamba fimbo iliyowapiga imevunjika;

kutoka mzizi wa huyo nyoka

atachipuka nyoka mwenye sumu kali,

uzao wake utakuwa joka lirukalo,

lenye sumu kali.

14:30 Isa 3:15; 25:4; 7:21-22; 8:21; 9:20; Sef 2:5Maskini kuliko maskini wote watapata malisho,

nao wahitaji watalala salama.

Lakini mzizi wako nitauangamiza kwa njaa,

nayo njaa itawaua walionusurika.

14:31 Isa 3:26; Yer 47:2; Eze 32:30; Isa 13:6; 41:25; Mwa 10:14; Yer 13:20; 46:20-24Piga yowe, ee lango! Bweka, ee mji!

Yeyukeni, enyi Wafilisti wote!

Wingu la moshi linakuja toka kaskazini,

wala hakuna atakayechelewa katika safu zake.

14:32 Za 51:18; Isa 37:9; Yak 2:5; Za 87:2; Isa 28:16; 44:28; 4:6Ni jibu gani litakalotolewa

kwa wajumbe wa taifa hilo?

Bwana ameifanya imara Sayuni,

nako ndani yake watu wake walioonewa watapata kimbilio.”

Read More of Isaya 14

Isaya 15:1-9

Unabii Dhidi Ya Moabu

15:1 Hes 21:28; 22:3-6; Kum 23:6; Hes 17:12; Yer 51:58; 48:24; 2Fal 3:25Neno kuhusu Moabu:

Ari iliyo Moabu imeangamizwa:

imeharibiwa kwa usiku mmoja!

Kiri iliyo Moabu imeangamizwa,

imeharibiwa kwa usiku mmoja!

15:2 Yer 48:35; Law 21:5; Ay 1:20; Hes 21:20; Isa 16:12; 2Sam 10:4; Law 13:40Diboni anakwea hadi kwenye hekalu lake,

mpaka mahali pake pa juu ili walie,

Moabu anaombolezea Nebo na Medeba.

Kila kichwa kimenyolewa

na kila ndevu limeondolewa.

15:3 Mao 2:11; Mik 1:8; Isa 3:24; Yos 2:8; Yer 48:38; Isa 14:31; Eze 7:18; Yer 47:2Wamevaa nguo za magunia barabarani,

juu ya mapaa na kwenye viwanja

wote wanaomboleza,

wamelala kifudifudi kwa kulia.

15:4 Hes 32:3; 21:23-25; Yos 13:26Heshboni na Eleale wanalia,

sauti zao zinasikika hadi Yahazi.

Kwa hiyo watu wenye silaha wa Moabu wanapiga kelele,

nayo mioyo yao imezimia.

15:5 Isa 16:11; Yer 48:31; 48:3-5; 4:20; Mwa 13:10; Hes 21:29Moyo wangu unamlilia Moabu;

wakimbizi wake wanakimbilia Soari,

hadi Eglath-Shelishiya.

Wanapanda njia ya kwenda Luhithi,

wanakwenda huku wanalia;

barabarani iendayo Horonaimu

wanaombolezea maangamizi yao.

15:6 Isa 19:5-7; Za 37:2; Hos 4:3; Yer 48:34; Isa 16:8; 33:9; 14:17; Yer 14:5Maji ya Nimrimu yamekauka

na majani yamenyauka;

mimea imekauka wala hakuna

kitu chochote kibichi kilichobaki.

15:7 Isa 30:6; Yer 48:36Kwa hiyo mali waliyoipata na kujiwekea akiba

wamezichukua na kuvuka Bonde la Mierebi.

15:8 Hes 21:16Mwangwi wa kilio chao umefika hadi mpakani mwa Moabu,

kilio chao cha huzuni kimefika hadi Eglaimu,

maombolezo yao hadi Beer-Elimu.

15:9 2Fal 17:25; Eze 25:8-11Maji ya Dimoni yamejaa damu,

lakini bado nitaleta pigo jingine juu ya Dimoni:

simba juu ya wakimbizi wa Moabu

na juu ya wale wanaobaki katika nchi.

Read More of Isaya 15

Isaya 16:1-14

Hali Ya Kukata Tamaa Ya Moabu

16:1 Isa 10:32; Amu 1:36; 2Fal 14:7; 2Nya 32:23; 2Fal 3:4; Oba 1:3Pelekeni wana-kondoo kama ushuru

kwa mtawala wa nchi,

Kutoka Sela, kupitia jangwani,

hadi mlima wa Binti Sayuni.

16:2 Mit 27:8; Hes 21:13-14; Yer 48:40; Hes 21:29Kama ndege wanaopapatika

waliofukuzwa kutoka kwenye kiota,

ndivyo walivyo wanawake wa Moabu

kwenye vivuko vya Arnoni.

16:3 1Fal 18:4“Tupeni shauri,

toeni uamuzi.

Wakati wa adhuhuri,

fanyeni kivuli chenu kama usiku.

Waficheni watoro,

msisaliti wakimbizi.

16:4 Isa 55:7; 9:4; 2:2-4Waacheni watoro wa Moabu wakae pamoja nanyi;

kuweni mahali pao pa salama ili kuepuka mharabu.”

Mtesi atafikia mwisho na maangamizi yatakoma,

aletaye vita atatoweka kutoka nchi.

16:5 1Sam 13:14; Mik 4:7; Isa 7:2; Dan 7:14; Mit 20:28; Isa 9:7; Lk 1:32Kwa upendo kiti cha enzi kitaimarishwa,

kwa uaminifu mtu ataketi juu yake,

yeye atokaye nyumba ya Daudi:

yeye ambaye katika kuhukumu hutafuta haki,

na huhimiza njia ya haki.

16:6 Eze 25:8; Yer 25:21; Law 26:19; Ay 20:6; Sef 2:8; Yer 49:16; Amo 2:1Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu:

kiburi chake cha kujivuna na udanganyifu,

kiburi chake na ufidhuli wake,

lakini majivuno yake si kitu.

16:7 1Nya 16:3; 2Fal 3:25; Yer 48:20; 49:3; Isa 13:6Kwa hiyo Wamoabu wanaomboleza,

wanaiombolezea Moabu kwa pamoja.

Wanaomboleza na kuhuzunika

kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi.

16:8 Ay 8:16; Hes 21:32; 21:25; Isa 15:6; 5:2; Ay 8:16; Za 80:11Mashamba ya Heshboni yananyauka,

pia na mizabibu ya Sibma.

Watawala wa mataifa

wamekanyaga mizabibu iliyo mizuri sana,

ambayo ilipata kufika Yazeri

na kuenea kuelekea jangwani.

Machipukizi yake yalienea

yakafika hadi baharini.

16:9 Isa 15:3; Eze 27:31; Yer 40:12; Ay 7:3; Hes 32:3; Ezr 3:13Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo,

kwa ajili ya mizabibu ya Sibma.

Ee Heshboni, ee Eleale,

ninakulowesha kwa machozi!

Kelele za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva

na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa.

16:10 Isa 24:7-8; Amu 9:27; Ay 24:11; Yer 25:30; Isa 5:2Furaha na shangwe zimeondolewa

kutoka mashamba ya matunda;

hakuna yeyote aimbaye wala apazaye sauti

katika mashamba ya mizabibu;

hakuna yeyote akanyagaye zabibu shinikizoni,

kwa kuwa nimekomesha makelele.

16:11 Isa 15:5; Hos 11:8; Flp 2:1; Ay 30:31; Isa 63:15Moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama kinubi,

nafsi yangu yote kwa ajili ya Kir-Haresethi.

16:12 Za 115:4-7; 1Kor 8:4; Hes 22:4; Isa 15:2; 1Fal 11:7; 18:29Wakati Moabu anapojitokeza mahali pake pa juu,

anajichosha mwenyewe tu;

anapokwenda mahali pake pa kuabudia miungu ili kuomba,

haitamfaidi lolote.

Hili ndilo neno ambalo Bwana ameshasema kuhusu Moabu. 16:14 Isa 25:10; Yer 48:42; Kum 15:18; 13:16; Isa 20:3; 37:30; Law 19:13Lakini sasa Bwana anasema: “Katika miaka mitatu, kama vile mtumishi aliyefungwa na mkataba angeihesabu, fahari ya Moabu na watu wake wengi watadharauliwa, nao walionusurika watakuwa wachache sana, tena wanyonge.”

Read More of Isaya 16