Hosea 6:1-11, Hosea 7:1-16 NEN

Hosea 6:1-11

Israeli Asiye Na Toba

6:1 Ay 16:9; Kum 32:39; Mao 3:11; Ay 5:18; Isa 10:20; 19:22; Hes 12:13; Yer 3:22; 30:17; Hos 14:4“Njooni, tumrudie Bwana.

Ameturarua vipande vipande

lakini atatuponya;

ametujeruhi lakini

atatufunga majeraha yetu.

6:2 Mit 2:1-9; Za 80:18; 30:5; Mt 16:21Baada ya siku mbili atatufufua;

katika siku ya tatu atatuinua,

ili tuweze kuishi mbele zake.

6:3 Ay 4:3; 29:23; Yoe 2:23; Hos 12:6; Za 72:6; Hos 11:10Tumkubali Bwana,

tukaze kumkubali yeye.

Kutokea kwake ni hakika kama vile

kuchomoza kwa jua;

atatujia kama mvua za masika,

kama vile mvua za vuli

ziinyweshavyo nchi.”

6:4 Hos 11:8; 7:1; 13:3“Nifanye nini nawe, Efraimu?

Nifanye nini nawe, Yuda?

Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi,

kama umande wa alfajiri utowekao.

6:5 Yer 5:14; 23:29; Ebr 4:12; Yer 1:9-10Kwa hiyo ninawakata ninyi vipande vipande

kwa kutumia manabii wangu;

nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu,

hukumu zangu zinawaka

kama umeme juu yenu.

6:6 1Sam 15:22; Mk 12:33; Yer 4:22; Hos 2:20; Mit 21:3; Mt 12:7; Za 40:6Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu,

kumkubali Mungu zaidi

kuliko sadaka za kuteketezwa.

6:7 Mwa 9:11; Yer 11:10; Hos 5:7; 8:1Wamevunja Agano kama Adamu:

huko hawakuwa waaminifu kwangu.

6:8 Hos 12:11Gileadi ni mji wenye watu waovu,

umetiwa madoa kwa nyayo za damu.

6:9 Yer 5:30-31; Eze 22:9; Za 10:8; Hos 4:2; Yer 7:9-10Kama wanyangʼanyi wamviziavyo mtu,

ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo;

wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu,

wakifanya uhalifu wa aibu.

6:10 Yer 5:31; Eze 23:7; Yer 23:14; Hos 5:3Nimeona jambo la kutisha

katika nyumba ya Israeli.

Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba

na Israeli amenajisika.

6:11 Yoe 3:12-13; Yer 51:33“Pia kwa ajili yako, Yuda,

mavuno yameamriwa.

“Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,

Read More of Hosea 6

Hosea 7:1-16

7:1 Eze 24:13; Hos 4:2; 6:4; Kut 22:2; Sef 2:7; Za 126:1kila mara nilipotaka kumponya Israeli,

dhambi za Efraimu zinafichuliwa

na maovu ya Samaria yanafunuliwa.

Wanafanya udanganyifu,

wevi huvunja nyumba,

maharamia hunyangʼanya barabarani,

7:2 Yer 14:10; 44:21; Mit 5:22; Yer 2:19; 4:18; Hos 8:13; Ay 35:15lakini hawafahamu kwamba

ninakumbuka matendo yao yote mabaya.

Dhambi zao zimewameza,

ziko mbele zangu siku zote.

7:3 Rum 1:32; Yer 28:1-4; Mik 7:3; Hos 4:2; 10:13“Wanamfurahisha sana mfalme kwa maovu yao,

wakuu wao kwa uongo wao.

7:4 Yer 9:2Wote ni wazinzi,

wanawaka kama tanuru

ambayo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchochea

kuanzia kukanda unga

hadi umekwisha kuumuka.

7:5 Isa 28:1, 7; Za 1:1Katika sikukuu ya mfalme wetu

wakuu wanawaka kwa mvinyo,

naye anawaunga mkono wenye mizaha.

7:6 Za 21:9Mioyo yao ni kama tanuru,

wanamwendea kwa hila.

Hasira yao inafoka moshi usiku kucha,

wakati wa asubuhi inalipuka

kama miali ya moto.

7:7 Za 14:4; Sef 1:6; Isa 9:13; Hos 13:10Wote ni moto kama tanuru;

wanawaangamiza watawala wao.

Wafalme wake wote wanaanguka,

wala hakuna yeyote kati yao aniitaye mimi.

7:8 Za 106:35; Hos 5:13; 7:11“Efraimu anajichanganya na mataifa;

Efraimu ni mkate ambao haukuiva.

7:9 Isa 1:7; Hos 8:7Wageni wananyonya nguvu zake,

lakini hafahamu hilo.

Nywele zake zina mvi hapa na pale,

lakini hana habari.

7:10 Hos 5:5; Isa 9:13Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yake,

lakini pamoja na haya yote

harudi kwa Bwana Mungu wake

wala kumtafuta.

7:11 Mwa 8:8; Hos 9:3; 11:11; Mao 5:6; Yer 2:18“Efraimu ni kama hua,

hudanganywa kwa urahisi na hana akili:

mara anaita Misri,

mara anageukia Ashuru.

7:12 Eze 12:13; 32:3; Law 26:14Wakati watakapokwenda,

nitatupa wavu wangu juu yao;

nitawavuta chini waanguke

kama ndege wa angani.

Nitakaposikia wakikusanyika pamoja,

nitawanasa.

7:13 Hos 9:12, 17; Yer 14:10; 51:9; Eze 34:4-6; Mt 23:37; Za 116:11Ole wao, kwa sababu

wamepotoka kutoka kwangu!

Maangamizi ni yao

kwa sababu wameniasi!

Ninatamani kuwakomboa,

lakini wanasema uongo dhidi yangu.

7:14 Ay 35:9; Yer 3:10; Hos 4:10; 13:16; Za 78:34-37; Amo 2:8Hawanililii mimi kutoka mioyoni mwao,

bali wanaomboleza vitandani mwao.

Hukusanyika pamoja kwa ajili ya nafaka na divai mpya,

lakini hugeukia mbali nami.

7:15 Za 2:1; 140:2; Nah 1:9; Hos 11:3Niliwafundisha na kuwatia nguvu,

lakini wanapanga mabaya dhidi yangu.

7:16 Za 78:57; Eze 23:32; Hos 9:3; 11:5; Mal 3:14Hawamgeukii Yeye Aliye Juu Sana,

wako kama upinde wenye kasoro.

Viongozi wao wataanguka kwa upanga

kwa sababu ya maneno yao ya jeuri.

Kwa ajili ya hili watadhihakiwa

katika nchi ya Misri.

Read More of Hosea 7